Waraka wa Tambwe Hizza kwa watanzania

Waraka wa Tambwe Hizza kwa watanzania

mbona hana madaraka yeyote mzee,kweli mna ufahamu mdogo sana wa siasa za nchi hii watu wa cdm
mkuu fikiri kabla ya kutenda ulanzi wa madaraka mmelewa nyote ninyi wanachama wa ccm pasipo kujijua ndo maana nikamalizia huko aliko hii inamaana hata wewe ulanzi wa madaraka umekulevya
 
zee limeishiwa sana hili, uropokaj nao siku hiz unaitwa waraka? Mwangosi hakuwah kufanya kaz na dhaifu hata siku moja, alimtumikia muajir wake chanel ten na wananch alowapenda wa Iringas
 
Double standard za polisi wetu ni vigumu kuwatetea kwani haiingii hakilini kuna WAISLAM wanawavamia hadi Makao makuu hata kirungu tu wasimpige mtu na CHADEMA ikifanya mkutano tena wa ndani bila maandamano wanazingirwa na kuuwa Mwandishi wa habari anayeoji kupata kujua kulikoni. Huyu HIZA japo sijawahi kumwona ninawasiwasi na uelewa wake, swali nini alichokifanya MAREHEMU chenye kuhatarisha AMANI hadi kuuawa.
Huyu ni MWANASIASA ambaye ni uchwara, naamini AMESHACHUJA hata CCM hawamhitaji tena.
WARAKA bila research ni KUJIDHALILISHA ni sawa na Ndg Yangu SUMAYE kuwahita Wandishi wa habari na KULEGEA miguu na Mikono kwa kushindwa kuongea kile Watanzania wasichokijua dhidi ya CCM, kwani kwa kusema Chaguzi za CCM bila PESA hakuna kupata UONGOZI ili @ Mtanzania analijua.
 
Hoja ya kuwa CDM walikaidi amri ya Polisi na hivyo kuua ni hoja halifu ambayo haiwezi kuafikiwa na mtu unless ana matatizo ya kufikiri. Tukumbuke ushauri ndege kong'ota alimpa mbayumbayu kuwa aende juu hewani ashuke kwa mwendo wa kasi sana aupigishe mdomo wake kwenye jiwe gumu ili mdomo wake ufanane na wa kong'ota. Mbayumbayu kuangalia hatari iliyokuwewpo kwa uhai wake kama angeiga tu akatekeleza mradi huu aliamua kuachana nao na hadi leo yu salama salmini. Tuaaswa kuwa hata AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZA KWAKO usiwe manasesere (Robot). Hili ni somo tosha kwa aliyeleta mada hii na polisi wake.
 
Nadhani ndugu Tambwe Hiza unatakiwa ujifunze kusoma alama za nyakati. Ndugu Yangu Watanzania wa sasa sio mabwege kama munavyofikiria kwamba unaweza kuwadanganya kama zamani. Hizi habari labda kijijini ambao mwamko bado mdogo watakuelewa.

Nawewe tukuulize swali moja tu
1. Je polisi wangeawaacha CHADEMA waendelee na kufungua tawi lao nani angezurika?
 
Mhhhh huyu kweli Tambwe mana naona anarasimisha uuaji wa polisi kwa Mwangosi. Swali kwake, mtu akikiuka sheria na taratibu astahili kuuwawa? Je, Mwangosi alikuwa anafanya kazi ya chadema? Je, polisi walikuwa wanampiga kwa kuzuia asiandike habari za chadema ama kutimiza wajibu wake kama mwanahabari? Na je, ni kosa kuandika habari za chadema? Mbona Tambwe sikupati hapo mkuu ama ndo unarudia ile tabia uliyofanya pale KARIMJEE kupeleka watoto ukumbini ili kuikomoa chadema (ulivyodhani) alhali ukiwanyima watanzania haki ya msingi? Je, ni nini dham,ira yako kutaka kuwafumba macho wana-Jamvi kujadili kitu ambacho ni dhahiri na kisheria kiko sahihi? Hakika Ukombozi kwa fikra hizi uko-mbaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaali
 
Hoja anayoitengeneza hapa ni mahusiano kati ya CDM kufanya shughuli zilizozuiliwa na Polisi na kutokea kwa kifo. Kwa lugha rahisi, anasema CDM wangetii amri ya Polisi kusingetokea kifo. Naheshimu mawazo haya. Lakini nina hofu kama akili ya mtu kama Tambwe inaweza kumtuma kufikiri kuwa Polisi wali-behave in a right way. U wapi weledi wa Jeshi hili?. Kama kweli Tambwe anadhani hivyo, I am afraid, he is trying to be patriotic to his stomach. Kutokutii amri hakujibiwi kwa kuvunja sheria. Mtu mwenye kufanya hivyo na kutetea wenye kufanya hivyo, ni mjinga tu, hana tofauti na mlevi anayechoma nyumba yake mwenyewe. Ndg, unachoma nyumba yako!

Nimepita kwa haraka, nimeona watu mmeweka hoja za msingi na nzito sana. Naamini hata hawezi kurudi na kutetea hoja yake. Kimsingi swala la sensa halina nguvu na mtu mwenye akili timamu hawezi kujenga hoja hiyo, kwa mfano mmoja tu wa kuzindua kampeni kule Bububu siku hiyo hiyo ya tukio la Iringa. Kama hiyo haitoshi, swala la utii wa sheria au utii wa amri ya polisi pia ni utoto kuliingiza, maana iko wazi kuwa CDM hawakuwa na mkutano wa hadhari, walikuwa wanafungua tawi, jambo ambalo halikuzuiliwa. Hata hivyo baada ya Polisi kuja eneo la tukio wale CDM walisalimu amri, walikaa chini, wakaambiwa watawanyike, wakatawanyika. That is why ukifuatilia picha waliobaki eneo la tukio zaidi ni Polisi na waandishi wa habari. tena waandishi hao wakitaka kujua tu uhalali wa kusambaratisha zoezi hilo la CDM kufungua tawi, wakiomba pia kujua tofauti kati ya mikutano ya ndani na ya nje. Ukisikiliza clips mbali mbali hakuna polisi hata mmoja aliyejaribu kufafanua au kujibu maswali ya wale waandishi wa habari zaidi ya kuwaonyesha ubabe na kuwajibu kwa madharau. SWALI bado linabaki hapa: Kama ni ukaidi wa CDM kwa Polisi, Kwanini Polisi wale walimzunguka Marehemu (Mwandishi wa habari), walimpiga, na kumlipua na bomu, lililosababisha kifo chake ? Hivi Merehemu alikaidi amri gani ? hakutii amri gani ? Hapakuwa na mvutano wowote kwa maneno, wala mabavu kati ya CDM na Police, WHY DID THE POLICE KILL AN INNOCENT PERSON ? Tambwe amekuja hapa kutukumbusha msiba na kutuamsha hasira. Nawaomba sana watu wenye mapenzi mema, mjitahidi kuhimili emotions, achana na ajenda za mtu anayejaribu kupindisha ukweli, Mungu anaona uonevu ule na mimi naamini Mungu pia atatengeneza malipo yanayofaa kwa unyama aliofanyiwa mwandishi yule pale Iringa (R.I.P Mwangosi)
 
Tambwe Hiza,

Sasa ndugu yangu Tambwe si ungeandika waraka wa kada wa CCM kwenda kwa wanachama na mashabiki wa CCM? Maana kuwaandikia watanzania ambao hawatumii magazeti ya udaku kama amani,kiu na ijumaa kama nyenzo za kufikiri na kufanya tafakari watakuona ni kichekesho tu. Sioni ni namna gani watu wanofikiri sawasawa wanaweza kuona maana ya hiyo maada yako kwa namna unavyotaka ionekane. Hapa unaonekana kutaja neno tafakuri, ukiwa unalenga kuwa wewe ni mchambuzi na unataka kuweka maada ambayo ni " critical and balanced" ili hatimaye kuweza kurutubisha bongo zetu bila kujali maslahi binafsi ya chama chako.

Ukitaka kuuandika mada kwa "Watanzania", kwanza vua koti lako la uchama na kuweka propaganda pembeni halafu jimwage kwenye mada. Bila hiyo wenye fikra watakuona poyoyo tu. Ila ulichofanikiwa ni kuandika propaganda kwa wana-CCM na mashabiki wake ila kwa kundi la wafanya tafakuri na wale wengine wanaojuwa mambo yalivyo umefeli mtihani wa litimasi.
 
Huyu naye alipewa fursa ya kukaa jukwaa kuu na kumnadi mgombea wa Chadema.
 
wapo wengi sio huyu pekee, Tatizoni kushusha wastani tunajua watu shule ipo kumbe makapa ndani ya waliosoma
 
aya zake mbili za mwisho zimebeba ujumbe inaonekana hakufurahishwa na jambo lile ila alitumikia siasa ujumbe uko wazi katika majumuisho yake
 
Huyu naye alipewa fursa ya kukaa jukwaa kuu na kumnadi mgombea wa Chadema.
Wewe nakuona umejaa propaganda za kipuuzi sana. Hukumsikia Tambwe akisema, "Naomba mnisamehe?" Kwa mujibu wa mafundisho ya dini yangu, mtu akiomba msamaha anapaswa kusamehewa. Hatuhitaji kuendeleza siasa za chuki, hizo tunawaachia nyie. By the way, nilichokiona Jangwani jana ni kuwa, "Watanzania wameamua kuidai nchi yao."
 
wakati akiandika hayo alikuwa hajui kuwa ccm ina wenyewe "alikuwa anatekeleza maelekezo kutoka ngazi za juu"

sasa amejitambua na ameomba msamaha.

Tumemsamehe Tambwe Hiza.
 
Back
Top Bottom