Ndio nashangaa! Eti double agent! Chaaaa! Alianza lini hiyo kazi?! Maana kama ni uhalifu anaohusishwa nao wa kwenye hayo masuala ya almasi sidhani kama umefanywa kwenye hiki kipindi kifupi cha Magufuli (ndio tuseme Magufuli alimtuma).
Hata hivyo mtu unajiuliza, u-double agent ni kwaajili ya kwenda kubomoa kabisa, au ni kwaajili ya kutoa taarifa mapema ili uharibifu usitokeee?! Sasa mtu kama alikuwa huko mda anafanya huo u-double agent wake ambao umeishia kulitia taifa hasara kubwa na kuendelea kulichakaza kwa umaskini?!!!! Hiyo intelijinsia aliyoikusanya wakati huo kwanini asingeitoa kwa wakati ili kulinusuru taifa na umaskini?!