Hapa ndipo ninapochoka, hebu Mkuu kisu tueleze 6 na Mwakyembe wanapigania nini ndani ya CCM ? Kuna usemi wa kiingereza unaosema,
when the going gets tough, the tough keep going ikiwa na maana kuwa shujaa utamtambua kwa matendo na si maneno. Tumeshuhudia kwa macho yetu hao jamaa wanvyofyata mikia yao mambo yanapowawia magumu na wanavyokosa ujasiri wa kutetea misimamo yao wanapowekwa kiti moto kwenye viako vya CCM.
Mwakyembe alifunika kombe mwanaharamu apite aliopoamua kuwakilisha ripoti ya Richmond isiyo kamilifu kwa lengo la kuisetiri serikali na si mara moja alipobanwa ameshindwa kukiri mapungufu dhahiri ya Kikwete na badala yake kumsifia. Sitta kwa upande wake alionyesha woga wa hali ya juu alipoamua kuufunga mjadala wa Richmond ili kuwapa ahueni viongozi wa juu wa serikali wasiumbuke. Hapana hawa wawili wameonyesha udhaifu mkubwa wanapokabiliwa na maamuzi mazito.
Bila shaka yoyote walichukua maamuzi hayo ili kulinda maslahi yao na pia kuendeleza tabia ya CCM ya kulindana na hawana tofauti yoyote na viongozi wengine humo ndani. Hakuna hata moja kati yao, kwa mfano, aliyelalamikia kitendo cha uongozi wa juu wa CCM kuwapigia kampeni vinara wa ufisadi katika uchaguzi uliopita. Hii peke yake yatosha kutuaminisha kuwa hawaoni tatizo lolote na watu hao ikiwa na maana kuwa wote ni wachafu kwani wanaogelea kwenye dimbwi moja hilo hilo lililochafu.
Hapana wanaochukia uchafu njia iko moja tu, kutoka na kuoga wasije wakanuka !