Wapiga debe Ubungo stendi wanasumbua sana abiria

OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,978
2,000
Hivi serikali ipo wapi?
Mbona wapiga debe hapa stendi ya Ubungo wanabughuthi sana abiria? Wanavutavuta abiria wanashikashika akina dada wengine wezi. Unakuta mwingine mchafu anakuja kukungangania?

Naishauri serikali ya mkoa iwapige marufuku na kuwaondoa wote. Tuwe wastaarabu. Kila basi wawe na ofisi abira ufike ofisini ukate tiketi ukapande basi
 
Jan 2, 2017
22
45
Ningeshauri kila basi wajenge ofisi zao kama walivyofanya Dar lux, Dar express na Kilimanjaro express.... Kwa sababu katika maeneo hayo hakuna hayo mambo ya wapiga debe
 

Mr. MTUI

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
7,892
2,000
Maana mimi tayar nina tiketi namuombia haelewi ananishika na mikono michafu anachafua T-shirt yangu nyeupe nikashikwa na jazba sana nikakuta teke limeshachomoka
Mkuu acha uongo.. Huo mwili unaweza rusha mawash gel kweli? Maana nilikuona walivyokuwa wanakuzonga (JOKES) Ila kiukweli wanakera...
 

Neylisious

Member
May 25, 2017
43
125
Ila kweli wanaboa sana jamani maana wanakuzonga mpk unashindwa uelekee wapi ustarabu unahitajika sana hasa Ubungo ni shida kwa kweli
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
140,841
2,000
Hivi serikali ipo wapi? Mbona wapiga debe hapa stendi ya Ubungo wanabughuthi sana abiria? Wanavutavuta abiria wanashikashika akina dada wengine wezi. Unakuta mwingine mchafu anakuja kukungangania? Naishauri serikali ya mkoa iwapige marufuku na kuwaondoa wote. Tuwe wastaarabu. Kila basi wawe na ofisi abira ufike ofisini ukate tiketi ukapande basi
Labda tuangalie namna nyingine kwakuwa hiyo serikali ya mkoa haijawahi kufaulu kwenye lolote
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom