Jaji Warioba: Sioni uwezekano wa kupata katiba kufika mwaka 2029. Serikali inaona bado hakuna kikubwa

Jaji Warioba: Sioni uwezekano wa kupata katiba kufika mwaka 2029. Serikali inaona bado hakuna kikubwa

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,217
Reaction score
3,796


Jaji mstaafu Joseph Warioba, ameonesha wasiwasi wake juu ya uwezekano wa nchi kupata Katiba Mpya kabla ya kuingia kwenye mchakato wa uchaguzi wa mwaka 2029.

Akizungumza leo Agosti 28, 2026, katika mkutano wa wadau wa masuala ya kidemokrasia uliofanyika katika makao makuu ya Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Jaji Warioba amesisitiza kuwa kutopatikana kwa katiba hiyo kutasababisha changamoto kubwa katika masuala ya uchaguzi ujao 2030

Jaji Warioba ameonya kuwa ikiwa nchi itaingia kwenye uchaguzi mkuu wa 2030 kwa kutumia mfumo na Tume ya Uchaguzi iliyopo sasa bila kupata Katiba Mpya, taifa litakabiliwa na madhara makubwa. Ameeleza kuwa muundo na utaratibu wa sasa wa uchaguzi haukidhi matarajio ya kuleta uwazi na haki inayotakiwa katika kuendesha mambo ya kidemokrasia.

Aidha, amegusia hali ya majeraha na maombolezo yanayoendelea miongoni mwa wananchi kutokana na matukio ya Oktoba 29 2025, huku akiikosoa Serikali kwa kuchukulia hali hiyo kama jambo la kawaida.
 
Katiba mpya sio mwarobaini wa matatizo yote yaliyo kwa hii nchi. Hakuna nchi duniani kwa sasa isiyolialia. Changamoto kubwa ninayoiona kwa Tanzania ni kutoishi maisha yetu ya asili. Asili ina nguvu sana tutake tusitake. Hizi vurugu tunazoziona za CCM kutokubali kutoka madarakani na kukuru kakara zote za kisiasa chini ya vyama vingi ni dalili tosha kutuonesha kuwa tunalazimisha kuvaa viatu visivyo vyetu.

Kuanzia kwa machifu huko hadi kwa TANU then CCM hii nchi was never about prulastic politics. Na Nyerere was clever kudesign system itakayokuwa jumuishi pamoja na asili zetu za uchifu ndio akaja na mambo ya demokrasia ndani ya chama kimoja. Kama watu wanataka madaraka kuongoza serikali fight ndani ya chama kimoja mpate madaraka hayo. Msitusumbue sisi raia wa kawaida tunaishi kwa kudra za Mwenyezi.
 
28 August 2026

WADAU WAONGEA


View: https://m.youtube.com/watch?v=ieUrniUezG0

1787911244418.png
 
Back
Top Bottom