Ndugu,
nakuandikia waraka huu kwa kuwa wewe ni katibu wa uenezi wa Chama Cha Mapinduzi,chama hiki ndicho kilichoshikilia dola kwa sasa.
Kumekuwa na mgogoro ndani ya CHADEMA na kwa muda wengi ambao tunaingia katika mitandao tumechangia kwa kiwango kikubwa kutoa maoni yetu.
Naandika waraka huu nikikerwa na jambo moja ambalo kwa maoni yangu naona linajenga jambo ambalo tutakuja kulijutia baadae.Naelewa kisiasa unaweza ukawa na furaha kuvugika kwa CHADEMA lakini kama una mtizamo mpana utaona ya kuwa kufa au kupotea kwa chama chochote cha upinzani hakuna tija kwa chama tawala na nchi kwa ujumla,nikipata muda nitalieleza hili kwa kina.
Kwa leo tuangalie udini,ukabila na ukanda unaojengwa na wapinzani wa CHADEMA (majority wakiwa ni wana CCM walio chini yako.)
Chuki dhidi ya wachaga nimeiona kwa macho yangu katika mikoa ya kusini hasa baada ya wao kununua maeneo na naona sasa inakilozwa moto katika mkoa wa kigoma.Hakuna anayekemea!!!!
Hivi kwa CCM kukemea jambo hili kutawagharimu nini ukilinganisha na kuliacha liendelee?
Waislamu (nami nikiwemo) wanalalamika kuhusu kudhulumiwa kunyanyaswa lakini hamjitokezi kutoa maelezo ya kina na mnaacha hisia zinaendelea kujengeka katika jamii,mtafaidika nini udini ukikomaa?
Ukatoliki wa Slaa umekuwa ni kigezo cha kutumika katika kuipinga CHADEMA,mbona hamkemei?
Kama kweli CHADEMA kina Uchaga,udini na ukanda kwa nini ushahidi usiwekwe mezani na kikafutwa mara moja?
Naamini si vizuri kufurahia ushindi wa kishindo wakati mnawagawa wananchi kwa ukabila na udini,CCM ni lazima ikemee jambo hili kwani likitokea la kutokea hamtabaki hata nyie.
Huu ni wajibu wako Nape!