Waraka wa Shigongo kwa Ze Original Komedi

Kwa kuwa Shigongo kakosea na inatazamwa kama hana maadili hata kushauri basi ZE COMEDY ORIJINO waendelee na tabia hiyo ya kuwacheka watu walioanguka.

Ndiyo ni tabia yao. Ni tabia yao kuanzia EATV walipomsakama Mr Nice, wakaja kwa wengine hata Mpakanjia, Mashaka na hivi karibuni mwanamuziki mgonjwa.

Ze comedy endeleeni kuifundisha jamii kuwa kumcheka aliyeanguka au aliyetaabani kutokana na masahibu yaliyomkuta ni jambo JEMA SANA.

Endeleeni kuinyea mikono mliyopitia kinyesi chote. Msisaze. Ifundisheni jamii hili nalo ni jema.

Ze comedy mdumu Shigongo zii.
 
Kwa kuwa Shigongo kakosea na inatazamwa kama hana maadili hata kushauri basi ZE COMEDY ORIJINO waendelee na tabia hiyo ya kuwacheka watu walioanguka.

Ndiyo ni tabia yao. Ni tabia yao kuanzia EATV walipomsakama Mr Nice, wakaja kwa wengine hata Mpakanjia, Mashaka na hivi karibuni mwanamuziki mgonjwa.

Ze comedy endeleeni kuifundisha jamii kuwa kumcheka aliyeanguka au aliyetaabani kutokana na masahibu yaliyomkuta ni jambo JEMA SANA.

Endeleeni kuinyea mikono mliyopitia kinyesi chote. Msisaze. Ifundisheni jamii hili nalo ni jema.

Ze comedy mdumu Shigongo zii.

Hakuna anaye kataa Shigongo kuwapa ushauri. Ukisoma post vizuri wengi wanauliza kwa nini kaamua kutoa ushauri huo kwenye magazeti? Ni kweli ze komedi siku hizi kiwango kime shuka ila huyo anae wapa ushauri wa maadili wenzie umeona magazeti yake? Magazeti yake mengi huuza kutokana na rumors mbali mbali na kuchafua watu kwenye magazeti. Kinacho ulizwa na wengi kwa ninvyoona ni je jamaa ana moral authority kutoa ushauri aliotoa wakati mwenyewe anauza magazeti kwa kuchafua watu. Lakini nakubaliana na wewe siyo vizuri hawa ze komedi kukashifu watu na kuwa tukana.
 
Wakuu nadhani ni vyema tujifunze kuvumiliana katika jamii.

Haya magazeti ya udaku kama wengine wanavyopenda kuyaita yanasomwa na dada zetu, kaka zetu, mama zetu etc..sasa sioni kwa nini huyu jamaa asulubiwe hapa. After all hata hii serikali yetu ya kifisadi imeyabariki kwa kuyapa kibali.

Nadhani wengi tunayaita ya udaku kwa sababu pengine sisi ni wasomi tunaopenda "researched and objective news". LAKINI vile vile ni vyema tuelewe kwamba kwenye jamii yetu wako wengi ambao hawajasoma na hawawezi kumudi gharama za hayo magazeti ya kisomi. Simply hawana interests na magazeti ya wasomi akina citizens na mwananchi...

Shigongo has his own dark side, lakini hapa tunaongelea biashara ambayo inamuwezesha kuishi. Kama kuna mtu anaona jamaa anaandika article isiyo basi iwekwe hapa na ijadiliwe. Otherwise..ndo jamii huwezi kutegemea raia 40 tukawa na fikira sawa za kupambanua mema na mabaya.

Kwamba anachafua majina ya watu hilo silijui na wala sitaliingilia..Kikubwa ni haya magazeti yake. Udaku upo wa kila aina..sema udaku wa magazeti yake upo kwenye kiswahili kitu ambacho hatujakizoea...(ingawa ukiwa udaku wa kiingereza kama magazeti ya huko ughaibuni watu wanaona sawa.

Otherwise..sitegemei msaidizi wangu wa kazi nyumbani asome daily news..So there must be something for him.
 
Duuh, JF tuna professionals wengi sana, wakiwemo mawakili !!!
 
Last edited by a moderator:
Ndugu zangu, mimi sijali Shigongo ni nani, lakini kusema kweli programme ya Ze Komedi last week niliiona, they just went off the mark.

What was the point Masanja kusema 'na haka ka TV kake (akimaanisha ITV) ni kabovu kabovu', really ITV ni mbovu mbovu? Na kwa nini TBC warushe maneno kama haya dhidi ya kituo kingine? Hivi ina maana TBC hakuna mtu wa ku-edit programu hii kabla haijarushwa? Wakasema Eddie Lunyamila wa Yanga eti choka mbaya, akiwashtaki watasemaje, eti alikuwa anamtegemea mkewe na alipokufa naye kwisha kazi, unaweza kumsimangia mtu kweli kifo cha mkewe?
 
Last edited:
  1. Shigongo huna JIPYA.
  2. Unajifanya umekomaa lakini tayari unataka kuingia vita na mdogo wako Seki, nani ana haja ya kujua kuwa ni YATIMA, inakuhusu nini au itatusaidia nini?
  3. Kama hupendi mambo ya kuanikana wewe unachotaka kukifanya kwa SEKI si ndio huo huo upuuzi unaoupinga.
  4. NIMECHOKA na nyie MATIRI na WEZI wakubwa wa kazi za wasaniii, unasema Mengi kawasaidia sana MAMBO hayo na COMEDY, je wewe umejaribu kufanya utafiti hao wasanii wamemuingizia PESA kiasi gani???? Acheni unyanyasaji jamani kila mtu ana mtaji wake hata kipaji ni MTAJI.
  5. Kuna tuhuma kuwa hata wewe ni MCHAFU SANA na unatumiwa na watu kwa maslahi binafsi, so YOU HAVE NO MORAL AUTHORITY TO POINT YOU FINGURE ...........
  6. HUWEZI KUMTOFAUTISHA SHIGONGO NA MAGAZETI YAKE, naona hii mnajidai kuitumia sana eti walaumiwe wahariri, shigongo mwenyewe ni mwandishi na mhariri pia, direct and indirect.
  7. Huna aibu wewe mpaka ulifikia hatua ya kimuanika Amina Chifupa kwa ugaomvi mliokuwa nao ukauweka hadharani huku ukijua afya yake ilivyo dhambi itakufuata......
  8. Hata nyie ze comedi jamani acheni kuwatusi watu kihivyo japokuwa mnachikiofanya hakitofautiani na magazeti ya shingongo na UTAMU... shigongo umewaanika wasanii wangapi kuhusu UGONJWA wao kama inakuuma na wewe sio sehemu ya gazzeti TUKUSIKIE UKILIKEMEA BASI japo with LIGHT TOUCH.
 
Watu bana ...yaani jamaa anatumia Uyatima wa Seki kumponda? Sasa kama ni yatima wewe Shigongo ulimsaidia angalau sukari?

Mi naona Shigongo unajikomba kwa Mengi endelea kujikomba....
 
7. Hata nyie ze comedi jamani acheni kuwatusi watu kihivyo ...


Hapo ndipo point ilipo, kwamba kumbe mabaya 'aliyonayo' Shigongo hayazuii kuwakosoa Original Comedy !! Basi kwa mwandiko huo uko ukurasa mmoja na Shigongo, jambo ambalo ndo linatakiwa.
 
Shigongo.....Mengi....Seki....!!!

Lakini kwa ujumla Zekomedi wamepoteza dira sasa hivi..Mimi i cant waste

even my microsecond to watch the shit that they vomit! Umaskini mbaya

Jamani...Wanatumiwa hawa vijana just like bloody horses!...Only if they

knew..
 
Nadhani kuna haja ya kuwasaidia watu waelewe aina ya sanaa wanayofanya orijino komedi, kuchekesha kwao kunatokana na maisha halisi ya watu.

Wamefanya hivi walipokuwa EATV na moja ya waathirika wa sanaa yao alikuwa ni Mheshimiwa John Komba alipotaka kulalamika umma ulimjia juu na kumuambia kuwa vijana hawa wanafanya sanaa tu.Hawakumuacha mtu katika mienendo yao tumeshuhudia kuanzia rais, first lady ( kama mnakumbuka huyu alioneshwa mara anasuka kwenye vibanda vya wamasai, mara ananunua mchicha gengeni) waziri mkuu (walimuandama na mavazi yake, mara wakamuonesha anakula kwa mama lishe, na baya zaidi walikufuru kwa kutania sura yake aliyoumbwa na mungu). Listi kwa ukweli ni ndefu na hakuna mtu maarufu ambaye hakuguswa na vijana hawa.

Kwa wanaojua sanaa hili halikuwapa shida sana kwani aina hii ya sanaa si ngeni duniani tena kwenye baadhi ya nchi kama Marekani ni sanaa inayopendwa sana. Na kwa watu kama akina Shigongo hili halikuwa tatizo kabisa tena alikuwa ni wakala wa kuwajengea umaarufu kupitia magazeti yake. Sasa leo kimebadilika nini hadi huyu Shigongo ageuke?

Kuna wingu kubwa limefunika ukweli huu ila kwa wakala huu Shigongo ametaja mambo machache tu kama kwenda ulaya, kuendesha 'HARIA' na mafanikio wanayo wawezesha kuwa VIP kila wanapo kwenda.

Inawezekana haya ndio yaliyomfanya shigongo anune na sio aina ya sanaa wanyofanya?
 
Hapa cha Msingi shigongo anajaribu kuwasaidia hawa madogo wasije dhani kuwa wamefika. bado safari ni ndefu.
 
Pamoja na mapungufu mengi katika waraka huu wa Erick Shigongo, Ze Original Komedi wameanza kupungua umaarufu... Naongezea... Nilikuwa sithubutu kuangalia nikiwa na watoto... Matusi yamezidi...Na vitendo vinavyochochea ushoga... Aaaah Wadau mimi siangalii tena Ze Original Komedi na sisomi magazeti ya Udaku... Tusker Bariiiidi tu kwa kwenda mbele...
 
HAYA YOTE NI MLOLONGO WA MATUMIZI MABAYA YA VYOMBO VYA HABARI...TATIZO HILI LITAIWEKA NCHI YETU MAHALI PABAYA SANA....

ZE COMEDY WANATUMIA VIBAYA TBC1 BADALA YA KUELIMISHA NA KUCHEKESHA JAMII WANATUKANA WATU...SHIGONGO NAYE ANATUMIA VIBAYA MAGAZETI YAKE KWA KURUHUSU WATU WACHAFULIWE NA KUWATIA KASHFA KIBAOO....

HAPA NAONA SHIGONGO IMEMUUMA KUPIGWA DONGO NA WATOTO AMBAO YEYE ANAZUGA KUWAPA USHAURI WA BURE....KWANI WATU AMBAO ALIWACHAFUA YEYE SHIGONGO WAKIMILIKI TV NA REDIO HAJUI IPO SIKU WATAMPA YEYE USHAURI WA BURE??...NDIOOO..WAPO KINA KIMAMBI WANALIA NA SHIGONGO NA MAGAZETI YAKE...

HAYA SIE KINA YAKHE TUSIO NA VYOMBO VYA HABARI ...YETU JF...we dare to talk openly...SHIGONGO ANAJITAZAMA KWENYE KIOO KISAFI ANAHISI NA YEYE NI MSAFI...ILA KWENYE ULIMWENGU HALISI NI MCHAFU ..kama walivyo ZE COMEDY...NDIO...NAO NI WACHAFU ...KAMA KAKA YAO SHIGONGO TU...marangapi wamewageza watu kwenye shoo zao??...na wakati mwingine wamewadhalilisha pia.....

HITIMISHO...shigongo usililie huruma ya jamii..pambana na vijana na usitudanganye kuwa unawashauri wadogo zako...wewe sio mshauri na hata hivyo ze comedy ni vibabu haviitaji kufunzwa mbinu mpya leo.....ZE COMEDY...BITTA NI BITTAH MURRAHH..huyu shigongo wala sio msafi saaana kuwashaurini...kama vipi na nyie mshaurini..ndio..anahitaji ushauri..mlipueni tena maana na yeye anaanda bomu la kumlipua seki next week.
 
Mimi ni mmoja wa wasiosoma magazeti ya udaku, hivyo isingeletwa hapa JF nisingeijua hii. Asante kuileta.
Naomba kumpongeza Eric kwa waraka huo. andiko leke ni andiko lenye busara, na ningemuomba sana Eric atumie busara hizo hizo kuchuja nini kitoke kwenye magazeti yake, na nini kisitoke.
Orijino komedi ni ngoma inayopigwa sana, karibu itapasuka.

Tembelea zaidi Global Publishers - Tanzania Newspapers uweze kuona waraka zake nyingine na kuzifurahia zaidi. Kwa kifupi hana burasa,nionavyo mie!

@Shigongo
Anza kujichunguza wewe ndo unyooshee wengine vidole, vinginevyo unajaza maji kwenye gunia. Wewe mwenyewe umechafua watu kibao na unaelewa hilo. Eti waraka, waraka bongo?! Kwanini kama umewajali hukuwaita na kuongea nao,naamini ingekuwa jambo la busara zaidi.

Kuhusu Seki ni mtoto yatima, so what?! Yes ni yatima na ulete huo waraka wake watu waone hizo hadithi zako zenye sehemu mpaka ya 50 haiishi. Unakumbuka wewe ulipotoka?!..Unafiki umeujaza tu, pia kumbuka 'tenda wema,uende zako' huna haja ya kujiweka juu kwa kusaidia watu. Wewe si ni mlokole, then amini huyo mungu wako anakuongezea maradufu kwa kusaidia watu!. Masikini akipata makalio hulia mbwata kijana.

Halafu watu wangapi wametolewa kuanzia comedy ile ya zamani, wewe ndo kimekutachi sana?


@New comedy-originale comedy
Ni kweli mambo yanabadilika,zamani wakati mnaanza mlikuwa mnavutia sana na watu wa rika lote walikuwa wanawasubiria alhamisi saa 12 jioni kuwaangalia. Kujiingiza kwenye siasa mbovu na vituko vilivyozidi mipaka ndo kunawafanya mshuke kama huyo kaka yenu shigongo anavyodai.

Seki na group yako, kama mnasoma JF na maoni ya wapenzi wa kipindi chenu huko mlipo then angalie mnapoteleza na kujirekebisha na mumwone kaka yenu shigongo kwa ushauri zaidi (sijui atawasaidiaje,zaidi ya kuwaandikia waraka tena kuwa mmemfuata na kuelezea chote,mnafiki).
 
Wasalaam,

Ni maneno mazuri sana, yamejaa hekima na busara, kama wakiyatendea kazi. lakini najua watayapuuza na kuona ni majungu na fitina na wifu, kama ilivyo kawaida yetu wabongo. lakini ukweli unabaki pale pale kwamba yachukuani maneno ya Erick muyatendee kazi. Munaweza kumpauuza Erick sawa. lakini maneno yake yachukueni muyatendee kazi.

Ni kweli wengi tumekuwa tukishangazwa na kikundi hiki kuanza kumkejeri mzee Mengi, na binafsi nimekuwa nikijiuliza maswali hivi kweli sisi watanzania tunanunulika kirahisi namna hii? Hata kama EATV hawakuwatendea haki.

Lakini kumbukeni ile ndio ilikuwa mbeleko yenu ya kuwafikisha hapo mulipo.

Leo hii mmempata Manji tayari mnasahau mazuri ya Mengi na mnathubutu kumkejeri? Ama kweli binadamu hana wema.

Na kama hamjui siku za umaarufu wenu zinahesabika nyinyi wenyewe mnaharibu kundi lenu, eti juzi bila aibu mnasema mtaongoza kuishangilia yanga. ni kweli nyie mnaipenda yanga? au bwana wenu kawaambia mkashangilie mmeshindindwa kukataa?

vijana wenzangu wa origino komedi rudini kwenye ule mstari wa kwanza. nawakumbuka kwa mara ya kwanza mnaanza maonesho yenu pale white sand hotel. kwa sasa mmwbadilika sio nyie pesa zimewalevya.

Kosa lenu kubwa ni kukubali kununuliwa na mmejitafutia maadui kwa makusudi.

Sawa ila acheni kumkejeli mzee Mengi sisi watanzania wenzenu tunamuheshimu, msiposikia hata asipoomba msaada wetu tutawashukia. Mpaka Manji aje kuwasaidia mambo yashakuwa mabaya.

Nyie ni washikaji tunakutana mikocheni, na kwenye viwanja vingine sio vizuri kutengeneza ugomvi na watu
 
Nimeona Shigongo alivyofanya ni sahihi kwani waraka huu japo kuwa umewahusu the comedy lakini naona na jamii kwa ujumla inapata kuelimika kwani ni kweli watanzania wengi huwa wanakawaida ya kulewa mapema na vi-pesa au sifa jambo ambalo limewafikisha wengi hapo walipo hata kufikia leo hii kuchekwa na ze comedy.Hivyo ninaona waraka huu utufikie watanzania wote.
 
Dear all,

I am in London, for a special mission, but have been irked by this debate and I would like to give my contribution without abusing. First of all let me remindf our contributors that 'If all of will decide to use abusive language, this forum won't be the home of great thinkers but the heaven of puppets.

Let's use this forum to debate not to shout or abuse our fellow contributors. Coming to the point, I think the comedy is losing direction just because of a very simple reason-they have never been to any school of arts or journalism, apart from being born naturally entertainers.

In Journalism or ordinary life, "Fairness" is the pillar of everything you do or write. I am not sure if we were born to celebrate the misfortune or the fall of others, but the truth is no one knows what will happen tomorrow except. God.

The Orijinol Comedy celebrated the Mbagala disaster. In America, a tv achor was fired in 2001 three days after September 11, just because he claimed in his comedy program that when Osama attacked US, bush was hiding in the safe caves.

The comedy is a good show that lacks editing and profesional guidance from editors or the producers. Seki has never gone to any serious school of journalism or arts or whatever you might call it, but he is today the producer of this program which at the end of the day is said to be watched by millions.

Shigongo lamented and ushered more praise on Tido Mhando, but one thing he doesn't understand is that 'the man is not what most people think he is'. It sounds interesting or annoying but Tido is part of the problem.

He joined RTD in 1971 as presenter, a fresh form four with lowest division and since then he worked very hard to early 1980s when he resigned and joined an advertising firm in Kenya while at the same time corresponding for BBC swahili division from Nairobi.

In 1991 after his life was threatened by the Moi regime, he was taken by the BBC to Bush House, where he worked for few years before he was appointed the head of Swahili division, reporting to Madam Kary Blackbun and another Somalian journalist.

In 2005, he played a crucial role in shaping the public opinions about JK through his popular opinion poll conducted by the BBC under his cordination. Due to his outstanding work, he was then rewarded the post at TBC after the expiry of his service within the BBC.

Shigongo, a medical officer or nurse from Mwanza region is also a symbol of struggle for young Tanzanians. He worked sometime as a small scale miner before embraking on pharmaceutical business in early 1990s. In 1998 he saw an oppoturnity among Tanzanians and decided to use by launching the gutter press, dwelling mainly in personalities.

Since this is what the majority of Tanzanians wanted to read because it was touching their everyday life, he made his fortune and is still doing well.

Now my message is very simple: Act profesionally, and responsibly. Remember that in life there's ups and downs, and it is very unfair to celebrate the downfall of others or the natural disasters that happen in our society.

These guys are not rich let alone being celebs. When Eric is talking about Magari ya Kifahari, I don't understand him. Toyota Chaser or GX100 0R 110 used from Japan is not a posh car or Porsche. In Bongo, we have given people the power and title they don't even deserve.

Amina Chifupa was groomed by the same gutter press before her downfall was contributed by the press. She wasn't that brilliant. The same goes to Mpakanjia whom today nobody cares where he is.

In Dar, where 80percent of vehicles cruising on the roads are used and reconditioned from Japan and Dubai, we have created non-existing millionaires.

In Dar I have there are not more than 10 Posh cars (Porsche Cayenne four wheels drive 2, Sports Mercedes Benz 4-Masha, Mkono, and Others, Pirrali owned by Tanil Somaiya anyway kwa shingo Upande there are also dozens of Vogues).

The Problem is we tend to say thing without doing a research. Magari ya Kifahari Kwa Komedi? Noway.

Finally naomba wote muwe wastaarabu msije mkashambuliana.
 
Last edited by a moderator:
Nahisi ameamua kuwaandika huo anaoita usia baada ze komedi kuazisha kile kipindi cha uchambuzi wa magazeti ya udaku na mengi ya magazeti wanayoyakandia ni ya Shigongo na kukandia habari za udaku ktk magazeti hayo.

Upande wangu mimi naona ze komedi wanawaelimisha watu na sio kuwacheka kina Lunyamila, Mr Nice na Banza na wengineo, turudi nyuma enzi zao walivyokuwa wana tamba ama kuwika Banza, Lunyamila, Mr nice wamefanya nini ktk jamii zaidi ya kuendekeza uhasherati, matanuzi yasio na lazima kwahiyo basi hii ni fundisho na kwa wengine pia maana hawa wasanii wa nyanja zote huwa wanajisahau kuwa wanapongara wanakuwa kioo cha jamii.

Ze komedi endeleeni kufichuwa wale wote waliochezea shilingi choni ikadumbukia ili waliobaki waone nini kinawatokea nao wakifuata ya wenzao walio chezea shilingi ******. "SAMAKI MKUNJE ANGALI MBICHI...AKIKAUKA ATAMEGUKA..."
 
Jamani sasa hivi lazima tuangalie alama za nyakati. Baada ya kuja hili la Mafisadi PAPA na NYANGUMI tutegemee mambo mengi mno kwa maana wapo watakaokuja kuegemea upande wa Papa na wapo ambao watafanya kuegemea upande wa nyangumi. Sasa sisi kama wananchi lazima tuelewe utaratibu unaoendelea la sivyo tutatumbukia kwa kuchanganywa na watu wachache. Lets get back to the real buzz (Rostam et al vs Mengi) Hawa komedi na huyu Shigongo wote vibaraka na wanatafuta kula vile vile
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom