Wapiga debe Ubungo stendi wanasumbua sana abiria

Hivi serikali ipo wapi? Mbona wapiga debe hapa stendi ya Ubungo wanabughuthi sana abiria? Wanavutavuta abiria wanashikashika akina dada wengine wezi. Unakuta mwingine mchafu anakuja kukungangania? Naishauri serikali ya mkoa iwapige marufuku na kuwaondoa wote. Tuwe wastaarabu. Kila basi wawe na ofisi abira ufike ofisini ukate tiketi ukapande basi
tatizo stand ni chafu kama hao wapiga debe. stand ingekua safi kama pale airport , wasingefanya haya wanayo Fanya sasa.

Stand ya Dar isiachwe kwenye halmashauri, inatakiwa ijengwe na tanroad,

nimeipenda sana kituo cha brt gerezani.
 
Hasa wale wadada wa mabasi ya Arusha na Moshi ndio wamezidi aisee! Kurembuliana macho na mwezi huu mtukufu...Halafu wanakupandisha basi la kuondoka usiku wakati safari yako ni mchana.
 
Hasa wale wadada wa mabasi ya Arusha na Moshi ndio wamezidi aisee! Kurembuliana macho na mwezi huu mtukufu...Halafu wanakupandisha basi la kuondoka usiku wakati safari yako ni mchana.
Unapandishwaje gari la usiku kama mzigo mzee..
 
Wanazingua sana, mimi huwa sikati tiketi mpaka nifike kwenye mlango wa basi na huwa natia ukauzu wa pekee
 
Tena wengine washenzi hasa akina mama ndo wanawaonea kweli. Kuna siku msamvu moro nimeshuhudia wananyang'anyana mzigo wa mama mmoja mpaka waka ufumua vitu vyote vikasambalatika. Yani aibu kweli, alafu hata awaonyeshi kujuta yani. Dah
 
Serikali ya mkoa chini ya Makonda haijawahi kufaulu kwa lolote, jamaa kila anachojaribu kufanya hafiki hata 30% ya malengo na mafanikio.

Kwa wale wa Moshi-Arusha ni Dar express na Kilimanjaro express tu ndio unakata tickets na kusubiri mda wa kuondoka kwenye lounge. Hakuna kuchafuana.
 
Back
Top Bottom