Waraka wa Tambwe Hizza kwa watanzania

Waraka wa Tambwe Hizza kwa watanzania

Is Tambwe Hiza still alive? if YES! still not machured?
 
ur in a big denial and anger...but it's nat gonna help either,jibu hoja kaka acha vioja
we umejibu hoja kwa style ipi?
Yakupaseni kujibiwa vivi, kwa kua hata hoja zikijibiwa mwisho wa siku hamzioni. Mmejaliwa macho hamtaki kuyatumia, masikio hamtaki kusikia. Mbeleko ipi iwabebe sasa?
 
This country bwana! yaani hata kilaza Tambwe anaweza kutoa waraka na great thinkers wakaujadili? Tambwe hana la kuweza kujadiliwa humu jamvini ni kapuku mzungu wa reli tu hana lolote wala jipya zaidi ya kuchumia tumbo tu.
 
hoja zimejibiwa tayari ila ukiwa ccm lazima uwe kipofu, kama wewe ulivyo huoni
Hoja ya msingi :
1:kwanini chadema ilishidwa vibaya kwa kupata viti 23 kati ya 239 kwenye uchaguzi uliopita?

2:Je kulikuwa na ulazima kwa CHADEMA kukaidi amri ya polisi ya kusubiri sensa ipite?

3:Je, ukaidi wa CHADEMA siyo chanzo cha maafa yaliyotokea na yanayotokea mara kwa mara nchini?

4:Je, ingekuwa sawa kwa jeshi la polisi kuwaachia CHADEMA kufanya shughuli ambayo walikwisha wazuia wasiifanye?

5:Je, polisi ingewaachia kufanya jambo ambalo walikwishawazuia wangekuwa wanatimiza sheria na wajibu wao?

6:Je walichukua hatua yoyote ya kisheria dhidi ya polisi au hawana imani na vyombo vya kisheria kama ambavyo Tundu Lissu anavyoziponda mahakama zetu bila kuheshimu kwamba zilimpa ushindi yeye binafsi katika kesi yake ya uchaguzi aliyofunguliwa na mgombea wa CCM, na zile zilizokipa ushindi chama chake zilizowavua ubunge wana CCM huko Sumbawanga na Igunga.

Hizi ni hoja za msingi sana ambazo hazijajibiwa so far zaidi zaidi naona watau wanatapa tapa tu na kumshambulia mtoa hoja binafsi badala ya hoja zake,ondokeni kwenye denial and anger jibuni hoja
 
Dhiki mbaya sana,Naukianza kula matapishi yako unatakiwa uwe makini mno!Matapishi yake yanamlevya msameheni!
 
Mbona kazini tulikuwa tunaenda kama sensa ilikuwa na umuhimu kiasi hicho

Mleta mada ameacha vitu vingi vya msingi sijui kama ni makusudi au bahati mbaya. Labda atuambie mkutano wa ndani ni nini? Je kuna tofauti gani kati ya ufunguzi wa tawi ambao ni kwa wanachama tu(insiders) na hauchukui zaidi ya saa moja na tulivyo kwenda kanisani jumapili wakati wa sensa?
Je askari waliowatawanya watu wasiofanya fujo wangeamua kiwalinda mwandishi angeuwawa?
Je mwandishi alikuwa sehemu ya the so called waandanaji?
Je Tambwe anasema nini kuhusu picha zinazoonyesha mateso na kifo cha mwandishi? What I mean aliuwawa katika mob accident au alikuwa isoleted kwa mujibu wa picha?
Je senario nzima ilivyo bado anazo nguvu za kuitetea police?
Mwisho kwa nini Tambwe asijiulize ni kwa nini jeshi la police limeshindwa kujitetea kama ilivyo desturi yake.
Maandishi yetu ni kipimo cha uelewa wetu, tutafakari.
 
NA RICHARD TAMBWE HIZA-PICHANI
WIKI hii waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali nchini waliandamana kulaani kuuawa kwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Chanel 10 huko Iringa, kifo cha mwandishi huyu kwa bahati mbaya na kwa mara nyingine tena kimewagawa wananchi katika makundi yanayotofautiana kifikra kuhusu chanzo na hatimaye kufariki kwake.

Wapo wanaoona na kuamini polisi wametumia nguvu kubwa katika kukabiliana na tatizo lililokuwepo, wapo wanaoamini kwamba jeshi la polisi lilikuwa linatimiza wajibu wake na madhara haya makubwa yaliyotokea yanatokana na CHADEMA kuendeleza ghasia katika nchi na kujaribu kuifanya isitawalike kama walivyoahidi baada ya kushindwa vibaya katika uchaguzi mkuu uliopita (walishinda viti 23 kati ya majimbo 239).

Hata hivyo, kabla ya kuingia katika tafakuri pana zaidi zinazotokana na msiba huu sina budi kutoa pole kwa familia ya Mwangosi, waandishi waliokuwa karibu naye katika kufanikisha majukumu yake ya uandishi wa habari, Kituo cha Channel 10 na Watanzania wote kwa ujumla, kwa kuondokewa na mwananchi mwenzetu katika mazingira ambayo wote hatukuyategemea.

Tumeshuhudia wakati taifa likiwa katika simanzi nzito kutokana na msiba huu, wapo wenzetu walioamua kuutumia kama turufu ya kuleta chuki baina ya jeshi la polisi na waandishi na zaidi umma wa Watanzania ambao usalama wao na mali zao unategemea sana uwepo wa jeshi hilo. Kuna mambo mengi ambayo nimekuwa najiuliza na ningependa Watanzania wote tujiulize, hivi ghasia zilizosababisha msiba huu zilisababishwa na nini/nani?

Je kulikuwa na ulazima kwa CHADEMA kukaidi amri ya polisi ya kusubiri sensa ipite? Je, ukaidi wa CHADEMA siyo chanzo cha maafa yaliyotokea na yanayotokea mara kwa mara nchini? Je, ingekuwa sawa kwa jeshi la polisi kuwaachia CHADEMA kufanya shughuli ambayo walikwisha wazuia wasiifanye? Je, polisi ingewaachia kufanya jambo ambalo walikwishawazuia wangekuwa wanatimiza sheria na wajibu wao? Na je, uhalali wa uwepo wa jeshi hilo ungeendelea kuwepo?

Wananchi wote tunapaswa kuheshimu sheria na polisi wana jukumu la kutulazimisha kufuata sheria tunapozikiuka vikiwemo vyama vya siasa, najua sheria ya vyama vya siasa inavipa fursa vyama kufanya maandamano na mikutano baada ya kutoa taarifa polisi, lakini sheria hiyo hiyo inasema vitafanya hivyo endapo tu kama havitapata amri pingamizi kutoka polisi (sheria ya vyama vya siasa 1992 kifungu cha 11).

Tujiulize kulikuwa na ulazima gani kwa CHADEMA ambao mwaka mzima wamekuwa wakiruhusiwa kufanya mikutano na maandamano kulazimisha kufanya mkutano uliosababisha kifo baada ya kupata amri pingamizi? Kama waliona polisi hawakuwafanyia haki je ilikuwa vyema kuandaa mapambano dhidi ya polisi? Jje walichukua hatua yoyote ya kisheria dhidi ya polisi au hawana imani na vyombo vya kisheria kama ambavyo Tundu Lissu anavyoziponda mahakama zetu bila kuheshimu kwamba zilimpa ushindi yeye binafsi katika kesi yake ya uchaguzi aliyofunguliwa na mgombea wa CCM, na zile zilizokipa ushindi chama chake zilizowavua ubunge wana CCM huko Sumbawanga na Igunga.

Naamini ili jeshi la polisi liweze kuendelea kulinda amani ndani ya nchi ni lazima tuliamini na lazima tujue kwamba lipo, likizuia jambo kwa mujibu wa sheria wote tuheshimu vinginevyo litakuwa halina sababu ya kuwepo. Si mara moja au mbili mamlaka za umma na vyombo vya sheria viliamua mambo muhimu katika maendeleo ya taifa, lakini yalipata upinzani hadi pale polisi ilipotumia nguvu kuhakikisha sheria inafuatwa na utekelezaji wake unatimia.

Je, kumfukuza waziri katika hafla ya kulaani mauaji na kumkaribisha mwana-CHADEMA Dk. Lweitama kuhutubia na kuilaani serikali ni sawa? Je, ni sawa kulilaumu jeshi zima la polisi kwa tatizo lililojitokeza sehemu moja ya nchi tena katika kutimiza wajibu wao? Kitendo cha kutowalaani walioanzisha uvunjaji wa sheria uliosababisha ndugu yetu Mwangosi kupoteza maisha katika umri mdogo kinaashiria nini kutoka katika taasisi zetu za habari?

Hapa ndiyo maswali mengine yasiyo na majibu yanapoanza, kwa nini tamko lililotolewa na CHADEMA na lile la wanahabari yanashabihiana. Kwa nini wanahabari hawakuilaumu CHADEMA hata mara moja kwa kutokutii sheria na kuanzisha ghasia zilizosababisha maafa ya ndugu yetu. Nadhani tunahitaji tafakuri pana zaidi. Je wametumwa? Wana hasira? au nao wameanza kushirikishwa katika ajenda za siri dhidi ya serikali na vyombo vyake?

Wote tumesikitishwa na msiba huu sidhani kama ni vyema kuendelea kushambulia jeshi la polisi bali kuangalia nani ameanzisha sokomoko ili awajibishwe kisheria, kama ikibainika aliyeua ni raia wa kawaida sheria ichukue mkondo wake, pia ikibainika muuaji ni askari akiwa katika kutimiza majukumu yake ni vyema taratibu za kijeshi na mahakama zitumike badala ya kuendeleza chuki zisizo na msingi.

Tusijisahau wote tunawahitaji polisi kama ambavyo tulikuwa tunamhitaji ndugu yetu Mwangosi nikiwemo mimi niliyeshirikiana naye katika shughuli mbalimbali. Tusiwe na hasira maana wahenga walisema hasira hasara. Tutafute suluhisho la yanayotokea yasijirudie.

Je kulikuwa na lazima gani jeshi la polisi:
1. kuzuia ufunguzi wa matawi ya chadema?
2. kumpiga na kumuua mwandishi wa habari na si wafuasi wala wa chadema waliokuwa na shughuli za uzinduzi?
3. Kutotoa ulinzi mwanana ili mauaji au vurugu zisitokee yaani njia pekee ni kuzuia ufunguzi?
4. Kufanya kazi pasi kufuata sheria?
5. Kufanya kazi kiukandamizaji?
6. Liwepo kama litafanya kazi za chama cha mapinduzi kama Tambwe anavyodhihirisha hapa pamoja na wengine

Kulikuwa na lazima gani Nchimbi kuwepo katika maandamano ya waandishi ili hali chombo anachokiongoza ndicho kinacholalamikiwa na waandishi,wananchi,jamii ya kitanzania na makundi maalumu mbalimbali.

Je! unataka kutuaminisha kuwa waandishi wa habari wooote ni CHADEMA hata Jane Mihanji?

ndugu yetu Tambwe ukitaka kula haramu chagua............
 
Kwani kipi kilianza kati ya kuomba kibali cha kufanya shughuli za chama ambayo yalikataliwa na kufanyika kwa shughuli hizo za chama zilizokataliwa ambazo yatokanyo na shughuli hiyo ni kifo,ukijibu hapa bila jazba utaweza kuona cdm walikua na nafasi ya kuepusha hiyo shari wakaiabuse na polisi ikabidi watimize wajibu wao kwa kuwalazimisha chadema kutii sheria ambayo ndio kazi yao tunayokatwa kodi kuwalipa kwa kuifanya hiyo kazi,matokeo yake kama unavyojua yakamkuta mtu asiehusika kutokana na ukaidi wa chadema ndio tunarudi palepale kwenye moja ya hoja za msingi za tambwe inayouliza hivi Je kulikuwa na ulazima kwa CHADEMA kukaidi amri ya polisi ya kusubiri sensa ipite?
 
Tambwe Hiza hajui siasa yeye no copy and paste. Alishindwa kuongoza klabu ndogo ya mpira iliyoitwa FURAHA F.C pale tandika sokoni kwa akina Nurdin Hoza. Achana naye kafilisika ndiyo maana alivunja nadhiri yake kuwa akirudi CCM atakuwa amelala na mama yake. Akili yake ipo gizani anashindwa na Nguruwe hampandi mama yake.
 
Huko ndio kumshika mtu kubaya? Yaani hata wewe hujui nani kamuua Mwangosi? Kweli akili ndogo
Hapana ambavyo nataka kufahamu ni hivi:

1:kwanini chadema ilishidwa vibaya kwa kupata viti 23 kati ya 239 kwenye uchaguzi uliopita?

2:Je kulikuwa na ulazima kwa CHADEMA kukaidi amri ya polisi ya kusubiri sensa ipite?

3:Je, ukaidi wa CHADEMA siyo chanzo cha maafa yaliyotokea na yanayotokea mara kwa mara nchini?

4:Je, ingekuwa sawa kwa jeshi la polisi kuwaachia CHADEMA kufanya shughuli ambayo walikwisha wazuia wasiifanye?

5:Je, polisi ingewaachia kufanya jambo ambalo walikwishawazuia wangekuwa wanatimiza sheria na wajibu wao?

6:Je walichukua hatua yoyote ya kisheria dhidi ya polisi au hawana imani na vyombo vya kisheria kama ambavyo Tundu Lissu anavyoziponda mahakama zetu bila kuheshimu kwamba zilimpa ushindi yeye binafsi katika kesi yake ya uchaguzi aliyofunguliwa na mgombea wa CCM, na zile zilizokipa ushindi chama chake zilizowavua ubunge wana CCM huko Sumbawanga na Igunga.
 
tumbo mbele uzalendo nyuma.ama kweli ukstaajabu ya musa utayaona ya filauni.ccm kwa khali hii mnapotea kwakukosa maarifa na visima vyamaarifa mmeviacha nakukumbatia walevi wa madaraka na vyeo kama hao kina tambi.
 
Tambwe Hiza hajui siasa yeye no copy and paste. Alishindwa kuongoza klabu ndogo ya mpira iliyoitwa FURAHA F.C pale tandika sokoni kwa akina Nurdin Hoza. Achana naye kafilisika ndiyo maana alivunja nadhiri yake kuwa akirudi CCM atakuwa amelala na mama yake. Akili yake ipo gizani anashindwa na Nguruwe hampandi mama yake.

hiyo alishajibu kwamba mama yake alikua ameshakufa wakati anatamka hayo hivyo alijua wazi hiyo nadhiri haiwezi kutekelezeka hata kama angependa kuitekeleza
 
NA RICHARD TAMBWE HIZZA

WIKI hii waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali nchini waliandamana kulaani kuuawa kwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Chanel 10 huko Iringa, kifo cha mwandishi huyu kwa bahati mbaya na kwa mara nyingine tena kimewagawa wananchi katika makundi yanayotofautiana kifikra kuhusu chanzo na hatimaye kufariki kwake.

Wapo wanaoona na kuamini polisi wametumia nguvu kubwa katika kukabiliana na tatizo lililokuwepo, wapo wanaoamini kwamba jeshi la polisi lilikuwa linatimiza wajibu wake na madhara haya makubwa yaliyotokea yanatokana na CHADEMA kuendeleza ghasia katika nchi na kujaribu kuifanya isitawalike kama walivyoahidi baada ya kushindwa vibaya katika uchaguzi mkuu uliopita (walishinda viti 23 kati ya majimbo 239).

Hata hivyo, kabla ya kuingia katika tafakuri pana zaidi zinazotokana na msiba huu sina budi kutoa pole kwa familia ya Mwangosi, waandishi waliokuwa karibu naye katika kufanikisha majukumu yake ya uandishi wa habari, Kituo cha Channel 10 na Watanzania wote kwa ujumla, kwa kuondokewa na mwananchi mwenzetu katika mazingira ambayo wote hatukuyategemea.

Tumeshuhudia wakati taifa likiwa katika simanzi nzito kutokana na msiba huu, wapo wenzetu walioamua kuutumia kama turufu ya kuleta chuki baina ya jeshi la polisi na waandishi na zaidi umma wa Watanzania ambao usalama wao na mali zao unategemea sana uwepo wa jeshi hilo. Kuna mambo mengi ambayo nimekuwa najiuliza na ningependa Watanzania wote tujiulize, hivi ghasia zilizosababisha msiba huu zilisababishwa na nini/nani?

Je kulikuwa na ulazima kwa CHADEMA kukaidi amri ya polisi ya kusubiri sensa ipite? Je, ukaidi wa CHADEMA siyo chanzo cha maafa yaliyotokea na yanayotokea mara kwa mara nchini? Je, ingekuwa sawa kwa jeshi la polisi kuwaachia CHADEMA kufanya shughuli ambayo walikwisha wazuia wasiifanye? Je, polisi ingewaachia kufanya jambo ambalo walikwishawazuia wangekuwa wanatimiza sheria na wajibu wao? Na je, uhalali wa uwepo wa jeshi hilo ungeendelea kuwepo?

Wananchi wote tunapaswa kuheshimu sheria na polisi wana jukumu la kutulazimisha kufuata sheria tunapozikiuka vikiwemo vyama vya siasa, najua sheria ya vyama vya siasa inavipa fursa vyama kufanya maandamano na mikutano baada ya kutoa taarifa polisi, lakini sheria hiyo hiyo inasema vitafanya hivyo endapo tu kama havitapata amri pingamizi kutoka polisi (sheria ya vyama vya siasa 1992 kifungu cha 11).

Tujiulize kulikuwa na ulazima gani kwa CHADEMA ambao mwaka mzima wamekuwa wakiruhusiwa kufanya mikutano na maandamano kulazimisha kufanya mkutano uliosababisha kifo baada ya kupata amri pingamizi? Kama waliona polisi hawakuwafanyia haki je ilikuwa vyema kuandaa mapambano dhidi ya polisi? Jje walichukua hatua yoyote ya kisheria dhidi ya polisi au hawana imani na vyombo vya kisheria kama ambavyo Tundu Lissu anavyoziponda mahakama zetu bila kuheshimu kwamba zilimpa ushindi yeye binafsi katika kesi yake ya uchaguzi aliyofunguliwa na mgombea wa CCM, na zile zilizokipa ushindi chama chake zilizowavua ubunge wana CCM huko Sumbawanga na Igunga.

Naamini ili jeshi la polisi liweze kuendelea kulinda amani ndani ya nchi ni lazima tuliamini na lazima tujue kwamba lipo, likizuia jambo kwa mujibu wa sheria wote tuheshimu vinginevyo litakuwa halina sababu ya kuwepo. Si mara moja au mbili mamlaka za umma na vyombo vya sheria viliamua mambo muhimu katika maendeleo ya taifa, lakini yalipata upinzani hadi pale polisi ilipotumia nguvu kuhakikisha sheria inafuatwa na utekelezaji wake unatimia.

Je, kumfukuza waziri katika hafla ya kulaani mauaji na kumkaribisha mwana-CHADEMA Dk. Lweitama kuhutubia na kuilaani serikali ni sawa? Je, ni sawa kulilaumu jeshi zima la polisi kwa tatizo lililojitokeza sehemu moja ya nchi tena katika kutimiza wajibu wao? Kitendo cha kutowalaani walioanzisha uvunjaji wa sheria uliosababisha ndugu yetu Mwangosi kupoteza maisha katika umri mdogo kinaashiria nini kutoka katika taasisi zetu za habari?

Hapa ndiyo maswali mengine yasiyo na majibu yanapoanza, kwa nini tamko lililotolewa na CHADEMA na lile la wanahabari yanashabihiana. Kwa nini wanahabari hawakuilaumu CHADEMA hata mara moja kwa kutokutii sheria na kuanzisha ghasia zilizosababisha maafa ya ndugu yetu. Nadhani tunahitaji tafakuri pana zaidi. Je wametumwa? Wana hasira? au nao wameanza kushirikishwa katika ajenda za siri dhidi ya serikali na vyombo vyake?

Wote tumesikitishwa na msiba huu sidhani kama ni vyema kuendelea kushambulia jeshi la polisi bali kuangalia nani ameanzisha sokomoko ili awajibishwe kisheria, kama ikibainika aliyeua ni raia wa kawaida sheria ichukue mkondo wake, pia ikibainika muuaji ni askari akiwa katika kutimiza majukumu yake ni vyema taratibu za kijeshi na mahakama zitumike badala ya kuendeleza chuki zisizo na msingi.

Tusijisahau wote tunawahitaji polisi kama ambavyo tulikuwa tunamhitaji ndugu yetu Mwangosi nikiwemo mimi niliyeshirikiana naye katika shughuli mbalimbali. Tusiwe na hasira maana wahenga walisema hasira hasara. Tutafute suluhisho la yanayotokea yasijirudie.

Tambwe umechelewa kudanganya, watu walishaamka siku nyingi wewe ndio unakuja na fikra mgando bana!!!!!
 
Rudi studio tambwe, sinema hii imegoma kueleweka na kukubalika.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Studio wataenda hao wasiokubali lakini kwa kutukio la Mwangosi kila kitu wazi; haya aliyosema Tambwe Hiza ni marudio tu kwa mwenye akili timamu hili lipo wazi na halina majadiliano!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Hiki Kituko bado Kipo!! Poor Him!! Hana Jipya!! Wakasaidiane na Makamba Kule Tegeta
 
kweli CCM wanayo kazi............ sasa huyu anatumia kichwa kufikili naye ama ndo kaingia leo tokea ughaibuni?Hiza tukushauri tu,rudi ulikokuwa umefungiwa tokea 2010 vinginevyo ako katumbo kako katatumbuliwa usaha
 
Tabwe Gizza, huwezi kurudi kwa staili hii. Tumeshakupoteza ktk medani ya siasa. Rest in peace Tabwe giizza.
 
Back
Top Bottom