Wapiga debe hawatambuliki kisheria, abiria ana haki ya kusafiri mazingira salama kusiwe na kelele

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
FRvEPGmWUAETWsO.jpg
Licha ya abiria wengi wa usafiri wa daladala na mabasi makubwa kukumbana na usumbufu wa wapigadebe katika vituo vya mabasi imeelezwa wapigadebe hao hawatambuliki kisheria.

Mwenyekiti wa Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (CHAKUA), Hassan Mchanjama anasema: "Kwenye sheria wapiga debe hawapo, abiria amekuwa hatendewi haki kwa sababu ya kuzongwazongwa, wengine wanaibiwa simu na pesa.

"Abiria ana haki ya kulipa nauli halali, kusafiri mazingira salama kusiwe na kelele wala bugudha, ana haki ya kupata usafiri mbadala pindi usafiri unapoharibika njiani na ana haki ya kulipwa fidia."

Source: East Africa Radio
 
Vijana wasio na kazi hujipatia pesa ya kusukuma maisha ya siku kupitia hiyo kazi tena bora hao wanapambana kupata pesa sio wale wazee wa mei mosi(vibarua) na sare zao walio ambulia "neno kamati" wakati Sheria zipo wazi kabisa
 
Back
Top Bottom