Waraka wa Kwanza (1) kwa Wasabato wote

PharaohMtakatifu

JF-Expert Member
Jul 3, 2023
659
1,074
Huu ni waraka kwanza Kwa wasabato wote mliomo humu JF na wengine wote.

Waraka utaendelea Hadi mtakapo tuambia na kuwaelewa dhahiri kuwa kwanini mkengeuka kiasi hiki! Yeyto atakae waandikia waraka ataendeleza. Yaani mpaka mseme na mtasema!

Wasabato Kwa hakika wengi wao ni wanafiki sana,watu wenye kukuona wao ndo watakatifu wao ndo wasafiri wa kwenda mbinguni wengine wooote ni wakwenda motoni.

Wasabato wamejaa unafiki na ubaguzi sio ajabu kuwaita watu wengine ni wa mataifa wao ndo watu wa Mungu.

Hata salamu Yao ya kanisani utasikia "watu wa Mungu sabato njema" Nao huitikia Njema sana hasa ya Leo! Wakimanisha hata Ile sabato iliyopita haikuwa njema(nzuri) Bali ilikuwa ni mbovu yenye maovu.

Wasabto mikutano Yao yote ni kuwakashifu wakathoric na walokole kuwa ni wadhambi wanakula Bata kitimoto na kuabudu sanamu na wafu!

Nimejifunza nanyi Kwa muda mrefu sana na vitabu vyenu nimenunua vingi tu baadhi mmenipa vya Bure Ahsanteni sana Kwa hili na hakika mafundisho yenu ni mazuri lakini matendo yenu hayaendani na mnayo tufundisha.

Baadhi ya vitabu nilivyo nunua
Ni kama
Kutayarisha njia1&2
Dhiki kuu
Tumaini kuu(Bure)
Kutoka maonjo Hadi ushindi
Daniel na siku zetu
Ufunuo wa mambo yajayo nk.

Nimewahi kusali kwenye kanisa na dodoma kati la wasabato. Siku hiyo kama hakuwa sabato ya wageni basi ilikuwa ni siku maalum Fulani Hivi pembeni yangu nilkuwa nimekaa na dada Fulani amevaa gauni lenye matobo likionyesha Hadi nguo ya ndani aliyo Vaa mapaja nk hakika siku hiyo niliilaani sana yule dada mwanzo nilijua huenda ni mgeni kitu kilicho nifanya nijue ni msabato ni kile kibahasha Cha zaka na sadaka (wenzetu Wana utaratibu huo) kwamba unaandika jina lako.

Then zaka Yako sadaka zako mbalimbali kama za ujenzi Nk.yule dada alikuwa amejaza kabisa kale kabahasha na no ya ushirika ilikuwepo.

Wasabato siku zote hukemea watu wa Nje lakini kanisani mwao hawakemei Katu maovu Yao wakiona umetenda kosa kubwa basi watakufuta ushirika. Mfn ukifuniwa au ukakamatwa wizi basi watakufuta ushirika na Wana kuhakikisha kuwa hata mbinguni hutoenda kama ushirika umefutwa Hadi utakapo batizwa upya!

Dhambi za unafiki,uongo,nk hizo hazikemewi. Hivi dhambi zinatofautiana? Mfano aliye iba na aliye sema uongo?(Tunaka maelezo ya kina hapa)

Haya nayajua kwasababu nimeshaalikwa sana kwenda kanisani kuabudu nao na mikutano kadhaa nimehudhuria kama wa Pela mwanza (UFUNUO WA MATUMAINI) Mark Finley ndo alihutubia na mingine kusikiliza Kwa njia ya Tv. Na mitandaoni.

Msabato ukimbana maswali Kwa maovu Yao watakuambia kabisa halitaanguka kamwe Bali washirki ndo wataanguka.

Swali kanisani njengo au kanisa ni watu(washirki)?

Kuna Uzi kadhaa mmeleta hapa kutunanga wakathoric eti papa karuhusu ushoga nk mmesahau ya kwenu mengi.

Nawapa waraka kemeeni ya kwenu kwanza ndo muanze na kuangalia wa ya waroma na walokole

Picha na video hizi ni vijana wa kisabato ambao ni viongozi wa kanisa la wasabato wajao.

Kwa mavazi haya mnapata wapi nguvu ya kuhubiri watu waache dhambi Wakati dhambi zimeshataga mayai kanisani mwenu! Hawa vijana wanafundishwa masomo yote na wanaijua biblia vzr lkn Hawa ndo wanavaa Hivi je kwenye mwaka 2040 si mtakuwa mnaingia kanisani na bikini?

FB_IMG_1701800345297.jpg
 
Asante kwa ujumbe mzuri.

Nazani umeeleweka.

Mafundisho ni mazuri na ndio maana sio wote watakaosema Bwana Bwana watauona ufalme wa Milele.

Kwa nini Roma/Papa?. Huyu hawezi kuacha kusemwa. Kitabu cha Daniel 7 kimemfunua sana.

Nakupa Mfano wa fungu moja tu.
Daniel 7;25 Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.

Ruma imeshajipa madaraka ya aliye juu - Mfano; Viongozi wake wanasamehe zambi wakati maandiko yanatambua anae samehe zambi yuko mbinguni. Rumi iliamua kubadili majira na sheria. na wanamambo yao kabisa wala hayajifichi.

Kuhusu mavazi - utaratibu wa mavazi uko wazi kabisa. Yaani kwa maana ya kanisa limesimama vizuri, ila kwa sababu kuna watu wanaingia kanisani kila siku na wanahitaji wokovu mara nyingi mtu anafundishwa taratibu hadi aelewe. Huwezi kuta kiongozi amevaa mavazi ya ajabu ajabu , kwa sasabu wanaelewa. Watu wengine wanaharibiwa na tamaduni zao na malezi, akija kanisani ndipo anaanza kujifunza taratibu.

Asante kwa walaka wako; kuna mambo ya kulekebisha ili mbingu ziendelee kukufunulia ili siku moja uungane na washika neno la Mungu na sio mapokeo.

Kuhusu dini nyingine - wengi wameshafata mafundisho ya rumi na hawajui kama wanaenda kinyume na aliyeko juu.
 
Kumbuka...
The Four Xtians Cults.
1. Seventh Day Adventis.
2. Jehova Witness.
3. Mormon.
4. Xtian Scientology.

Usiumize kichwa Wasabato siyo wakristo ila ni kikundi cha Wahuni kinachojifananisha na Wakristo kikutumia bidhaa za Wakristo kama Biblia
Kwani Wakisto ni watu gani?! Catholic, Lutheran, Tag, Eagt, Sabato....?!!

Wakristo ni wafuasi wa Masihi(Kristo).

Yesu hakuleta dini, dini ni utaratibu wa mwanadamu kumtafuta MUNGU.

Ila WOKOVU ni mpango/utaratibu wa MUNGU kumtafuta mwandamu.

Tunapenda dini zetu kuliko kumpenda MUNGU.

Yesu Kristo anasema kwenye hili andiko;
Yohana 14:15
"Mkinipenda, mtazishika amri zangu"
 
Huu ni waraka kwanza Kwa wasabato wote mliomo humu jf na wengine wote.
Waraka utaendelea Hadi mtakapo tuambia na kuwaelewa dhahiri kuwa kwanini mkengeuka kiasi hiki! Yeyto atakae waandikia waraka ataendeleza. Yaani mpaka mseme na mtasema!

Wasabato Kwa hakika wengi wao ni wanafiki sana,watu wenye kukuona wao ndo watakatifu wao ndo wasafiri wa kwenda mbinguni wengine wooote ni wakwenda motoni.
Wasabato wamejaa unafiki na ubaguzi sio ajabu kuwaita watu wengine ni WA mataifa wao ndo watu wa Mungu
Hata salamu Yao ya kanisani utasikia "watu wa Mungu sabato njema" Nao huitikia Njema sana hasa ya Leo! Wakimanisha hata Ile sabato iliyopita haikuwa njema(nzuri) Bali ilikuwa ni mbovu yenye maovu.

Wasabto mikutano Yao yote ni kuwakashifu wakathoric na walokole kuwa ni wadhambi wanakula Bata kitimoto na kuabudu sanamu na wafu!

Nimejifunza nanyi Kwa muda mrefu sana na vitabu vyenu nimenunua vingi tu baadhi mmenipa vya Bure Ahsanteni sana Kwa hili na hakika mafundisho yenu ni mazuri lakini matendo yenu hayaendani na mnayo tufundisha!
Baadhi ya vitabu nilivyo nunua
Ni kama
Kutayarisha njia1&2
Dhiki kuu
Tumaini kuu(Bure)
Kutoka maonjo Hadi ushindi
Daniel na siku zetu
Ufunuo wa mambo yajayo nk.

Nimewahi kusali kwenye kanisa na dodoma kati la wasabato
Siku hiyo kama hakuwa sabato ya wageni basi ilikuwa ni siku maalum Fulani Hivi pembeni yangu nilkuwa nimekaa na dada Fulani amevaa gauni lenye matobo likionyesha Hadi nguo ya ndani aliyo Vaa mapaja nk hakika siku hiyo niliilaani sana yule dada mwanzo nilijua huenda ni mgeni kitu kilicho nifanya nijue ni msabato ni kile kibahasha Cha zaka na sadaka (wenzetu Wana utaratibu huo) kwamba unaandika jina lako
Then zaka Yako sadaka zako mbalimbali kama za ujenzi Nk.yule dada alikuwa amejaza kabisa kale kabahasha na no ya ushirika ilikuwepo.

Wasabato siku zote hukemea watu wa Nje lakini kanisani mwao hawakemei Katu maovu Yao wakiona umetenda kosa kubwa basi watakufuta ushirika. Mfn ukifuniwa au ukakamatwa wizi basi watakufuta ushirika na Wana kuhakikisha kuwa hata mbinguni hutoenda kama ushirika umefutwa Hadi utakapo batizwa upya! Dhambi za unafiki,uongo,nk hizo hazikemewi. Hivi dhambi zinatofautiana? Mfano aliye iba na aliye sema uongo?(Tunaka maelezo ya kina hapa)

Haya nayajua kwasababu nimeshaalikwa sana kwenda kanisani kuabudu nao na mikutano kadhaa nimehudhuria kama wa Pela mwanza (UFUNUO WA MATUMAINI) Mark Finley ndo alihutubia na mingine kusikiliza Kwa njia ya Tv. Na mitandaoni.

Msabato ukimbana maswali Kwa maovu Yao watakuambia kabisa halitaanguka kamwe Bali washirki ndo wataanguka
Swali kanisani njengo au kanisa ni watu(washirki)?

Kuna Uzi kadhaa mmeleta hapa kutunanga wakathoric eti papa karuhusu ushoga nk mmesahau ya kwenu mengi.

Nawapa waraka kemeeni ya kwenu kwanza ndo muanze na kuangalia wa ya waroma na walokole

Picha na video hizi ni vijana wa kisabato ambao ni viongozi wa kanisa la wasabato wajao.

Kwa mavazi haya mnapata wapi nguvu ya kuhubiri watu waache dhambi Wakati dhambi zimeshataga mayai kanisani mwenu! Hawa vijana wanafundishwa masomo yote na wanaijua biblia vzr lkn Hawa ndo wanavaa Hivi je kwenye mwaka 2040 si mtakuwa mnaingia kanisani na bikini?

View attachment 2835285View attachment 2835286
View attachment 2835289
Hao ulioweka kwenye picha ni wanafunzi, kutoka shule mojawapo ya sekondari

Kama ni wasabato sawa ila hawaliwakilishi kanisa bali ni imani yao ambayo imewaleta huku

Sasa mkuu kama hadi kusema Sabato njema , wewe unaumia kuna kosa gani hapo??😂

Kweli chuki mbaya sana, all in all Njoo kwa Yesu na Sabato ndio kanisa sahihi
 
Kumbuka...
The Four Xtians Cults.
1. Seventh Day Adventis.
2. Jehova Witness.
3. Mormon.
4. Xtian Scientology.

Usiumize kichwa Wasabato siyo wakristo ila ni kikundi cha Wahuni kinachojifananisha na Wakristo kikutumia bidhaa za Wakristo kama Biblia
Nimesoma sana hizi mambo lakini wote wameshindwa kuelezea namna gani SDAs ni true Christian. Wamejaribu kutengeneza ngonjera nyingi ilimradi tu wafanikiwe kuwapata watu kama wewe.

Mwandishi mmoja alijisema mwenyewe kuwa ni ngumu sana kusema SDAs ni cults or not.

Nikuhakikishie tu kwamba kati ya watu wanamjua Yesu ni SDAs na wanafuata mafundisho yake haswa. Na tunatumia ufunuo 14;12 kama njia ya kuishi kama christo.
 
Back
Top Bottom