Warembo wangu, upo tayari kufunga ndoa bila sherehe?

Uliponea chupu chupu kuuwawa au?
Aisee,wanawake wa kinyakyusa huwezi kuoa bila sherehe,utakuwa unatengeneza ugomvi kuanzia ngazi ya familia hadi ukoo. Ni watu wa kufuatiliana sana kimaisha,namshukuru Mungu niliponea chupu chupu.
 
Mimi sijaolewa na mnyaki, baba yangu hakuoa mnyaki (mama); aunts zangu wengi wameolewa na makabila mengine na tunadunda. Kushindwana kwako na mnyaki sio conclusion kwamba wote waliooa/kuolewa na wanyaki ndoa ziliwashinda. Au hao ambao wanapeana talaka kila siku ni wanyaki tu?
Acha niishie hapo,itoshe kusema tu wanyakyusa wanapaswa kuoana wenyewe kwa wenyewe.
 
Hapa wanajifanya hawapendi shughuli ilaaa... Wadada ukizungumzia ndoa basi kichwani inakuja pcha ya shela la bei, matarumbeta, ukumbi uliopambwa vizuri rangi ya sare aipendayo.
 
Tena kwa maisha ya sasa, no fresh tu...lengo limeshatimia (ndoa) mengine nu ziada tu
 
Sio siri mi sipendi sherehe stress yake ni noma aisee, unachanika mifuko mpaka basi. Shida ni wazazi ndo wanashikiliaga mambo ya sherehe. Amini kwamba wanandoa weng walitaman wafunge tu wasepe.

Mzazi hasa wamama utasikia nimewachangia na mm wanichangie. Mi sitaki sherehe bana
 
Leo humu kila mwanamke hapendi sherehe. Tehe teh.
Any matured lady, anayejua majukumu ni nini hawezi kupenda sherehe. Wapenda sherehe ni watu wa show off, yupo radhi atumie iphone 12 wakat anakaa room ya 50k per month ili watu wamuone. But a matured lady atatumia Nokia ya tochi huku akitimiza majukumu muhimu kama kipato chake hakiruhusu!
 
Wote tunafahamu kuwa suala la ndoa ni jambo la heshima na baraka katika misingi ya kijamii na kiimani.

Swala la kufanya ndoa kama sherehe kubwa liko katika maamuzi na mapenzi ya wanandoa wenyewe japo linaweza chagizwa na wazazi ama walezi pia.

Leo nataka nipate tathmini kutoka kwa wachumba esp. wadada je, wewe upo tayari kufunga ndoa bila kuinvolve sherehe?
sherehe sio ndoa cha muhimu ni kufunga ndo takatifu
 
Back
Top Bottom