Augustine Moshi
JF-Expert Member
- Apr 22, 2006
- 2,554
- 1,382
Ni vema tukaelewana kuhusu misamiati tunayotumia kwenye huu mjadala. Baada ya kupitia michango mbalimbali, nimeona uelewa wetu wa neno serikali unatofautiana.
Tunaweza kukubali kutumia neno serikali kama primitive term, maana hatuwezi kutoa definition ya kila neno. Ziko primitive terms nyingi kwenye lugha zote. Line, plane, point, etc. are some examples of primitive terms in Euclidean Geometry.
Kwa sasa Tanzania kuna serikali ngapi? Sio mbili tu. Kila wilaya ina serikali yake. Mkuu wa serikali ya wilaya ni DC. Hachaguliwi kidemokrasia lakini hilo ni tatizo tofauti. Kuna mahakama za wilaya, na madiwani ni legislative arm ya wilaya. Miji na majiji nayo yana serikali zao. Kwa hivyo basi, hili swali la serikali moja, mbili au tatu labda linahusu serikali kuu moja mbili au tatu.
Nchi moja haiwezi kuwa na serikali kuu tatu zinazolingana. Tume ya Warioba haijapendekeza serikali kuu tatu zenye madaraka sawa.
Kiuchumi, tatizo sio wingi wa serikali bali ni ukubwa wa serikali. Kwa sasa tuna serikali kuu mbili, lakini gharama yake ni kubwa sana. Serikali ya Muungano peke yake ina zaidi ya mawaziri 60!
Muundo tulio nao sasa wa nchi moja yenye serikali kuu mbili sio mzuri. Matatizo yake tumeyaona. Mwalimu alijaribu kupunguza hayo matatizo kwa kuwa na chama tawala kimoja kinachoongoza serikali zote, lakini haikotosha. Matatizo yaliendelea hata kikafika kile kipindi akatumia nguvu dhidi ya Rais wa Zanzibar (Jumbe).
Stability inataka tuwe nchi moja, yenye serikali kuu moja ya JMT, na serikali za Zanzibar na Tanganyika. Wakuu wa serikali za Zanzibar na Tanganyika wakiitwa Magavana (kama inavyopendekeza Tume) au majina mengine si hoja. Cha msingi ni kwamba wote hao wataapa kuilinda Katiba ya JMT (pamoja na katiba za serikali zao).
Muundo wa serikali za Tanganyika na Zanzibar na ya serikali ya muungano utatakiwa uwe kwenye katiba moja yenye vipengele vyote. Nilitegemea Tume ya Warioba itoe mapendekezo ya KATIBA MOJA, SERIKALI TATU. Na ndio maana Tume ina wawakilishi toka sehemu zote za muungano.
Tunachopashwa kujali sana basi sio wingi wa serikali bali wingi wa katiba zinazojitegemea.