Hapa lazima niwe mkali kwa wasioona mchango wa wapiganaji. Hawa wapiganaji ni "outliers" ndani ya CCM, na kama ninavyofahamu mimi, outliers siku zote, pamoja na kuwa zinaweza kuwa chache lakini effect yake ni kubwa na inahitaji uchambuzi wa kina. Pengine mjaribu kufanya "sensitivity analysis" kuona kama hawa wapiganaji (outliers) wasingekuwepo kabisa hali ingekuwaje? Richmond leo zingekuwa ngapi? Wizi kutoka E.P.A leo ungekuwa umefikia bil.ngapi? Mwanakijiji na wenzio, mmewahi kujiuliza kama leo Mwalimu angekuwepo (MUNGU amrehemu), mambo tunayoyaona leo kwa mfano nyaraka, zingekuwepo? Kwani Mwalimu hakuwa mwana CCM? Hii ndiyo sensitivity analysis mnayotakiwa kufanya. Mimi nadhani mnahitaji kulaaniwa kwa kukosa busara. Walioanzisha harakati za kudai uhuru wa nchi hii ni wakuhesabu, na si ajabu wapo waliowapinga kama mwanakijiji na wenzio, kwani leo uhuru hatuna? Mandela alikaa jela zaidi ya miaka 20, wengi walimuona kama mwendawazimu ku-sacrifice maisha yake, leo ni mmoja kati ya watu wanaoheshimika duniani, mwanakijiji, si ajabu hata hujawahi kushikana naye mkono tu! Mimi nasema, sidanganyikiii, ukombozi wa nchi hii toka mikononi mwa mafisadi utaletwa na wachache kama walivyoanza outliers.
Keen,
Wapiganaji unaowatetea wamelala Usingizi. Kama wangekuwa macho na makini, wangeona mapungufu ya Serikali na Chama chao kabla ya sisi kuanza kuhoji kilichotokea.
Binafsi, mimi ni mmoja wa watu wa kwanza walioanza kuhiji mkataba wa Richmond ulipotokea mwaka 2005/2006. Niliuliza kwa kina mantiki ya kuingia mkataba na kampuni ya Kimarekani ambayo ilikosa mkopo Marekani na hivyo kwenda kuomba kibali Ikulu ili CRDB iwape mkopo.
Hayo ya Richmond, niliyasoma kwenye magazeti ya Tanzania na nikaanza kuhoji wazi mpaka pale "Wapiganaji" walipoamka na kuanza kujidai kuwa nao ndio wanalifanyia kazi na wakati walipozinduka ilikuwa miezi 18 baada ya mimi kuandika kwa mara ya kwanza kuhoji na kulifanya ni jambo la kuzungumziwa kwenye hizi kumbi!
Njoo jambo la BOT; EPA, Meremeta, Kagoda na kila ovu BOT. Ni sisi tulioshikia bango suala hili la Uhujumu na aliyetupa nguvu na kuutangazia umma tulichokuwa tukikizungumzia alikuwa ni Dr. Slaa na si Mwakyembe au Kimaro!
Ufisadi wa Radar, Ndege ya Rais, ATCL, TRL, Dawasco, Madini na mwingineo uliotokea katika miaka mitano iliyopita ni sisi jamii za JF, Young African na hata zama za BCS, ndio tulioanzisha vuguvugu la kutaka Serikali yetu iamke na kufanyia kazi uhujumu.
Kundi la kina Mwakyembe limeanza kujitutumua na kufanya hoja ya Ufisadi kuwa ni yao baada ya Bunge la mwezi Novemba 2007 walipopewa mamlaka ya kuchunguza suala la Richmond.
Hivyo kwa anayedai kuwa kina Mwakyembe ndio wapewe sifa na tuzo na si Pundit, Moelex, Mwanakijiji, Mkandara, Kishoka, Fair Player, FMES, Kichuguu, Bin Maryam, Kitila Mkumbo, Nyani Ngbu, Kuhani, GT na wengine wengi humu ndani hususan Invisible, na Kanzi, na Manzi wengine waliohatarisha ajira na uhai wao kwa kutoa nyaraka za siri kama mkataba wa Buzwagi, utakuwa huwafanyii haki!
Niliowataja hapo juu, ndio wapiganaji wa kweli, hata kama mtasema mbona hatuwajui majina yao ya ukweli.
Wapiganaji wa JF hawakimbili majukwaa na kutaka sifa au tukuzo au kuudanganya umma kuwa wao ndio pekee wenye haki ya kuongelea Ufisadi.
Wapiganaji wa JF, Young African, KLH News ni watu ambao hawafungamani na Chama au kutaka kazi zao ziwe za chama kimoja, bali ni watu ambao wanataka kila aliye kiongozi wa Tanzania alitumikie Taifa la Tanzania kwa manufaa ya Watanzania ili kuleta maendeleo kwa kila mtu na si kauli kwenye majukwaa.
Ndiyo maana binafsi, nakataa kulaghaiwa na hizi sifa kuwa "Wapiganaji Wabunge" wa CCM wana nia ya kuleta maendeleo kwa Tanzania!