The Prophet
JF-Expert Member
- Mar 17, 2011
- 682
- 94
Vijana tunakiamini chama cha demokrasia na maendeleo,kwa namna kinavyosimama na kuibua na kuhoji mambo muhimu sana katika jamii yetu.
Hata wazazi wetu wanaamini chadema ndio kimbilio letu, licha ya wao kutuonya kuhusu kujitokeza mbele sana kwenye harakati za siasa, wakihofia usalama wetu.
Ila sasa viongozi wetu mnapoonekana kuvutana kwa ajiri ya tamaa za madaraka na ruzuku, ni aibu sana na ipo siku vijana wengi watafuatilia kiundani mambo ya chama chetu na ikiwa watabaini ukweli ulio tofauti na hisia zao, basi wataingia msituni kwani hawataamini mabadiliko kupitia chama cha siasa.
Ikiwa CHADEMA hakitabadilika kimtazamo, kisera na ki-organisation, hakuna mafanikio, nawaomba sana Mbowe, Slaa na Zitto kubalini kukaa na kushauriana.
I dnt understant wht the deal with uwenyekiti, tafadhali sana vijana vyuoni sasa wameanza kuhoji undani wa ugomvi wa Mbowe na Zitto kila wanapo onana.
Na ni kwa nini wanaonekana kutosikilizana hata kwa jambo la maana, tunajitahidi kujibu maswali magumu sana kutoka kwa vijana wasiojua CHADEMA, ila tunafanikiwa kuwatuliza na kuwapa moyo, ila wakati mwingine unajibu mtu na unaona haimwingii akilini.
Please msituumize kabisaaa.
ninakutunuku nishani maalum kwa kuwa memba wa kwanza mpya wa JF kuingia jamnvini na ku-post hoja yenye mantiki.