Abdulhalim
Platinum Member
- Jul 20, 2007
- 17,216
- 3,126
Nadhani wachangiaji wengi wame miss lengo la Kanisa Katoliki. Lengo lao sio kuwaelimisha wananchi kuhusu haki na namna ya kupiga kura. Lengo lao ni kuwaelimisha WAUMINI haki na namna ya kupiga kura. Waroma wanaamini kuwa Roman Catholic Church is the only true church. Kwa hiyo waumini hasa ni wafuasi wa kanisa katoliki. Ili kuhakikisha kuwa nchi inaendeshwa kwa mwelekeo wa kiumini kwa mujibu wa kanisa lao, basi ni lazima waumini wao wachague viongozi wa nchi kutokana na wao.
Naona hapa kuna kazi kubwa mno ya kuwaelimisha watu wenye kutaka kupotosha ukweli. Unasema watu wengi wame-miss lengo la kanisa katoliki yaani unasema haya kwa uhakika kabisa kana kwamba wewe ndiye uliyeanzisha na unaye-implement hilo lengo. Do you hera yourself mazee?
Halafu una hiyo sentensi niliyoi-bold, sasa sijui ni matatizo ya uelewa au ni chuki iliyozidi kipimo. Kanisa katoliki kutaka kuewaelimisha waumini wake imekuwa kero, je wangetaka kuwaelimisha waTz wote kwa ujumla si mngetangaza jihadi? Inashangaza kanisa katoliki linapojishughulisha na mambo mengine ya kijamii kama kujenga mashule, zahanati, n.k.hampigi kelele, ila linapokuja suala la uchaguzi kila mtu anang'aka kama paka anayenyonyesha aliyechukuliwa wanawe.
Huu ni mkakati wa muda mrefu wa Kanisa Katoliki tangu enzi za Nyerere na ndio maana mpaka sasa hajapatikana Rais mkristo ambaye si Mkatoliki.
Do you listen to yourself here? Yaani unataka kusema kanisa Katoliki lina mabavu kiasi cha kuamua nani awe rais na nani asiikaribie Magogoni...lol..this is too low. Sasa kama wana uwezo huo, how come mpaka sasa Mzee Mwinyi na JK ni waislam na wameikamata Nyumba Nyeupe? Huo mkakati ulifeli wapi mpaka hawa 'wageni' wakaikamata Ikulu? Halafu kama kweli kanisa katoliki lina mibavu kiasi hicho, kwa nini lisikae tu chini na kunywa mvinyo na badala yake sasa linahangaika kwa gharama zake kuwaelimisha waumini wake kuhusu medani za kushinda uchaguzi wakati tayari wanao uwezo wa kubonyeza kitufe tu na rais wanayemtaka anatokea?
Hii habari ya kanisa kufanya juhudi hizo kupinga ufisadi ni upuuzi mtupu kwani kanisa katoliki halina history ya kupinga ufisadi kwani limekuwa na matokeo mengi ya kifisadi na ufuska hasa kwa vijana wadogo wa kiume. Hata hapa hapa kwetu Tanzania mafisadi wamekuwa wachangiaji wakubwa wa kanisa.
Kwa mujibu wako, unasema kanisa katoliki halina historia ya kupiga vita ufisadi, fine enough..nikikuuliza takwimu au chanzo cha hii conclusion yako nitakuwa nakuonea, maana it is too big kwa mtu kama wewe..ninachotaka uniambie tu ni hiki..ni dhehebu lipi au dini nyingine ipi yenye hiyo historia ya kuushinda ufisadi ili tuweke vizuri rekodi zetu.
Ama kuhusu kuharibu watoto, this is one of the cheapest shots ambazo zimezoeleka kana kwamba kila child molester au pedofile ametumwa na kanisa katoliki au ni mkatoliki..sina sababu ya kukwambia ufanye research on this, maana this will be too much for you kwa sababu conclusion tayari unayo kichwani based on chuki.
Tatizo la sasa lililo sukuma kanisa katoliki kuamsha juhudi hizi ni baada ya kuona kuwa Rais Kikwete anajaribu ku balance uteuzi wa viongozi wa serikali kwa kuteuwa wakristo wa madhehebu zote na waislamu kwa uwiano badala ya kupendelea waroma kama ilivyokuwa huko nyuma. Sasa Kanisa Katoliki linaona limeanza ku loose grip ya utawala ukulinganisha na huko nyuma. Kwa hiyo solution kwa muono wao ni kuwahamasisha WAUMI wao kuchagua WAUMINI wenzao.
Sijaelewa hapa naona chuki imekufanya mpaka unaanzisha point halafu unaipinga mbeleni. Kama kanisa kaatoliki linao ubavu wa kumuweka mtu Magogoni sasa linashindwaje kuweka watu wake kwenye nafasi za uwaziri, manaibu, makatibu wakuu na watu wengine wa kada za chini ? Kuna logic yeyote hapa? Hakuna. Pili hilo la kuwachagua waumini wa dhehebu la kwao ni hoja muflis, ktk tanzania unapoomba kupigiwa kura sidhani kuna sehemu ya kujaza dhehebu hivo ni ajabu mtu mzima unaweza kukaa chini kubonyeza keyboard kuandika upupu kama huu.
Kwa hiyo madhehebu nyingine ya dini nayo yafanye hivyo kama yanaona hiyo ndio solution ya kuendeleza imani zao through kuakamata dola.
Kama kila mtu akiwa na mawazo kama yako, sidhani kama nchi yetu ingekuwa salama mpaka dakika hii. Sidhani kama imani yeyote Tanzania inaweza ikakua kwa kukamata Nyumba Nyeupe, ni jambo la kushangaza baadhi ya watu walivyo na mawazo ya hovyo kama haya.