Wapinzani wa nchi hii Uchaguzi huru na haki ni mpaka nyie mshinde? ACT- Wazalendo Konde mmeshinda kwa Tume gani ya Uchaguzi?

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
983
1,000

Hivi upinzani wa nchi hii Uchaguzi huru na haki ni mpaka nyie mshinde tu | Je! ACT- Wazalendo Konde mmeshinda kwa tume gani ya Uchaguzi? Hongera Rais Samia kwa kusimamia demokrasia nchini​

"Hakuna kama Samia "​


Upinzani wa nchi hii umekuwa ukipoteza sifa ( credibility ) siku baada ya siku kutokana na kauli na matendo ya viongozi wake pale uadilifu na uaminifu wao unapolinganishwa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi | Chama tawala yaani CCM ni kama mashariki na magharibi,

Upinzani wa Tanzania ukitaka kuwaamini hawaaminiki ukitaka kuwasikiliza wanapiga kelele,Ukiwahurumia wanasema umewaogopa kwa kifupi Wapinzani wa Tanzania hawajui wanataka nini,

Wakati Chadema wanasusia Uchaguzi kwa kisingizio cha Tume ya Uchaguzi Tanzania kuwa si huru wakati huohuo ACT Wazalendo wanashinda Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Konde huko Zanzibar kwa tume hii hii ya NEC|ZEC "nimazingaombwe haya"

Chaajabu zaidi,Upinzani wa Tanzania adui yake namba moja ni dola wala sio Umasikini wa Watanzania, wala sio maradhi ya Watanzania wala sio Ujinga wa Watanzania wao kutwa ni ligi na Rais, ligi na IGP, ligi na Msajili, ligi na spika kwa kifupi hawajui wanataka nini kwa nani na kwanini.

Kwa msiofahamu,Vyama hivi vimepoteza sana dira za vijana wengi kwa vijana hao kutokufahamu origin ya vyama hivyo kabla ya kujiunga, hebu fikiria Chadema ni matokeo ya Ugomvi baina ya Mwl Nyerere na Gavana Edwin Mtei ndio ikazaliwa Chadema wewe unayejiita kamanda Chama zao la mgogoro unadhani kitakufikisha au kitafika wapi kama sio migogoro kila siku? au Ugomvi wa Mbowe na Zitto ikazaliwa ACT-Wazalendo vyie Ngome ya Vijana kwanini mtumike kuchagiza gomvi za watu !? Is there any bright future kweli ACT | CHADEMA ?

Hivi kweli mtu aache kuchagua SGR toka Dar-Mwanza masaa 9,aache MW 2,115 toka JNHPP aache kuvuta Umeme kwa Tshs 27,000,aache chama kinachonunua ndege mpya 16,aache kuchagua chama kinachosomesha watoto wake wote bure,aache chama kinachotoa mikopo ya HESLB kwa wanachuo wote,aache chama kinachosimamia mikopo kwa riba ya 10%,aaache chama kinachosimamia bando kwa bei chee Africa nzima, aache chama kinachouza umeme chee Africa Mashariki yote ni $0.099/KWh leo achague hizo NGOs zenu kweli, don't waste your time bro's & sisters,

" Ukweli mchungu,Tanzania bado hakuna Chama mbadala wa CCM tukitegemee labda miaka ya 2060 "

#VIJANA NJOONI CCM TUMSAIDIE MAMA SAMIA KUJENGA NCHI TUNAJUA MNAZO NGUVU ACHENI KUCHAGIZA MIGOGORO YA WATU HUKO,

photo_2021-10-10_03-58-10.jpg


MBUNGE MTEULE ACT-WAZALENDO

ILA TUME NI ILEILE ISIYOHURU-ZEC
 

AGGGOT TZ

JF-Expert Member
Sep 14, 2018
735
500
Watanzania wameshawagundua kuwa ni wababaishaji hasa huku bara.

Tanzania Upinzani hakuna ila kunawapiganaji wa kusaka chochote.

Angalia maisha ya viongozi wao.

CHAMA NI CCM TU TANZANIA NA RAIS NI SAMIA
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
43,515
2,000
Rudi kwenye shule ya propaganda, hapa ni kama unapaka upepo rangi. Hiki sio kizazi cha ccm, kuendelea kukaa madarakani kwa shuruti hakuwasaidii.

Rejea idadi ndogo sana ya wapiga kura huko Ushetu ndio ujue hiki sio kizazi cha ccm. Maendeleo yanaletwa na kodi za watanzania sio mishahara ya wanaccm. Kama miradi ya maendeleo ni kigezo cha kukaa madarakani, makuburu wa Afrika kusini walipaswa kuwa madarakani mpaka leo.
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
43,515
2,000
Watanzania wameshawagundua kuwa ni wababaishaji hasa huku bara,
Tanzania Upinzani hakuna ila kunawapiganaji wa kusaka chochote,
Angalia maisha ya viongozi wao,

CHAMA NI CCM TU TANZANIA NA RAIS NI SAMIA

Kizazi kimeshaamka hiki, watu wamepuuza zoezi la uchaguzi maana matokeo yanabakwa ili kuweka viongozi majizi. Kuendelea kukaa madarakani kwa shuruti hakuwabebi, kila kizazi kina matakwa yake. Hiki sio kizazi cha nyimbo za Ottu jazz na Sikinde boss.
 

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
983
1,000
Rudi kwenye shule ya propaganda, hapa ni kama unapaka upepo rangi. Hiki sio kizazi cha ccm, kuendelea kukaa madarakani kwa shuruti hakuwasaidii. Rejea idadi ndogo sana ya wapiga kura huko Ushetu ndio ujue hiki sio kizazi cha ccm. Maendeleo yanaletwa na kodi za watanzania sio mishahara ya wanaccm. Kama miradi ya maendeleo ni kigezo cha kukaa madarakani, makuburu wa Afrika kusini walipaswa kuwa madarakani mpaka leo.
Ushetu,

Cherehani kura 106-CCM
Nkwambi kura 3,500 -ACT
 

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
983
1,000
Kizazi kimeshaamka hiki, watu wamepuuza zoezi la uchaguzi maana matokeo yanabakwa ili kuweka viongozi majizi. Kuendelea kukaa madarakani kwa shuruti hakuwabebi, kila kizazi kina matakwa yake. Hiki sio kizazi cha nyimbo za Ottu jazz na Sikinde boss.
Kwanini hamjashiriki Uchaguzi?
 

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
983
1,000
Kwa hiyo wananchi walewale ambao waliichagua CCM kwa kishindo katika uchaguzi huu huu ambao matokeo yake yalifutwa ndiyo sasa hivi wamegeuka na kuamua kuichagua ACT?😁😁😁
Ndio kwakuwa CCM tumebadili mgombea,

Kwenye ushindi mgombea anabeba 40% ya Ushindi
 

potokaz

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
440
500
Kwani 2015 zile kura 6m za Lowassa tume ilikuwa ipi?

Chadema lengo lenu sio nzuri kwa nchi tunajua
Nyie inabidi muombe mechi ya malumbamo ya HOJA Club House au Twitter Space.
Sometime mnaonekana kusimamia mambo ya kiujanjaujanja zaidi.
Inabidi tutoke huko.

Hivi wewe Ukaambiwa Kuna Mechi ya Simba na Yanga halafu Ukaambiwa Refa mi Manara. Hayo matokeo yatakuwa na uhalali kwa kiasi gani.
Yanakuwaje halali wakati Refa ana upande?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom