Warioba usiwatishe Watanzania!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Warioba anazungumza kana kwamba msimamo wake na mawazo yake ndiyo sahihi na kwenda kinyume nayo ni hatari kwa taifa. Wamependekeza serikali tatu na inaonekana wamependekeza kwa sababu tu wanataka 'kuuokoa Muungano' si kwa sababu nyingine yeyote ile. Sasa hajatuambia kwanini wanataka kuuokoa Muungano? Lakini zaidi hajasema kama wananchi wengi wanataka Muungano uokolewe!

Sasa hivi inaonekana kuna kampeni ya wapenzi wa 'Serikali tatu" kulazimisha nchi nzima kufuata njia hiyo. Hii si sahihi na si kweli. Zipo njia nyingi za kuuokoa Muungano mojawapo na labda sahihi zaidi ni kuuvunja kwanza! Baada ya kuuvunja nchi mbili zikae chini na kuamua kama wanataka Muungano tena na kwa masharti gani. Lakini njia sahihi ambayo ni chini ya kuuvunja na kupendekeza kwenda serikali na nchi moja mifumo mbalimbali; ni kama ilivyo Canada, UK, China na hata Marekani. Serikali tatu siyo SULUHISHO pekee la kuukoa Muungano - kama unahitaji kuokolewa.

Kwa vile amekuwa Mwenyekiti wa Tume hii ya kusikiliza maoni Warioba anataka watu waogope kupinga misimamo ya tume hiyo na mapendekezo yake ambayo mengine yanapakana na upuuzi. Sasa wananchi wanayo haki, uwezo na sababu wa kupinga ikibidi mapendekezo yote au mapendekezo yale ambayo yanaonekana kusukumwa na ajenda zilizoshindwa.

Wanaotaka serikali tatu wana haki sawa ya kutoa maoni kama vile wale wanaotaka serikali moja; na yeye kama Mwenyekiti wa Tume kusukumiza maoni yake kwa wananchi ni kutumia nafasi yake vibaya!
 
Muungano nimemchoka, siupendi na siutaki. Ukiendelea kuwapo nitaukubali kwasababu ni matakwa ya wengi. Watu tuwe huru kuamua na tusikandamizwe.
 
Ni kweli mwanakijiji, Mzee Warioba anacheza mpira na akiwa referee wakati huo huo.
 
Ni kweli Warioba na Tume anayoiongoza wanaonekana kutaka kuwalazimisha watu wakubali mapendekezo yao. Wakumbuke kuwa yao ni mapendekezo tu, kazi na mamlaka ya kuamua ni kipi mwisho wa siku ndio kitajenga katiba mpya yapo mikononi mwa watanzania.
Warioba na tume wasijione kuwa wana mamlaka zaidi ya watanzania katika kuamua aina ya katiba tuitakayo

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Huu muungano mimi sioni umuhimu wake...

Tunataka katiba ya Tanganyika haraka sana tuachane na haya mambo ya Katiba ya Muungano ni Ujinga!
 
Mzee Mwanakijiji Warioba amepewa nchi na muungano wake ukiwa kama ''Going Concern" na hakutakiwa kuuvunja bali kupendekeza tiba ya kuuimarisha.
 
Ni nani aliye wadanganya ati katiba mpya ya Watanzania itapatikana chini ya uongozi wa maCCM ?
 
Hili tuliliona mapema sisi Waznz na ndio maana tulimuonya warioba kuingiza mambo yake binafsi kwenye katiba hii, leo ninakuungamikono na miguu M.M kwa jambo la kuuvunja kwanza nchi zote mbili ziwe huru kuamua ni muungano gani watauridhia bila ya malumbano. Hii inakuja kivyovyote vile kama itakua wizara, jumuiya, mkataba au taasisi tu itakayosimamia mambo ya muungano.
 
umenena vyema hata mimi nilimsikiliza huyu warioba yeye kwenye serikali tatu ni kuokoa muungano tuu, lakini alisahau kusema kama wenye muungano huo wanaupenda au lah, na kwanini hawakutoa nafasi ya watu kuujadili au kuupigia kura za maoni na tukajua hatima yake na badala yake naona nguvu nyingi zina tumika kuokoa kitu ambacho ni wazi wengi hawakipendi. Kama kweli tanzania ingekuwa nchi ya kidemokrasia basi watu wangepewa fursa ya kuujali huu muungano na kuupigia kura za maoni na ukweli ukajulikana kuliko kuleteana mizigo hisiyo na msingi na kwenye huu muungano kwa nini watanganyika wanateseka sana kuulinda kuliko wazanzibari hasa ukiangalia ki rasilimali ni wazi tanganyika ndio wanatumia rsilimali nyingi kuulinda kuliko wazanzibari. Kwanza watwambie nini mchango wa wazanzibari kwenye huu muungano?
 
Mzee Mwanakijiji Warioba amepewa nchi na muungano wake ukiwa kama ''Going Concern" na hakutakiwa kuuvunja bali kupendekeza tiba ya kuuimarisha.

Mkuu hapo kwenye red, possibly ulikusudia kuandika ceasing concern. "Ndoa ya kulazimisha kamwe haidumu"
 
Mzee Mwanakijiji,

Mimi nadhani huenda serikali tatu ndio itatufundisha kwamba tunachemka na kurudi kwenye serikali moja...

Note: Ile tume ina watu zaidi ya 30 yale sio mawazo ya Warioba mwenyewe.
 
Warioba sio kama anataka kama anataka watu waogope warioba kafuata demokrasia kasikiliza kilio cha watu wa pande zote mbili kuhusu mungano uliopo

Viongozi wetu wamezoea kuwaburuza wananchi, wanajiona wao ndio wenye akili kuliko raia mwengine yoyote yule na ndio maana nchi za Africa aziishi matatizo,hamna mtu asietaka mungano lakini huu mungano ulipo sasa kati ya Tanganyika na Zanzibar haufai,period
 
Warioba anazungumza kana kwamba msimamo wake na mawazo yake ndiyo sahihi na kwenda kinyume nayo ni hatari kwa taifa. Wamependekeza serikali tatu na inaonekana wamependekeza kwa sababu tu wanataka 'kuuokoa Muungano' si kwa sababu nyingine yeyote ile. Sasa hajatuambia kwanini wanataka kuuokoa Muungano? Lakini zaidi hajasema kama wananchi wengi wanataka Muungano uokolewe!

Sasa hivi inaonekana kuna kampeni ya wapenzi wa 'Serikali tatu" kulazimisha nchi nzima kufuata njia hiyo. Hii si sahihi na si kweli. Zipo njia nyingi za kuuokoa Muungano mojawapo na labda sahihi zaidi ni kuuvunja kwanza! Baada ya kuuvunja nchi mbili zikae chini na kuamua kama wanataka Muungano tena na kwa masharti gani. Lakini njia sahihi ambayo ni chini ya kuuvunja na kupendekeza kwenda serikali na nchi moja mifumo mbalimbali; ni kama ilivyo Canada, UK, China na hata Marekani. Serikali tatu siyo SULUHISHO pekee la kuukoa Muungano - kama unahitaji kuokolewa.

Kwa vile amekuwa Mwenyekiti wa Tume hii ya kusikiliza maoni Warioba anataka watu waogope kupinga misimamo ya tume hiyo na mapendekezo yake ambayo mengine yanapakana na upuuzi. Sasa wananchi wanayo haki, uwezo na sababu wa kupinga ikibidi mapendekezo yote au mapendekezo yale ambayo yanaonekana kusukumwa na ajenda zilizoshindwa.

Wanaotaka serikali tatu wana haki sawa ya kutoa maoni kama vile wale wanaotaka serikali moja; na yeye kama Mwenyekiti wa Tume kusukumiza maoni yake kwa wananchi ni kutumia nafasi yake vibaya!

Kabla ya kuunga mkono hoja yako, ni lazima unifafanulie ToRs za Tume anayoiongoza pengine aliambiwa auokoe badala ya kuuvunja?
 
Muungano nimemchoka, siupendi na siutaki. Ukiendelea kuwapo nitaukubali kwasababu ni matakwa ya wengi. Watu tuwe huru kuamua na tusikandamizwe.

hayo matakwa ya wengi yametoka wapi? au ulimaanisha baraza la mawaziri na marais wake.

haya ni matakwa ya watu wachache ni vyema hapa demokrasia itumike kuamua hili si kuweka serikali tatu
 
umenena vyema hata mimi nilimsikiliza huyu warioba yeye kwenye serikali tatu ni kuokoa muungano tuu, lakini alisahau kusema kama wenye muungano huo wanaupenda au lah, na kwanini hawakutoa nafasi ya watu kuujadili au kuupigia kura za maoni na tukajua hatima yake na badala yake naona nguvu nyingi zina tumika kuokoa kitu ambacho ni wazi wengi hawakipendi. Kama kweli tanzania ingekuwa nchi ya kidemokrasia basi watu wangepewa fursa ya kuujali huu muungano na kuupigia kura za maoni na ukweli ukajulikana kuliko kuleteana mizigo hisiyo na msingi na kwenye huu muungano kwa nini watanganyika wanateseka sana kuulinda kuliko wazanzibari hasa ukiangalia ki rasilimali ni wazi tanganyika ndio wanatumia rsilimali nyingi kuulinda kuliko wazanzibari. Kwanza watwambie nini mchango wa wazanzibari kwenye huu muungano?

Haistahiki ena hapa tulipo kujua znz inatoa nini au inapata nini kwenye muungano huu uliyobakia thulusi kukatika, kinachotakiwa kujadiliwa ni jinsi ya kuuvunja kwakua Warioba anaungangania uwepo na yeye umri wake ushaenda anataka atuachie watanzani migogoro au na yeye anadhani atadumu kama walivofikiria walipita mpaka leo ndo hapa walipotufikisha.
 
Mzee Mwanakijiji tafadhari tudadavulie kuhusu muungano wa UK. Binafsi napendekeza sera ya majimbo, halafu kutoka hapo Zanzibar liwe ni mojawapo ya majimbo ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Iwe represented na gavana tu sawasawa na majimbo mengine yatakayoundwa na si kuwa na marais wawili wawili katika nchi moja. Au hiyo habari ya kwenda kwenye serikali tatu. I hate serikali tatu.Tuchukue mfumo wa muungano wa USA.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mzee Mwanakijiji, niko na wewe pamoja kuupinga huu mkakati wa Jaji Warioba kuwafundisha Watanganyika cha kusema na kufikiri kuhusu hii rasimu yake, lkn still kuna mambo ambayo inaonekana ni dhambi kuyajadili hapa Tanzania na sijui kwa nini.

Huu muungano una faida gani kwa Mtanganyika?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom