Wapi nianike Chupi yangu?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,579
Reaction score
161,432
Mwanzoni nilikuwa nikianika bafuni, kuna siku tumbo la kuaibisha likanishika. Nikatoka nduki hadi bafuni kwetu ambako choo na bafu viko ndani ya chumba kimoja, huko kilichonitokea sitakaa nisahau. Nilikuta mke wa mpangaji mwenzangu akiitumia chupi yangu niliyokuwa nimeifua asubuhi kujisugulia mwilini mwake. Tumbo langu la kuhara likaishia hapo na yule bibie sikumuuliza kisa cha yeye kuifanya chupi yangu dodoki lake la mwilini. Tangu siku hiyo nikawa naanika chumbani.

Jana nimetembelewa na mke wangu mtarajiwa. Yeye anajiendeleza katika chuo cha mahakama kilichopo Lushoto.
Alipoona chupi nimeanika chumbani akaanza nigombeza kuwa ni mwiko na aibu kuanika chupi chumbani. Nimejaribu kumuuliza kuwa nianike wapi? Badala ya kunielewesha kaanza kunilaumu kuwa simjali wala simsikilizi. Mimi ni mtu jeuri nisiyemthamini na kumuenzi.
Tangu jana hadi muda huu kanuna.
Jamani wana MMU nyie chupi zenu mnaanika wapi nami nije kuanika yangu?
 
mdau mpaka leo wavaa chupi duh utamtia kilema huyo..... subiri waje wavaaji
 
mimi huwa nakadust bin kangu ka chupi
wiki nzima nikivua nazitupa huko
wkend naloweka kama lisaa nazifua mdogomdogo nasugua nasuuza fresh naanika kwenye kamba mchana live
haya mambo ya kufua chupi na maji uliyoogea yenye mapovu ya sabuni ndo maana mafangasi hayawaishi huko down
kuna watu uchi umezeeka maana..sabuni na uvundo vimezila

kama huwezi kutunza chupi asi usivae
 
kwa afya anika juani....mbona hakuna shida ktk hilo,chupi zenyewe si mali kitu siku hizi....wamachinga wanatembeza mikononi,zinamwaga barabarani.....kujipa fangazi wa bure kwa kuanika ndani wamuogopa nani hasa???
 
"Boxer" ni neno la kigeni lenye kumaanisha nguo ya ndan ya kiume kwa muktadha huu,yangu mm huanika nje ili ikauke kwa jua,
 

huyo mchumba wako anamapepo.
 
Du! Kiongozi bado wavaa kyupi! Bora boxer mwonekano wake unaanika hadharani kama uko kwenye upangaj wachumba! Lakini kama uko kwako sidhani kama inasumbua kuanika hata kama ni kyupi!
 
Wakati unafua, fua na nguo nyingine kama shati au shuka, anika nje funikia na shuka au sharti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…