Waraka wangu kwa Nape Nnauye

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
3,542
2,000
Ndugu,
nakuandikia waraka huu kwa kuwa wewe ni katibu wa uenezi wa Chama Cha Mapinduzi,chama hiki ndicho kilichoshikilia dola kwa sasa.
Kumekuwa na mgogoro ndani ya CHADEMA na kwa muda wengi ambao tunaingia katika mitandao tumechangia kwa kiwango kikubwa kutoa maoni yetu.
Naandika waraka huu nikikerwa na jambo moja ambalo kwa maoni yangu naona linajenga jambo ambalo tutakuja kulijutia baadae.Naelewa kisiasa unaweza ukawa na furaha kuvugika kwa CHADEMA lakini kama una mtizamo mpana utaona ya kuwa kufa au kupotea kwa chama chochote cha upinzani hakuna tija kwa chama tawala na nchi kwa ujumla,nikipata muda nitalieleza hili kwa kina.
Kwa leo tuangalie udini,ukabila na ukanda unaojengwa na wapinzani wa CHADEMA (majority wakiwa ni wana CCM walio chini yako.)
Chuki dhidi ya wachaga nimeiona kwa macho yangu katika mikoa ya kusini hasa baada ya wao kununua maeneo na naona sasa inakilozwa moto katika mkoa wa kigoma.Hakuna anayekemea!!!!
Hivi kwa CCM kukemea jambo hili kutawagharimu nini ukilinganisha na kuliacha liendelee?
Waislamu (nami nikiwemo) wanalalamika kuhusu kudhulumiwa kunyanyaswa lakini hamjitokezi kutoa maelezo ya kina na mnaacha hisia zinaendelea kujengeka katika jamii,mtafaidika nini udini ukikomaa?
Ukatoliki wa Slaa umekuwa ni kigezo cha kutumika katika kuipinga CHADEMA,mbona hamkemei?
Kama kweli CHADEMA kina Uchaga,udini na ukanda kwa nini ushahidi usiwekwe mezani na kikafutwa mara moja?
Naamini si vizuri kufurahia ushindi wa kishindo wakati mnawagawa wananchi kwa ukabila na udini,CCM ni lazima ikemee jambo hili kwani likitokea la kutokea hamtabaki hata nyie.
Huu ni wajibu wako Nape!
 

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,619
2,000
Upo sahii,kwa gharama yoyote lazima mtu wa kaskazini achukue hii nchi mwaka 2015,ama slaa au lowassa.Wao ndo wame2bip kaskazini tunapiga na fweza 2nazo.
 

Ringo Edmund

JF-Expert Member
May 10, 2010
4,884
0
Nafikiri huwezi pata jibu la maana kwa nape ukizingatia wanahubiri kingine na kutenda kingine.mfano jana mwenyekiti wao anamsifia mandela kwa kuwasamehe waliomtesa na kutuasa tuwe tunasamehe wakti ameifunga familia nzima kwa ajili ya kiungo ambacho hata hakipo mwilini mwake.
 

Kilaga

JF-Expert Member
Feb 23, 2013
2,148
2,000
Mawazo mazuri, lakini hawa akina Nape ndiyo wanaokuza na kupamba mambo hayo, kweli wanaweza shaurika? They are doing it purposely, and so they're loughing at us. Ccm ni wa aajabu sana.......
 

Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,873
1,500
Mimi huwa najiuliza hivi siku watanzania wakiaminishwa hivyo na CCM kwamba CDM ni chama cha Wakiristu na watu wa Kasikazini.

Halafu CUF ni chama cha Waislamu na Wapemba, God forbid na Watanzania wakaamini hivyo. Swali langu ni hivi WAPIGA kura wa CCM watakuwa nani?!

Mchimba kisima huingia mwenyewe!
 

swagazetu

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
4,089
2,000
naona hapa michango ya akina magetsita na msalani haina nafasi mbona siwaoni..wanajua zao wakiguswa mku....ni kimya mpaka rungu litoke.imewaingia eh!
 

microX

JF-Expert Member
Feb 6, 2011
482
500
Upo sahii,kwa gharama yoyote lazima mtu wa kaskazini achukue hii nchi mwaka 2015,ama slaa au lowassa.Wao ndo wame2bip kaskazini tunapiga na fweza 2nazo.

Hujui unachokindika kikombe cha vita ya ukabila upo tayari kukinywa?
 

simbilisi

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
792
0
chadema ni chama cha wachaga na wakristo, mimi sio mwana CCM ni mtanzania wa kawaida kabisa

hoja yako umeijenga kuwa wanaosema uchaga na ukristo ni wana CCM ndipo ulipochemka

hauwajui watanzania, haujui tanzania, pole sana

chadema ni saccos
 

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
3,542
2,000
chadema ni chama cha wachaga na wakristo, mimi sio mwana CCM ni mtanzania wa kawaida kabisa

hoja yako umeijenga kuwa wanaosema uchaga na ukristo ni wana CCM ndipo ulipochemka

hauwajui watanzania, haujui tanzania, pole sana

chadema ni saccos
Kama CHADEMA ni SACCOS kwa nini ruzuku ipelekwe kwenye SACCOS.Kumbuka ruzuku vyama vinayopewa ni pesa ya walipa kodi,how on earth upeleke pesa ya walip kodi wako kwenye SACCOS ya wachaga?
Unajenga ukabila ambao hautakusaidia!
Hoja yangu ni kuwa Chama cah Mapinduzi kihakikishe kuwa kinakemea watu woye wanaojenga udini na ukabila na ikiwa kweli CHADEMA ni cha wakristo na wachaga na kama ushahidi kifutwe!
 

wauwau

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
705
170
Watu wanaoisema cdm hivyo ni wale cdm wanaoudhika na matendo yake yanayoonyesha sura halisi ya cdm na kwa kweli ukiongea nao wamechoka. Bado kuna misukule toka hasa kaskazini humu ndama inajipa moyo katika hayo. Si muda muda mrefu matokeo utayaona
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom