'Wapiganaji' walioko CCM wanapigania nini hasa?

Wakuu zangu,
Waacheni wapiganaji waifanye kazi yao..mimi sioni tatizo liko wapi..Yawezekana mimi nakosea lakini ndivyo vita inavyopigana..Mafisadi wanahitaji mashambulizi toka pande zote nje na ndani ndipo tunaweza kufanikiwa kwani hasira ya wananchi sio kwa chama CCM kama chama, isipokuwa viongozi wabovu waliomo ndani ya chama CCM...Chama ni watu.

Tukumbuke tu kwamba hata wakati wa kumwonda Hitler kulikuwepo na wapiganaji toka ndani ya utawala wake wakiitwa resistance group, hawa ndio waliofanya kazi kubwa ya kumwangusha Hitler ktk kila utawala alochukua iwe France, Urusi, na kwingineko.. Majeshi ya nchi za nje yalipokuwa yakiingia yalipata taarifa na sehemu na nyaraka za siri za Hitler hivyo kurahisisha mashambulizi.. kazi ambayo imekuwa ikifanyika kwa muda mrefu sasa hivi nyumbani kiasi kwamba Mafisadi wanahaha!.

Binafsi Mwanakijiji kama mpiganaji akijiunga na CCM na kuahidi kuwaangusha Mafisadi nitamtazama sawa na mgombea mwingine maadam imani yangu ni huyu mwanakijiji na kile anachokisimamia. Chadema, TLP au CUF haina maana hakuna mafisadi ndani ya vyama hivyo, wapo wengi tu isipokuwa tunachoomba ni utawala mzima kutokuwa wa kifisadi hivyo agenda za watu binafsi zitakosa nafasi.

Tumeyaona nchi za jirani kama Zambia, Malawi na Kenya ambako mafisadi wametokea vyama ambavyo havikutegemewa kabisa kwani fisadi ni mtu sio chama. Kwa maana kubwa nasema hivi mchafu wa tabia ni binadamu sio dini yake. Mkandara hapa kam ni jambazi basi nafanya Ujambazi sii kwa sababu mimi ni mkristu au Muislaam ati nilibadili dini nitabadilika...hjapana kinachotakiwa ni mimi kuokoka na kazi kubwa ya jumuiya ni kumweka Lupango Mkandara iwe hata ndugu yangu akipiga simu Polisi nikakamatwa huo ndio uzalendo.

Mafisadi ni WATU, tafsiri nyingine nje ya imani hiyo mimi siikubali pamoja na kwamba naweza kuwa nimekosea sana. Sidhani kama CCM inawafundisha wanachama wake kuubeba Ufisadi ila kuna kundi la watu ndani ya CCM wanaoukumbatia.. na hakuina njia bora zaidi ya kuwakosesha nguvu hawa jamaa ila kuwaondoa ktk madaraka, kesho watajipanga upya wakifahamu sababu iliyowaangusha. Tumeyaona KANU, ZAPU, na vyama vinginevyo vilivyotangulia ktk nchi za jirani.

Nakubaliana na Mkuu Mkandala kuwa mafisadi ni watu na sio chama. Ukiangalia sera za chama cha mapinduzi ASILIA utaona kuwa kilikuwa kinajali sana watu na maendeleo yao na sio fedha kama ilivyo sasa; na kama mnakumbuka mpaka mwalimu alidiliki kusema FEDHA SIO MSINGI WA MAENDELEO. Hivyo kama ndivyo basi ni vizuri chama cha mapinduzi kikajisafisha kwa kuwaondoa mafisadi katika chama ili kiwezekuendeleza sera zake za kuwajali na kuwaletea maendeleo wanannchi. Tukirejea mfano aliotoa Mwanakijiji wa tenga la matunda, hilo tenga kama lina matunda mazima na yale mabovu, ukiwa kama mfanyabiashara utachukua hatua gani? Nadhani itakuwa sahihi kwa kuyaondoa matunda mabovu ili ubakie na matunda ambayo hayajaharibika ama sivyo yote yataharibika; kwahiyo basi kwa misingi hiyo hiyo ya tenga la matunda CCM ili ikiokoe chama haina budi kuwafukuza wanachama wote wanaohisiwa na pia kuthibitika kuwa mafisadi na kuwaacha wanachama safi kuendelea na chama chao na hii naona ndio sababu kubwa inayowafanya hawa wapambanaji wabakie humo walimo.!!
 
Mimi niliwahi kusema kuwa Vita vya ufisadi sio ya CCM, wao walidandia hoja kwa mbele kwa ajili ya politica agenda na sio yao. Walikuwa wapi siku zote mpaka pale CHADEMA walisema na kuanza NEno( UFISADI) mwasisi wa neno hili ni Dr Slaa na Tindu Lissu!! Nakumbuka ndugu yangu Mabere Marando alikuwa ana hojiwa na ITV alisema" Wale ambao watapewa kibao na CCM kwa ajili ya kupambana na ufisadi basi CCM pamoja na Kamati zao watoe kibano vizuri ili watoke huko" ni kweli kabisa. CCM ndio wapo Tenga moja. Wana agenda zao za siri na hawa, wanadanganya watu, Tazama hata Kesi Za EPA na madudu mengine, yako wapi leo KAGODA???? Mbona kimnya
 
Wapiganaji Sio Mwanzilishi wa Neno Ufisadi miongoni mwa Watanzania. Mimi nawaona kama vile wasaliti wa umma wa Tanzania. Leo wanaibuka na kusema hivyo je walikuwa wapi siku zote mpaka vita ile ianzishie Mwenye yanga Temeke 2007..!! CHADEMA ndio waanzilishi wa vita hii .. hivyo leo kama kuna mitafaruku katika CCM basi wameyataka haya kwa kuwa wao wanajua kuwa walikuwa wanafanya hivyo kwa leo gani na kwa ajili ya nani?? Leo inakuwa ngumu kucheza ngoma ya ukae** ngoma ya asili wakati wewe mwenyewe ndio muhusika..!!
 
Mzee Mwanakijiji, hao makamanda dhidi ya ufisadi wamegawanyika makundi mawili, miongoni mwao wamo wanapinga ufisadi kwa sababu wanauchungu wa dhati na umasikini wa Watanzania ambao ufisadi umechangia kuongezeka kwa umasikini na unaendelea kuitafuna nchi na utaendelea kwa miaka kadhaa ijayo.

Kundi la pili ni la wapinga ufisadi wanaopigania nafsi zao, wanahasira kwa sababu nao wanataka share yao kwenye huo mkate na nafasi zikiwakalia vazuri, nao watafisidi vile vile hivyo nawaweka kundi moja na mafisadi tuu.Kwa mtazamo huo kuna makamanda wenye uchungu na makamanda mafisadi.

Swali ni jee ndani ya CCM, wanapigania nini?. Jibu langu la jumla ni kuwa wanapigania nafsi zao just for survival na wakishapata uhakika wa survival baada ya 2010, mtawashuhudia nao wakifisidi ushahidi ni 'time will tell'.

Kitu kibaya zaidi kuhusu baadhi ya hawa makanda ambacho mtakishuhudia ni kwa baadhi yao kuwapigia magoti mafisadi ili kuwanusuru na panga la CCM kupitishwa kugombea 2010 na wakishapitishwa, wataungana na kuwa kitu kimoja kwa ajili ya kuweka mikakati ya 2015.

Baadhi watakao piga magoti ni wale ambao nguvu ya mafisadi kuhakikisha hawateuliwi na CCM kugombea itatumika, na wakisha toswa na CCM, watatamani kukimbilia upinzani sio ili kuendeleza mapambano, bali kujaribu kuokoa mkate wao wa kila siku na nawahakikishieni, kama mafisadi watamwaga fedha kuhakikisha makamanda hawapiti, na wakihamia upinzani, ndio kwanza sasa chama kitamwaga mapesa zaidi kuhakikisha hakishindwi.

Baadhi ya makamanda watapigwa chini na hapo ndipo itakuwa mwisho wa habari yao, kitakachofuatia ni kwenda kuwalamba miguu mafisadi kwa kurejea CCM wakiwa wametahayari kama alivyofanya yule kinara wa kundi la G-55.

Hizi harakati za kujipambanua kwa pamoja na kuzungukiana majimbo ya wapiganaji zamu kwa zamu huku wakitoa michango ya shilingi 500,000 walizopewa na mshitiri, wakisindikizwa na ka 'kipindi maalum' ndani ya taarifa za habari (no 10min news clip) ya kwenye TV ya mshitiri, hizi ni nyimbo tuu za shangwe na mapambio ya kujinusuru na panga la uteuzi wa CCM mwaka 2010, baada ya hapo kutakuwa hawana hili wala lile.

Sibezi juhudi za makamanda, bali mbinu zilizotumika kuwapambanua bungeni tukianzia kwenye ripoti ya Richmond iliyotumika kumchapa bakora EL kwa kumuhukuma bila kupewa fursa ya kusikilizwa, hivyo ukamanda wao unapimwa ni kwa kiasi gani wanaweza kuzungumza kwa jazba na mapokezi makubwa makubwa kuashiria wananchi wanawakubali.

Wapiganaji wa kweli ni wale ambao wako tayari to take risk kwa kusimama mbali na uvundo kuwathibitishia watanzania kuwa huku tuliko chama kimetekwa na mafisadi, hivyo baada tuu ya kuvunjwa Bunge mwakani, wataonyesha waliposimama na wananchi watawachagua kwenye chama chochote watakacho simama nacho na hawa ndio watakuwa wapiganaji wa kweli kweli.

Wale makamanda wanaopigania nafsi zao, mtawatambua kwa kutokubali kurski nafasi zao ndani ya CCM ambako mafisadi wana upper hand. Hawa watasubiri mpaka watakapo temwa na CCM ndipo waje upande wa pili kujaribu kamari ya upinzani, hawa ndio watakao kwenda na maji kwa sababu upinzani Tanzania ni kwenye baadhi tuu ya maeneo, kuna maeneo mengi CCM inachaguliwa sio kwa sababu imekubalika sana, bali kwa sababu ya mazoea tuu na kukosekana kwa elimu ya uraia.

Kuna sehemu hata akisimamishwa mgombea kiazi vipi, atapita tuu.Kwa vile CCM ina wenyewe, na baadhi ya wenyewe hao ndio hao hao mafisadi na wengine wao ndio hao makamanda, hapa ni mwendo wa mwenye kisu kikali ndie anayekula nyama, na ili ukubaliwe kula nyama ni lazima uchague upande, either with us, or against us, maadamu wenye guvu ni mafisadi, mwenye nguvu mpishe, hao makamanda watajikuta kuliko kuriski loosing, wakijua hawawezi kuwashinda, watatumia formular ya 'if you can't beat them, join them' watajiunga nao na wote wakuwa kwenye tenga moja la samaki, na wote watakuwa ndio hao hao.
 
Last edited by a moderator:
Naungana mkono na MwanaVillage.....!!!
Tunazugwa Watanzania hakuna mpinga ufisadi ndani ya CCM...Hivi hawa kina Selelii,Sendeka,Kilango na wengine kwanini wasiseme hadharani kwenye vikao vya NEC....??Yaani wanakuwa wakali nje ndani wanakaa kimya....Wakati Spika Sitta anasulubiwa kule Dodoma wao walikuwa wapi kumtetea,walikaa kimya wakimwacha mzee mzima anaumia...
Anyway suala ni kwamba wote wao wamebebwa na Ufisadi co ni vigumu kuupinga..CCM ndio baba yao na ndo nyumba ya mafisadi.
2po pamoja wapiganaji woote....
 
PAsco, Hawa Makamanda dhidi ya ufisadi ni kweli wana nia ya dhati?? Je ni kwanini huwa wanawashambulia watu kama wakina Dr. Slaa na wengine walio wengi katika CHADEMA, tutakuta wao ndio watu wa kwanza kwenda kuwapigia Kampeni mafisadi katika majimbo yao. Vita hii sio yao na haifanani kabisa na CCM
 
Bila ya kuubomoa mfumo wa utawala wa kifisadi uliowaunda. tunaweza vipi kuwaondoa mafisadi wa sasa na kuwazuia wa baadaye?
 
Naungana Kabisa na Mzee wangu Mwanakijiji, Utaona mwakani Ngojera ya nyimbo ya ufisadi ndio itazidi kupamba moto kila upande, ila kwa kusema ukweli hata hizi kesi ni Danganya toto tu, maana hakuna dhamira ya kweli kwa ajili ya kutokomeza, Ila kama kama wana nia ya dhati iweje leo wabaki wanagombana na mtu ambaye wanaye ndani ya CHama chao?? je ni kwanini kama kweli wana nia ya dhati wangefukuzwa uanachama haraka sana.. Je mzee Mwanakijiji umesahau kuwa yale ya Butiamu na kubaki midomo wazi?? Je walikuwa wapi kipindi chote?? Kama tuna system ambayo ni corrupt kama hivi kila mtu atakuwa analinda maslahi yake, Hata hawa Makamanda baada ya kuona wakina Zitto na Slaa wanajenga umaarufu kupitia ufisadi na sasa wai wamegeuza mwimbo wao, Lakini siku zote Vita hivi hawawezi kupigana wao hata siku moja. Tazama trend ya Bunge toka kwa kusimamishwa kwa Kabwe Zitto. Ndio nao wakaanza kucheza ngoma ambayo sio yao.
 
Bila ya kuubomoa mfumo wa utawala wa kifisadi uliowaunda. tunaweza vipi kuwaondoa mafisadi wa sasa na kuwazuia wa baadaye?

MMKJJ, kwanza baada ya kukubali ufisadi ndio mfumo unaounda utawala wetu wa sasa, yaani ni system, halafu tunataka kugombea kisu huku walioshika mpini ndio hao hao, unategemea nini?.There is always one and only way ya kuchange system, system kamwe haibadiliki, lazima ibadilishwe, kama system imeundwa na mafisadi na kuendeshwa na mafisadi ili kuzidi kufisidi, hao wa kuibadilisha ni kina nani kama sio kutaka kuja kuibadilisha ili wapokezane zamu za kufisidi, na unawazuiaje mafisadi wa baadae wakati wengi wa wanasiasa wetu wanaingia kwenye siasa kama ajira kupigania nafsi zao?.Wanatakiwa wapatikane watu wa Calibre ya Dr. Slaa wengi wa kutosha na sio hao waimba mapambio kwa jina la makamanda.Hapa inatakiwa kitu kama the 'Bolshevic ya Octoba 1917' ama 'The American ya 1886' vinginevyo ni tunacheza makida makida.
 
Wakuu zangu,
Waacheni wapiganaji waifanye kazi yao..mimi sioni tatizo liko wapi..Yawezekana mimi nakosea lakini ndivyo vita inavyopigana..Mafisadi wanahitaji mashambulizi toka pande zote nje na ndani ndipo tunaweza kufanikiwa kwani hasira ya wananchi sio kwa chama CCM kama chama, isipokuwa viongozi wabovu waliomo ndani ya chama CCM...Chama ni watu.

Tukumbuke tu kwamba hata wakati wa kumwonda Hitler kulikuwepo na wapiganaji toka ndani ya utawala wake wakiitwa resistance group, hawa ndio waliofanya kazi kubwa ya kumwangusha Hitler ktk kila utawala alochukua iwe France, Urusi, na kwingineko.. Majeshi ya nchi za nje yalipokuwa yakiingia yalipata taarifa na sehemu na nyaraka za siri za Hitler hivyo kurahisisha mashambulizi.. kazi ambayo imekuwa ikifanyika kwa muda mrefu sasa hivi nyumbani kiasi kwamba Mafisadi wanahaha!.

Binafsi Mwanakijiji kama mpiganaji akijiunga na CCM na kuahidi kuwaangusha Mafisadi nitamtazama sawa na mgombea mwingine maadam imani yangu ni huyu mwanakijiji na kile anachokisimamia. Chadema, TLP au CUF haina maana hakuna mafisadi ndani ya vyama hivyo, wapo wengi tu isipokuwa tunachoomba ni utawala mzima kutokuwa wa kifisadi hivyo agenda za watu binafsi zitakosa nafasi.

Tumeyaona nchi za jirani kama Zambia, Malawi na Kenya ambako mafisadi wametokea vyama ambavyo havikutegemewa kabisa kwani fisadi ni mtu sio chama. Kwa maana kubwa nasema hivi mchafu wa tabia ni binadamu sio dini yake. Mkandara hapa kam ni jambazi basi nafanya Ujambazi sii kwa sababu mimi ni mkristu au Muislaam ati nilibadili dini nitabadilika...hjapana kinachotakiwa ni mimi kuokoka na kazi kubwa ya jumuiya ni kumweka Lupango Mkandara iwe hata ndugu yangu akipiga simu Polisi nikakamatwa huo ndio uzalendo.

Mafisadi ni WATU, tafsiri nyingine nje ya imani hiyo mimi siikubali pamoja na kwamba naweza kuwa nimekosea sana. Sidhani kama CCM inawafundisha wanachama wake kuubeba Ufisadi ila kuna kundi la watu ndani ya CCM wanaoukumbatia.. na hakuina njia bora zaidi ya kuwakosesha nguvu hawa jamaa ila kuwaondoa ktk madaraka, kesho watajipanga upya wakifahamu sababu iliyowaangusha. Tumeyaona KANU, ZAPU, na vyama vinginevyo vilivyotangulia ktk nchi za jirani.

Mhe. Mkandara,

Mawazo yako nayakubali.

'Wapiganaji' wanayo haki kama Mtanzania mwingine yeyote kuelezea hisia zao kuhusu suala lolote linalohusu mustakabali wa nchi yetu. Kuwa ni wanachama wa CCM - chama ambacho kinashutumiwa kulea na kuendekeza ufisadi isiwe sababu ya kutaka kuwanyamazisha wanaosema na watakaotaka kusema dhidi ya ufisadi hata kama ni wanachama wa CCM ndani ama nje ya vikao vya CCM. Isitoshe, hawa waliojitokeza ni Wabunge ambao sauti zao zinaweza kusikika zaidi kuliko mtu kama mie Bibi Ntilie nikianza kujitokeza leo na kupaza sauti ya kukemea ufisadi, nani atanisikiliza ipasavyo?

Mimi nadhani, badala ya kuhoji ama kuwahoji au kujaribu kuwawekea vipingamizi na vigingi vya maneno ama vitendo, tunachopaswa kufanya, sie tunaoona kwamba ufisadi ni hatari kwa taifa letu, ni kuwapa moyo na kuwatie shime kwa sababu sote tunayaona ama kuyajua vyema madhara yanayotokana/yanayoletwa na ufisadi nchini mwetu.
 
Nakubaliana na baadhi ya wachangiaji hapo juu. Nionavyo mimi suala la vita juu ya ufisadi ni letu sote. Kila mmoja wetu lazima ajitahidi kupambana na ufisadi.

Wale wanasiasa waliojitolea kupambana na ufisadi moja kwa moja lazima tuwape pongezi za hali ya juu kabisa. Kwa kuwa wamejitolea na wapo tayari kubeba ghalama yoyote kwa ajili ya vita hii. Tunaweza kutofautiana kimtazamo juu ya mbinu wanazo zitumia wenzetu...lakini vita ni vita.

Na sio kweli kuwa CCM ni chama kinachopenda mafisadi, la hasha!!! Kwa mtazamo wangu ni kuwa kuna baadhi ya wanachama wachache sana katika CCM wanaoendekeza mambo haya ndio maana ndani ya CCM kuna wale wanaopinga ufisadi...na hao ni wengi sana zaidi ya wale tunao waona katika vyombo vya habari.

Hivyo basi wanaJamii wenzangu, tusiwakwamishe wale waliokwisha jitolea kupigana labda tueleweshane ni njia gani muafaka zaidi....
 
Bila ya kuubomoa mfumo wa utawala wa kifisadi uliowaunda. tunaweza vipi kuwaondoa mafisadi wa sasa na kuwazuia wa baadaye?
Mzee Mwanakijiji,hivi unafikiri kwa nini kubadili mfumo wa healthcare Marekani imekuwa kimbembe na Obama pamoja na ujanja wake anaelekea kukwaa kisiki? Mzee wangu,jibu la swali hili litakueleza kwa nini kuna ugumu wa kubadili mfumo wa utawala Tanzania ,aidha jibu lake pia litakueleza kwa nini Rais Banda wa Zambia piga ua kaamua Chiluba lazima achomoe pamoja na kelele za wananchi na pia jibu lake litakueleza kwa nini Mugabe ana survive hadi leo na pia utapata jibu kwa nini Kenya walifanikiwa kuiondoa KANU,it is one and the same answer,Good afternoon Sir.
 
unajua ni nani alikua anakusanya...ofisi ya mkuu wa mkoa ndio wenye kitengo cha maafa muulize RC, Mwakipesile.
MWAKIPESILE anaendelea na hii vita ya umbea majungu na nudaku dhidi ya Mwakyembe,
Mwakipesile hawezi shinda ubunge hata kama mwakyembe ataamua kutogombea othewise kama si JK oleo angekua kwake ukonga anamwagilia maji kwenye maua maana siku hizi pamechakaa ile mbaya.
Mmmmhhh too personal Mdau!
 
Nakubaliana na baadhi ya wachangiaji hapo juu. Nionavyo mimi suala la vita juu ya ufisadi ni letu sote. Kila mmoja wetu lazima ajitahidi kupambana na ufisadi.

Wale wanasiasa waliojitolea kupambana na ufisadi moja kwa moja lazima tuwape pongezi za hali ya juu kabisa. Kwa kuwa wamejitolea na wapo tayari kubeba ghalama yoyote kwa ajili ya vita hii. Tunaweza kutofautiana kimtazamo juu ya mbinu wanazo zitumia wenzetu...lakini vita ni vita.

Na sio kweli kuwa CCM ni chama kinachopenda mafisadi, la hasha!!! Kwa mtazamo wangu ni kuwa kuna baadhi ya wanachama wachache sana katika CCM wanaoendekeza mambo haya ndio maana ndani ya CCM kuna wale wanaopinga ufisadi...na hao ni wengi sana zaidi ya wale tunao waona katika vyombo vya habari.

Hivyo basi wanaJamii wenzangu, tusiwakwamishe wale waliokwisha jitolea kupigana labda tueleweshane ni njia gani muafaka zaidi....

Naanza kuamini msemo kuwa "diversity is the mother of life"! Kwani wewe unaamini kwenye nadharia kuwa chama ni mali ya wanachama wote? Au unaamini kuwa kampuni ni mali ya wanashea wote kuanzia wenye 50% shares hadi wale wenye 0.0001% shares? Je kama baba na mama ni wezi na baadhi ya watoto ni watu wazuri hiyo familia ni ya watu wasafi? Kazi bado ipo kweli kweli!!:confused:
 
Kaeni mkijidanganya na hao "Wapiganaji" wenu sijui "Makamanda"!

None of them are serious enough to challenge the status quo!

Walikuwa na Nafasi Butiama, wakaizembea. Wakapati nafasi ingine juzi Dodoma, wakalegea na kuwekwa chini kifo cha Mende, halafu mnafikiri watakuwa na uwezo kuleta mabadiliko?

Wanatakiwa kuleta msukumo wa Mabadiliko ndani ya Chama chao na kuushinda Ufisadi ndani ya Chama na kuwaondoa Mafisadi na makuwadi wao ndani ya chama kwanza, kabla hawaja kwenye Uwanja wa Taifa!
 
MMKJJ, kwanza baada ya kukubali ufisadi ndio mfumo unaounda utawala wetu wa sasa, yaani ni system, halafu tunataka kugombea kisu huku walioshika mpini ndio hao hao, unategemea nini?.There is always one and only way ya kuchange system, system kamwe haibadiliki, lazima ibadilishwe, kama system imeundwa na mafisadi na kuendeshwa na mafisadi ili kuzidi kufisidi, hao wa kuibadilisha ni kina nani kama sio kutaka kuja kuibadilisha ili wapokezane zamu za kufisidi, na unawazuiaje mafisadi wa baadae wakati wengi wa wanasiasa wetu wanaingia kwenye siasa kama ajira kupigania nafsi zao?.Wanatakiwa wapatikane watu wa Calibre ya Dr. Slaa wengi wa kutosha na sio hao waimba mapambio kwa jina la makamanda.Hapa inatakiwa kitu kama the 'Bolshevic ya Octoba 1917' ama 'The American ya 1886' vinginevyo ni tunacheza makida makida.
Mkuu Pasco ukizungumzia Tanzania kufanya yale ya 1917 Urussi na 1886 Marekani kwa lugha nyingine unatamani Bongo tuchinjane? au? maana nisije nikawa nimekuelewa vibaya Mkuu.
 
Nakubaliana kabisa na Reverend kuhusu hilo. Hawa makamanda ni danganya toto kwa ajili ya Upinzania hakuna kitu humo maana ukijaribu kutazama utaona ni wale wale tu hakuna jipya humu
 
Mkuu Pasco ukizungumzia Tanzania kufanya yale ya 1917 Urussi na 1886 Marekani kwa lugha nyingine unatamani Bongo tuchinjane? au? maana nisije nikawa nimekuelewa vibaya Mkuu.

Bishanga,

Kuchinjana maana yake nini? Kwani sasa hivi hatuuani? Kama ikiwezekana kuchinjana mara moja ni heri kuliko kumalizana kwa slow killing strategy za mafisadi!
 
Back
Top Bottom