Rufaro
JF-Expert Member
- May 7, 2022
- 222
- 340
Sijui niseme ni kukosa hekima au ni makusudi.
Baadhi ya makampuni ya mabasi waliamua kukodi ama kujenga vituo vyao binafsi vya mabasi kwa ajili ya urahisi kwa abiria wao na kuepuka usumbufu usio wa lazima kutoka kwa wapiga debe huko stendi na hata wizi.
Na naamini kama ni kukodisha ina mana wanalipa kodi ya mtu binafsi na serikali, kama kuna huduma zinaendelea kama mgahawa na mengineyo ina mana kuna risiti za efd na kodi inalipwa. Je, kutaka kulazimisha mabasi hayo pamoja na abiria wapande usafiri wa daladala waende kupandia stendi kuu ni HAKI?
Ni kwamba serikali inaona wivu au chuki kwa wananchi hao hawapati usumbufu?
Katika hali ya kustaajabisha, leo katika moja ya kituo binafsi cha mabasi yanayoenda mikoani, abiria wameshushwa kwenye gari na kulazimishwa kupanda daladala tena kwa garama zao na kwenda stendi kuu, na basi kulazmishwa kwenda kupakilia stendi kuu, na hio imepelekea abiria kuchelewa sana kuondoka ..je hii ni sawa? Tumefikia huku? Mbona kama akili za kihayawani hizi?
Waacheni wawekezaji WAZAWA wa usafirishaji wafanye biashara zao alimradi wanalipa kodi na tozo zenu, waacheni wawajali abiria wao na kuwatengenezea mazingira mazuri, nalaani sana kitendo hicho kilichofanyika.