Hii ni makala ya kichochezi. Manyerere hapa anaonyesha uzalendo uliopotoka (misplaced patriotism).
Tofauti kati ya Tanzania na Rwanda bado kabisa hazijafikia hata chembe ya hatua ya kuzilazimu nchi hizi kwenda vitani. Hivi endapo ingekuwa nchi zikiwa na tofauti kidogo tu kati yao basi inabidi ziende vitani hii dunia ingekalika kweli?
Kama watu wote wangekuwa na mawazo kama ya Manyerere basi saa hizi China ingekuwa inapigana na Japan (mgogoro kuhusu visiwa vya Senkaku au Diaoyu), India ingekuwa inapigana na Pakistan (mgogoro kuhusu eneo la Kashmir), Urusi ingekuwa inapigana na Japan (mgogoro kuhusu visiwa vya Kuril), Kenya ingekuwa inapigana na Uganda (suala la kisiwa cha Migingo), Marekani ingekuwa inapigana na Urusi (suala la Edward Snowden), Ethiopia ingekuwa inapigana na Misri (mgogoro kuhusu maji ya Mto Nile)
.orodha ni ndefu.
Sitashangaa Manyerere, kutokana na uchungu alionao kwa Tanzania, akishauri tupigane na Rwanda na Malawi kwa wakati mmoja. Haya mambo ya vita yamepitwa na wakati. Tulipigana na Uganda zaidi ya miaka 30 iliyopita na athari zake tunaziona hadi leo. Anachofanya Paul Kagame ni kupiga kelele tu na sidhani kama makelele yake ni tishio kwa Tanzania kwa namna yoyote ile.