Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,941
- 9,947
mzee haijalishi; watakapochoka na matatizo na kuamua kweli wanataka kujiandaa kutawala wataamua la kufanya.
CHADEMA ndio imeshika moyo wa upinzani hapa nchini na wananchi wameweka matumaini juu ya Chama hiki. Wananchi wameiamini CHADEMA na kuipa wabunge lukuki kama ambavyo walivyoiamini NCCR-Mageuzi mwaka 1995. Kwa hiyo basi ni jukumu la CHADEMA kuienzi imani ya wananchi kwa kuwatumikia kwa uadilifu. Kinachotokea sasa kwa CHADEMA ni kama wamekuwa na muhemuko wa Madaraka. Kwa mfano kuna wabunge wachache sana ambao wanaojenga hoja ndani na nje ya bunge wengine ni ubabe tu na kukosa hoja. Ndani ya CHADEMA kumeanza kuonekana minyukano ya hapa na pale. Nimesikia na huko Mwanza nako hali si shwari, Shinyanga Shibuda naye ameondolewa kukaimu na ana kinyongo. Kuongezeka kwa ruzuku nako kunaleta sintofahamu ndani ya Chama. CHADEMA imeaminiwa kwa niaba ya wapinzani wote isipoangalia itaishia kuwa kama NCCR-MAgeuzi ya mwaka 2000 baada ya kunyukana. Na hii itakuwa ni pigo kubwa kwa Watanzania wote kwa kuwa watakosa imani kwa vyama vya upinzani. CHADEMA angalieni ndani ya nyuma kunaonekana kamoshi!