Wapinzani na wazalendo wa nchi hii anzisheni chama kipya chenye sura ya kitaifa mtafanikiwa kuungwa mkono na wananchi kipindi hiki muhimu sana!

sambulugu

JF-Expert Member
Jun 1, 2021
3,941
7,403
Nasema hivo kwa sabau zifatazo:.

•CCM imekuwa madarakani tokea kaundwa kwake mwaka 1977 na kwa sababu hiyo kutokana na hurka za wanadamu kimeonesha kupoteza ushawishi kadri siku zinavoenda.

•CCM kukosa sera au kupungukiwa mawazo mbadala kutokana na mfumo wake ila kwa sasbubu CCM inamuundo wenye sura ya kitaifa imekuwa ikikubarika katika maeneo mengi kutoka na wananchi kujisikia huru kukichagua hata kama hawakitaki au wamekichoka kwa kujihisi kuwa huru zaidi ukilinganisha na vyama vingine vyenye kukosa sura ya kitaifa!

•CHADEMA chama hiki kimekuwa na ukuaji mzuri ila kinachangamoto ya kuonekana na baadhi ya watanzania kuwa ni chama chenye chembechembe za ukabila na ukanda na kwa sababu hiyo kupoteza mvuto kwa baadhi ya watu katika jamii.

•CHADEMA imeonekana hususani katika siku za hivi karibuni kugeuka kuwa chama cha wanaharakati zaidi na kukosa sera madhubuti kwa ajili ya wananchi, hali hii imeadhiri sana ukuaji wa chama hiki kwa siku hizi!

•ACT WAZALENDO! ni chama kichanga lakini kinachangamoto ya kukosa sura ya kitaifa kwa kuegemea zaidi katika upande ya dini ya kiislam na kukifanya kupoteza mvuto katika maeneo mengi yasiyokuwa na waumimi wengi wa dini hiyo! Hili unaweza kuliona kwenye safu yake ya uongozi!

•ACT WAZALENDO ikumbukee kuwa ukuaji wake pia umechagizwa zaidi na mgogoro ndani ya chama cha CUF kwa hiyo bado ni chama kichanga sana hususani kwa tanzania bara!

•CUF ni chama kikongwe lakini kilichokosa ubunifu na kuibuka kwa migogoro ndani yake na kusababisa kusambaratika kwa wafuasi wake kwa kiasi kikubwa upande wa zanzibar!

•CUF ni chama kilichojiwekeza zaidi maeneo ya pwani na kukosa ushawishi wa kitaifa kwa miaka mingi kwa hiyo si chama chenye matumaini tena kwa watanzania kwa sasa!

PENDEKEZO
Nawaomba wazalendo na wapinzani wa kweli ndani ya nchi yetu wajitokeze ili kuunda chama kipya chenye sura ya kitaifa, na hili likifanyika mapema ili kuweza kukitamburisha kwa wananchi na ninauhakika kitatoa upinzani mkubwa sana kwa CCM 2025. Na kwa hilo tutapata serkali bora yenye kaundwa na watu wenye mawazo mseto kwa mustakabari mwema wa taifa letu!

HITIMISHO
Watanzania waliowengi wanasubiri sana chama kitakachowapa matumaini mapya katika kizazi hiki! Kuna na vyama vya upinzani vyenye sura ya kitaifa ni muhimu sana ili kufikia ndoto ya kuwa na demokrasia makini na chaguzi zenye ushindani. Naomba Mungu awabariki sana!
 
Act wazalendo ikija kuacha sera za kiislam itakuwa tegemeo kwa watanzania tofauti na sasa ambapo safu yake tu ya uongozi ni kama baraza la idd au kama chama cha muslim brotherhood cha misri kilichopigwa marufuku.
Mimi na watanzania wengine wazalendo tunasubiri ACT Wazalendo kiwe chama cha kizalendo kitoe matumaini mapya kwa watanzania.
 
Naunga mkono mkuu!
 
1. Utaifa ni nini?

2. Nikweli hakuna vyama vyenye sura ya kitaifa? Tanzania
Hapana! Kweli hatuwezi kupata kwa asilimia mia ila CCM imejitahidi ila pumzi imeisha hakina jipya tena kwa watanzania!
 
Hujajibu swali, usitake tupoteze mda hapa

1. Utaifa ni nini?

2. Nikweli hakuna vyama vyenye sura ya kitaifa? Tanzania
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Tuna haki ya kutofautiana kimawazo ndio mjadala wenyewe,wewe binafsi umeifanyia nini nchi hii kwenye wazo lako hili au ndio umejifungia kwenye comfort zone yako na familia Huku ukitaka wengine wakupiganie!middle class wa kitanzania waliojaa woga hadi kuogopa vivuli vyao.
 
Hujajibu swali, usitake tupoteze mda hapa

1. Utaifa ni nini?

2. Nikweli hakuna vyama vyenye sura ya kitaifa? Tanzania
Utaifa maana yake kinahusisha watu wa jamaa zote kwa ukubwa kwa mfano utamkuta mndengeko,mmasai ,mchanga n.k na pia mwislamu na mkiriston.k
 
Nasema hivo kwa sabau zifatazo:.
•CCM imekuwa madarakani tokea kaundwa kwake mwaka 1977 na kwa sababu hiyo kutokana na hurka za wanadamu kimeonesha kupoteza ushawishi kadri siku zinavoenda.
•CCM kukosa sera au kupungukiwa mawazo mbadala kutokana na mfumo wake ila kwa sasbubu CCM in

Hili wala sio jambo jipya bali ni mpango wa ccm unaoratibiwa na Tiss kuwa na chama kingine cha upinzani, kwani ccm inajua fika imechokwa na umma, bali inaona aibu kushindwa na Cdm. Mpango huu wa Tiss unalenga kuanzisha chama kipya kitakachofanya siasa zinazoendana na utashi wa kiccm.

Mpango huu ulivujishwa na wenzenu wenye kiherehere baada ya kutoka kwenye huo mpango. Kwenye kila Mtandao wa kijamii kwa sasa kuna huu ushawishi kuwa kianzishwe chama kingine nje ya ccm, kwani kinachoendelea kwa sasa kwenye chaguzi zetu ni aibu. Ccm haishindi tena kwa kura bali uporaji, na hawako tayari kushindwa na Cdm kwani kwa mtazamo wao ni chama cha kikanda.

Ni hivi, hiki mnachopanga kuanzisha nyie Tiss hasa nyie wenye mawazo ya kizee kimepitwa na wakati, kwani kizazi hiki sio cha kuchaguliwa mke. Kubalini tu kushindwa na Cdm, kisha ccm mjipange upya kwani mlishafanya kosa kuacha Cdm kuwa kikubwa hivi kilivyo, na kimeteka nyoyo za kizazi hiki. Hicho chama mtakianzisha lakini hakitapata watu na kuishia kuchezea fedha za umma tu. Hicho chama kinachosubiri hujuma ndio kianze, nadhani mnatarajia kianzishwe na mgogoro utakaotokea ndani ya ccm, na uzuri wanaccm wote hawana ushawishi tena kwa umma.

Cc: msemaji ukweli, paskali mayalla, BAK, misuli, bams, salary slip, joka kuu, nguruvi3, mag3, sky eclat
 
Hili wala sio jambo jipya bali ni mpango wa ccm unaoratibiwa na Tiss kuwa na chama kingine cha upinzani, kwani cc
Kwa hiyo hata mimi ni mwana CCM? sio kila anayetoa post hapa anamawazo ya kutumwa na CCM najua nimesema ukweli hivyo vyama vya upinzani vya sasa bado havina sura ya kitaifa!
 
Kianzisheni hicho chama mnangoja nini? Msubiri mpaka mmepoteza ushawishi ndio nyie nyie mje kwa mlango wa nyuma kutaka kutuanzishia chama ili kutunze uchafu wenu mliofanya kwenye nchi hii?

Sasa hivi watu hawajitokezi tena kupiga kura kwasababu mnashurutisha kubaki madarakani kwa mtutu wa bunduki. Mmeona hatari ya kuondolewa madarakani kwa machafuko, hivyo nyie nyie wachafu mnataka muanzishe chama fake kwa mlango wa uani ili kuendelea kutupiga. Kizazi hiki tunajitambua vilivyo, anzisheni hicho chama cha matapeli muone kama kitapata watu. Kwa sasa tunataka chama tunachokitaka, sio chama cha kuchomekewa na nyie wazee. Endeleeni kupora chaguzi, huku mkiua, kufanya ukatili, uhayawani na uchafu kama huo, lakini mjue mtatoka madarakani na watoto wenu.
Utaifa maana yake kinahusisha watu wa jamaa zote kwa ukubwa kwa mfano utamkuta mndengeko,mmasai ,mchanga n.k na pia mwislamu na mkiriston.k
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Nasema hivo kwa sabau zifatazo:.
•CCM imekuwa madarakani tokea kaundwa kwake mwaka 1977 na kwa sababu hiyo kutokana na hurka za wanadamu kimeonesha kupoteza ushawishi kadri siku zinavoenda.
•CCM kukosa sera au kupungukiwa mawazo mbadala kutokana na mfumo wake ila kwa sasbubu CCM inamuundo wenye sura ya kitaifa imekuwa ikikubarika katika maeneo mengi kutoka na wananchi kujisikia huru kukichagua hata kama hawakitaki au wamekichoka kwa kujihisi kuwa huru zaidi ukilinganisha na vyama vingine vyenye kukosa sura ya kitaifa!
•CHADEMA chama hiki kimekuwa na ukuaji mzuri ila kinachangamoto ya kuonekana na baadhi ya watanzania kuwa ni chama chenye chembechembe za ukabila na ukanda na kwa sababu hiyo kupoteza mvuto kwa baadhi ya watu katika jamii.
•CHADEMA imeonekana hususani katika siku za hivi karibuni kugeuka kuwa chama cha wanaharakati zaidi na kukosa sera madhubuti kwa ajili ya wananchi, hali hii imeadhiri sana ukuaji wa chama hiki kwa siku hizi!
•ACT WAZALENDO! ni chama kichanga lakini kinachangamoto ya kukosa sura ya kitaifa kwa kuegemea zaidi katika upande ya dini ya kiislam na kukifanya kupoteza mvuto katika maeneo mengi yasiyokuwa na waumimi wengi wa dini hiyo! Hili unaweza kuliona kwenye safu yake ya uongozi!
•ACT WAZALENDO ikumbukee kuwa ukuaji wake pia umechagizwa zaidi na mgogoro ndani ya chama cha CUF kwa hiyo bado ni chama kichanga sana hususani kwa tanzania bara!
•CUF ni chama kikongwe lakini kilichokosa ubunifu na kuibuka kwa migogoro ndani yake na kusababisa kusambaratika kwa wafuasi wake kwa kiasi kikubwa upande wa zanzibar!
•CUF ni chama kilichojiwekeza zaidi maeneo ya pwani na kukosa ushawishi wa kitaifa kwa miaka mingi kwa hiyo si chama chenye matumaini tena kwa watanzania kwa sasa!
PENDEKEZO
Nawaomba wazalendo na wapinzani wa kweli ndani ya nchi yetu wajitokeze ili kuunda chama kipya chenye sura ya kitaifa, na hili likifanyika mapema ili kuweza kukitamburisha kwa wananchi na ninauhakika kitatoa upinzani mkubwa sana kwa CCM 2025. Na kwa hilo tutapata serkali bora yenye kaundwa na watu wenye mawazo mseto kwa mustakabari mwema wa taifa letu!
HITIMISHO
Watanzania waliowengi wanasubiri sana chama kitakachowapa matumaini mapya katika kizazi hiki! Kuna na vyama vya upinzani vyenye sura ya kitaifa ni muhimu sana ili kufikia ndoto ya kuwa na demokrasia makini na chaguzi zenye ushindani. Naomba Mungu awabariki sana!
Umeongea pumba.
 
Hiyo ACT ilianzishwa na genge la kina JK, Membe, Mwigulu nk. Lengo ilikuwa ni kuipa backup ccm iliyozidiwa nguvu na Cdm. Kwa bahati mbaya kizazi cha sasa kinakubali Cdm kuliko chama kingine chochote cha upinzani. Na ccm haiko tayari kushindwa na Cdm kwani ni aibu sana kwake.

Kwa bahati mbaya Magufuli alipoingia madarakani hakuwa na uwezo wa siasa za ushawishi zaidi ya kutumia Maguvu. Pia hakuwa na mahusiano mazuri na kundi la JK, hivyo alitupilia mbali mipango karibia yote ya JK. Hii ilisababisha mpango wa kuinyanyua ACT dhidi ya Cdm ufe pia. Hiki kitendo cha ACT kufaidika na mgogoro wa CUF na kuchukua mahasimu wa kisiasa wa ccm huko Znz kumefanya mpango huo uwe njia panda. Hivyo namna pekee ni TISS kwa kushirikiana na ccm, kuwa na mpango wa kuanzisha chama kingine cha siasa, lakini kwa bahati mbaya, ccm na hao tiss wanaojiita system wamepoteza ushawishi kwa umma,na Cdm imeendelea kubaki mioyoni mwao vijana wa kizazi hiki. Hivyo kinachofanyika hivi sasa ikiwemo Mbowe kubambikiwa kesi ni ili kuiua Cdm, kisha kianzishwe chama kingine ili kichukue nafasi ya wafuasi wa Cdm, halafu chama hicho kifanye siasa kwa utashi wa ccm. Ni kama ccm inajiribu kurudi kwa mlango wa nyuma. Kwa matarajio yako ACT kuwa kubwa au kubadilika ni ngumu, maana ushawishi wake ni mdogo. Namna pekee ya kubadili upepo ni kuifuta Cdm kwani kawa sasa ni zaidi ya chama, na imekuwa imani.

Back
Top Bottom