'Wapiganaji' walioko CCM wanapigania nini hasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Wapiganaji' walioko CCM wanapigania nini hasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 7, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 7, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Nimejaribu kujiuliza kuwa hawa ndugu zetu ambao wamebatizwa jina la “Makamanda” wa vita ya ufisadi walioko CCM wanachopigania hasa ni nini? Ujumbe wao unaotufanya tusimame nyuma yao na kuwaunga mkono hasa ni kitu gani? Kama kuna mtu ambaye bado ni dhaifu na hajaamua kuchagua upande hawa wapiganaji watamshawishi vipi ili awaunge mkono; wanamuahidi nini?

  Ninajiuliza maswali hayo na mengine mengi kwa sababu ukiondoa madai makubwa mawili bado najaribu kutafuta ujumbe wa wapiganaji wetu ili niweze kuelewa kama wana nafasi ya kushinda au watakuwa na athari ya kuvutia mikutano na kuuza magazeti na majina yao kutangaa lakini itakapofika muda wa kura wakajikuta wanatupwa nje ya ulingo.

  Zafanana
  Kitu kimoja hata hivyo naweza kukisema kwa uhakika zaidi ni kuwa kuna mfanano wa ajabu kati ya wanasiasa watetezi wa mafisadi (makuwadi wa ufisadi) na wale wanasiasa wanaowapinga mafisadi (wapinagaji). Kufanana huku ni muhimu kukuelewa kwani kimsingi kabisa kunafanya wapiganaji wawe na kazi kubwa zaidi ya kuushawishi umma kuhusu lengo na madhumuni yao hasa ni nini.

  Wanafanana kwani makundi yote mawili yako kwenye chama kimoja; CCM imekuwa kama tenga lililobeba ndani yake matunda mabivu na matunda ambayo hayajaiva na pamoja na hao matunda wadudu wa kila aina wanaofuata uchafu. Makundi yote mawili yako kwenye tenga moja na hivyo moja linaweza kubeza jingine kuwa halijaiva sana au bado ni bichi au limeoza na lile jingine likalalamika kuwa linaonewa na kuwa kinachofanyika ni “chuki binafsi”. Lakini ukweli unabakia hadharani kuwa wote wawili wako kwenye tenga moja.

  Wanafanana kwa sababu wote wanagombania nafasi ndani ya chama hicho hicho kimoja. Tumeshuhudia Dodoma wiki chache zilizopita jinsi gani makundi haya mawili yako kwenye muelekeo wa kugongana kusikoepukika. Lakini pamoja na mgongano huo tunaona kuwa makundi yote mawili yanagombania zaidi nafasi zao ndani ya chama. Hadi hivi sasa kundi la watetezi wa watuhumiwa ufisadi linaonekana kuongoza na kupata mashabiki wengi zaidi.

  Ni nani kati yao atakayeweza kuwa na nafasi ya kutengeneza wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi hususan kwenye Ubunge ifikapo 2010? Itakuwaje kama kundi la makuwadi litapata kuunga mkono zaidi ndani ya chama na kundi la wapiganaji likajikuta linaungwa mkono zaidi nje ya chama? Jibu ni jepesi; makuwadi watakuwa na wagombea wengi zaidi chamani na hivyo kutuamulia viongozi wetu wajao ni kina nani.

  Hata hivyo kufanana ninakozungumzia mimi siyo kufanana kwa aina hiyo. Ni kufanana kwa kile wanachogombania mwakani ni nini hasa. Makundi yote mawili yanagombania kuchaguliwa tena.

  Baada ya matukio ya kihistoria ya Februari 2008 yaliyosababisha kujiuzulu kwa Waziri Mkuu kwa kuhusishwa na kashfa ya Richmond mpasuko mkubwa umetokea ndani ya CCM. Mpasuko ambao hauwezi kuisha kwa vikao, mazungumzo, makubaliano au muafaka wa aina fulani. Mpasuko huu ni mkubwa sana kwani makundi mawili yanayoshindana hayawezi kurudi nyuma hata kidogo kwani kufanya hivyo itakuwa ni sawa na kujitia kitanzi wao wenyewe.

  Kundi la watetezi wa Lowassa haliwezi kurudi nyuma kwani hawa wanaamini kabisa kuwa kitendo cha Lowassa kubanwa na kamati teule ya Bunge kilikuwa kimekusudiwa, kupangwa na kufanikishwa na watu mbalimbali miongoni mwao ni Spika wa Bunge la Muungano Bw. Samweli Sitta na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo teule Dr. Harrison Mwakyembe pamoja na wajumbe wengine wa kamati hiyo.

  Hivyo kundi hili la Lowassa, mashabiki wake, wanufaika wa utawala wake, mashabiki na marafiki wake wa karibu waliapa toka wakati ule kulipa kisasi na kuhakikisha kuwaangusha wahusika wote na hatimaye kusababisha mchakato mpya utakaomsafisha Lowassa na wenzake na kitendo kile wanachoamini kuwa ni cha “uonevu mkubwa”. Kama nilivyodokeza siku chache baada ya matukio yale kundi hili halitokoma mpaka Lowassa atakaposimama tena akiwa safi na akiwa kiongozi. Chini ya hapo hakuna mapatano.

  Kundi la kina Mwakyembe linaamini kabisa kuwa lilifanya kazi yake kwa uadilifu na weledi na halikumuonea mtu yeyote na zaidi kuwa wangeweza kufanya makubwa zaidi kama wangetaka. Hawa wamejipanga wakati wowote kumwaga “mchele kwenye kuku wengi” endapo itabidi iwe hivyo hasa pale hatima yao ya kisiasa itakapokuwa mashakani. Kundi hili linaamini kabisa kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu ilihusika moja kwa moja na suala la Richmond na kwa hilo hawako tayari kumuomba msamaha mtu yeyote.

  Hawa nao mashabiki wao, wapambe wao na wale wanaowaunga mkono hawako tayari kurudi nyuma wala kusalimu amri. Sasa hawa wamepania kabisa kutetea viti vyao vya Ubunge na nafasi zao katika chama.

  Hivyo basi tunaweza kuona kuwa pande hizi mbili haziwezi kupatana kwa kadiri ya kwamba kila moja inaamini kuwa iko sahihi katika mtazamo wake wa matukio ya Februari 2008. Hawawezi kukaa meza moja; hawawezi kujadili sera pamoja na kwa hakika kwa upande wao hakuna mapatano yoyote na wale wa utetezi wa kundi la ufisadi isipokuwa ushindi tu.

  Ushindi hauji chee
  Hapo kwenye ushindi ndio tatizo. Kama nilivyoanisha katika makala zangu kadhaa zilizopita ni kuwa vitani ushindi hauji mezani bila kumlazimisha adui kusalimu amri. Ushindi katika vita unakuja kwa kumzidi adui uwezo na kumuweka kama kwenye kabali hivi na kumlazimisha anyanyue mikono kuomba radhi na kuingia katika meza ya makubaliano ya kusitisha vita kwa kusalimu amri.

  Ili upande mmoja ushinde ni lazima uwe na ujumbe, mbinu, na zana na utaalamu wa kutosha kumshinda adui. Nasikitika kusema kuwa upande wa watetezi wa Lowassa na wale wanaowatetea mafisadi (kama wanaomtetea Mkapa) umejipanga vizuri zaidi, ujumbe wake unagusa wanufaika wengi wa ufisadi na kwa hakika wana uwezo na zana za kuwamaliza wapinzani wao.

  Ndio maana hapa nimeuliza hawa wapiganaji wetu wao wanaujumbe gani zaidi ya zile mbili tulizozizoea na ambazo ukweli wake unakubalika katika akili za Watanzania wengi? Ni zipi unauliza..?

  Kwanza kuna ujumbe kuwa mafisadi wanaeneza fedha na mikakati ya kuwang’oa katika viti vyao vya Ubunge. Hili tumelisikia kwa muda na lina mantiki ndani yake. Kwamba, wale walioathirika wanataka kuwaangusha wale waliowaathiri ni sehemu ya siasa. Ninachokiona ni kuwa watetezi wa ufisadi wanatumia sayansi na sanaa ya siasa kuwaangusha wabaya wao. Katika hili mbinu na njia mbalimbali zitatumika hata zile ambazo ni kinyume cha sheria.

  Sasa wapiganaji wetu wamekuwa wakilia na kulalamika juu ya hili. Lakini wataendelea kulia lia huku hadi uchaguzi mkuu utakapofika ili kiwe nini? Sawa mafisadi wanataka kuwaangusha kwenye majimbo ya uchaguzi wao walitarajia nini? Hivi walifikiri baada ya matukio ya Februari wangetumiwa zawadi ya maua na keki kutoka kwa walioangushwa kwa fedheha na aibu?

  Wanachofanya makuwadi wa mafisadi si kingine bali kutumia siasa kulipa kisasi na Dodoma ilikuwa ni mwanzo tu. Watapiga tena.

  Ujumbe wao wa pili ni kuwa kuna mafisadi na mafisadi ni lazima washindwe. Sasa ukweli wa huu tunaujua kuanzia enzi za kipindi cha “Mikingamo” na matangazo ya “Liangalieni limbukeni hili”. Mafisadi wamekuwepi nchini kwa muda mrefu na wamekuwepo ndani ya CCM kwa muda mrefu (na siyo wanne tu kama mmoja alivyotaka tuamini).

  Sasa kutuambia kuwa mafisadi wanasambaza fedha na vipeperushi n.k kwenye majimbo katika mbinu ya kuwaangusha wapiganaji kunaweza kutufanya tuwaonee huruma lakini hiyo ni sehemu ya siasa. Kama watetezi waliweza kujipanga vizuri hadi kuweza kuleta hoja nzito dhidi ya Spika kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu na kwa kutumia njia za kisiasa basi hatuna budi kukubali kuwa hii ni sehemu ya siasa na makuwadi wa ufisadi wako tayari kutumia mchakato wa kisiasa kutimiza malengo yao.

  Pia kutuambia ukweli kuwa ufisadi na mafisadi wapo na wana nguvu na wako tayari kufanya lolote ni ukweli ambao wengi wetu tunaufahamu.

  Wananchi wanahitaji na wanastahili zaidi ya jumbe hizo mbilli. Watanzania wanataka kujua hawa wapiganaji zaidi ya kupigana ili kuokoa meli zao kabla ya uchaguzi ni kitu gani kingine ambacho ni kikubwa na wanakipigania ambacho kitawafanya wananchi wawaunge mkono na kuwarudisha Bungeni?

  Je, wao wapiganaji wanatumia vipi mchakato wa kisiasa kuwazidi kete makuwadi wa ufisadi? Je wanafanya kila kinachowezekana kuhakikisha kuwa makuwadi wa ufisadi na wenyewe hawarudi Bungeni na kushika nafasi mbalimbali?

  Ninaamini katika mvutano huu ni ushindi wa upande mmoja tu utakaosababisha mjadala kuisha ndani ya CCM. Hadi hivi sasa wanaoelekea kushinda ni watetezi wa ufisadi na dakika ni hizi za majeruhi. Je, wale wapiganaji wetu zaidi ya kuhutumia mikutano ya kutupa jumbe zao mbili wana kitu gani zaidi wanachogombania ndani ya CCM na kwenye Taifa ambacho kitatufanya tuamini kuwa kitu hicho ni cha thamani zaidi kuliko fedha na ahadi za makuwadi wa ufisadi?

  Ni kitu gani wapiganaji wetu wanagombania hasa ukiondoa wao kuchaguliwa tena kwenye Bunge la 2010?
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Sep 8, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,867
  Trophy Points: 280
  Wanapitishwa na wana CCM wenzao ili kugombea nafasi hizo za ubunge, wanashikamana na chama na serikali yao katika maamuzi mbalimbali ndani ya bunge. Leo kila mtu kawapa jina la makamanda, si ajabu na imewahi tokea tangu tukiwa na mfumo wa chama kimoja kwa wabunge fulani ndani ya CCM kuonekana wakali na wapigania maslahi, lakini at the end tupo pale pale.

  Kwa miaka minne sasa tunapiga kelele zile zile, wanaona na wanajua kuwa,tunapenda waongeaji na tunapenda kweli kusikia.Hakuna aliyeenda jela, hakuna aliyerudisha fedha zetu, lakini BADO KUNA WATU WANAWAITA MAKAMADA WA UFISADI!

  Wanakutana kwenye vikao vyao, wanagonga glass! huku watu wakiwa na matumaini ni makamanda, I once said, CCM dampo, na yeyoye aliye humo anaishi kwenye taka hata kama yeye siyo taka, utawezaje ishi kwenye hali hiyo!

  Afadhali uishi na mwanamke asiye zaa, na unaweza kumvumilia hata utakaposikia kumbe hata kizazi hana, ngau anaweza kukupa huduma zingine! lakini si haivumiliki CCM miaka zaidi ya 40 sasa

  'Makamanda' msi weza kujievaluate kuwa mmeweza nini basi hamna kitu.Msiseme uwazi alama za nyakati zinaonyesha kuwa ni nyakati za uwazi na hazizuiliki! si kwa kuwa kuna watu wanapiga kelele bungeni

  Wanataka ubunge tena, na watapewa miaka mingine 5!
   
 3. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mwanakijiji,


  Heri umeniwahi, lakini wewe unawaonea haya "Wapiganaji", ni wakati muafaka kuwalazimisha wawe wakweli na waache kutudanganya na kulialia hovyo.
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Sep 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wakuu zangu,
  Waacheni wapiganaji waifanye kazi yao..mimi sioni tatizo liko wapi..Yawezekana mimi nakosea lakini ndivyo vita inavyopigana..Mafisadi wanahitaji mashambulizi toka pande zote nje na ndani ndipo tunaweza kufanikiwa kwani hasira ya wananchi sio kwa chama CCM kama chama, isipokuwa viongozi wabovu waliomo ndani ya chama CCM...Chama ni watu.

  Tukumbuke tu kwamba hata wakati wa kumwonda Hitler kulikuwepo na wapiganaji toka ndani ya utawala wake wakiitwa resistance group, hawa ndio waliofanya kazi kubwa ya kumwangusha Hitler ktk kila utawala alochukua iwe France, Urusi, na kwingineko.. Majeshi ya nchi za nje yalipokuwa yakiingia yalipata taarifa na sehemu na nyaraka za siri za Hitler hivyo kurahisisha mashambulizi.. kazi ambayo imekuwa ikifanyika kwa muda mrefu sasa hivi nyumbani kiasi kwamba Mafisadi wanahaha!.

  Binafsi Mwanakijiji kama mpiganaji akijiunga na CCM na kuahidi kuwaangusha Mafisadi nitamtazama sawa na mgombea mwingine maadam imani yangu ni huyu mwanakijiji na kile anachokisimamia. Chadema, TLP au CUF haina maana hakuna mafisadi ndani ya vyama hivyo, wapo wengi tu isipokuwa tunachoomba ni utawala mzima kutokuwa wa kifisadi hivyo agenda za watu binafsi zitakosa nafasi.

  Tumeyaona nchi za jirani kama Zambia, Malawi na Kenya ambako mafisadi wametokea vyama ambavyo havikutegemewa kabisa kwani fisadi ni mtu sio chama. Kwa maana kubwa nasema hivi mchafu wa tabia ni binadamu sio dini yake. Mkandara hapa kam ni jambazi basi nafanya Ujambazi sii kwa sababu mimi ni mkristu au Muislaam ati nilibadili dini nitabadilika...hjapana kinachotakiwa ni mimi kuokoka na kazi kubwa ya jumuiya ni kumweka Lupango Mkandara iwe hata ndugu yangu akipiga simu Polisi nikakamatwa huo ndio uzalendo.

  Mafisadi ni WATU, tafsiri nyingine nje ya imani hiyo mimi siikubali pamoja na kwamba naweza kuwa nimekosea sana. Sidhani kama CCM inawafundisha wanachama wake kuubeba Ufisadi ila kuna kundi la watu ndani ya CCM wanaoukumbatia.. na hakuina njia bora zaidi ya kuwakosesha nguvu hawa jamaa ila kuwaondoa ktk madaraka, kesho watajipanga upya wakifahamu sababu iliyowaangusha. Tumeyaona KANU, ZAPU, na vyama vinginevyo vilivyotangulia ktk nchi za jirani.
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mkuu Mzee Mwanakijiji,

  Naomba na mimi niungane na Mkandara kwamba pamoja na ukweli kwamba watu ni wale wale, chama kile kile, sera zile zile, kuna umuhimu wa kuwaunga mkono hawa (makamanda wa kupinga ufisadi ndani ya CCM). kinacho takiwa kwa sisi ambao tuko nje ni kuongeza nguvu harakati za mapambano huku nje nawao watapata nguvu.

  Mkandara ametolea mfano wa resistance group ktk utawala wa Hitler, ukijakwetu mfano wake ni watu walioko ndani ya CCM wanao toa taarifa za siri za ubadhirifu wa viongozi wa serikali/CCM kwetu na sisi ni kuzifanyia kazi na hapo tutawaunga mkono vilivyo. Angalia timu ya Makamba, Rostam, Lowasa, Guninita n.k. wanachukia kuona siri za wizi wanaoufanya zikijulikana na kujulikana kwa siri hizi ndio mchango wa wapiganaji waliomo ndani, sisi tuzifanyie kazi hizo siri na hatimaye tutashinda.

  Nawaomba resistance group ndani ya CCM wazidi kutupa siri nyingi zaidi ili tuziweke hadharani mbele ya umma na kuuelimisha umma na kufanya hivyo tunaweza kuibuka na ushindi dhidi ya dhalimu Lowasa.
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  Sep 8, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Mzee Mwanakijiji heshima kwako,

  Wapiganaji hawa wanamalengo yaliyo wazi kisiasa, kwanza kulinda raslimali za nchi yetu mbili kulinda maslahi yao kisiasa.

  Sasa mbinu wanazotumia zinaweza kuwa sahihi ama laah itategemea na mtizamo wako umeegemea wapi.


  Katika chama cha Mapinduzi, ukiwa unamisimamo kama ya Kina Mwakyembe ,SELELII, OLE SENDEKA NA wengine hakika harakati zako kisiasa zinelekea ukingoni kama walivyomfanya Thomas Nyimbo na watu wengine wakariba hiyo.

  Sasa makamanda hao wa ccm wameunganisha nguvu wakijua hatari ilio mbele yao. wanaitisha CCM, kua wakiwafukuza wao sasa ni maarufu sana kuliko makamba na msekwa hivyo wanaweza kuibomoa kiasi CCM.

  Kwahiyo kinachoendelea ni aina ya mpambano...je mbinu zao zitalipa au laah ni swala la wakati.
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Magezi na Mkandara,

  Naomba tusaidiane kidogo ili tuwekane sawa. Kwa uelewa wangu kuna vitu viwili hapa. Kuna watu mafisadi na mfumo (system) wa kifisadi; na hapa namaanisha CCM. Mtu ambaye ana sifa ya kwanza huu mfumo unamfaa sana. Ila kama mtu siyo fisadi basi huo mfumo siyo wake na hawezi kujidai mbele ya umma kuwa anachukia ufisadi! Kama anauchukia basi hawezi kuishi kwenye mfumo wa kifisadi. Sasa hawa watu wanaoongelewa hapa wanaishi na kula na mafisadi katika mfumo wa kifisadi. Wanatoa wapi ujasiri wa kuukemea kama siyo kutuzuga? Naamini kama mwanangu anachukia tabia zangu basi atajitenga nami. Hawezi kushinda anajizungusha na kuchafua makochi yangu, akiangalia luninga yangu na kuchekelea halafu eti anikemee kwamba nimepata vitu hivyo kwa wizi. Haijawahi kutokea na haitakuwepo kuukata mkono unaokulisha, labda mjinga tu!
   
 8. w

  wasp JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi sioni kama kuna wapiganaji huko. Hili ni changa la macho la CCM la kupata kura za walalahoi. Wapiganaji wa kweli walitangaza majina ya mafisadi mchana kweupe bila kumumunya maneno pale Mwembe Yanga - Temeke. Hawa wengine wanaokutana Nzega kuzindua VIKOBO na huku wakiubiri ilani ya uchanguzi ya CCM sioni kama ni wapiganaji. Huwezi kupigana vita na adui unaeishi na kula naye nyumba moja kwa sababu mbinu zako za kivita unazotumia anazijua.
   
 9. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #9
  Sep 8, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  unaweza kudhani hivyo wakati fulani kumbuka hii ni vita kamili, simpambano huu, kamati kuu imedhamilia kuwaondoa katika kinyang'anyiro cha uongozi 2010.....harakati za hawa watu zimesambaratisha serilkali, zimemkosanisha JK na Lowasa, zimewakosesha akina Dialo ulaji, zimemporomosha Zakhia hamdan Meghji katika siasa za nchi hii, wako wapi kina Mramba, Yona......hii ni vita kamili ndugu yangu.
   
 10. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkuu,

  Nitakuunga mkono kwa hilo.Ni kweli hawa CCM wanaipa joto na CCM wanalitambua hilo na ndio maana wanafanya kuwa-undermine kila leo ila pale watakapojitenga na Chama ndio suala litakuwa nzito.

  Hawa Wapiganaji wanachokipigania wanapaswa kukipigania to the end.Suala la kuwataja mafisadi then wanapotea as if they had nothing to do with that na kujipongeza kwamba wanatetea maslahi ya nchi, haitoshi tuu!Thats a very small part of the fight!

  We need to see more na ndio maana watu wengine hawaoni hicho kinachodaiwa kupiganiwa!
   
 11. E

  Engineer JF-Expert Member

  #11
  Sep 8, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtu huyo huyo anajiita mpiganaji huku anaiba hata michango ya maafa ya wananchi kweli huyo ni mpiganaji?

  Upiganaji ni mradi wa kisiasa, uzuri tunajua na wengi wao tutawaumbua 2010.


  Watawadanganya ambao hamuwajui kwa karibu.
   
 12. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #12
  Sep 8, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  hauko wazi nani anaiba michango ya maafa...? udaku....?
   
 13. N

  Ndaga Senior Member

  #13
  Sep 8, 2009
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 164
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Mkandara,
  Nadhani umejibu hoja vizuri,
  hata kama hawatapata Ubunge lakini tumeona yaliyo ndani ya CCM kuliko walio kimya, nadhani tuwape support ya kuendelea mbele, tusiwakatishe tamaa.
  Ujumbe wa mwanakijiji hauonyeshi njia bali unarudisha nyuma moral support ya sisi tunaokubali kazi yao japo katika uchanga wake.nilitegemea Mwanakijiji atatoa dira ya kuwasaidia kwa jinsi anavyoweza kuchambua na kufikirisha mawazo yaletayo mabadiliko na angeweza kuwasaidia hawa wapiganaji na siraha zao duni kuwa na siraha kali za kifikra ili wasikose kuendelea kupiga kelele ambazo kwakweli zimeifanya serikali ianze kujipanga utendaji wake uwe makini zaidi.
  Tuwasupport kimawazo na zaidi TUWAOMBEE kwa MUNGU wapate ujasiri wa kusema.
  asante.
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Sep 8, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Samaki mmoja akioza elewa kuwa tenga zima limeoza.
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Sep 8, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Siasa za Mbeya naona zimekuathiri sana mkuu.
   
 16. I

  IMBOMBONGAFU Senior Member

  #16
  Sep 8, 2009
  Joined: Jun 7, 2009
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nguvumali

  Michango ya watu waliokumbwa na mafuliko Kyela haikuwafikia walengwa.Mpiganaji alipigwa swali hilo na wanakijiji majuzi kigugumizi kikamshika.Huu sio udaku Mwakyembe na timu yake wanatakiwa wajibu hili swali....Nguvumali unasema ni udaku?anyway Miaafrika ndivyo tulivyo..kama swala halikuhusu unaona kama kelele tu.
   
 17. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #17
  Sep 8, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  WANAPIGANA KUYANEEMESHA MATUMBO YAO!period
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Sep 8, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kumbukeni wakuu hawa wanao jiita wapiganaji wanapigania matumbo yao
   
 19. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #19
  Sep 8, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  unajua ni nani alikua anakusanya...ofisi ya mkuu wa mkoa ndio wenye kitengo cha maafa muulize RC, Mwakipesile.
  MWAKIPESILE anaendelea na hii vita ya umbea majungu na nudaku dhidi ya Mwakyembe,
  Mwakipesile hawezi shinda ubunge hata kama mwakyembe ataamua kutogombea othewise kama si JK oleo angekua kwake ukonga anamwagilia maji kwenye maua maana siku hizi pamechakaa ile mbaya.
   
 20. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #20
  Sep 8, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Nimefurahishwa na heading,maana mimi niliitoa siku chache zilizopita niliandika(Wanaweza kuwa wapiganaji ndani ya ccm?) japo hakuna aliechangia.Ni suali ambalo najiuliza sana na mpaka sasa bado nimekataa kuamini kuwa wanaweza kuwa wanaharakati ndani ya ccm.Siasa ni mchezo mchafu sana pale mfumo unapokuwa umejengwa katika siasa chafu.Ndani ya mfumo mchafu huwezi kupambana ili kuleta mfumo safi wa kiutawala.Ili uwe huru ni lazima ujitoe ndani ya mfumo taka.Mi naona hawa mabwana wanatudanganya kwani bado wanaamini ccm ni mama na baba yao hawataki kuasi.Wanasahau hata maneno ya mwl.nyerere kuwa wapinzani makini watatoka ndani ya ccm.wanachofanya wanaendelea kunikumbusha msemo ''siasa ni uongo''yaani ili ufanikiwe kwenye siasa lazima udanganye.Muungwana ni vitendo,Uzalendo wa kweli unaonekana kwa matendo.Kamati kuu ya ccm imewafukuza japo wanafikiri aliyekuwa anaandamwa ni sitta,sitta alikuwa chambo tu chama hakiwataki kwani wanahatarisha ulaji wa wakubwa.
  Wakiamua kuondoka/kuasi watakuwa wamenipa raha sana.......
   
Loading...