Waraka kwa Mbowe na Zitto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka kwa Mbowe na Zitto

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbwazoba, May 5, 2011.

 1. M

  Mbwazoba Member

  #1
  May 5, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vijana tunakiamini chama cha demokrasia na maendeleo,kwa namna kinavyosimama na kuibua na kuhoji mambo muhimu sana katika jamii yetu.

  Hata wazazi wetu wanaamini chadema ndio kimbilio letu, licha ya wao kutuonya kuhusu kujitokeza mbele sana kwenye harakati za siasa, wakihofia usalama wetu.

  Ila sasa viongozi wetu mnapoonekana kuvutana kwa ajiri ya tamaa za madaraka na ruzuku, ni aibu sana na ipo siku vijana wengi watafuatilia kiundani mambo ya chama chetu na ikiwa watabaini ukweli ulio tofauti na hisia zao, basi wataingia msituni kwani hawataamini mabadiliko kupitia chama cha siasa.

  Ikiwa CHADEMA hakitabadilika kimtazamo, kisera na ki-organisation, hakuna mafanikio, nawaomba sana Mbowe, Slaa na Zitto kubalini kukaa na kushauriana.

  I dnt understant wht the deal with uwenyekiti, tafadhali sana vijana vyuoni sasa wameanza kuhoji undani wa ugomvi wa Mbowe na Zitto kila wanapo onana.

  Na ni kwa nini wanaonekana kutosikilizana hata kwa jambo la maana, tunajitahidi kujibu maswali magumu sana kutoka kwa vijana wasiojua CHADEMA, ila tunafanikiwa kuwatuliza na kuwapa moyo, ila wakati mwingine unajibu mtu na unaona haimwingii akilini.

  Please msituumize kabisaaa.
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  May 5, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hoja kama hii badala ya kufanyiwa tafakuri na viongozi wa CHADEMA na kutoa majibu muafaka na yenye upeo basi utaambiwa umetumwa au una spin!!
   
 3. Jiwejeusi

  Jiwejeusi JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni kweli mkuu, hawa watu wawili wanatuchanganya sana. Endapo wakiendelea tutawafukuza wote wawili, ili wakatafute vyama vya kurumbania sio chadema. Mbowe na Zitto tutawafukuza chamani, uwezo huo tunao.
   
 4. emmathy

  emmathy Senior Member

  #4
  May 5, 2011
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kama hali hiyo ipo ndani ya chama, basi Mungu aepushie mbali mana chama kikiparaganyika hakuna atakae baki salama zaid ya kila mwananch kujiona kiongoz na nguvu ya umma kua tegemeo zaidi la ukomboz kuliko kupitia vyama vya siasa.
   
 5. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Mimi naomba sana,viongozi hawa wote wawili wawaonee huruma vijana waliojitoa maisha yao kwa ajili ya nchi nyuma ya mwavuli wa cdm.
  Kabla ya kusonga na ndoto yako ya kuwa nani baadae, naomba ufikirie kwanza ulionao au walio nyuma yako.
   
 6. v

  vngenge JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Haiwezekani watu wawili wakakubaliana kila kitu kila siku, Hata hivyo kwa watu nyeti kama hawa waangalie wasije athiri chama. chama ni bora kuliko wao na maslahi ya watanzania ni bora zaidi kuliko wao hivyo wawe makini hata wanachama tufuatilie kwa kina na kutumia baraza la wazee kutatua tofauti zao ili chama kisonge mbele
   
 7. M

  Molemo JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hizo ni propaganda za CCM tu.Achana na magazeti uchwara yanayoripoti hizo habari za uongo..Chadema ni kanyaga twende.Mbowe angekuwa na ugomvi na Zitto angemteua kuwa Naibu Katibu mkuu? Au angemteua kuwa Naibu Kiongozi wa upinzani bungeni?? Je, angemteua kuwa waziri kivuli wa Fedha?? Achana na propaganda broo...Zitto Slaa na Mbowe kanyaga twende..Sasa hivi wote wako njiani kuelekea Mbeya kuongoza maandamano lkesho..
   
 8. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Na nyie vijana mnazo kweli ? kweli CDM ni chama cha kwenda au na nyie ni waganga njaa kama Mbowe na Zitto inapofika wakati wa kujadili maslahi na tena yanayo husu harufu ya pesa? tafakari zingatia
   
 9. m

  mkulimamwema Senior Member

  #9
  May 5, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vijana wa ccm wanajulikana mapema humu ndani kutokana na uwezo wao mdogo wa kujenga hoja mimi nakwambia tunatumia kauli hii:Its your choice either to join us or to be against us' anguko kuu la chama tawala Tanzania ni 2015 shime wananchi njoni tulikate kichwa joka hili linalomeza maendeleo yetu
   
 10. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kweli ukipenda hata chongo hulioni, upo dunia ipi ambayo hujui CDM hali si shwari ? kwenda na gari moja si hoja ww, na hivyo vyeo ulivyotaja Zitto kupewa na Mbowe, sio kwamba alimpa bali vikao ndio vilimpa, na anastahili Zitto kwa uwezo wake. Mbowe ni fisadi katu hawezi kuelewana na Zitto
   
 11. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkuu umejiunga lini vile? ngoja nikukumbushe basiJoin Date : 14th April 2011
  Posts : 76
  Thanks0Thanked 3 Times in 3 Posts

  Rep Power : 21

  Huna jipya humu jamvini !
   
 12. Mbutunanga

  Mbutunanga Senior Member

  #12
  May 5, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 183
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa mtu mwenye akili timamu na ambae si mshabiki wa chama chochote humu ndani lazima ajiuliza, kwa nini kila inapokuja ishu ya kujadiliwa hukusu Zitto kwa nini wanaoonekana kuiponda Chadema na kuishabikia CCM wanamsupport Zitto?
   
 13. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naona kuna point ya msingi hapa viongozi zingatieni haya.
  CHADEMA hakitadharau hoja au ushauri wa mtu yeyote awaye mwanachama au si mwanachama,mtanzania au mgeni.
  RED LINE:
  Fuatilieni na kutekeleza ushauri wa MBWAZOBA
   
 14. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Swala lako, kwanza lingeanzia kwa Mh spika kule bungeni ndio uje kuchokonoa CHADEMA.:israel:
   
 15. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #15
  May 5, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Chadema ni chama chenye watu mahiri wa kujenga hoja,kwa hiyo ni lazima kuwe na misuguano.Vita ya chadema ni mapambano ya fikra
  Mbao zikisuguana haziwezi kutoa cheche,huko ni CCM
  Vyuma vikisuguana hutoa Cheche,huko ni Chadema

  Hata hivyo,ni lazima kuwe na balancing of power.Ni lazima mtu au taasisi ndani ya chama acheze balancing role(anakuwa buffer Individual au buffer Institution) ili kupunguza msuguano kwa kile kinachoonekana/kusemekana ni kambi mbili tofauti

  Pia,Vile vile ni Lazima misimamo mikali ichukuliwe dhidi ya wale wote wanaohatarisha institutional establishment ya chama>hakuna kuoneana haya,tuwe kama Orange democratic movement (ODM) ya Kenya au PDP ya Nigeria na Action Congress(AC) ambako mtu haonewi haya.ni lazima tuwe na disciplinary political establishment ili tusijekuwa na serikali legelege baada ya kuchukua madaraka.Huwa mara nyingi napendekeza hatua kali au Upanga wa moto upite kwa yeyote yule anayetaka kuhodhi establishment ya institution at an Individual capacity,hata kama ni mimi.
   
 16. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #16
  May 5, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Uko sahihi kwa sababu Huyu Mdau mtoa hoja amejiunga Leo tu hivyo atakuwa katumwa na watu!
  Kimsingi Kutofautian ndiyo Kuelewana ,CDM tunaruhusu tofauti za Kimawazo,Kila Kiongozi au Mwanachama ana Uhuru wa Kuwasilisha mawazo yake BILA Unafiki wa NDIYO kwa Kila kitu......Hizi tofauti Ndizo zinazokijenga Chama na Kukiweka Hapo Kilipo na Cha Msingi ni Kwamba Mwisho wa Siku Kuna Makubaliano na Mambo yanaenda Mbele! Huo ndiyo Msingi wa Demokrasia tunayoidai..Ni lazima Ianzie Ndani ya Chama
   
 17. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #17
  May 5, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,583
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  Naamini utakuwa umeelewa!
   
 18. P

  PETERMKALI New Member

  #18
  May 5, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtandao ambao mbowe anaujenga na wenzake unaoonyesha busara ndogo za mbowe na umesababisha vitendo vya sirisiri ndani ya chadema dhidi ya watu fulani, hii haijengi umoja ndani ya chama.

  Busara ndogo za mbowe zinaonekana pale anapofikiria vitendo na maneno ya godbless lema yatakuwa siku zote kwa masilahi ya chadema kwasababu tu ni mmachame mwenzie.

  Tukumbuke ni lema huyo huyo ndiye aliyekuja chuo kukuu cha dodoma na kutuhonga ( kutupa rushwa) ili tuandamane kupinga shibuda kuonyesha mtazamo tofauti ndani ya bunge, bahati nzuri wanafunzi wenzetu ambao hawakupata hela walikuwa wakali dhidi ya hili.

  Bila ya shaka lema alifanya kitendo hiki bila ya kuwa na upeo wa kujuwa kwamba kinaweza kuchafua jina la chadema na kuharibu umoja ndani na nje ya chama.

  Chuo kikuu cha dodoma kina watu wakabila mbalimbali, asifikirie wanafunzi wa chuo kikuu cha dodoma wanaamini mtu ambaye anaweza kutetea masilahi yao ni yule ambaye kazi yake nikusema ndio bwana mkubwa kwa mbowe.

  Mimi binafsi naweka imani yangu kwa mwanasiasa mwenye mawazo huru na ambaye hawezi kuburuzwa na mtu au kundi lolote. Najiuliza je hawa watu washawahi kusikia kuhusu joe lieberman wa democratic party aliyeenda kuhutubia katika mkutano wa kuzindua kampeni za republican party na kumpinga mgombea wa chama chake(obama wa democratic party).

  Labda mbowe kuna kitu anatakiwa kujifunza kutoka kwa obama au democratic party; obama anaelewa pale kura za chama chake hazitoshi ndani ya bunge mtu ambaye anaweza kumtumia kupata kura za wabunge wa republican ni joe lieberman(shibuda), kwasababu ameonekana mawazo yake yako huru.

  Kama kuna mtu yoyote ndani ya chadema ambaye anaweza kushawishi wabunge wa ccm wapige kura za ndio kwajambo ambalo chadema wanataka, basi mtu huyo ni shibuda.


  Watu wa shinyanga wametumia uhuru wao vizuri kuchagua mtu ambaye wanamtaka, lakini kuna watu wachache (mbowe na lema) wanataka kuwachagulia watu wa shinyanga kiongozi ambaye kazi yake itakuwa ni kujipendekeza kwa mbowe.

  Watu wa shinyanga wanajuwa shibuda anavyojitolea hasa ukizingatia chadema sio chama chenye uwezo kifedha. Tumemuona akitumia muda na hela binafsi kutatua matatizo ya watu wa maswa, iwe siasa (uchaguzi) au uchumi; hapa nazungumzia juhudi binafsi sio za chadema.


  Umefika wakati wa kukubali ukweli kwamba mbowe hana sifa wala busara za kujenga chadema imara, bora achaguliwe mtu mwingine (dr. Slaa).

  Tukumbuke ukiwa ndani ya chadema sio maana yake wewe sio fisadi, sio maana yake wewe ni msafi. Ukichunguza historia ya mbowe au lema unaweza ukakuta hawana tofauti na rostam azizi.

  Lazima tuwe makini nani tunampa madaraka ya kutuongoza. Tusiwape watu ambao wanatafuta nafasi za kufanya ufisadi. Mmesikia kuhusu ufisadi wa magari mitumba chadema.
   
 19. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #19
  May 5, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Kuna watu wanapewa kazi ambazo hawaziwezi,unajua kabla hujamuajiri mtu ni lazima umfanyie training? Naona JF inazidi kufurika
   
 20. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #20
  May 5, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  tunawajua, wala hambabaishi CDM. Mhe.Zitto na Mbowe songa mbele, achana na wapiga majungu-tunawajua.
   
Loading...