Wapinzani na wazalendo wa nchi hii anzisheni chama kipya chenye sura ya kitaifa mtafanikiwa kuungwa mkono na wananchi kipindi hiki muhimu sana!

Nasema hivo kwa sabau zifatazo:.
•CCM imekuwa madarakani tokea kaundwa kwake mwaka 1977 na kwa sababu hiyo kutokana na hurka za wanadamu kimeonesha kupoteza ushawishi kadri siku zinavoenda.
•CCM kukosa sera au kupungukiwa mawazo mbadala kutokana na mfumo wake ila kwa sasbubu CCM inamuundo wenye sura ya kitaifa imekuwa ikikubarika katika maeneo mengi kutoka na wananchi kujisikia huru kukichagua hata kama hawakitaki au wamekichoka kwa kujihisi kuwa huru zaidi ukilinganisha na vyama vingine vyenye kukosa sura ya kitaifa!
•CHADEMA chama hiki kimekuwa na ukuaji mzuri ila kinachangamoto ya kuonekana na baadhi ya watanzania kuwa ni chama chenye chembechembe za ukabila na ukanda na kwa sababu hiyo kupoteza mvuto kwa baadhi ya watu katika jamii.
•CHADEMA imeonekana hususani katika siku za hivi karibuni kugeuka kuwa chama cha wanaharakati zaidi na kukosa sera madhubuti kwa ajili ya wananchi, hali hii imeadhiri sana ukuaji wa chama hiki kwa siku hizi!
•ACT WAZALENDO! ni chama kichanga lakini kinachangamoto ya kukosa sura ya kitaifa kwa kuegemea zaidi katika upande ya dini ya kiislam na kukifanya kupoteza mvuto katika maeneo mengi yasiyokuwa na waumimi wengi wa dini hiyo! Hili unaweza kuliona kwenye safu yake ya uongozi!
•ACT WAZALENDO ikumbukee kuwa ukuaji wake pia umechagizwa zaidi na mgogoro ndani ya chama cha CUF kwa hiyo bado ni chama kichanga sana hususani kwa tanzania bara!
•CUF ni chama kikongwe lakini kilichokosa ubunifu na kuibuka kwa migogoro ndani yake na kusababisa kusambaratika kwa wafuasi wake kwa kiasi kikubwa upande wa zanzibar!
•CUF ni chama kilichojiwekeza zaidi maeneo ya pwani na kukosa ushawishi wa kitaifa kwa miaka mingi kwa hiyo si chama chenye matumaini tena kwa watanzania kwa sasa!
PENDEKEZO
Nawaomba wazalendo na wapinzani wa kweli ndani ya nchi yetu wajitokeze ili kuunda chama kipya chenye sura ya kitaifa, na hili likifanyika mapema ili kuweza kukitamburisha kwa wananchi na ninauhakika kitatoa upinzani mkubwa sana kwa CCM 2025. Na kwa hilo tutapata serkali bora yenye kaundwa na watu wenye mawazo mseto kwa mustakabari mwema wa taifa letu!
HITIMISHO
Watanzania waliowengi wanasubiri sana chama kitakachowapa matumaini mapya katika kizazi hiki! Kuna na vyama vya upinzani vyenye sura ya kitaifa ni muhimu sana ili kufikia ndoto ya kuwa na demokrasia makini na chaguzi zenye ushindani. Naomba Mungu awabariki sana!
We pimbi badala ya kuja na mkakati wa kupata katiba mpya Ili domorasia ipanuke zaidi Ili vyama viwe huru kufanya siasa vitanue viwe vya kitaifa

We unaleta blah blah tu
 
Hiyo ACT ilianzishwa na genge la kina JK, Membe, Mwigulu nk. Lengo ilikuwa ni kuipa backup ccm iliyozidiwa nguvu na Cdm. Kwa bahati mbaya kizazi cha sasa kinakubali Cdm kuliko chama kingine chochote cha upinzani. Na ccm haiko tayari kushindwa na Cdm kwani ni aibu sana kwake.

Kwa bahati mbaya Magufuli alipoingia madarakani hakuwa na uwezo wa siasa za ushawishi zaidi ya kutumia Maguvu. Pia hakuwa na mahusiano mazuri na kundi la JK, hivyo alitupilia mbali mipango karibia yote ya JK. Hii ilisababisha mpango wa kuinyanyua ACT dhidi ya Cdm ufe pia. Hiki kitendo cha ACT kufaidika na mgogoro wa CUF na kuchukua mahasimu wa kisiasa wa ccm huko Znz kumefanya mpango huo uwe njia panda. Hivyo namna pekee ni TISS kwa kushirikiana na ccm, kuwa na mpango wa kuanzisha chama kingine cha siasa, lakini kwa bahati mbaya, ccm na hao tiss wanaojiita system wamepoteza ushawishi kwa umma,na Cdm imeendelea kubaki mioyoni mwao vijana wa kizazi hiki. Hivyo kinachofanyika hivi sasa ikiwemo Mbowe kubambikiwa kesi ni ili kuiua Cdm, kisha kianzishwe chama kingine ili kichukue nafasi ya wafuasi wa Cdm, halafu chama hicho kifanye siasa kwa utashi wa ccm. Ni kama ccm inajiribu kurudi kwa mlango wa nyuma. Kwa matarajio yako ACT kuwa kubwa au kubadilika ni ngumu, maana ushawishi wake ni mdogo. Namna pekee ya kubadili upepo ni kuifuta Cdm kwani kawa sasa ni zaidi ya chama, na imekuwa imani.
Mkuu hawawezi fanikiwa, cdm otadumu na 2025 inachukua dola
 
Back
Top Bottom