Jabali la Siasa
JF-Expert Member
- Jul 10, 2020
- 2,542
- 2,158
Hivi upinzani wa nchi hii Uchaguzi huru na haki ni mpaka nyie mshinde tu | Je! ACT- Wazalendo Konde mmeshinda kwa tume gani ya Uchaguzi? Hongera Rais Samia kwa kusimamia demokrasia nchini
"Hakuna kama Samia "
Upinzani wa nchi hii umekuwa ukipoteza sifa ( credibility ) siku baada ya siku kutokana na kauli na matendo ya viongozi wake pale uadilifu na uaminifu wao unapolinganishwa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi | Chama tawala yaani CCM ni kama mashariki na magharibi,
Upinzani wa Tanzania ukitaka kuwaamini hawaaminiki ukitaka kuwasikiliza wanapiga kelele,Ukiwahurumia wanasema umewaogopa kwa kifupi Wapinzani wa Tanzania hawajui wanataka nini,
Wakati Chadema wanasusia Uchaguzi kwa kisingizio cha Tume ya Uchaguzi Tanzania kuwa si huru wakati huohuo ACT Wazalendo wanashinda Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Konde huko Zanzibar kwa tume hii hii ya NEC|ZEC "nimazingaombwe haya"
Chaajabu zaidi,Upinzani wa Tanzania adui yake namba moja ni dola wala sio Umasikini wa Watanzania, wala sio maradhi ya Watanzania wala sio Ujinga wa Watanzania wao kutwa ni ligi na Rais, ligi na IGP, ligi na Msajili, ligi na spika kwa kifupi hawajui wanataka nini kwa nani na kwanini.
Kwa msiofahamu,Vyama hivi vimepoteza sana dira za vijana wengi kwa vijana hao kutokufahamu origin ya vyama hivyo kabla ya kujiunga, hebu fikiria Chadema ni matokeo ya Ugomvi baina ya Mwl Nyerere na Gavana Edwin Mtei ndio ikazaliwa Chadema wewe unayejiita kamanda Chama zao la mgogoro unadhani kitakufikisha au kitafika wapi kama sio migogoro kila siku? au Ugomvi wa Mbowe na Zitto ikazaliwa ACT-Wazalendo vyie Ngome ya Vijana kwanini mtumike kuchagiza gomvi za watu !? Is there any bright future kweli ACT | CHADEMA ?
Hivi kweli mtu aache kuchagua SGR toka Dar-Mwanza masaa 9,aache MW 2,115 toka JNHPP aache kuvuta Umeme kwa Tshs 27,000,aache chama kinachonunua ndege mpya 16,aache kuchagua chama kinachosomesha watoto wake wote bure,aache chama kinachotoa mikopo ya HESLB kwa wanachuo wote,aache chama kinachosimamia mikopo kwa riba ya 10%,aaache chama kinachosimamia bando kwa bei chee Africa nzima, aache chama kinachouza umeme chee Africa Mashariki yote ni $0.099/KWh leo achague hizo NGOs zenu kweli, don't waste your time bro's & sisters,
" Ukweli mchungu,Tanzania bado hakuna Chama mbadala wa CCM tukitegemee labda miaka ya 2060 "
#VIJANA NJOONI CCM TUMSAIDIE MAMA SAMIA KUJENGA NCHI TUNAJUA MNAZO NGUVU ACHENI KUCHAGIZA MIGOGORO YA WATU HUKO,
MBUNGE MTEULE ACT-WAZALENDO
ILA TUME NI ILEILE ISIYOHURU-ZEC