Waraka wa Shigongo kwa Ze Original Komedi

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,565
836
Wekezeni, acheni kiburi cha umaarufu na fedha

Kwenu wadogo zangu.

Masanja, Joti, Mpoki, Wakuvwanga, McRegan, Seki na Vengu.

Nianze kwa kuwakumbusha msemo wa Kiingereza usemao “You can not be a champ for life, one day you will go off and some else will come” sikumbuki vizuri msemo huu kwa mara ya kwanza ulisemwa na nani lakini ni wa zamani hapa duniani na maana yake haichuji kila siku ni mpya, kwamba huwezi kuwa bingwa milele lazima uondoke bingwa mwingine aje!

Najua mlitarajia kwa jambo mlilonifanyia ningeibuka na kisasi, mimi si mtu wa aina hiyo, mwenzenu Dudubaya aliwahi kupewa saa nzima kwenye kipindi cha Nani ni Nani Channel Ten, akanitukana matusi yote aliyoyafahamu lakini sikulipa kisasi, baadaye alipowekwa ndani akikaribia kufungwa ni mimi niliyemtoa mahabusu! Sikufanya hivyo kwa kutafuta sifa bali kutimiza kile kisemacho Wasamehe waliokukosea, leo hii Godfrey Tumaini ni rafiki yangu mkubwa...

Uamuzi niliouchukua si kupigana nanyi, maana ugomvi wa sisi kwa sisi hautasaidia chochote, bali nimeamua kuwapeni ushauri ili mfahamu kwamba kila enzi ina mabingwa wake, leo hii ninyi ni mabingwa lakini mfahamu kwamba wengine watakuja ninyi mtaondoka hivyo badala ya kuwacheka na kuwatukana watu, ni vizuri mkawekeza.

Enzi zile za Hitler aliyeua Wayahudi milioni sita duniani kote hakuna binadamu aliyewahi kuwaza eti siku moja angekuja kutokea mtu aitwaye Osama Bin Laden autingishe ulimwengu kwa mauaji na kusakwa bila mafanikio! Enzi zile za tajiri John D. Rockerfeller hakuna mwanadamu aliyewahi kufikiri atakuja mtu aitwaye Bill Gates au Warren Buffet na kuwa tajiri namba moja.

Enzi zile za Pele hakuna binadamu aliyewahi kufikiri atakuja kutokea mtu aitwaye Christiano Ronaldo au Messi, enzi zile za Mohamed Ali akiwa bingwa wa Ndondi wa dunia hakuna mtu aliyewahi kufikiri atakuja kutokea mtu aitwaye Mike Tyson na katika enzi za King Majuto, Mzee Small au Jangala aliyetuweka kila siku usiku tumezunguka redio kusikiliza michezo ya kuigiza, hakuna Mtanzania aliyewahi kufikiri kwamba ipo siku mngekuja kutokea ninyi. Kweli kila enzi na watu wake.

Mmekuja na mtapita kama walivyopita wengine wengi waliotangulia kabla yenu, ambao leo hii ukiwatafuta utashangazwa na maisha wanayoishi ingawa waliwahi kutingisha Taifa letu na wengine Dunia, baadhi wanateseka wakisubiri kusaidiwa! Kwenu hivi sasa jua linawaka lakini giza linakuja.

Mifano niliyoitoa ya watu niliowaongelea hapo juu inaonesha kwamba hakuna binadamu anayeweza kubaki bingwa siku zote, lazima aondoke ili kutoa nafasi kwa mabingwa wengine, tutake tusitake ni lazima tuondoke hivyo ni lazima kufanya mambo sahihi wakati huu tukiwa katika ubingwa wetu. Huu ndiyo ujumbe wangu kwenu leo.

Swali linalowasumbua watu wengi duniani na ambalo kila mtu mwenye akili timamu ni lazima ajiulize ni hivi siku nitakayotupwa nje nitafanya nini? Itakuwaje siku nitakayokuwa siwezi kucheza soka? Nitafanya kitu gani siku nitakayokuwa siwezi kuchekesha luningani na watu kunishangilia kila ninakopita? Kama binadamu mwenye akili timamu ambaye umaarufu haukupagawishi ni vizuri kujiuliza maswali haya kwani kila mmoja wetu siku moja atajikuta yupo nje ya mchezo.

Wadogo zangu,
Ilikuwa niwaandikie Waraka huu tangu wiki mbili zilizopita baada ya kunitoa kwenye kipindi chenu cha Orijino Comedi na rafiki yangu mpendwa aliyewahi kuwa mshindani wangu wa Biashara huko nyuma Mashaka Matongo au Abiola! Ingawa hamkututaja majina yetu lakini kila mtu aliyekiona kipindi hicho alielewa mliwalenga nani na nani na nina uhakika aliyetoa wazo hilo ni Sekioni David kwa sababu yeye ndiye aliwahi kuwa rafiki wa karibu sana na Mashaka Matongo enzi hizo wakiigiza pamoja katika kikundi cha MAMBO HAYO, pia akiwa mfadhili wake mkubwa.

Kwa wale ambao hawakubahatika kukiona kipindi hicho nitawasimulia kidogo; kilichotangazwa na vijana hao maarufu hivi sasa nchini Tanzania wakitembelea magari ya kifahari na kufanya kila aina ya starehe wanayoona inafaa ni kumwonyesha Bw. Mashaka Matongo ambaye huko nyuma aliwahi kumiliki magazeti kadhaa Pendwa akiwa amefilisika vibaya! Kazi yake hivi sasa eti ni kunyoa nywele huko Sinza na kuomba misaada kwa watu! Wakanionesha mimi kama mtu aliyefanikiwa ‘sana’ kuliko Mashaka Matongo katika kazi hiyo na kumcheka wakimfanya mjinga.

Inawezekana kwa kunionesha mimi niko juu na mwenzangu akiwa amefilisika mlifikiri ningefurahishwa na kitendo hicho, naomba niwaeleze wazi kwamba mimi si mtu wa aina hiyo, wanaonifahamu wanaelewa na kitendo hicho hakikunifurahisha hata kidogo, sipendi umaarufu wa bei nafuu (Cheap popularity) napenda ninapopewa sifa iwe ni halali na ya kutolea jasho. Mpaka leo ninapowaandikia makala hii binafsi sielewi mwenzangu alijisikiaje baada ya dhihaka hiyo kurushwa na TBC 1 ambayo Mkurugenzi wake ni mtu ninayemheshimu sana katika fani hii, Tido Mhando.

Kilichonituma niandike makala hii ni kuwakumbusha wadogo zangu wa Orijino Komedi kwamba, maisha ni safari ndefu. Kwa kuonekana kwenye luninga kila Alhamisi na Jumapili, kupita huku na kule wakishangiliwa, wasijione wamefika kwenye kilele cha mafanikio na kuanza kucheka wenzao, ninachofahamu mimi na uelewa wangu mdogo juu ya mafanikio ni kwamba safari kwao ndiyo kwanza imeanza.

Safari ya maisha ni ndefu wadogo zangu, hakuna sababu ya mtu kumcheka mwenzake. Mzee mmoja aliwahi kuniambia ni kama safari ya kwenda umbali wa kilometa elfu moja kwa miguu, kila mtu ataondoka kwa staili yake. Mwingine atakimbia mwingine atatembea au kutambaa zote hizo ni safari lakini hakuna mwenye uhakika kwamba atafika mwisho wa safari yake salama kiasi cha kuwacheka wenzake, hiki ndicho ninachotaka kuwaeleza wadogo zangu wa Orijino Komedi.

Ninachojua mimi hakuna anayeweza kukimbia umbali wa kilometa elfu moja bila kupumzika, lazima mahali fulani mbele ya safari atachoka na kuketi chini ya mti ili kuwapisha wengine wapite na pengine huo ndiyo ukawa mwisho wa safari yake huku uliowaacha nyuma wakitembea taratibu wakipita na kukuambia “Mzee tunatangulia” huu ni ukweli.

Inavyoonekana kwa hivi sasa wadogo zangu wa Orijino Komedi mmeanza safari yenu kwa kukimbia kiasi cha kujiona ni wajanja kuliko wanaotembea hata kufikia hatua ya kuwacheka kama mlivyofanya kwa Mashaka Matongo ambaye huko nyuma alimlisha na kumtunza Sekioni! Mmesahau kwamba mbele ya safari ni lazima mahali fulani mtapumzika na waliokuwa wakitambaa na kutembea wakaja na kuwapita mkiwa chini ya mti, nimekwishawaeleza hapo juu kwamba binadamu huwezi kuwa bingwa milele lazima siku moja utoke na wengine waingie, kumbukeni walikuwepo mzee Majuto na Small kabla ninyi hamjaja.

Kibaya zaidi na kinachositikisha ni kwamba mmeanza hata kuwatukana watu waliowasaidia kufika mlipo leo! Hiki ni kitendo cha ukosefu wa shukrani cha kiwango cha juu kabisa ambacho nimewahi kukiona chini ya jua. Kila Mtanzania anafahamu mlipotokea, namna ambavyo mtu kama Reginald Mengi na vyombo vyake vya habari amesaidia kuwafikisha ninyi kwenye mwanga, ambaye hakika hamuwezi kusimama mahali popote duniani kutoa historia yenu mkaacha kutaja jina lake, lakini huyu ndiye amekuwa mtu wa kutukanwa kila siku katika vipindi mnavyofanya! Hili ni jambo la kusikitisha sana.

Najua mnatiwa kiburi na utajiri wa fedha na umaarufu ambao hivi sasa mnao! Mmethibitisha ile kauli kwamba hakuna kitu kigumu duniani kwa mwanadamu kuwa na fedha au mafanikio halafu akabaki yule yule! Fedha na umaarufu ni shetani, huwabadilisha watu na kuwapa tabia ambazo huko nyuma hazikuwahi kuonekana, sitaki kuwahukumu wadogo zangu lakini jambo hili limethibitika kwa matendo mnayoyafanya hivi sasa.

Najua mnatumiwa na watu kutimiza malengo yao, mambo mnayoyafanya si yenu yote, baadhi ni ya kuwafurahisha watu wanaowaweka mjini! Lakini kumbukeni mfano wa Mzee Kijiti aliyesafiri kwenda miji ya mbali akimwacha mke wake nyumbani, akiwa huko ashki ya tendo la ndoa ilimshika na kujikuta akitafuta mwanamke wa kuondoa haja yake.

Akifahamu kuna gonjwa la Ukimwi mzee huyo alilazimika kutafuta mpira wa kujikinga na gonjwa hilo. Kwa mahali alipokuwa ilikuwa kazi kidogo kupata mpira huo, akazunguka huku na kule kwenye vibanda bila mafanikio, mwili wake ukiwaka tamaa ya ngono. Mwisho mhudumu wa nyumba ya wageni aliyofikia alimpa mpira mmoja, akafurahi na kuingia chumbani ambako alifanya shughuli yake mpaka kufikia tamati akauvua mpira na kuutupa sakafuni tena akasikia kinyaa na kujilaumu kwa kitendo alichokifanya kusaliti ndoa yake.
“Ichukue” Akamwambia mwanamke aliyekuwa naye.

“Ichukue wewe” Mwanamke akakataa.
Baadaye wote wawili waliondoka na kuuacha mpira huo sakafuni, sasa wakiwa na akili timamu kondomu haikuwa na umuhimu tena, ilishawasaidia kuwaepusha na Ukimwi basi ilikuwa inatosha, kazi yake ilishakwisha.
Wadogo zangu,

Kwa mfano huu wa Mzee Kijiti naamini mtakuwa mmenielewa vizuri, jiepusheni sana na kutumiwa na watu wenye malengo yao ambao mwisho wa siku yakitimia watawatupa kule kama Kondomu na hawatawajali tena. Mkilijua hili mtafanya mambo mawili, la kwanza ni kuwekeza na la pili ni kujiepusha na matusi kwa watu waliowasaidia kufika mlipo kwani kesho ni lazima mtarudi kwao kuwashika mikono, hivyo ndivyo Mungu anavyofanya kazi.

Jiepusheni na starehe na kulewa umaarufu, jua haliwaki siku zote, kuna mchana na usiku. Muda huu mkiwa juu, ni vizuri kujiuliza giza litakapoingia na mwanga kupotea, au siku tutakapotupwa tutaishi vipi? Anasa hazina mwisho, zipo tu, mlizikuta, mtaziacha na wengine watazikuta na kuziacha hivyo ni vizuri kuwa makini katika kipindi hicho ambacho neema bado ipo, maana mchekaji huwa mchekwaji kesho na mchekeshaji huwa mchekeshwaji kesho kutwa.

Mmekwishanitukana mimi mara nyingi lakini mimi sijali, nimekwishazoea, katika miaka kumi na moja niliyofanya kazi hii ngumu ninao maadui wanaoweza kufanya chochote ili wanichafue, kinachoniuma sana ni kitendo mnachokifanya kwa mzee Mengi ambaye bila yeye TBC1 wasingewaona, kwa umri wake mzee huyu ni sawa na mzazi wenu na mnachokifanya ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu sababu tu mmelipwa!

Inawezekana mkawa hamfahamu kwamba umaarufu wenu unapotezwa na kitendo hiki, Watanzania hawapendi watu wenye maringo na kujisifu tabia ambayo hivi sasa imewagubika ninyi mkiwa mwanzo tu mwa safari ya maisha! Mnakumbuka kilichowapata uwanja wa Taifa siku ile mlipopigwa kwa chupa na makopo ya soda? Hilo linapaswa liwe fundisho ili mjiangalie upya, mimi naamini mnaweza kurejesha hali mliyokuwa nayo zamani kwa kujiepusha na matusi kwa watu waliowasaidia.

Mkiendelea na tabia hii si tu mtachukiwa bali mtailetea TBC1 matatizo makubwa sana ya kulipa watu mabilioni ya fedha jambo ambalo najua kabisa TBC1 hawatakuwa tayari kulifanya, hivyo kuamua kujiepusha nanyi! Hata kama TBC1 ni chombo cha serikali, inaelewa kabisa kuna mahakama na hakuna aliye juu ya sheria, kitendo cha wao kuwaruhusu ninyi kuendelea kutukana watu kwa maneno ya uongo, kitakuja kuwaingiza kwenye matatizo makubwa ambayo hatimaye yatavunja ndoa yenu.

Najua maneno yangu yatawaumiza lakini naomba msikasirike kwani tiba ya ugonjwa siku zote inauma lakini mwisho wa siku inaponyesha! Naomba mnivumilie na myafanyie kazi yale mtakayoona yanafaa, binadamu hatujatimia, tunayo mapungufu mengi na kila siku tunafanya kazi kurekebisha sehemu mbalimbali maishani mwetu, nanyi nawasihi mchukue hatua hiyo. Mtu hahitaji kuwa na elimu kubwa sana kuelewa kitakachowapata kama mkiendelea na mtiririko huu mnaokwenda nao.

Sisi sote ni Watanzania tuacheni kuchekana bali tuwatie moyo waliovunjika na tuwasaidie kusimama walioanguka! Matendo hayo ndiyo yatakuwa akiba yetu mara giza litakapoingia hawa mnaowacheka na kuwatukana leo si ajabu ndiyo watakaowasaidia ikitokea siku moja kigogo anayewafadhili sasa akawa hafanyi kazi na ninyi tena jambo ambalo si ajabu kutokea.

Naomba niseme neno moja natumaini sitamuudhi mtu. Watanzania tuna tatizo ambalo ni lazima tulishughulikie kama kweli tunataka kupata mafanikio ya kweli maishani mwetu, tuna tabia ya kuridhika mapema hata kwa mafanikio kidogo. Hapo mlipo wadogo zangu wa Orijino Komedi tayari mmesharidhika, lakini kumbukeni kufika Uingereza au kuendesha ‘Haria’ peke yake haitoshi, kuna mambo mengi sana ya kufanya, kama kufika nje na kuendesha gari ingekuwa kila kitu basi watu wangekwisha acha kufanya kazi.

Hili ni kosa kubwa sana ambalo sisi Watanzania tunalifanya, mafanikio kidogo tu yanatulewesha na kuanza kutukana watu bila kujua kwamba kuna kesho, hata Orijino Komedi mtakubaliana nami katika hili! Wadogo zangu mmelewa sifa mapema, kila mahali mnapoingia mnataka huduma ya VIP? Kumbukeni wanaojikweza hushuswa bali wanaojishusha hukwezwa! Chapeni kazi wadogo zangu, bado hamjafika popote, mafanikio ni safari ndefu mnahitaji sana watu kuliko mnavyohitaji fedha.

Nimeongea mengi sana wadogo zangu, lakini huu ndiyo Waraka wangu kwenu sisi ni ndugu lazima tuelekezane kwa maneno ya ukweli na si visasi, ni vizuri mkakumbuka mlikotoka badala ya kujisikia mmefika mwisho na kuanza kuwatukana watu waliowasaidia kufika juu! Ni vizuri kuelewa hamtakuwa mabingwa siku zote, pengine mtakapokuwa mnaporomoka hawa mnaowatukana leo watakuwa bado wako juu na mtahitaji msaada wao.

Naomba niishie hapo.

Jipu limepasuka siwezi kuwa adui kwa kusema kile ninachoamini ni ukweli. POLE SANA MASHAKA MATONGO, MANENO YA ORIJINO KOMEDI YASIKUVUNJE MOYO, PAMBANA TU HATIMAYE UTAFIKA JUU, YOTE YAWEZEKANA, IF THEY CAN, YOU CAN!

Wiki ijayo nitamwongelea Sekioni David, yatima aliyesaidiwa na Reginald Mengi ambaye hivi sasa kila kukicha anamtukana mzee huyo sababu leo hii anafadhiliwa na Yusuph Manji.
 
Sasa kama sekioni ni yatima tatizo ni nini ? Sekioni alikuwa anaishi kimara baruti na hakuwahi kulelewa na reginald mengi kama shigongo anavyotaka tuamini
 
Anacho jaribu kusema ni kuwa seki alisaidiwa sana na Mengi tokea mambo hayo ina rushwa ITV mpaka EATV. Sijui kama ni kweli au la. Lakini uki chukulia hypothetically kwamba ni kweli Mengi kamsaidia Seki anacho jaribu kusema ni kuwa Seki wakati ni yatima na ana hitaji msaada ali saidiwa na Mengi.
 
Last edited:
Anacho jaribu kusema ni kuwa seki alisaidiwa sana na Mengi tokea mambo leo ina rushwa ITV mpaka EATV. Sijui kama ni kweli au la. Lakini uki chukulia hypothetically kwamba ni kweli Mengi kamsaidia Seki anacho jaribu kusema ni kuwa Seki wakati ni yatima na ana hitaji msaada ali saidiwa na Mengi.

Hapo kwenye bold ulikusudia Mambo Hayo?

Kama ni Mambo Hayo, ndio kusema kuwa wasanii wote waliokuwa Mambo Hayo walikuwa wakisaidiwa na Mengi?

Ni Mengi anayetaka sifa au ni Shigongo anakuza mambo? Hata siku moja huwezi kumsaidia mtu especially yatima ili aje akupe fadhila baadae. Tenda wema nenda zako, usingoje shukrani.

Shigongo hebu pisha huko, huna moral authority ya kuwaambia kitu hawa watoto kwa sababu na wewe ni mchafu, mnafiki na mharibifu.
 
Hivi huu waraka aliutoa ktk gazeti au ulikufikiaje? km aliutoa ktk gazeti basi amekusudia kufanya hivyo kwa lengo la kujiongezea umaarufu kuwa yeye ni "mzee wa busara", na wasomaji wake wamuone hivyo.
Ameshindwaje kuwakabili wahusika na kuwamwagia "busara" zake?
 
Ametoa kwenye gazeti na kasema pia wiki ijao atatoa waraka kwa Seki. Kama kweli ana nia nzuri si ange watafuta privately awape ujumbe?
 
Bw. Mashaka Matongo ambaye huko nyuma aliwahi kumiliki magazeti kadhaa Pendwa akiwa amefilisika vibaya! Kazi yake hivi sasa eti ni kunyoa nywele huko Sinza na kuomba misaada kwa watu! Wakanionesha mimi kama mtu aliyefanikiwa ‘sana' kuliko Mashaka Matongo katika kazi hiyo na kumcheka wakimfanya mjinga.
Shigongo acha unafiki wewe mlokole.....

Kuna mtu mchafuzi wa watu kama wewe tz? Amina chifupa ulimuandama na kumchafua kama weye msafi sana....hiki kijamaa ukikisikiliza unaweza dhani mt yosefu hapo anauma na kupuliza......
 
I don't want to judge him but sielewi mlokole ata milikije magazeti anayo miliki yeye. There are immoral, they are degrading, they are full of rumors & they live off of others misfortunes. Tatizo wengi hawaishi kama wanavyo hubiri.
 
Sasa kama sekioni ni yatima tatizo ni nini ? Sekioni alikuwa anaishi kimara baruti na hakuwahi kulelewa na reginald mengi kama shigongo anavyotaka tuamini

...,
AMESEMA ATAMUONGELEA,HAJA ANZA NI WIKI IJAYO.HICHO KICHWA CHA HABARI KUVUTIA WASOMAJI.
Subiri akianza amalize uone kilichomo
.My take, ushauri alio toa ni muhimu ingawa amerudiarudia maneno hadi inachosha
 
Wekezeni, acheni kiburi cha umaarufu na fedha

Wekezeni nini? Wapi?

Kwenu wadogo zangu.
Very unprofessional, unaongelea hawa kama professionals au kama watu wa familia yako? Kwa nini kuleta mambo ya "wadogo zangu"? Isn't this a condescending way of lording over them?

Masanja, Joti, Mpoki, Wakuvwanga, McRegan, Seki na Vengu.
Nianze kwa kuwakumbusha msemo wa Kiingereza usemao "You can not be a champ for life, one day you will go off and some else will come" sikumbuki vizuri msemo huu kwa mara ya kwanza ulisemwa na nani lakini ni wa zamani hapa duniani na maana yake haichuji kila siku ni mpya, kwamba huwezi kuwa bingwa milele lazima uondoke bingwa mwingine aje!
Hivi ililazimu kutafuta msemo wa kiingereza usioujua ili kueleza hili jambo? Kiswahili kina misemo mingapi ambayo tunaijua vizuri na ingeweza kutumika vizuri kuliko msemo huu uliouokoteza bila kuujua? Au ndio kujionyesha ujuaji shurti "utie msisitizo" kwa kiingereza kilichopinda?

Najua mlitarajia kwa jambo mlilonifanyia ningeibuka na kisasi,
Jambo gani? Mbona una assume kila mtu anafuatilia na kujua wamekufanyia nini? Hii ni barua ya wazi au barua persoanal? Kama ya wazi mbona unaandika kama kila mtu ni kama yupo vichwani mwa hawa The Original Komedi?

mimi si mtu wa aina hiyo,
Waache watu waseme wewe ni/ au si mtu wa aina gani, wewe mwenyewe utajipamba sana au kujiskosoa sana.

mwenzenu Dudubaya aliwahi kupewa saa nzima kwenye kipindi cha Nani ni Nani Channel Ten, akanitukana matusi yote aliyoyafahamu lakini sikulipa kisasi, baadaye alipowekwa ndani akikaribia kufungwa ni mimi niliyemtoa mahabusu!
Hukulipa kisasi moja kwa moja, lakini ulitaka kulipa kisasi kwa kuja kutamba baadaye kwamba hukulipa kisasi.Mtu ambaye halipi kisasi kweli huwa halipi kisasi, halafu wala hajigambi kwamba halipi kisasi, watu wengine wataona na kusema, usipolipa kisasi moja kwa moja na kujitapa kwamba hujalipa kisasi unakuwa umeshalipa kisasi kwa kujifanya wewe uko above it all, kwamba wewe ni mtu mzuri na mtakatifu zaidi, wanasema wenyewe holier than though.Nothing but a passive aggressive Machiavellian complex.

Sikufanya hivyo kwa kutafuta sifa
Anhaaa, umeshajiwahi mwenyewe.Hili swala la sifa limekujaje? Nani kwakwambia hili? Kuna kisauti kichwani mwako kilikuwa kinakusuta ukajua kuwa umejifanya kutolipiza kisasi kwa kutafuta sifa siyo?

bali kutimiza kile kisemacho Wasamehe waliokukosea, leo hii Godfrey Tumaini ni rafiki yangu mkubwa...
Unapenda kuwaweka watu mfukoni, unajua kwa u Makaveli uliomfanyia atakuwa hana sauti kwako, ndiyo maana umemfanya awe rafiki yako, sasa hivi una remote control.

Uamuzi niliouchukua si kupigana nanyi,
Unapigana kwa kutopigana, kwa kutupa madongo yaliyokuwa disguised kama eminent and constructive criticism.

maana ugomvi wa sisi kwa sisi hautasaidia chochote, bali nimeamua kuwapeni ushauri
Ushauri wewe kama nani?

ili mfahamu kwamba kila enzi ina mabingwa wake, leo hii ninyi ni mabingwa lakini mfahamu kwamba wengine watakuja ninyi mtaondoka hivyo badala ya kuwacheka na kuwatukana watu, ni vizuri mkawekeza.

Enzi zile za Hitler aliyeua Wayahudi milioni sita duniani kote hakuna binadamu aliyewahi kuwaza eti siku moja angekuja kutokea mtu aitwaye Osama Bin Laden autingishe ulimwengu kwa mauaji na kusakwa bila mafanikio!
Apparently he is not well acquinted with the crusades, the hero worship,Islamofascism and the coming of Mahdi.

Enzi zile za tajiri John D. Rockerfeller hakuna mwanadamu aliyewahi kufikiri atakuja mtu aitwaye Bill Gates au Warren Buffet na kuwa tajiri namba moja.
Aparently he is not acquinted with H.G Wells

Enzi zile za Pele hakuna binadamu aliyewahi kufikiri atakuja kutokea mtu aitwaye Christiano Ronaldo au Messi, enzi zile za Mohamed Ali akiwa bingwa wa Ndondi wa dunia hakuna mtu aliyewahi kufikiri atakuja kutokea mtu aitwaye Mike Tyson na katika enzi za King Majuto, Mzee Small au Jangala aliyetuweka kila siku usiku tumezunguka redio kusikiliza michezo ya kuigiza, hakuna Mtanzania aliyewahi kufikiri kwamba ipo siku mngekuja kutokea ninyi. Kweli kila enzi na watu wake.
Anajionyesha asivyo na substance, point yake ni nini? Anakanusha pointi ambayo haijawasilishwa, anajipa ushindi wa chee mwenyewe kwa kujichagulia maswali rahisi ambayo hajaulizwa.

Mmekuja na mtapita kama walivyopita wengine wengi waliotangulia kabla yenu, ambao leo hii ukiwatafuta utashangazwa na maisha wanayoishi ingawa waliwahi kutingisha Taifa letu na wengine Dunia, baadhi wanateseka wakisubiri kusaidiwa! Kwenu hivi sasa jua linawaka lakini giza linakuja.
Nani asiyepita? Jua litapita, ulimwengu utapita, kupita kwenyewe kutapita, sasa unachojaribu kusema hapa ni nini? Una wivu ama? Kila mtu ana uhuru wa kufanya anachotaka, ilimradi havunji sheria, hii inajumuisha uhuru wa kukosea, ndiyo kujifunza, sasa wewe ni nani utake kuwa polisi wa maadili na uchumi wa hawa watu? Una mamlaka gani? Kakupa nani?

Mifano niliyoitoa ya watu niliowaongelea hapo juu inaonesha kwamba hakuna binadamu anayeweza kubaki bingwa siku zote, lazima aondoke ili kutoa nafasi kwa mabingwa wengine, tutake tusitake ni lazima tuondoke hivyo ni lazima kufanya mambo sahihi wakati huu tukiwa katika ubingwa wetu. Huu ndiyo ujumbe wangu kwenu leo.
Sasa unataka wakupishe ukafanye comedy wewe?

Swali linalowasumbua watu wengi duniani na ambalo kila mtu mwenye akili timamu ni lazima ajiulize ni hivi siku nitakayotupwa nje nitafanya nini? Itakuwaje siku nitakayokuwa siwezi kucheza soka? Nitafanya kitu gani siku nitakayokuwa siwezi kuchekesha luningani na watu kunishangilia kila ninakopita? Kama binadamu mwenye akili timamu ambaye umaarufu haukupagawishi ni vizuri kujiuliza maswali haya kwani kila mmoja wetu siku moja atajikuta yupo nje ya mchezo.
Wewe utajuaje mipango ya watu? Utawapangiaje maisha? Kama hawataki kuishi maisha marefu je? Kama wanataka kutumia zote leo je? Mbona tunataka kuleta unafiki wa kujitia tunawajali watu kuliko wanavyojijali wenyewe kumbe shida yetu ni umbea tu na kutaka kuwasimanga watu tu? Kama unawa mind sana kwa nini usikae nao chini mkaongea faragha? Kwa nini unawaanika kwa kila mtu ajue mambo yao? Mbona huna hata sense ya privacy wewe uliyekosa uungwana ukabaki na ila na inda za kujifanya muungwana usiye kisasi? Je, hiki si kisasi? Huku kuwaumbua hadharani si kisasi?

Wadogo zangu,
Kujivika kilemba cha ukoka

Ilikuwa niwaandikie Waraka huu tangu wiki mbili zilizopita baada ya kunitoa kwenye kipindi chenu cha Orijino Comedi
Ahaa, kumbe hii ndiyo sababu, unawaandika kwa sababu wamekuanika na sasa unataka kujifaragua tu, mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu, wewe ushazoea kuwaanika watu kwenye magazeti yako, ukianikwa wewe unaona uchungu.

na rafiki yangu mpendwa aliyewahi kuwa mshindani wangu wa Biashara huko nyuma Mashaka Matongo au Abiola! Ingawa hamkututaja majina yetu lakini kila mtu aliyekiona kipindi hicho alielewa mliwalenga nani na nani na nina uhakika aliyetoa wazo hilo ni Sekioni David kwa sababu yeye ndiye aliwahi kuwa rafiki wa karibu sana na Mashaka Matongo enzi hizo wakiigiza pamoja katika kikundi cha MAMBO HAYO, pia akiwa mfadhili wake mkubwa.
Sema tu mna beef, na hapa upo katika warfare, sio unajidai kutoa ushauri hapa wakati mwenyewe unajianika na kutoa motive yako.Siku zote ulikuwa wapi kutoa ushauri ukasubiri mpaka ulipomulikwa?

Kwa wale ambao hawakubahatika kukiona kipindi hicho nitawasimulia kidogo; kilichotangazwa na vijana hao maarufu hivi sasa nchini Tanzania wakitembelea magari ya kifahari na kufanya kila aina ya starehe wanayoona inafaa ni kumwonyesha Bw. Mashaka Matongo ambaye huko nyuma aliwahi kumiliki magazeti kadhaa Pendwa akiwa amefilisika vibaya! Kazi yake hivi sasa eti ni kunyoa nywele huko Sinza na kuomba misaada kwa watu! Wakanionesha mimi kama mtu aliyefanikiwa ‘sana' kuliko Mashaka Matongo katika kazi hiyo na kumcheka wakimfanya mjinga.
Kwa uhadithia hiki kipande unajionyesha ni jinsi gani ulivyo deep katika kuwa passive aggressive, yaani umeona upumbavu ulioonyeshwa kwenye TV hautoshi ukaamua kuja kuusimulia zaidi, ili mradi roho yako isafishike, i guess utasema tena hupendi sifa and all that jazz

Inawezekana kwa kunionesha mimi niko juu na mwenzangu akiwa amefilisika mlifikiri ningefurahishwa na kitendo hicho, naomba niwaeleze wazi kwamba mimi si mtu wa aina hiyo, wanaonifahamu wanaelewa na kitendo hicho hakikunifurahisha hata kidogo, sipendi umaarufu wa bei nafuu (Cheap popularity) napenda ninapopewa sifa iwe ni halali na ya kutolea jasho.
I guessed it, jamaa yuko predictable kuliko Rambo. Yaani yeye kazi yake ni kujijazia kwa kusema hapendi kujijazia, halafu anatonesha na kuongezea story akijifanya kama anazikandya kumbe haja yake anataka kutoa details hata watu waliokosa kuona kwenye TV wajue yeye yuko safi na mshkaji wake kalosti.

Mpaka leo ninapowaandikia makala hii binafsi sielewi mwenzangu alijisikiaje baada ya dhihaka hiyo kurushwa na TBC 1 ambayo Mkurugenzi wake ni mtu ninayemheshimu sana katika fani hii, Tido Mhando.
You just threw your "friend" under the bus, with friends like these, he doesn't need enemies.

Kilichonituma niandike makala hii ni
Kilichokutuma ni kisasi na udaku, kutaka kui "lord it" over other people na kuji appoint kuwa mtunza maadili wakati wewe mwenyewe huna moral authority na vigazeti vyako va soft-pron, mlokole indeed.

kuwakumbusha wadogo zangu
Lording over, wadogo zako kivipi? Ulizaliwa nao au?

wa Orijino Komedi kwamba, maisha ni safari ndefu. Kwa kuonekana kwenye luninga kila Alhamisi na Jumapili, kupita huku na kule wakishangiliwa, wasijione wamefika kwenye kilele cha mafanikio na kuanza kucheka wenzao, ninachofahamu mimi na uelewa wangu mdogo juu ya mafanikio ni kwamba safari kwao ndiyo kwanza imeanza.
Kucheka watu ni sehemu ya kazi ya comics, na kama art yao iko offensive kwako bila sababu ya msingi inayoweza kusababisha rational people waone kuna insensitive remarks/ acts basi wanafanya kazi yao vizuri.

Safari ya maisha ni ndefu wadogo zangu, hakuna sababu ya mtu kumcheka mwenzake.
Wengine wasipowacheka watu hawana kazi, hivi unaweza kumwambia Chris Rock asimcheke mtu? We utakuwa una akili? Inaelekea wewe bwana unayejifanya gwiji wa literature huelewi idea nzima ya comedy, kiasi umewachukulia seriously hawa comedians mpaka wewe ndiye unayechekesha sasa.Ease up, comedians wanatakiwa kuwatania mpaka marais na viongozi, itakuwa wewe na rafiki yako?

Mzee mmoja aliwahi kuniambia ni kama safari ya kwenda umbali wa kilometa elfu moja kwa miguu, kila mtu ataondoka kwa staili yake. Mwingine atakimbia mwingine atatembea au kutambaa zote hizo ni safari lakini hakuna mwenye uhakika kwamba atafika mwisho wa safari yake salama kiasi cha kuwacheka wenzake, hiki ndicho ninachotaka kuwaeleza wadogo zangu wa Orijino Komedi.
Sasa kama unajua kila mmoja kivyake vyake kwa style yake, mbona unataka kuwapangia maisha?

Ninachojua mimi hakuna anayeweza kukimbia umbali wa kilometa elfu moja bila kupumzika
Hujalisikia LearJet bado

lazima mahali fulani mbele ya safari atachoka na kuketi chini ya mti ili kuwapisha wengine wapite na pengine huo ndiyo ukawa mwisho wa safari yake huku uliowaacha nyuma wakitembea taratibu wakipita na kukuambia "Mzee tunatangulia" huu ni ukweli.
Mbona una state the obvious? Kwani nani kakubishia hili? Hata hao Ze Komedi wanajua hili ndio maana hawachelewi kukandamiza wakati wako on top, wewe unataka wasubiri mpaka watakapoanguka? Acha kijicho!

Inavyoonekana kwa hivi sasa wadogo zangu wa Orijino Komedi mmeanza safari yenu kwa kukimbia kiasi cha kujiona ni wajanja kuliko wanaotembea hata kufikia hatua ya kuwacheka kama mlivyofanya kwa Mashaka Matongo ambaye huko nyuma alimlisha na kumtunza Sekioni! Mmesahau kwamba mbele ya safari ni lazima mahali fulani mtapumzika na waliokuwa wakitambaa na kutembea wakaja na kuwapita mkiwa chini ya mti, nimekwishawaeleza hapo juu kwamba binadamu huwezi kuwa bingwa milele lazima siku moja utoke na wengine waingie, kumbukeni walikuwepo mzee Majuto na Small kabla ninyi hamjaja.
Inaonekana kama unawaombea washindwe, tena mapema sana.So much kutoka kwa mtu asiye kinyongo wala kisasi.

Kibaya zaidi na kinachositikisha ni kwamba mmeanza hata kuwatukana watu waliowasaidia kufika mlipo leo! Hiki ni kitendo cha ukosefu wa shukrani cha kiwango cha juu kabisa ambacho nimewahi kukiona chini ya jua. Kila Mtanzania anafahamu mlipotokea, namna ambavyo mtu kama Reginald Mengi na vyombo vyake vya habari amesaidia kuwafikisha ninyi kwenye mwanga, ambaye hakika hamuwezi kusimama mahali popote duniani kutoa historia yenu mkaacha kutaja jina lake, lakini huyu ndiye amekuwa mtu wa kutukanwa kila siku katika vipindi mnavyofanya! Hili ni jambo la kusikitisha sana.
Unanunua legitimacy na sympathy kwa kuchomeka vineno

Najua mnatiwa kiburi na utajiri wa fedha na umaarufu ambao hivi sasa mnao! Mmethibitisha ile kauli kwamba hakuna kitu kigumu duniani kwa mwanadamu kuwa na fedha au mafanikio halafu akabaki yule yule! Fedha na umaarufu ni shetani, huwabadilisha watu na kuwapa tabia ambazo huko nyuma hazikuwahi kuonekana, sitaki kuwahukumu wadogo zangu lakini jambo hili limethibitika kwa matendo mnayoyafanya hivi sasa.
Kama fedha na umaarufu ni shetani funga vigazeti vyako na uache kuandika, unataka kuleta unafiki tu, fedha na umaarufu ni shetani halafu wakati huo huo unatafuta fedha na umaarufu. Humdanganyi mtu hapa.

Najua mnatumiwa na watu kutimiza malengo yao, mambo mnayoyafanya si yenu yote, baadhi ni ya kuwafurahisha watu wanaowaweka mjini! Lakini kumbukeni mfano wa Mzee Kijiti aliyesafiri kwenda miji ya mbali akimwacha mke wake nyumbani, akiwa huko ashki ya tendo la ndoa ilimshika na kujikuta akitafuta mwanamke wa kuondoa haja yake.
Akifahamu kuna gonjwa la Ukimwi mzee huyo alilazimika kutafuta mpira wa kujikinga na gonjwa hilo. Kwa mahali alipokuwa ilikuwa kazi kidogo kupata mpira huo, akazunguka huku na kule kwenye vibanda bila mafanikio, mwili wake ukiwaka tamaa ya ngono. Mwisho mhudumu wa nyumba ya wageni aliyofikia alimpa mpira mmoja, akafurahi na kuingia chumbani ambako alifanya shughuli yake mpaka kufikia tamati akauvua mpira na kuutupa sakafuni tena akasikia kinyaa na kujilaumu kwa kitendo alichokifanya kusaliti ndoa yake.
"Ichukue" Akamwambia mwanamke aliyekuwa naye.

"Ichukue wewe" Mwanamke akakataa.
Baadaye wote wawili waliondoka na kuuacha mpira huo sakafuni, sasa wakiwa na akili timamu kondomu haikuwa na umuhimu tena, ilishawasaidia kuwaepusha na Ukimwi basi ilikuwa inatosha, kazi yake ilishakwisha.
Wadogo zangu,
Umerudi kule kule, hata kwenye eminent criticism kumekushinda unarudi kwenye udhaifu wako wa kila siku, all your thinking is done between the legs, you can't even disguise that for a minute!

Kwa mfano huu wa Mzee Kijiti naamini mtakuwa mmenielewa vizuri, jiepusheni sana na kutumiwa na watu wenye malengo yao ambao mwisho wa siku yakitimia watawatupa kule kama Kondomu na hawatawajali tena. Mkilijua hili mtafanya mambo mawili, la kwanza ni kuwekeza na la pili ni kujiepusha na matusi kwa watu waliowasaidia kufika mlipo kwani kesho ni lazima mtarudi kwao kuwashika mikono, hivyo ndivyo Mungu anavyofanya kazi.
Wewe unamjua mungu wewe au unafiki tu? Unvyoharibu watoto wadogo nako huko ni kumjua mungu?

Jiepusheni na starehe na kulewa umaarufu, jua haliwaki siku zote, kuna mchana na usiku. Muda huu mkiwa juu, ni vizuri kujiuliza giza litakapoingia na mwanga kupotea, au siku tutakapotupwa tutaishi vipi? Anasa hazina mwisho, zipo tu, mlizikuta, mtaziacha na wengine watazikuta na kuziacha hivyo ni vizuri kuwa makini katika kipindi hicho ambacho neema bado ipo, maana mchekaji huwa mchekwaji kesho na mchekeshaji huwa mchekeshwaji kesho kutwa.
Nani kakuomba ushauri? AU wewe ndiye self appointed moral authority? Na yale mapicha ya ajabu unayoyachapisha kwenye magazeti yako, nayo ni moral authority ile?

Mmekwishanitukana mimi mara nyingi lakini mimi sijali,
Kama hujali kwa nini unaandika hapa?

nimekwishazoea, katika miaka kumi na moja niliyofanya kazi hii ngumu ninao maadui wanaoweza kufanya chochote ili wanichafue, kinachoniuma sana ni kitendo mnachokifanya kwa mzee Mengi ambaye bila yeye TBC1 wasingewaona,
Hii ni kufuru, hasa kwa mtu anayejifanya kumjua sana mungu. Unataka kusema Mzee Mengi ndiye mgawa riziki? Kwamba bila Mzee Mengi wasingefanikiwa? Unataka kuingia katika somo la alternative history? Wacha kujifanya una ki crystal ball na umeona maisha ya watu bila Mengi yalikuwaje wewe.

kwa umri wake mzee huyu ni sawa na mzazi wenu na mnachokifanya ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu sababu tu mmelipwa!
Whats your point?

Inawezekana mkawa hamfahamu kwamba umaarufu wenu unapotezwa na kitendo hiki, Watanzania hawapendi watu wenye maringo na kujisifu tabia ambayo hivi sasa imewagubika ninyi mkiwa mwanzo tu mwa safari ya maisha! Mnakumbuka kilichowapata uwanja wa Taifa siku ile mlipopigwa kwa chupa na makopo ya soda? Hilo linapaswa liwe fundisho ili mjiangalie upya, mimi naamini mnaweza kurejesha hali mliyokuwa nayo zamani kwa kujiepusha na matusi kwa watu waliowasaidia.
Kwa hiyo na wewe ndio unataka kuwasindikiza kaburini kabisa na kujiongezea umaarufu hapo hapo sio? So much kwa mtu asiye kinyongo wala kisasi.

Mkiendelea na tabia hii si tu mtachukiwa bali mtailetea TBC1 matatizo makubwa sana ya kulipa watu mabilioni ya fedha jambo ambalo najua kabisa TBC1 hawatakuwa tayari kulifanya, hivyo kuamua kujiepusha nanyi! Hata kama TBC1 ni chombo cha serikali, inaelewa kabisa kuna mahakama na hakuna aliye juu ya sheria, kitendo cha wao kuwaruhusu ninyi kuendelea kutukana watu kwa maneno ya uongo, kitakuja kuwaingiza kwenye matatizo makubwa ambayo hatimaye yatavunja ndoa yenu.
Si uwashtaki basi, wapige libel suit.Mwenzako Rostam kashinda mabilioni. do you even know what is freedom of speech?

Najua maneno yangu yatawaumiza lakini naomba msikasirike kwani tiba ya ugonjwa siku zote inauma lakini mwisho wa siku inaponyesha! Naomba mnivumilie na myafanyie kazi yale mtakayoona yanafaa, binadamu hatujatimia, tunayo mapungufu mengi na kila siku tunafanya kazi kurekebisha sehemu mbalimbali maishani mwetu, nanyi nawasihi mchukue hatua hiyo. Mtu hahitaji kuwa na elimu kubwa sana kuelewa kitakachowapata kama mkiendelea na mtiririko huu mnaokwenda nao.
Mjua yote, ushajua watu watakavyofikiri bila hata ya kuwasikiliza.

Sisi sote ni Watanzania tuacheni kuchekana bali tuwatie moyo waliovunjika na tuwasaidie kusimama walioanguka! Matendo hayo ndiyo yatakuwa akiba yetu mara giza litakapoingia hawa mnaowacheka na kuwatukana leo si ajabu ndiyo watakaowasaidia ikitokea siku moja kigogo anayewafadhili sasa akawa hafanyi kazi na ninyi tena jambo ambalo si ajabu kutokea.
Collectivism at it's best, ili tutie akili inabidi tuchekane, wengine waone kweli kuchemsha noma,kesho watatia akili.Tusipochekana ndipo tunaendeleza mediocrity kila siku, si hamna kuchekana.

Naomba niseme neno moja natumaini sitamuudhi mtu. Watanzania tuna tatizo ambalo ni lazima tulishughulikie kama kweli tunataka kupata mafanikio ya kweli maishani mwetu, tuna tabia ya kuridhika mapema hata kwa mafanikio kidogo. Hapo mlipo wadogo zangu wa Orijino Komedi tayari mmesharidhika, lakini kumbukeni kufika Uingereza au kuendesha ‘Haria' peke yake haitoshi, kuna mambo mengi sana ya kufanya, kama kufika nje na kuendesha gari ingekuwa kila kitu basi watu wangekwisha acha kufanya kazi.
Wewe huna haja ya kuwapa ushauri, kama ungetaka kuwapa ushauri unge watafuta au hata kuwaandikia barua.Kitendo cha kuchapa haya mambo public kinaonyesha unataka vita na kisasi zaidi ya kutaka kuwapa ushauri.Acha unafiki.

Hili ni kosa kubwa sana ambalo sisi Watanzania tunalifanya, mafanikio kidogo tu yanatulewesha na kuanza kutukana watu bila kujua kwamba kuna kesho, hata Orijino Komedi mtakubaliana nami katika hili! Wadogo zangu mmelewa sifa mapema, kila mahali mnapoingia mnataka huduma ya VIP? Kumbukeni wanaojikweza hushuswa bali wanaojishusha hukwezwa! Chapeni kazi wadogo zangu, bado hamjafika popote, mafanikio ni safari ndefu mnahitaji sana watu kuliko mnavyohitaji fedha.
Watanzania wako wengi na wa kila aina, ni matusi kuwalundika wote katika kundi moja.Unajionyesha ulivyo hamnazo.

Nimeongea mengi sana wadogo zangu, lakini huu ndiyo Waraka wangu kwenu sisi ni ndugu lazima tuelekezane kwa maneno ya ukweli na si visasi, ni vizuri mkakumbuka mlikotoka badala ya kujisikia mmefika mwisho na kuanza kuwatukana watu waliowasaidia kufika juu! Ni vizuri kuelewa hamtakuwa mabingwa siku zote, pengine mtakapokuwa mnaporomoka hawa mnaowatukana leo watakuwa bado wako juu na mtahitaji msaada wao.
Naomba niishie hapo.
Unajionyesha uantaka waporomoke kwa kisasi na mameno ya uongo umejaza pomoni.

Jipu limepasuka siwezi kuwa adui kwa kusema kile ninachoamini ni ukweli.
Unasema nimekuwa adui kwa kusema uongo, unatubu mwenyewe sasa.

POLE SANA MASHAKA MATONGO, MANENO YA ORIJINO KOMEDI YASIKUVUNJE MOYO, PAMBANA TU HATIMAYE UTAFIKA JUU, YOTE YAWEZEKANA, IF THEY CAN, YOU CAN!
Huu unafiki mtupu, unawachoma visu huku unasema "die die" huku unajidai kutoa pole na maneno ya busara.

Wiki ijayo nitamwongelea Sekioni David, yatima aliyesaidiwa na Reginald Mengi ambaye hivi sasa kila kukicha anamtukana mzee huyo sababu leo hii anafadhiliwa na Yusuph Manji.
Hata kabla ya kujua "ushauri" wako umechukuliwa vipi ushaandaa mawe mengine ya wiki ijayo, unajionyesha jinsi gani usivyojali ushauri na unavyotaka kuleta unafiki wa kidaku tu.
 
Last edited:
Bluray napenda ulivyo chambua kipengele hadi kipengele. Huyu baba hana lolote. Ninacho jiuliza ni kwanini kaamua kuweka magazetini kila mtu asome? Kwa nini asingewafuata privately na kuwaambia yote hayo? He himself is guilty of what he is accusing them of.
 
Kila mtu na uelewa wake,
Binafsi naona kafanya vyema, na kwa mara ya kwanza walau Magazeti yake, yamekuja na kitu constructive!

Yaani kuwatafuta private wakati wao wanatumiwa na mafisadi na kutelevise upuuzi wao?, Sema basi tu, nadhani inge faa naye achukue kipindi maalumu TBC arushe huu waraka wake, ili hadhira yote inao watazama hao vijana ipate kuona upande mwingine wa shilingi

Kwamba hawa vijana wanako kwenda siko.. mafisadi wamewakama wanawatumia wapendavyo, hata humu JF tulikuwa tukiwalalamikia kwamba siku hizi wanaboa hawako creative wanazidiwa hata na FUTUHI wa star TV why?

Ni kwa sababu sasa hivi wanasubili amri kutoka kwa mafisadi kwamba kamseme huyu hivi, kafanye hivi kile usiguse,

Any way tusiandikie mate, siku zao nao zina hesabika, na ujue jamii iki kuchoka mhhhh..
 
Rwabugiri;

Ni kweli alicho kisema kinaweza kuwa na ukweli lakini kwa nini aandika kwenye gazeti wakati maudhui ya hiyo waraka ni kama anaongea nao binafsi? Na kama kaweza kuwaandika kwenye gazeti kashindwaje kuwa fuata na kuwaambia? Whether he was saying the truth is beyond the point.

What is being questioned is the aim of what he wrote na kwa nini kaamua kuweka public? kama ushauri anawapa hao sasa iweje aandike kwenye gazeti kila mtu aone? Hao ze komedi siyo viongozi wa kitaifa na wala hawana nguvu yoyote.

Sawa wanatumika na mafisadi kama unavyo sema lakini tokea lini mtu aka make an opinion from a comedy show? The show haina credibility politically kama mtu ukiwa fuatisha basi na wewe ni ze komedi pia.

Kaandika kama barua lakini kaiweka public ya nini? Sawa ze komedi nao wamezidi sifa lakini na yeye kuweka barua yake public si kutaka sifa pia?

You can't accuse someone while doing the same thing.
 
Mimi ni mmoja wa wasiosoma magazeti ya udaku, hivyo isingeletwa hapa JF nisingeijua hii. Asante kuileta.

Naomba kumpongeza Eric kwa waraka huo. Andiko lake ni andiko lenye busara, na ningemuomba sana Eric atumie busara hizo hizo kuchuja nini kitoke kwenye magazeti yake, na nini kisitoke.

Orijino Komedi ni ngoma inayopigwa sana, karibu itapasuka.
 
Mimi ni mmoja wa wasiosoma magazeti ya udaku, hivyo isingeletwa hapa JF nisingeijua hii.

Binafsi sijui undani wa wasifu wa Eric kama nilivyojaribu kusoma comments za wanaJF. Lakini nimesoma walaka wake wote. My take huu ni walaka kwa vijana wote wakitanzania. Binafsi nimeupenda sijui bifu lililopo kati ya magroup hayo lakini ni ujumbe mzuri wenye kujenga.
 
Ujumbe wake upo sawa tu, mie sijaona kosa. Ila kuna baadhi ya watu hawampendi Shigongo, sababu wanajua wao.

Ila kuhusu magazeti yake ya udaku na habari zake yy hana kosa, ule ni mtaji na biashara yake, wa kulaumiwa ni waandishi wake na sio Shigongo. Eti wanamsema mnafiki! Sijaona hata Unafiki wa wake.

Kama ulokole wake una sehemu yake wala haungiliani na kazi yake ya habari.
 
Ujumbe wake upo sawa tu, mie sijaona kosa. Ila kuna baadhi ya watu hawampendi Shigongo, sababu wanajua wao.

Hakuna sababu ya kum chukia wala kumpenda. Wengi wetu hapa hatumjui binafsi labda kama wapo ndiyo wanaweza kutoa honest opnion about the persons character. Wengi hapa wana jadili kitendo chake siyo personality yake.

ilakuhusu magazeti yake ya udaku na habari zake yy hana kosa, ule ni mtaji na biashara yake, wa kulaumiwa ni waandishi wake na sio Shigongo.

1. Hata zeutamu(kama umewahi kuisikia) nao ni mtaji but it doesn't make it morally right
2. Ni mkurugenzi mtendaji na mmiliki wa wa magazeti uta semaje wakulaumiwa waandishi? Kwani yeye haoni wanavyo andika? Mtoto akifanya kosa basi mzazi asisemwe kwa kumyamazia alaumiwe mtoto tu?

etiwanamsema mnafiki! Sijaona hata Unafiki wa wake. Kama ulokole wake una sehemu yyake wala haungiliani na kazi yake ya habari.

Umeona wapi mtu akiwa mlokole kwenye upande mmoja tu wa maisha yake? Kwa hiyo mchungaji aki hubiri watu wasizini kanisani ni ruhusa akitoka akazini? Ulokole is a way of life for those who know what ulokole means. Sasa ulokole wake una maana gani kama anaitumia anapo taka yeye tu?
 
Back
Top Bottom