Bajeti Kuu ya Mwaka wa Fedha 2026/2027 inasomwa Leo Bungeni; Je, Italeta Unafuu wa maisha au Mzigo Mpya kwa Mwananchi?

Bajeti Kuu ya Mwaka wa Fedha 2026/2027 inasomwa Leo Bungeni; Je, Italeta Unafuu wa maisha au Mzigo Mpya kwa Mwananchi?

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
962
Reaction score
1,909
Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/27 inatarajiwa kusomwa bungeni jijini Dodoma, na kila mmoja wetu anasubiri kwa hamu kujua mwelekeo wa maisha yetu kwa mwaka ujao.

Ni bajeti ya kwanza kusomwa inayoanza kutekeleza Dira Mpya ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2050 (Vision 2050).

Akitoa mwelekeo wa dhamira ya Serikali kuelekea mwaka huu wa fedha, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, alisisitiza:

"Bajeti ya mwaka 2026/27 ni ya kihistoria kwa kuwa ndiyo inayoanza kutafsiri kwa vitendo Dira mpya ya Taifa ya Maendeleo ya 2050. Tumejipanga kuhakikisha sekta za uzalishaji zinachochewa kwa kasi ili kupanua wigo wa ajira kwa vijana, kuimarisha uchumi wa kidijitali, na kupunguza ukali wa maisha kwa mwananchi wa kawaida chini ya msingi wa kujitegemea zaidi."

Wewe binafsi una matarajio gani makubwa kutoka kwenye bajeti ya kesho?

Vipaumbele vyako ni vipi?
Unadhani Serikali inapaswa kuelekeza nguvu na mabilioni ya fedha kwenye maeneo gani zaidi kati ya haya:
  • Elimu na Mikopo ya Elimu ya Juu
  • Afya na Bima kwa Wote
  • Kilimo, Mifugo na Ruzuku za Pembejeo
  • Kodi, Biashara, na Fursa za Ajira kwa Vijana
Je, unatarajia kusikia unafuu wa kodi kwenye bidhaa gani muhimu zinazogusa maisha yako ya kila siku?
 
Hakuna Jipya! Nadhani wangeisoma jumatatu ijayo!
Kwa kesho macho na masikio ya Watanzania wengi yataelekezwa Mahakamani kufuatilia kesi ya Lissu na Kombe la dunia.
Hata waisome mwezi ujao kuna mtu atakaa kusikiliza ?
 
Back
Top Bottom