Waraka wangu wa Mwaka Mpya Kwa wana MMU … | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka wangu wa Mwaka Mpya Kwa wana MMU …

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by HorsePower, Jan 1, 2012.

 1. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Wana MMU, Heri ya Mwaka Mpya 2012!

  Nimepata msukumo wa ndani ya Moyo wangu kuwaandikia waraka huu, kwa upendo mwingi sana, ninyi ndugu na rafiki zangu wakubwa wa MMU nikiwashukuru kwa ushauri na ushirikiano mkubwa mliouonyesha kwa mwaka huo tulioupoteza wa 2011.
  Binafsi kuingia 2012 kwangu naona kama miujiza mikubwa sana. Leo hii nilikuwa nikitafakari ndugu kadhaa ambao TUMEWAACHA ktk mwaka uliopita. Ni siku chache tu tumewapoteza watangazaji Halima na John Ngayhoma. Siku kadhaa nyuma tuliwapoteza ndg zetu wengi kutoka Zanzibar kwa ajali ya Kuzama Meli. Wapo waliobaki mwaka 2011 kwa vifo vya kikatili mno kama walioteketea kwa moto kwa ajali ya basi huko chalinze! Wapo waliopoteza maisha kwa ajali mbaya za Pikipiki za kupondwa vichwa vyao! Wapo waliobaki mwaka 2011 kwa vifo vy ajali za gari na kukatwa vipande vipande kiasi cha kushindwa kutambulika. Wapo waliobaki kwa vifo vya wenzao kujilipua kwa kujitoa Mhanga. Pia wapo waliomezwa na mafuriko na wakafa vifo vibaya kabisa vya kunywa maji machafu mpaka kifo. Vita na maandamo ya kupinga watawala dhalimu iliwabakiza wengi! Magonjwa nayo hayakubaki nyuma! Vipo vikundi vya nyimbo na burudani ambavyo pia vilibaki kwa namna mbaya ya ajali isiyoelezeka!
  Siwezi kutaja kila janga na namna ambavyo wenzetu wameshindwa kuingia 2012, lakini tujiulize sisi ni nani mpaka tupate neema hii ya kuuona mwaka huu mpya? Au tumefanya jambo gani zuri la kutubakiza kwa mwaka 2012? Hebu tafakari, na mshukuru Mungu wako aliyekulinda na mabaya yote ya 2011 na kukupa neema ya kuingia 2012!

  Kipindi hiki cha kuanza mwaka mpya ni kizuri sana kutafakali yale ambayo uliyapanga mwaka uliopita ukashindwa kuyatekeleza. Kwa sasa chukua muda huu, kupanga malengo yako mapya na jitahidi kuhakikisha mwaka huu unamudu kuyatimiza, uliyoyapanga mwaka huu na yale yaliyosalia ya mwaka jana.

  Waliobahatika kupata ndoa mwaka 2011, mzilinde ndoa zenu. Jiepusheni na watu wanaojifanya kuwapenda angali mna ndoa, hao ni hatari kwa maisha yenu ya sasa na baadaye, waogope kama ukoma. Kamwe msijihushishe na mambo ya kukumbushia enzi na wale wa zamani, mtaumia. Kataeni aina zote za mahusiano machafu na yale yasiyo halali, muogopeni Mungu.
  Kwa wale mliopoteza ndoa zenu au wapenzi wenu, poleni sana. Nawaombea Mungu ayaponye majeraha yenu mliyopewa na wenzi wenu. Nawashauri kutulia, mkiyasahau yale ya 2011 na kuanza maisha mapya 2012. Naamini ukimtegemea Mungu, iko siku utampata wa kukufaa maisha yako yote.

  Najisikia kuwashauri wale wote wanaofanya kazi, tujipange mwaka huu tufanye kazi kwa bidii. Wanafanyabiashara, Wakulima na waliojiajiri kwa namna yeyote ile tukaze buti, tuweze kuyatimiza malengo yetu.
  Kwa wenye familia tukumbuke kuzitunza familia zetu kwa upendo mwingi. Tukumbuke kwenda kwenye ibada mara kwa mara kumuomba Mungu atulinde na kutukinga na mabalaa ya aina zote.

  Niwatakie kila namna ya mafaniko katika mwaka huu Mpya. Upendo na amani vitawale maisha yako. Mikosi ya aina zote, ajali, magonjwa, kuchukiwa bila sababu, roho ya uvivu na mateso ya namna zote yakuepuke.

  Happy New Year,

  HorsePower
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  who do u think you are????
  Kikwete????
   
 3. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  hapana, mimi siyo Kikwete! Mimi ni HorsePower, nipo kwa kukutakia heri ya Mwaka Mpya, sina la ziada!
   
 4. Binti Magufuli

  Binti Magufuli JF-Expert Member

  #4
  Jan 1, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 7,460
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Tunashukuru saaaaaaaaaaaaana kwa hotuba hii tamu na ya kutuandaa kusafiri salama kwa mwaka 2012 kama tukiishi kulingana na mausia haya!! Lakin pia nipende kusema kuwa Hotuba yako imegusa kila sector isipokuwa tu mambo ya mazingira (haiko environmental friendly kabisa), climate change na madhara mengine yatokanayo na kutothamini mazingira ni janga la dunia......tukumbushane production and consumption energy efficiency based kama mojawapo ya njia kuu ya kukabiliana na tatizo hili kwa mwaka 2012
   
 5. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2012
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  thanks ujumbe mzuri!
   
 6. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #6
  Jan 1, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  ahsante Mkuu,nami nakutakia heri na mafanikio 2012!
   
 7. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #7
  Jan 1, 2012
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  ....dahhh, ahsante kaka....heri ya mwaka mpya na maazimio yote mema tutayojaaliwa nayo kwa mwaka huu.
  INSHAALLAH.
   
 8. neggirl

  neggirl JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2012
  Joined: Jul 30, 2009
  Messages: 4,830
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145

  Mmmmhh! The Boss mzima wewe?
   
 9. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #9
  Jan 1, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Asante kwa mawaidha mema na kututaka tujiandae kwa mwaka huu
  Heri ya mwaka mpya pia kwako
   
 10. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #10
  Jan 1, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  heri ya mwaka mpya
   
 11. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #11
  Jan 1, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Ni mimi tu sijatoa salamu/waraka wa mwaka mpya.
  Ngoja niende library nikaandae....
   
 12. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Thank you.
  Tutaufaniya kazi huu waraka wa ukweli.
   
 13. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Asante kwa maoni, ujumbe wako automatically umekuwa added kwenye waraka huu.

  Many thanks,
  HP
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nimekusoma mkuu................nakutakia mwaka mpya mwema 2012, uumalize salama ili mwakani 2013 uje na waraka mwingine, lakini usio na matukio ya kutisha kama haya, naamini inshaallah mwaka huu utakuwa na mengi mema ya kujivunia.
   
 15. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #15
  Jan 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  na wewe pia..
   
 16. A

  Aine JF-Expert Member

  #16
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ahsante sana, na ubarikiwe, ni kweli wengi walitamani mioyoni mwao wauone mwaka 2012, lakini hawapo tena dunia hii, sisi ni nani, na tumetenda mazuri gani hata tukauona mwaka huu wa 2012!! tunamshukuru Mungu aliyetuwezesha kuuona mwaka huu, na kwa wale wote waliofikwa na majanga mbalimbali hata hawakuusherehrkea vizuri mwaka, tunawapa pole sana, hata hivyo na wao wanapaswa kumshukuru Mungu kwa kufika mwaka 2012
   
 17. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #17
  Jan 2, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Asante sana,nawe nakutakia mwaka mpya wenye mafanikio.
   
 18. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #18
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  asanta kwa wakara mzuri HP.
  heri ya mwaka mpya kwako pia.
   
 19. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #19
  Jan 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,088
  Likes Received: 6,554
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu HP.
   
Loading...