Waraka wangu kwa JWTZ, Watanzania

Waraka wangu kwa JWTZ, Watanzania

huniju sikujui! majukumu ya jeshi sio kufa hata kwa vita za kijinga zinazoletwa na rais wenu dhaifu! ameshindwa kutujenga katika ustawi sasa anatumia njia mbadala ya kuunganisha wananchi kwa kutumia external aggressions!
Anataka nikujue kwani we -ke,kaza mwandiko huo muda ukifika utaingia kambini na tutakuvua uraia huo na utaingia front line..,jeshin hakuna siasa.
 
utakuwa na raha gani kuishi kwa starehe zote huku jirani yako akiishi bila kujitambua atauwawa kwa risasi saa ngapi? kuwa na usawa watu wote tunastahili kuwa na utulivu na maisha ya amani bila kujali wewe ni nani, ili tuweze kuendelea kiuchumi, TATIZO la rwanda wanafikiri wanaostahili kuwa na amani na uchumi ulio bora ni wao tu, kwa hiyo wapo tayari kuvamia, kuua, kupora raia wa nchi nyingine yoyote ilimradi tu wasiwe watusi wenzao, hili halikubaliki UN wameliona na tanazinia tumeliona pia TUNAPIGANIA MAISHA YA AMANI ENEO LA MAZIWA MAKUU.

Yakwetu hapa Tanzania kama vile Janga la madawa ya kulevya ambapo vijana wengi wanateketea hatutakuwa na taifa la kesho, wakina mama na watoto, vijana na wazee kuteketea kwa kukosa huduma za afya na elimu isiyofaa.

Tunawauwaji wa mapadri kule zanzibar, wauwaji wa shekhe kule zanzibar, wamwagia tindikali yaani mashehe zanzibar na Arusha pia kubenea na mwenzake, watesaji wa akina ulimboka na kibanda, wachomaji wa makanisa na walipuaji wa mabomu.

Hiyo huruma ya kuacha kushughulika na matatizo yako nakuruka mipaka unaipata wapi? je amani unayoitafuta kwa wakongomani na kwa wanyarwanda tunayo hapa kwetu? naomba ufafanuzi.
 
Yeyote anayemtetea KAGAME ni mwendawazimu. Niko pamoja na Manyerere, akileta za kuleta APIGWE tu huyu Kagame.
Na atapigwa tu,nasubiri ilo jeshi lake lililopo mpakani liue Jwtz DRC..
 
Unasubiri ukiwa wapi nyuma ya keyboard au mgahawani? very low. wapiganaji wako milimani huko wewe umekesha hapa ukipost pu.mba, hata maana vita hujuwi.
 
Wana JF, tangu jana kumekuwapo mjadala mkali baada ya kuweka uzi unaojadiliwa hapa. Wapo wanaotukana. Hao wamekosa hekima. Kwenye uzi wangu sikuhamasisha vita, bali nilichosema ni kwamba sisi kama nchi, ni lazima tuwe tayari kujihami. Kujihami huko ni muhimu sana hasa kutokana na ndugu zetu hawa wa Rwanda ambao wana desturi ya kuibua madai ya kutaka 'kutambuliwa' pale wanapokuwa wameishi kwa muda mrefu.
Watu wenye akili watakubaliana nami kwamba haiwezekani chuki ya Kagame itokane na ushauri tu (rudia kusema 'ushauri tu) aliopewa na Rais Kikwete. Matusi, kejeli na songombingo zote alizozitoa Kagame na wafuasi wake, tena wengine wakiwa humu JF, ni ushahidi kwamba Watanzania tunapaswa kukaa mkao wa kujilinda.

Sasa amepeleka bataliani mbili mpakani. Ukweli ni kwamba amezipeleka ili ziweze kuwaokoa M23 ambao ni Wanyarwanda. Hapa hatuhitaji kutambua kuwa tayari Kagame ameamuru majeshi yake yapigane na majeshi ya Tanzania. Vita tayari. Ndiyo maana nasema tufanye kila linalowezekana ili ikiwezekana Kagame tumtoe madarakani. Hiyo ndiyo njia ya kurejesha amani katika eneo hili la Maziwa Makuu.

Kagame akakasirika kwa sababu tunawapiga watu wake (m23), tumekatalia ardhi yetu, tumewafurisha wahamiaji haramu na kubwa zaidi ni la kuona 'mgodi' wake ndani ya DRC unafungwa! Lazima tukomae.
 
JWTZ piga, ua hao wavamizi na mwisho tukutane Kigali kwa ajili ya breakfast.
 
Unasubiri ukiwa wapi nyuma ya keyboard au mgahawani? very low. wapiganaji wako milimani huko wewe umekesha hapa ukipost pu.mba, hata maana vita hujuwi.
Niko fiti kijeshi na sio kimaandishi,nasubiria nipewe watu kama nyie hata kama mlikuwa mnataga mayai yataisha..
 
Manyerere Jackton mkuu wangu naomba ufafanuzi tafadhali kwa dukuduku zangu.

Jana uliandika mwishoni mwa habari yako kama hii hapa chini.

Njia pekee ya kumwondoa Rais Kagame ni hii aliyotusaidia kuiweka, yaani vita. Kuichokoza Tanzania ni njia ya kuelekea ukingoni mwa utawala wake. Amepigana kwa muda mrefu na wasiojua vita. Amejaribu kuitisha Tanzania akidhani atafanikiwa. Kinachotakiwa sasa ni kumwonyesha kazi. Safari iliyoanzia Goma inastahiki ihitimishiwe Kigali. Kama kasahau, arejee kwenye historia ili ajue kilichompata nduli Iddi Amin Dadaa. Buriani Kamanda Khatibu Mshindo.

Leo umekanusha na kuandika hivi post #285

1.
Kwenye uzi wangu sikuhamasisha vita
,

Ulipoandika na kuhanikiza kuanzia Goma mpaka kigali ulimaanisha nini?

post hiyohiyo #285 umeandika
Kujihami huko ni muhimu sana hasa kutokana na ndugu zetu hawa wa Rwanda ambao wana desturi ya kuibua madai ya kutaka 'kutambuliwa' pale wanapokuwa wameishi kwa muda mrefu.

leo asubuhi nimesikiliza BBC idhaa ya kiswahili, kati ya waliotimuliwa ni wazee wa miaka zaid ya 60, na wengine waishi zaidi ya miaka arobaini.

swali towa ushahidi kuthibitisha kwamba wanyarwanda hawa walishawahi kufanya madai hayo hapa tanzania? narudia miaka zaid ya arobaini nilini wamefanya madai hayo? weka hapa utetezi wa hoja yako.

Naukaendelea tena #285
Sasa amepeleka bataliani mbili mpakani. Ukweli ni kwamba amezipeleka ili ziweze kuwaokoa M23 ambao ni Wanyarwanda.

1. Tanzania ilipeleka majeshi yetu kulinda amani au kupigana? kama kupigana ulidhani nini kitokee au watokeo ya kupiga nini hasa kama sio kupigana.

Na hii
Kagame akakasirika kwa sababu tunawapiga watu wake (m23), tumekatalia ardhi yetu, tumewafurisha wahamiaji haramu na kubwa zaidi ni la kuona 'mgodi' wake ndani ya DRC unafungwa! Lazima tukomae

1. kwahiyo wewe ulitaka kupiga tu wao watulie?

2. Mgodi wa Kagame kufungwa huko DRC sisi kama watanzania unatufaidishaje? na je migodi yetu hapa Tanzania inatufaidi kihaki kiasi kwamba tunawapugania wakongo hapa kwetu panaamani? mfano kiwira coal mine unaipiganiaje mwandishi wetu

Baada ya hayo machache nataka kufaham sababu za msingi kabisa kutoka taaluma yako zipi kutufanya kuingia vitani.
 
Last edited by a moderator:
Wakati wa uhai wake mzalendo wa bara hili Kwame Nkrumah alipigania sana umoja miongoni mwa Waafrika kama wa jamii moja na taifa moja.

Aliwakumbusha Waafrika mfano wa Marekani jinsi wanamapinduzi ktk jamii hiyo walivyokuwa na uelewa mkubwa wa haja ya umoja miongoni mwa wananchi.
Hivyo walipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe ili kuulinda umoja wa kisiasa wa taifa lao ambao ulikuwa ukitingishwa na baadhi ya wasiopenda maendeleo (Kagame na washirika wake DRC).

Kutokana na mfano wa Marekani,ni wazi kuwa sisi tuliomo Afrika tunazo rasilimali na uwezo wa kuanzisha jamii ambayo tuna hamu nayo KUIJENGA.
Tunatambua kuwa Afrika ni bara la pili kwa ukubwa duniani.
Utajiri wa asili uliomo Afrka unakadiriwa kuwa unazidi wa bara lingine lolote Ulimwenguni.

Ili Waafrika tunufaike na rasilimali tuliyonayo na uwezo tulionao,tuweze kupata mafanikio ya Amani na maisha bora yatubidi tuunganishe juhudi zetu,rasilimali zetu,ujuzi wetu na shabaha zetu.(Ndiyo maana tupo DRC)
Kwa kulinganisha yaliyotokea Ulaya,ambayo nasi Waafrika yalituathiri vikubwa,yawe fundisho kubwa kwetu sote.
Kwa kukazania umoja wa kitaifa,vita vimepiganwa kwa karne kadhaa; vita ambavyo vilihatarisha amani na kuangamiza maisha ya mamilioni ya watu,wakiwemo Waafrka,na kuleta hali ya wasiwasi.
Sababu ya kutokea hali hiyo ni kwamba,Ulaya huko nyuma haikujenga misingi imara ya umoja wa kisiasa na uelewano.(Tupo DRC kuwasaidia Wananchi wa DRC kulitambua hili)

Tumejifunza kutoka kwenye mataifa yaliyoendelea kwamba maendeleo yanapatikana kwa harakati za kihistoria zenye mfuatano wa mapinduzi ya kisiasa,utamaduni na uchumi.

Nchi zilizopiga hatua katika mapinduzi ya viwanda,huko nyuma hazikukazania vitega uchumi bali zilikazania maendeleo ya kisiasa na utamaduni.
Huko Marekani,Ulaya Magharibi na hivi karibuni Japani na China,usalama wa kisiasa ulihimizwa KWANZA.

Hata jirani Kenya kaisadia Somalia katika utengamano wa kisiasa na leo hii anavuna jitihada zake katika taifa la Somalia,Tanzania nayo iachwe ikitafuta ustawi wa kisiasa kwa washirika wake kwa dhana nzima ya kustawisha shughuli za kiuchumi katika ukanda huu wa Afrika mashariki.

Amani na utengamano wa kisiasa DRC ni muhimu sana kwa Tz,hivyo hatuna budi kushirikiana na Mataifa yanayoitakia kheri DRC.
 
Mifano mingine haingii hata akilini, kenyata kashambuliwa sana na wasomali amekwenda somalia kwaababu ya uhuni wa wasomali.

Tuambie sisi watanzania tumeshambuliwa marangapi hata tuende vitani? jiulizeni kwanza enyi wazalendo feki ambao kutwa kucha kuwavika watanzania wenzenu utusi kwa propaganda chafu za ccm na magogoni.

Kwahiyo ulitaka tukae hadi tupigwe? Hapana dawa ni kupiga kabla hujapigwa.
 
Wakati wa uhai wake mzalendo wa bara hili Kwame Nkrumah alipigania sana umoja miongoni mwa Waafrika kama wa jamii moja na taifa moja.

Aliwakumbusha Waafrika mfano wa Marekani jinsi wanamapinduzi ktk jamii hiyo walivyokuwa na uelewa mkubwa wa haja ya umoja miongoni mwa wananchi.
Hivyo walipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe ili kuulinda umoja wa kisiasa wa taifa lao ambao ulikuwa ukitingishwa na baadhi ya wasiopenda maendeleo (Kagame na washirika wake DRC).

Kutokana na mfano wa Marekani,ni wazi kuwa sisi tuliomo Afrika tunazo rasilimali na uwezo wa kuanzisha jamii ambayo tuna hamu nayo KUIJENGA.
Tunatambua kuwa Afrika ni bara la pili kwa ukubwa duniani.
Utajiri wa asili uliomo Afrka unakadiriwa kuwa unazidi wa bara lingine lolote Ulimwenguni.

Ili Waafrika tunufaike na rasilimali tuliyonayo na uwezo tulionao,tuweze kupata mafanikio ya Amani na maisha bora yatubidi tuunganishe juhudi zetu,rasilimali zetu,ujuzi wetu na shabaha zetu.(Ndiyo maana tupo DRC)
Kwa kulinganisha yaliyotokea Ulaya,ambayo nasi Waafrika yalituathiri vikubwa,yawe fundisho kubwa kwetu sote.
Kwa kukazania umoja wa kitaifa,vita vimepiganwa kwa karne kadhaa; vita ambavyo vilihatarisha amani na kuangamiza maisha ya mamilioni ya watu,wakiwemo Waafrka,na kuleta hali ya wasiwasi.
Sababu ya kutokea hali hiyo ni kwamba,Ulaya huko nyuma haikujenga misingi imara ya umoja wa kisiasa na uelewano.(Tupo DRC kuwasaidia Wananchi wa DRC kulitambua hili)

Tumejifunza kutoka kwenye mataifa yaliyoendelea kwamba maendeleo yanapatikana kwa harakati za kihistoria zenye mfuatano wa mapinduzi ya kisiasa,utamaduni na uchumi.

Nchi zilizopiga hatua katika mapinduzi ya viwanda,huko nyuma hazikukazania vitega uchumi bali zilikazania maendeleo ya kisiasa na utamaduni.
Huko Marekani,Ulaya Magharibi na hivi karibuni Japani na China,usalama wa kisiasa ulihimizwa KWANZA.

Hata jirani Kenya kaisadia Somalia katika utengamano wa kisiasa na leo hii anavuna jitihada zake katika taifa la Somalia,Tanzania nayo iachwe ikitafuta ustawi wa kisiasa kwa washirika wake kwa dhana nzima ya kustawisha shughuli za kiuchumi katika ukanda huu wa Afrika mashariki.

Amani na utengamano wa kisiasa DRC ni muhimu sana kwa Tz,hivyo hatuna budi kushirikiana na Mataifa yanayoitakia kheri DRC.

Nitakujibu kifupi tu, mwalimu JK Nyerere aliweza kupambana na aduwi zake si tu kwa kupeleka wanajeshi kule bali alitoa hifadhi kwa waathilika, wengi walikaa hapa nyumbani na kuendeleza harakati vizuri waliporudi makwao wanatukumbuka watanzania kwa wema mpaka leo msumbiji, Angola, SA Zimbabwe Nk.

Mh kikwete hawezi hata siku moja kufanana na ulichokiandika hapo juu, sera na msimamo wake wa fukuza fukuza, ubaguzi na fitina kwa majirani zake hasa kwenye jukwaa la kimataifa ndiyo imetufikisha hapa tulipo. Unategemea hatakama Kagame ataangushwa hawa aliowafukuza kama mbwa watahitaji ushirikiano naye? wameondoka na kumbukumbu gani ya uwema wetu watanzania ua ukatili wetu wanzania?

Mwalimu Alikuwa mwerevu, na hata baada ya kupigana na Idd Amin, bado hakuwafukuza waganda, Pamoja na kwamba hajawahi kuwa na uhusiano mzuri na Kenyatta hakuwahi wafukuza wakenya. Kwasbabu alifahamu amani ni tunda la haki na upendo ambao mh kikwete hana.

Tutaweza kuungana kama tunaviongozi wenye vision na malengo yakweli kufikia umoja wa faida kwa majirani wote.
 
Manyerere Jackton mkuu wangu naomba ufafanuzi tafadhali kwa dukuduku zangu.

Jana uliandika mwishoni mwa habari yako kama hii hapa chini.

Leo umekanusha na kuandika hivi post #285

1. ,

Ulipoandika na kuhanikiza kuanzia Goma mpaka kigali ulimaanisha nini?

post hiyohiyo #285 umeandika

leo asubuhi nimesikiliza BBC idhaa ya kiswahili, kati ya waliotimuliwa ni wazee wa miaka zaid ya 60, na wengine waishi zaidi ya miaka arobaini.

swali towa ushahidi kuthibitisha kwamba wanyarwanda hawa walishawahi kufanya madai hayo hapa tanzania? narudia miaka zaid ya arobaini nilini wamefanya madai hayo? weka hapa utetezi wa hoja yako.

Naukaendelea tena #285

1. Tanzania ilipeleka majeshi yetu kulinda amani au kupigana? kama kupigana ulidhani nini kitokee au watokeo ya kupiga nini hasa kama sio kupigana.

Na hii

1. kwahiyo wewe ulitaka kupiga tu wao watulie?

2. Mgodi wa Kagame kufungwa huko DRC sisi kama watanzania unatufaidishaje? na je migodi yetu hapa Tanzania inatufaidi kihaki kiasi kwamba tunawapugania wakongo hapa kwetu panaamani? mfano kiwira coal mine unaipiganiaje mwandishi wetu

Baada ya hayo machache nataka kufaham sababu za msingi kabisa kutoka taaluma yako zipi kutufanya kuingia vitani.

Ndugu yangu Balali, salaam. Nashukuru kwa hoja zako zenye mashiko. Umekuwa tofauti na wale mabingwa wa kutukana!

Hoja ya kwanza, ni kweli kama ulivyonukuu hapo juu. Ukisoma sentensi hiyo utaona nasema "Njia pekee ya kumwondoa Rais Kagame ni hii aliyotusaidia kuiweka, yaani vita". Hapa utaona kuwa si sisi tulioanzisha vita, bali ni Kagame kupitia M23. Kwanza kubali kwamba M23 ni kundi la Kagame. Ukilikubali hilo, hutapata shida ya ninachokisema. Kwa hiyo sisi si waasisi wa hii vita, isipokuwa Kagame mwenyewe kupitia M23.

Pili, Madai kwamba kuna wazee wa miaka 60 wengine wakiwa wameishi hapa nchini miaka 40, kwa hiyo si watu hatari, huko ni kujidanganya. Kama hawajawahi kudai, basi ujue huu ndiyo mwanzo wa kudai. tukiwaacha hivi hivi, wakimaliza DRC wataingia Ngara na Karagwe. Kwa hiyo hapa nahamasisha kuchukua hatua za tahadhari ili yasitufike yaliyowafika wenzetu wa Mashariki mwa DRC.

Tatu, ukidhani tumeendea DRC kulinda amani utakuwa unajidanganya. Angalia chapter 7 tunayoitumia kule katika kuwapoka silaha hao waasi. kama lingekuwa ni suala la kulinda tu, vifaru na madege yote ya UN ya nini? KUmbuka, chapter ya DRC ni tofauti na ile ya Darfur ambayo inasababisha upigwe bila kujibu. Kwa hiyo makamanda na wapiganaji wetu wako vitani. Vitani na nani? Vitani na majeshi ya Rwanda lililojivika ngozi ya M23.

Nne, kuna sababu nyingi za kuingia vitani. Kumbuka maneno ya waasisi wetu kama kina Kwame Nkrumah na Mwalimu Nyerere ya kwamba "Tanzania au Ghana haitakuwa huru hadi hapo kila nchi katika Afrika itakapokuwa huru". Huo ndiyo msimamo. Bila kuwa na amani ya kudumu hapo DRC, huku kwetu maendeleo yatakuwa ndoto tu.

tano, kama tunawalaani wazungu kupora madini yetu, iwe hivyo hivyo kwa sisi kuwalaani wazungu weusi -kina Kagame-kupora madini katika nchi nyingine ya Waafrika. Heri sisi tunaoambuliwa asilimia nne ya mrabaha, kuliko DRC ambao wanaambuliwa kubakwa, kuuawa na kudhalilishwa ndani ya nchi yao.

Ndugu yangu Balali, nadhani kwa hapo tunaelewana kidogo.
 
Kwahiyo ulitaka tukae hadi tupigwe? Hapana dawa ni kupiga kabla hujapigwa.

Upigwe kwasababu zipi? orodhesha sababu za wantanzania kupigwa na wanyarwanda hapa. Tena rejea kauli ya waziri wao alisema watanzania ni jirani wa kweli na ni ndugu zao, na kwa wale waliokigali wasiwenawasisi wala mashaka waendelee na shughuli zao.

Nyinyi ndiyo wazushi wa mambo ya kitoto kati ya mh kikwete na kagama mipasho yao ndiyo itughalimu watanzania?
 
Nina wasiwasi na uraia wako.
Pili sisi huwa hatuogopi kuingia gharama,
tumekomboa kote kuanzia Afrika Kusini hadi Uganda na bado....
ndivyo tulivyo, na tulizaliwa kwa ajili hiyo.

Mwalimu aliwahi kusema kuwa
Tanzania itakuwa huru pale ambapo Mataifa yote ya Afrika yatakapokuwa huru.
Sasa nami nasema Tanzania itakuwa huru pale Kagame atakapoondoka Kongo,

Hatujali mapovu mnayotoa ninyi vibaraka wake....tunapiga tu...na tutapiga...hakuna namna. Tumeshawafukuza kwetu na mkiendeleza ngebe tutawapiga.

Mkuu, punguza mkwara. Utafanya watu waihame nchi! Lakini huu ndiyo uzalendo tunaoutaka. Hatuwezi kuchezewa na Kagame kisha tukae kimya. Anatumia vyombo vyote kutukana Watanzania. Nimepata kusema hata kama Rais wetu hatumpendi, hiyo haihalalishi kubariki matusi dhidi yake. Tuungane kulinda, siyo heshima ya Kikwete, bali Tanzania na Watanzania wote.
 
Ndugu yangu Balali, salaam. Nashukuru kwa hoja zako zenye mashiko. Umekuwa tofauti na wale mabingwa wa kutukana!

Hoja ya kwanza, ni kweli kama ulivyonukuu hapo juu. Ukisoma sentensi hiyo utaona nasema "Njia pekee ya kumwondoa Rais Kagame ni hii aliyotusaidia kuiweka, yaani vita". Hapa utaona kuwa si sisi tulioanzisha vita, bali ni Kagame kupitia M23. Kwanza kubali kwamba M23 ni kundi la Kagame. Ukilikubali hilo, hutapata shida ya ninachokisema. Kwa hiyo sisi si waasisi wa hii vita, isipokuwa Kagame mwenyewe kupitia M23.

Pili, Madai kwamba kuna wazee wa miaka 60 wengine wakiwa wameishi hapa nchini miaka 40, kwa hiyo si watu hatari, huko ni kujidanganya. Kama hawajawahi kudai, basi ujue huu ndiyo mwanzo wa kudai. tukiwaacha hivi hivi, wakimaliza DRC wataingia Ngara na Karagwe. Kwa hiyo hapa nahamasisha kuchukua hatua za tahadhari ili yasitufike yaliyowafika wenzetu wa Mashariki mwa DRC.

Tatu, ukidhani tumeendea DRC kulinda amani utakuwa unajidanganya. Angalia chapter 7 tunayoitumia kule katika kuwapoka silaha hao waasi. kama lingekuwa ni suala la kulinda tu, vifaru na madege yote ya UN ya nini? KUmbuka, chapter ya DRC ni tofauti na ile ya Darfur ambayo inasababisha upigwe bila kujibu. Kwa hiyo makamanda na wapiganaji wetu wako vitani. Vitani na nani? Vitani na majeshi ya Rwanda lililojivika ngozi ya M23.

Nne, kuna sababu nyingi za kuingia vitani. Kumbuka maneno ya waasisi wetu kama kina Kwame Nkrumah na Mwalimu Nyerere ya kwamba "Tanzania au Ghana haitakuwa huru hadi hapo kila nchi katika Afrika itakapokuwa huru". Huo ndiyo msimamo. Bila kuwa na amani ya kudumu hapo DRC, huku kwetu maendeleo yatakuwa ndoto tu.

tano, kama tunawalaani wazungu kupora madini yetu, iwe hivyo hivyo kwa sisi kuwalaani wazungu weusi -kina Kagame-kupora madini katika nchi nyingine ya Waafrika. Heri sisi tunaoambuliwa asilimia nne ya mrabaha, kuliko DRC ambao wanaambuliwa kubakwa, kuuawa na kudhalilishwa ndani ya nchi yao.

Ndugu yangu Balali, nadhani kwa hapo tunaelewana kidogo.

Sawa kiongozi naomba tutembee pamaja katika majibu yako.

Kwahiyo kauli yako kwamba hukuhamasisha vita umeikana kwamba ni ya uwongo? Unawezaje kusema kuanzia Goma hadi kigali. Tuambie hapa Tanzania tuna mkowa unaitwa GOMA? kama hatuna watanzania kuanzia goma drc hadi Kigali ruanda sio uchochezi na kuhamasisha vita? maslahi ya kisiasa kwa watu binafsi siyo Taifa.

Nataka ufaham fika kwamba M23 anapigana Kongo drc, na Ufaham kwamba baadhi yao nikutoka majeshi ya kabila yaani waasi. wameasi baada ya kuona demosia inafinywangwa na wengine kutoka makundi na sababu mbalmbali, lakini sinasababu kujadili zaidi ya wakongomani, labda utueleze ya Kabila, M23 na watanzania yanauhusianogani? Nakuuliza hivyo kwasababu moja tu. Ndugu yangu mbona hapa kwetu tunahao M23 ambao wanatesa watanzania Kibanda, Ulimboka na wanachinja watu Usa River, wanalipuwa mabomu, wanauwa mapadri na mashekhe na kumwagia wengine tindikali. Wasiwai wangu kwako Manyerere, umeinua karamu yako kuchochea vita kwa jiran hii vita yetu hujaiona? umechukuwa hatuagani hasa kuanzia hapa nyumbani? Je na kwa wauza dawa za kulevya amabao wanateteketza Taifa lakesho? Huruma kwa wakongomani inatoka wapi? Nini kimekusukuma ukaacha uzalendo kwa watanzania ukauvaa ule wa wakongomani?

Nitaendelea namba 2, 3, 4, na Tano naomba maelezo.
 
Mkuu, punguza mkwara. Utafanya watu waihame nchi! Lakini huu ndiyo uzalendo tunaoutaka. Hatuwezi kuchezewa na Kagame kisha tukae kimya. Anatumia vyombo vyote kutukana Watanzania. Nimepata kusema hata kama Rais wetu hatumpendi, hiyo haihalalishi kubariki matusi dhidi yake. Tuungane kulinda, siyo heshima ya Kikwete, bali Tanzania na Watanzania wote.

Pamoja sana mkuu. Nimefanya kusudi kumjibu huyu Balali anayejivika utanzania halafu anashindwa kuwaza na kuandika kama Mtanzania.
 
Last edited by a moderator:
Nina wasiwasi na uraia wako.
Pili sisi huwa hatuogopi kuingia gharama,
tumekomboa kote kuanzia Afrika Kusini hadi Uganda na bado....
ndivyo tulivyo, na tulizaliwa kwa ajili hiyo.

Mwalimu aliwahi kusema kuwa
Tanzania itakuwa huru pale ambapo Mataifa yote ya Afrika yatakapokuwa huru.
Sasa nami nasema Tanzania itakuwa huru pale Kagame atakapoondoka Kongo,

Hatujali mapovu mnayotoa ninyi vibaraka wake....tunapiga tu...na tutapiga...hakuna namna. Tumeshawafukuza kwetu na mkiendeleza ngebe tutawapiga.

Ukisikia unapoteza mwelekeo ndio hapa unapokosa hekima na welevu na kuvaa miwani ya mbao kushabikia usichokifahamu. tena umekuwa mjinga kuungana nawale wanaovuwa wenzao uraia wakidhani wao ndiyo wazalendo halisi kumbe wajinga wakutupwa. Huwezi kuwa na mashaka na uraia wangu ninapo hoji mambo ya msingi.

Uzalendo wako upo kongo lakini huna huruma wala wasiwasi na wabosi wa dawa za kulevya kwako Tanzania bora iteketee ila DRC ipate amani unajiona upo sawa kichwani?

Uzalendo wako upo kongo lakini huna huruma wala wasiwasi na wanaotesa na kuuwa watanzania waziwazi umeihoji serikali kudhihilisha unaumwa na kwamba hupendi watanzania waendelee kuteseka na kuwawa ovyo? kwako Tanzania bora iteketee ila DRC ipate amani na unajitamba eti ni raia wa nchi hii kiposi mkubwa wewe wa akili.

Uzalendo wako upo kongo lakini huna huruma wala wasiwasi na watanzanzania wanaopoteza maisha kila siku kwa kukosa matibabu na wanakufa wengi kwelikweli lakin kwako Tanzania bora iteketee ila DRC ipate amani

Uzalendo wako upo kongo lakini huna huruma wala wasiwasi na Tanzania ya kesho, watoto wanafeli mpaka kufikia 90% kwako Tanzania bora iteketee ila DRC ipate amani. huu ni ujinga ulopitiliza.

hebu chungulia uraia wako na wangu uone nani mzalendo wa kweli

Mpaka sasa hakuna hata mmoja wenu wachumia tumbo ambaye ametoa sababu fasaha za msingi kuingia vitani.
 
Back
Top Bottom