Wadanganyika hakika mnanishangaza sana...
Sasa ikiwa Mbowe atakuwa dikteta na kukataa kabisa kukaa na watu wanaopingana naye ktk maswala yoyote yale kama alivyokuwa mwalimu ndio mtampenda?... kwa uhakika najua mtachukia sana na pengine hata kulaani mfumo mzima wa kiutawala..Lakini Leo hii Mbowe na Zitto wanapolumbana kimtazamo ni wajibu wetu kutafuta ukweli kwanza kuelewa kinachoendelea kabla hatujachukua side au kuhukumu mgogoro wote. Mlitaka itokee kitu gani yaani kusiwepo na kutokubaliana ndani ya chama!
Binaafsi haya malumbano ya Zitto na Mbowe hayanipi homa kabisa kwa sababu ndio makuzi ya demokrasia ndani ya chama. Sitaki kuona ya mwalimu kukosana na Kambona, mzee Mtei au Jumbe na kufikia maamuzi ambayo yalikidhoofisha chama ktk ujenzi wa fikra mpya na ndio maana CCM hadi leo bado imekumbatia siasa za Ujamaa ambazo ktk dunia ya leo ndio chimbuko la Ufisadi wa viongozi wa juu.
Kama Mbowe na Zitto wanagombania nafasi zao kwa uchaguzi wa mwaka 2015, waacheni wagombane muhimu watuonyeshe uwezo wao kifikra na yule mwenye karizma ndiye atapendwa na wanachama zaidi na kufuatwa kwa sababu CDM haichagui sura wala hatumpongezi mtu kwa kusema sana. Zitto ataendelea kuwa Zitto na atakuwa na watu wasiopenda msimamo wake ndani ya chama na nje ya chama, Mbowe vile vile lakini wote wakitumikia itikadi ya chama.
Mbowe anaweza kuwa na matatizo lakini kama mwenyekiti lazima ifahamike kwamba hiki si cheo cha utendaji kazi bali ni nafasi inayotakiwa hekima na busara kuweza kuwa msikivu, muumini na mtaalam wa imani iliyokijenga chama. Uwezo wa ku preach kile unachokiamini (katiba) pasipo kudadisi ama kuzungumza yanayotoka kichwani mwako.
Nakumbuka nimesoma mahala ndugu yetu Waberoya kasema kitu kama hiki kuhusiana na maisha yake ya Ulokole, jinsi alivyoweza kutambua utumishi mbaya wa viongozi wa dini ambao hu preach mambo ambayo hayamo ktk Biblia hivyo ilimlazimu yeye kuisoma Biblia na kufuata tu yale yaliyoandikwa ndani ya kitabu ktk mahubiri yake, na hakika ina imani kwa kufanya hivyo utapata wafuasi wenye kuvutiwa na dawa utakayowapa...
Na kwa hali ya kisiasa ndani ya Chadema Zitto ni mmja wa wachungaji anayefundisha mambo yanayotoka kichwani mwake, hafuati yaliyomo ktk kitabu ila mtazamo wake yeye akilenga faida ya wananchi hivyo kuunda dhehebu au niseme mrengo tofauti na ule unaojengwa na chama.
Upande mwingine kwa Mbowe, leo anaonekana ni dikteta kwa sababu anapingana na Zitto iwe toka kugombea nafasi ya Uenyekiti lakini muhimu tufahamu kwamba Zitto bado kabisa hajakomaa kisiasa na nadhani yeye sii mwanasiasa kitaaluma bali anaweza kuwa mtendaji mzuri tofauti na Mbowe ambaye he is a Politician.. na ndani ya Politics, udikteta unatumika sana kulinda chama na itikadi kwa sababu kinachosimama for each party ni itikadi sio sura za viongozi wake.
Mwisho nachoweza kusema ni kumkanya Zitto zaidi ya Mbowe apate kufahamu kwamba Siasa ya chama ina imani na lazima mtu uwe na mwongozo unaokupa fikra mpya na sii kutazama upepo unakwenda wapi kama zile mashua zinazosubiri monsoon wind. Chama kina dira na lazima kiongozi au mwanachama awe na fikra zinazoendana na mwongozo huo na sii kufikiria toka kichwani maadam unafikiri uko sawa.. kwa Chama kikianza kudandia fikra za watu binafsi ndio huanza kupoteza mwelekeo na hakika kupinga mawazo binafsi yanaopingana na mwongozo wa chama ni hali isiyotakiwa ndani ya chama.
CCM wamepoteza mwelekeo kwa sababu hii hii. CCM wameruhusu mawazo binafsi wakati mwongozo wa chama ni siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ambayo ndani ya ubepari imezaa Ufisadi na Ubinafsi kinyume kabisa cha malengo ya chama. na kwa bahati mbaya sana ndani ya CCM kuna watu wenye imani tofauti na naweza kusema majority wa wananchama wa chama hiki hawaamini siasa za Ujamaa na Kujitegemea. Vichwa vya watu vinatofautiana kabisa na malengo ya chama, hivyo wanachokipata ni mkusanyiko wa mawazo mgando na waigaji wa sera maana hakuna mwongozo.
Chadema kwa kuelewa hivyo hakiwezi kupoteza mwelekeo wake kwa sababu kuna watu wanafikiria kwamba Chadema ni chama cha Mbowe, Wachagga, sijui wakristu au Mbowe ni dikteta. well tunachotakiwa kusoma ni Biblia ya chama inasema nini na Mbowe anafundisha nini. Kama Mbowe anafundisha kinyume cha mafundisho ya chama na anaeneza gospel yake hapo tuna kila sababu ya kulaumu lakini Mbowe kusimama thabiti, kutetea malengo ya chama dhidi ya propaganda kubwa zinazojengwa kila siku, basi bila shaka huyu ndiye mwenyekiti tunayemtaka.
Zitto afahamu kwamba anatumika pasipo yeye kuelewa kwa sababu kila anapokutana na wanaCCM na kuzungumza mambo mengi ya ndani ya chama, hao hao huenda na kuwafahamisha viongozi wa CDM juu ya malalamiko yake... Na wapo marafiki zake ambao kazi yao ni kumnukuu maneno yake na kuyasambaza pasipo yeye kujua kwamba anatumiwa kwa sababu Zitto anachotumia zaidi ni elimu na hisia zake badala ya mwongozo wa chama.
Lakini wakati huo huo wapo washabiki wa Mbowe ambao hawapimi kitu isipokuwa kwa mapenzi ya Mbowe kutokana na heshima alojivunia. Lakini kumheshimu Mbowe hakuwezi kufunga kabisa vichwa vyenu mkashindwa kufikiri nje ya kabati..Washabiki hawa wameunda chuki binafsi dhidi ya Zitto pasipo kuelewa kitu ila kuunda fitan tu ndani ya chama.
Nakumbuka sana kuna wakati Zitto alisema wazi kwamba yeye na Mbowe hawana matatzo akini Zitto alitukanwa na kufuatwa kuchambuliwa ktk kila alichogusa. Zitto alikuwa na right ya kugombea uenyekiti na hata kama hakufaa kushika wadhifa huo maamuzi yalifanyika na alikubali maamuzi ya wazee lakini hadi leo anafuatwa kama vile kaua mtu...nakumbuka Nyerere aliwahi kuwakataa Salim na JK kushika madaraka ya juu kutokana na umri wao lakini sikusikia malalamiko kama ya haya..
Mbowe will always be Mbowe na Zitto atabakia Zitto wote wakiwakilisha chama kwa nafasi tofauti. Chadema haiwezi kubadilisha vichwa kwa sababu tunafikiria nafasi hiyo ina msuit fulani pasipo vigezo..