Waraka wa Tambwe Hizza kwa watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka wa Tambwe Hizza kwa watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAUMZA, Sep 16, 2012.

 1. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  NA RICHARD TAMBWE HIZZA

  WIKI hii waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali nchini waliandamana kulaani kuuawa kwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Chanel 10 huko Iringa, kifo cha mwandishi huyu kwa bahati mbaya na kwa mara nyingine tena kimewagawa wananchi katika makundi yanayotofautiana kifikra kuhusu chanzo na hatimaye kufariki kwake.

  Wapo wanaoona na kuamini polisi wametumia nguvu kubwa katika kukabiliana na tatizo lililokuwepo, wapo wanaoamini kwamba jeshi la polisi lilikuwa linatimiza wajibu wake na madhara haya makubwa yaliyotokea yanatokana na CHADEMA kuendeleza ghasia katika nchi na kujaribu kuifanya isitawalike kama walivyoahidi baada ya kushindwa vibaya katika uchaguzi mkuu uliopita (walishinda viti 23 kati ya majimbo 239).

  Hata hivyo, kabla ya kuingia katika tafakuri pana zaidi zinazotokana na msiba huu sina budi kutoa pole kwa familia ya Mwangosi, waandishi waliokuwa karibu naye katika kufanikisha majukumu yake ya uandishi wa habari, Kituo cha Channel 10 na Watanzania wote kwa ujumla, kwa kuondokewa na mwananchi mwenzetu katika mazingira ambayo wote hatukuyategemea.

  Tumeshuhudia wakati taifa likiwa katika simanzi nzito kutokana na msiba huu, wapo wenzetu walioamua kuutumia kama turufu ya kuleta chuki baina ya jeshi la polisi na waandishi na zaidi umma wa Watanzania ambao usalama wao na mali zao unategemea sana uwepo wa jeshi hilo. Kuna mambo mengi ambayo nimekuwa najiuliza na ningependa Watanzania wote tujiulize, hivi ghasia zilizosababisha msiba huu zilisababishwa na nini/nani?

  Je kulikuwa na ulazima kwa CHADEMA kukaidi amri ya polisi ya kusubiri sensa ipite? Je, ukaidi wa CHADEMA siyo chanzo cha maafa yaliyotokea na yanayotokea mara kwa mara nchini? Je, ingekuwa sawa kwa jeshi la polisi kuwaachia CHADEMA kufanya shughuli ambayo walikwisha wazuia wasiifanye? Je, polisi ingewaachia kufanya jambo ambalo walikwishawazuia wangekuwa wanatimiza sheria na wajibu wao? Na je, uhalali wa uwepo wa jeshi hilo ungeendelea kuwepo?

  Wananchi wote tunapaswa kuheshimu sheria na polisi wana jukumu la kutulazimisha kufuata sheria tunapozikiuka vikiwemo vyama vya siasa, najua sheria ya vyama vya siasa inavipa fursa vyama kufanya maandamano na mikutano baada ya kutoa taarifa polisi, lakini sheria hiyo hiyo inasema vitafanya hivyo endapo tu kama havitapata amri pingamizi kutoka polisi (sheria ya vyama vya siasa 1992 kifungu cha 11).

  Tujiulize kulikuwa na ulazima gani kwa CHADEMA ambao mwaka mzima wamekuwa wakiruhusiwa kufanya mikutano na maandamano kulazimisha kufanya mkutano uliosababisha kifo baada ya kupata amri pingamizi? Kama waliona polisi hawakuwafanyia haki je ilikuwa vyema kuandaa mapambano dhidi ya polisi? Jje walichukua hatua yoyote ya kisheria dhidi ya polisi au hawana imani na vyombo vya kisheria kama ambavyo Tundu Lissu anavyoziponda mahakama zetu bila kuheshimu kwamba zilimpa ushindi yeye binafsi katika kesi yake ya uchaguzi aliyofunguliwa na mgombea wa CCM, na zile zilizokipa ushindi chama chake zilizowavua ubunge wana CCM huko Sumbawanga na Igunga.

  Naamini ili jeshi la polisi liweze kuendelea kulinda amani ndani ya nchi ni lazima tuliamini na lazima tujue kwamba lipo, likizuia jambo kwa mujibu wa sheria wote tuheshimu vinginevyo litakuwa halina sababu ya kuwepo. Si mara moja au mbili mamlaka za umma na vyombo vya sheria viliamua mambo muhimu katika maendeleo ya taifa, lakini yalipata upinzani hadi pale polisi ilipotumia nguvu kuhakikisha sheria inafuatwa na utekelezaji wake unatimia.

  Je, kumfukuza waziri katika hafla ya kulaani mauaji na kumkaribisha mwana-CHADEMA Dk. Lweitama kuhutubia na kuilaani serikali ni sawa? Je, ni sawa kulilaumu jeshi zima la polisi kwa tatizo lililojitokeza sehemu moja ya nchi tena katika kutimiza wajibu wao? Kitendo cha kutowalaani walioanzisha uvunjaji wa sheria uliosababisha ndugu yetu Mwangosi kupoteza maisha katika umri mdogo kinaashiria nini kutoka katika taasisi zetu za habari?

  Hapa ndiyo maswali mengine yasiyo na majibu yanapoanza, kwa nini tamko lililotolewa na CHADEMA na lile la wanahabari yanashabihiana. Kwa nini wanahabari hawakuilaumu CHADEMA hata mara moja kwa kutokutii sheria na kuanzisha ghasia zilizosababisha maafa ya ndugu yetu. Nadhani tunahitaji tafakuri pana zaidi. Je wametumwa? Wana hasira? au nao wameanza kushirikishwa katika ajenda za siri dhidi ya serikali na vyombo vyake?

  Wote tumesikitishwa na msiba huu sidhani kama ni vyema kuendelea kushambulia jeshi la polisi bali kuangalia nani ameanzisha sokomoko ili awajibishwe kisheria, kama ikibainika aliyeua ni raia wa kawaida sheria ichukue mkondo wake, pia ikibainika muuaji ni askari akiwa katika kutimiza majukumu yake ni vyema taratibu za kijeshi na mahakama zitumike badala ya kuendeleza chuki zisizo na msingi.

  Tusijisahau wote tunawahitaji polisi kama ambavyo tulikuwa tunamhitaji ndugu yetu Mwangosi nikiwemo mimi niliyeshirikiana naye katika shughuli mbalimbali. Tusiwe na hasira maana wahenga walisema hasira hasara. Tutafute suluhisho la yanayotokea yasijirudie.
   
 2. J

  Jembe_Ulaya Senior Member

  #2
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 154
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Waraka umetolewa kisiasa zaidi!
   
 3. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,825
  Trophy Points: 280
  Rudi studio tambwe, sinema hii imegoma kueleweka na kukubalika.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 4. p

  politiki JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  maswali yake Tambwe Hiza yote ni non sense na yamejaa umbumbumbu mkubwa sheria.

  chadema hawakutii sheria hiyo hai justify kuuwawa mtu kwani hili ni kosa minor under civil disobedience act.

  kuhusu majaji na Tundu Lissu kwamba hawafai ushahidi huko wazi kwa uvivu wako umeshindwa kufuatilia idadi
  ya majaji ambao hukumu zao zimekuwa nullified for failure to meet legal standard. majaji wamemsaidia kushinda
  kesi yake, Tundu Lissu hakuwahi kusema kuwa majaji wote hawafai alisema ni wachache ndio mabomu.

  kuhusu kufukuzwa kwa waziri, maandamano yale yalikuwa ni ya waandishi kulaani mauaji ya mwandishi, wauaji hao wametoka kwenye ofisi ya nchimbi sasa anahandamana kulaani nini?? pili waandishi wenyewe wana mamlaka ni nani na yupi azungumze au asizungumze kwenye shughuli yao na siyo kazi yako wewe HIZA kuwachagulia nani aongee kwenye shughuli yao.

  kuhusu kufuata sheria inabidi wewe hiza umuombee nchimbi awakumbushe vijana wake kutii sheria kwani mtu hakuna sheria inayompa mamlaka polisi kuua raia kwa kosa la kuandamana.

  kuhusu waandishi kutowalaumu chadema kwa kutotii sheria that is non sense kwani chadema haikuwahi kuuwa mtu isipokuwa anayetakiwa kuchukua lawama zote ni aliyeua na si mwingine. aliyeua mwandishi mwenzao ni polisi na siyo chadema, waandishi wana akili na busara kuliko wewe unayeangalia mambo kiunazi kwa kufuata vyama vya siasa na wanamjua aliyemuhua ndugu yao ni nani na ndiye wataendelea kumlaumu, nenda kwa DCI umkambushe kuwa awafikishe mahakamanina chadema wamesahau bahati mbaya according to Bongo lala Tambwe Hiza.
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,775
  Likes Received: 4,998
  Trophy Points: 280

  ..he is still debating with himself kama Mwangosi ameuawa na polisi, au ameuawa na raia wa kawaida. hivi kwanini CCM wamepoteza muelekeo namna hii?
   
 6. y

  yaya JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni script mbovu ya sinema ya TZ ambayo sijapata kuona.
  Namshauri producer aachane nayo, haitauzika kamwe!
   
 7. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Kumbe analytical and thinking capacity ya Hizza iko hivi?!
   
 8. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  Tambwe Hiza, with all due respect wewe ni kijana wa vijiweni Temeke, ninakufahamu vizuri.

  Katika suala hili Polisi na waliowatuma wamefanya kitendo kisichokubalika kwa hali yoyote ile, kuua mwandishi wa habari, asiye na silaha, akiwa kazini,huku amezungukwa na Polisi wenyewe, wengine wakiwa wa vyeo vya juu kabisa mkoani Iringa.

  Tatizo hili ni kubwa na lina msingi katika ukosefu wa utekelezaji wa General Police Orders na mafunzo ya vijana na maofisa wa leo.
  kwamba Serikali imejikanyaga sana katika suala hili ni dhahiri.

  Aidha kwa malayman kama sisi , Polisi sasa imekuwa dubwana lisilo na kanuni za uongozi unaoeleweka, na taswira inayotoka sasa ni kwamba, polisi wako juu ya sheria.
  Kwa vyovyote vile, maujai ya kinyama ya Nd Mwangosi hayakubaliki, kwa vile yalikosa sababu na maelezo ya aina yoyote ile.
   
 9. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Tambwe real a realize kuwa umekwisha kisiasa.
   
 10. Munambefu

  Munambefu JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 895
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 60
  Huyo ndiye kiongozi anayetegemewa na CCM kukijenga chama!Anafikiri kwa kutumia tumbo au masaburi kama kawaida yao.Niliwahi kumsikia kwenye mkutano mkubwa wakati akiwa CUF pale temeke akisema "sitarudi CCM labda nimlale mama yangu"na sasa yupo huko,je huyu si punguani?Haraka ameshasahau kwamba CCM ilizindua kampeni huko bububu,hakukuwa na sensa?si Tz?polisi ni wa upande wa bara tu?Njaa mbaya jamani mhurumieni.
   
 11. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kama kosa ni la Chadema kwa nini Mahakamani kapelekwa yule askari aliyelipua bomu na hawakupelekwa Chadema?
   
 12. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Sasa nimeelewa hapo kwenye red kumbe ana laana
   
 13. t

  tenende JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tatizo alikimbia umande!..
   
 14. o

  obwato JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Jamani wana j3 mumsamehe ndugu yetu Tambi Hizo,shibe imeshamlevya kasahau madhila yote ya polisi eti leo anawasifu,walimtwanga sana mabomu na mabosi wake toka akiwa TLP,CUF sasa amehamia kwao anawasifu kwa kutekeleza sheria,mbona hawakupiga mabomu Bububu kwenye lampeni au Mwanza kwenye Fiesta kama kweli ajenda ni sensa?
   
 15. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hoja anayoitengeneza hapa ni mahusiano kati ya CDM kufanya shughuli zilizozuiliwa na Polisi na kutokea kwa kifo. Kwa lugha rahisi, anasema CDM wangetii amri ya Polisi kusingetokea kifo. Naheshimu mawazo haya. Lakini nina hofu kama akili ya mtu kama Tambwe inaweza kumtuma kufikiri kuwa Polisi wali-behave in a right way. U wapi weledi wa Jeshi hili?. Kama kweli Tambwe anadhani hivyo, I am afraid, he is trying to be patriotic to his stomach. Kutokutii amri hakujibiwi kwa kuvunja sheria. Mtu mwenye kufanya hivyo na kutetea wenye kufanya hivyo, ni mjinga tu, hana tofauti na mlevi anayechoma nyumba yake mwenyewe. Ndg, unachoma nyumba yako!
   
 16. o

  obwato JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hivi ndugu 'Tambi Hizi' anafahamu kuwa wakati wanashangilia ubunge wao wa Bububu walioupata kwa kula ambazo hazifikii hata nusu ya kula za diwani wa Temeke kura (3000) tena za kuchakachua mpaka wanandoa wenzao wamelalamika kuchezewa faulo kuna mtoto wa miaka 15 ameuawa kwa risasi? Hapo vipi amri ya sensa ilikuwa inaendelea? Na Chadema hawakurusha kitu kizito? ukiendekeza njaa utu wako huwezi kuuheshimu lazima utaongea utumbo ili kitumbua kisiungue. Hongera Tambi kwa kutuonesha uwezo wako wa kufikiri.
   
 17. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #17
  Sep 17, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  ndio nimafahamu kwanini wanasiasa wetu wanachuja kama wacheza waingipo simba na yanga.Hawana uwezo wa kupredict path wanayochagua.Waliambiwa msiape kwa mbingu wala nchi,yeye kaapa kwa kufuru na mamake. Walisema usivunje daraja kwani utalihitaji kurudia.yeye kachoma.sasa kazi aliyofanya CUF illimsaidia nini?si bor angewasaidia kuondoa udini?

  Makamba alipasua life katk media kuwa uwepo wake tuu CCM inakosa kura.
   
 18. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #18
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Mkuu... Don't even bite your lips... Tambwe mwenyewe haamini hip waraka
  Ccm is out of touch
   
 19. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #19
  Sep 17, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,240
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Daaaah ama kweli, kama vijana wa ccm wenyewe ndio kama huyu basi ni balaa, Laaa ya kutusi mama yake inamtafuna.

  Nilidhani mgonjwa ni Nape tu, kumbe nape ni afadhari kuliko hili dubwana.
   
 20. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #20
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Mbona kazini tulikuwa tunaenda kama sensa ilikuwa na umuhimu kiasi hicho
   
Loading...