Warioba: CCM ijiandae kuwa chama cha Upinzani

Mtoa hoja amesema kweli. ccm wenyewe wanajua wazi kwamba hiki ndio kipindi chao cha mwisho kutawala. Ndio maana utaona kuwa majority ya mipango ya ccm(kudidimiza uchumi, ufisadi) inaishia 2015
 
basi ccm tumenchagua mrithi wetu ni TLP!2015 SISI TUNARUDI ZETU KWA BABA , NA WALA HAMTUONI TENA! UNASEMA JE!
Kwanini TLP na wala sio chama kingine chochote?

Kuna uhusiano gani kati ya CCM na TLP?

Kwanini isiwe CUF imbayo mmefunga nayo ndoa rasmi?
 
Badala ya kukandya wapinzani kila mara na kusema hawataingia Ikulu ni vema CCM ikajiandaa kwa kuweka mazingira muafaka hasa ya kimtazamo na kisaikolojia kama wapinzani wataingia Ikulu. Wapinzani ni watanzania lakini chama kimoja kianawaona kama wanyamulenge. Nasema hivo kwa kunukuu maneno ya msemaji mmoja wa CCM kuwa kuunga mkono chadema ni kunahitaji roho ya shetani kwani chadema kimedhamiria kuifanya damu za wtz kama kafara.
mtizamo huu ni hatari sana kwani ikiwa wanachi wataamua kukipa chadema kura nyingi hapatakuwa na uhusiano mzuri baadae kati ya vyama hivi.
mwisho ni vizuri kuyandaa mazingira kama haya kwa usalama wa taifa letu na kwa faida ya CCM kama itashidwa. pia wananchi wataweza kuamua wenyewe kwa hiari yao bila kuhisi wanaunga mkono mashetani au la. Taanzania ni moja lakini vyama ni vingi. Tanzania si CCM; si CDM; si CUF n.k. bali Tanzania kuna CCM, CDM, CUF n.k.Watanzania wana haki ya kuchagua kimojawapo.
 
kazi ipo watanzania tujiandae kwa mabadiliko hakuna wakutuletea isipokua ni sisi wenyewe tusiishie kuonge jamvini tu

Hapa ndipo Nape anatakiwa kuwa makini kuona ni wapi wanaweza kusaidia kurejesha heshima na kukubalika kwa CCM. Hali ilivyo sasa hasa serikalini inatisha kidogo.

Wenzetu waliopewa madaraka; mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya wamegeuza serikali kuwa duka lao. Kila mmoja yuko mbio mbio kuchukua fedha kwa matumizi binafsi au yanayonufaisha rafiki zake.

Majuzi tu Serikali ilitoa waraka unaozuia kununua magari yanayozidi cc 3000. lakini tazama mashangingi yanvyoendelea kununuliwa. na unajua kazi ya mashangingi hayo? ni kupeleka watoto wa vigogo shule na kumbi za starehe.

Tunakwenda wapi? Matumizi kwenye serikali ni makubwa bila sababu yoyote ya msingi. Hili linaudhi watumishi wa chini na kuwafanya waichukie serikali. Tafadhali Bw. Nape na Bw. Mwigulu if you are really for politics wakanyeni makada wenu. waache mchezo huu.
 
Inawezekana lakini ongea kwa data sio kwa ndoto za mchana.tembo na mbuzi wapi na wapi
 
Hofu hii ya ccm kuwa chama cha upinzani ndio inayowafanya watumie mbinu nyingi sana tena chafu kuhakikisha hawafiki huko. Pamoja na mbinu hizo bado wanasahau kuwa watanzania wa leo sio wale wa enzi za kidumu chama .........

Hawa ni watanzania walioelimika na wanajua kila dhuluma inayoendelea. Kama sio kuchanganyikiwa na kasi ya wapinzani ni nini?Angalia nguvu kubwa inayotumika kudhibiti upinzani?angalia agenda za kurubuni waganga njaa ili kusaliti upinzani.Haya yote yanafanyika kwa sababu taa nyekundu inawaka kuashiria muda wa CCM umekwisha. Kama mnabisha kwa nini mnatumia juhudi kubwa sana kuwadhibiti wapinzani.Hii ni ishara ya kutokujiamini

Ishara ya pili ni idadi ya makundi yaliyoko kwenye chama chenu. Kimekuwa kama nyumba la mbao linalobomoka na kila mtu anakimbilia kuchukua ubao wake.

Kama kweli mnabisha acheni hizo faulu kisha twende uwanjani muone kama upinzani hawajawaweka pembeni mwakani.
 
Mada tatu zinazofanana, ni mtu mmoja mwenye ID tofauti? kumbe inawezekeana CHADEMA humu ni 10 tu ila wana ID kibao kibao kila mtu.
 
Hakuna kipya alichosema Warioba.Hilo lichama linasubiri kuzikwa tu,hayo yote yanajulikana tangu enzi ya akina Kolimba kazi kwetu watanzania wapenda mabadiliko kuitimisha tu.
 
Kwakeli Nimechoka Kuwa Mpinzani Nasubiria October Ukawa Ndani Ya Mjengo. Hapa Tupia Adha Mbalimbali Ambazo Umezipata Ukiwa Mpinzani Maana Mda Simrefu Tunapata Uhuru Wa Pili.
 
Back
Top Bottom