Waraka wa Tambwe Hizza kwa watanzania

Waraka wa Tambwe Hizza kwa watanzania

Chadema wanaamini kuwa kwa kushindwa vibaya sana kwenye kura za Watanzania "(walishinda viti 23 kati ya majimbo 239)." hawatoweza kuingia madarakani kwa kura za wengi hata siku moja katika Uhai wa Mbowe na Slaa.

Kinachobaki wanafanya kila hila kuleta fujo ili uongozi uliopo madarakani uonekane mbaya. Ikiwa chadema wanaweza kuwanunuwa Waandishi wa Habari sishangai kuwa chadema wanawanunua wengi tu wenye tamaa.
 
Tambwe kawaandikie warundi wenzako huko kwenu Burundi. Huna la maana kwa vile wewe licha ya kuwa kizabazabina si raia ingawa unajifanya msambaa wewe na Makamba wakati ni warundi.
 
NA RICHARD TAMBWE HIZA-PICHANI Kuna mambo mengi ambayo nimekuwa najiuliza na ningependa Watanzania wote tujiulize hivi ghasia zilizosababisha msiba huu zilisababishwa na nini/nani?

Je kulikuwa na ulazima kwa CHADEMA kukaidi amri ya polisi ya kusubiri sensa ipite?

Je, ukaidi wa CHADEMA siyo chanzo cha maafa yaliyotokea na yanayotokea mara kwa mara nchini? Je, ingekuwa sawa kwa jeshi la polisi kuwaachia CHADEMA kufanya shughuli ambayo walikwisha wazuia wasiifanye?

Je, polisi ingewaachia kufanya jambo ambalo walikwishawazuia wangekuwa wanatimiza sheria na wajibu wao?

Na je, uhalali wa uwepo wa jeshi hilo ungeendelea kuwepo?

Naamini ili jeshi la kuwepo. Si mara moja kulilaumu jeshi zima la polisi kwa tatizo lililojitokeza sehemu moja ya nchi tena katika kutimiza wajibu wao?.

Maswali tu ya utangulizi yanaonyesha mwelekeo wa mawazo ya mwandishi. Maswali ya utangulizi yanahitimisha makala kabla hata ya kujadili alichokusudia kuandika. Huyu si ndiyo mlopokaji mstaafu wa magamba enzi za makamba?
 
Mkuu... Don't even bite your lips... Tambwe mwenyewe haamini hip waraka
Ccm is out of touch

Huyu Tambwe ana upeo gani wa uelewa? Anaishi dunia gani?
CDM ndiyo pekee waliopaswa kusitisha shughuli zao kuipisha sensa? Mbona maeneo mengine nchini kulikuwepo na mikusanyiko ya watu?
Kulikuwa na ulazima gani kumlipua Mwangosi, kwa sababu tu CDM kutotii amri? Na amri hiyo ilikihusu Chadema tu? na wala si vikundi vingine au shughuli nyingine?

Tambwe is nothing, but an idiot!
 
NA RICHARD TAMBWE HIZA-PICHANIWIKI hii waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali nchini waliandamana kulaani kuuawa kwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Chanel 10 huko Iringa, kifo cha mwandishi huyu kwa bahati mbaya na kwa mara nyingine tena kimewagawa wananchi katika makundi yanayotofautiana kifikra kuhusu chanzo na hatimaye kufariki kwake.Wapo wanaoona na kuamini polisi wametumia nguvu kubwa katika kukabiliana na tatizo lililokuwepo, wapo wanaoamini kwamba jeshi la polisi lilikuwa linatimiza wajibu wake na madhara haya makubwa yaliyotokea yanatokana na CHADEMA kuendeleza ghasia katika nchi na kujaribu kuifanya isitawalike kama walivyoahidi baada ya kushindwa vibaya katika uchaguzi mkuu uliopita (walishinda viti 23 kati ya majimbo 239).Hata hivyo, kabla ya kuingia katika tafakuri pana zaidi zinazotokana na msiba huu sina budi kutoa pole kwa familia ya Mwangosi, waandishi waliokuwa karibu naye katika kufanikisha majukumu yake ya uandishi wa habari, Kituo cha Channel 10 na Watanzania wote kwa ujumla, kwa kuondokewa na mwananchi mwenzetu katika mazingira ambayo wote hatukuyategemea.Tumeshuhudia wakati taifa likiwa katika simanzi nzito kutokana na msiba huu, wapo wenzetu walioamua kuutumia kama turufu ya kuleta chuki baina ya jeshi la polisi na waandishi na zaidi umma wa Watanzania ambao usalama wao na mali zao unategemea sana uwepo wa jeshi hilo. Kuna mambo mengi ambayo nimekuwa najiuliza na ningependa Watanzania wote tujiulize, hivi ghasia zilizosababisha msiba huu zilisababishwa na nini/nani?Je kulikuwa na ulazima kwa CHADEMA kukaidi amri ya polisi ya kusubiri sensa ipite? Je, ukaidi wa CHADEMA siyo chanzo cha maafa yaliyotokea na yanayotokea mara kwa mara nchini? Je, ingekuwa sawa kwa jeshi la polisi kuwaachia CHADEMA kufanya shughuli ambayo walikwisha wazuia wasiifanye? Je, polisi ingewaachia kufanya jambo ambalo walikwishawazuia wangekuwa wanatimiza sheria na wajibu wao? Na je, uhalali wa uwepo wa jeshi hilo ungeendelea kuwepo?Wananchi wote tunapaswa kuheshimu sheria na polisi wana jukumu la kutulazimisha kufuata sheria tunapozikiuka vikiwemo vyama vya siasa, najua sheria ya vyama vya siasa inavipa fursa vyama kufanya maandamano na mikutano baada ya kutoa taarifa polisi, lakini sheria hiyo hiyo inasema vitafanya hivyo endapo tu kama havitapata amri pingamizi kutoka polisi (sheria ya vyama vya siasa 1992 kifungu cha 11).Tujiulize kulikuwa na ulazima gani kwa CHADEMA ambao mwaka mzima wamekuwa wakiruhusiwa kufanya mikutano na maandamano kulazimisha kufanya mkutano uliosababisha kifo baada ya kupata amri pingamizi? Kama waliona polisi hawakuwafanyia haki je ilikuwa vyema kuandaa mapambano dhidi ya polisi? Jje walichukua hatua yoyote ya kisheria dhidi ya polisi au hawana imani na vyombo vya kisheria kama ambavyo Tundu Lissu anavyoziponda mahakama zetu bila kuheshimu kwamba zilimpa ushindi yeye binafsi katika kesi yake ya uchaguzi aliyofunguliwa na mgombea wa CCM, na zile zilizokipa ushindi chama chake zilizowavua ubunge wana CCM huko Sumbawanga na Igunga.Naamini ili jeshi la polisi liweze kuendelea kulinda amani ndani ya nchi ni lazima tuliamini na lazima tujue kwamba lipo, likizuia jambo kwa mujibu wa sheria wote tuheshimu vinginevyo litakuwa halina sababu ya kuwepo. Si mara moja au mbili mamlaka za umma na vyombo vya sheria viliamua mambo muhimu katika maendeleo ya taifa, lakini yalipata upinzani hadi pale polisi ilipotumia nguvu kuhakikisha sheria inafuatwa na utekelezaji wake unatimia.Je, kumfukuza waziri katika hafla ya kulaani mauaji na kumkaribisha mwana-CHADEMA Dk. Lweitama kuhutubia na kuilaani serikali ni sawa? Je, ni sawa kulilaumu jeshi zima la polisi kwa tatizo lililojitokeza sehemu moja ya nchi tena katika kutimiza wajibu wao? Kitendo cha kutowalaani walioanzisha uvunjaji wa sheria uliosababisha ndugu yetu Mwangosi kupoteza maisha katika umri mdogo kinaashiria nini kutoka katika taasisi zetu za habari?Hapa ndiyo maswali mengine yasiyo na majibu yanapoanza, kwa nini tamko lililotolewa na CHADEMA na lile la wanahabari yanashabihiana. Kwa nini wanahabari hawakuilaumu CHADEMA hata mara moja kwa kutokutii sheria na kuanzisha ghasia zilizosababisha maafa ya ndugu yetu. Nadhani tunahitaji tafakuri pana zaidi. Je wametumwa? Wana hasira? au nao wameanza kushirikishwa katika ajenda za siri dhidi ya serikali na vyombo vyake?Wote tumesikitishwa na msiba huu sidhani kama ni vyema kuendelea kushambulia jeshi la polisi bali kuangalia nani ameanzisha sokomoko ili awajibishwe kisheria, kama ikibainika aliyeua ni raia wa kawaida sheria ichukue mkondo wake, pia ikibainika muuaji ni askari akiwa katika kutimiza majukumu yake ni vyema taratibu za kijeshi na mahakama zitumike badala ya kuendeleza chuki zisizo na msingi.Tusijisahau wote tunawahitaji polisi kama ambavyo tulikuwa tunamhitaji ndugu yetu Mwangosi nikiwemo mimi niliyeshirikiana naye katika shughuli mbalimbali. Tusiwe na hasira maana wahenga walisema hasira hasara. Tutafute suluhisho la yanayotokea yasijirudie.
je kutotii kwa sheria ilikuwa kwa chama cha siasa kimoja tu ,kwa sababu wakati chadema wanaendelea na ufunguzi wa ofisi matawini yaani vikao vya ndani ccm walikuwa wanafanya chaguzi za viongozi wao kote nchini na walikuwa wanaselebuka kweli na pia walikuwa wanafanya mikutano ya chaguzi ndogo huko bububu wakiwa na vyama vingine je mwandishi hulioni hili usiwe na upendeleo wa mawazo
 
heeee kumbe bado yupo? Anatafuta tena kutajwa na vyombo vya habari
 
Jamaa anaganga njaa hapa, record zinaonyesha kuwa propaganda za huyu bwana mwisho wake ulikuwa pale Makamba alipotemwa ukatibu mkuu. Sasa anasaka impression!
 
mbona upande wa pili hajiulizi ??

hivi kama polisi wangesubiri shughuri ile ifanyike kwa ulinzi wao kisha wawachukulie hatua (kama zipo) nini kingekuwa kibaya ???

Mwangosi alikuwa akifungua tawiiiii ???

Kwa nini Pro. Mwandosya alikemea mauaji yanayo fanywa na polisi naye ni wa Chadema ???

Nchimbi aliitwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari. Yeye aliunda kamati asuri majibu baada mwezi kisha awaite waandishi awape matokeo kule alikwenda kufanya nini wakati kamati yake inaendelea na uchunguzi ??

Chadema wana silaha za kuulia watu ??

Kwa nini Tambe hukemei japo kidogo tu jeshi la polisi kwa kitendo cha kutumia nguvu kubwa mno, na kuua wasio hatia wala silaha unataka tukuelewe vipi ??

KWA MAWAZO YA HIZA NADHANI CCM WALIKUWA SAHIHI KUFUTA KITENGO CHA PROPADANDA. Hiza ndiye aliye sababisha kifutwe anapaswa kujuta mno
 
Chadema wanaamini kuwa kwa kushindwa vibaya sana kwenye kura za Watanzania "(walishinda viti 23 kati ya majimbo 239)." hawatoweza kuingia madarakani kwa kura za wengi hata siku moja katika Uhai wa Mbowe na Slaa.

Kinachobaki wanafanya kila hila kuleta fujo ili uongozi uliopo madarakani uonekane mbaya. Ikiwa chadema wanaweza kuwanunuwa Waandishi wa Habari sishangai kuwa chadema wanawanunua wengi tu wenye tamaa.
kutoka viti 5 hadi 23 achilia mbali mlivyo chakachua lakini hivi 23 vinaongoza nchi kuliko 216 vyenu

jambo la msingi si viti vya bungeni vyenye tija ila mawazo kutetea wanyonge wote pasipo ufisad
i
 
je kutotii kwa sheria ilikuwa kwa chama cha siasa kimoja tu ,kwa sababu wakati chadema wanaendelea na ufunguzi wa ofisi matawini yaani vikao vya ndani ccm walikuwa wanafanya chaguzi za viongozi wao kote nchini na walikuwa wanaselebuka kweli na pia walikuwa wanafanya mikutano ya chaguzi ndogo huko bububu wakiwa na vyama vingine je mwandishi hulioni hili usiwe na upendeleo wa mawazo
 
Du Tambwe yupo kweli dhambi ya usaliti mbaya Tambwe mpaka uwezo wa kufikiri umekwisha. Hajui hata anaandika nn
 
Chadema wanaamini kuwa kwa kushindwa vibaya sana kwenye kura za Watanzania "(walishinda viti 23 kati ya majimbo 239)." hawatoweza kuingia madarakani kwa kura za wengi hata siku moja katika Uhai wa Mbowe na Slaa.

Kinachobaki wanafanya kila hila kuleta fujo ili uongozi uliopo madarakani uonekane mbaya. Ikiwa chadema wanaweza kuwanunuwa Waandishi wa Habari sishangai kuwa chadema wanawanunua wengi tu wenye tamaa.

Wewe acha ushabiki, jadili waraka wa tambwe hiza na sio slaa na mbowe. Upo nje ya bit,behave mkuu ata kama ni ushabiki wewe umepitiliza.
 
Back
Top Bottom