Wapi hapa Dar naweza kupata motor/mashine bora zaidi za kusaga nafaka?

TensorFlow

JF-Expert Member
Feb 11, 2020
449
500
Habari zas sasa,

Naomba kujua kutoka kwa wabobezi humu, wapi hapa Dar naweza kupata motor/mashine nzuri kwa ajili ya kusaga na kukoboa nafaka? Aina ipi ya ya motor, na vifaa vingine associated ni bora zaidi? Bei ni kiasi gani, na duka gani ambalo halina vifaa fake na la kuaminika naweza kupata hizo motor? Nini cha kuzingatia wakati wa kufanya manunuzi?

tf
 
wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
21,407
2,000
Nenda posta mtaa wa lindi kuna maduka ya motor na mashine pia huko huko unapata na motor ungesema unataka ya h.p ngapi
 
Abel Tesfaye

Member
Jun 6, 2021
10
45
Nenda mtaa wa kisutu pale along stand ya mwendokasi kuna maduka mengi sana pale wana motors na machine nyingi
 
TensorFlow

JF-Expert Member
Feb 11, 2020
449
500
Hebu nipeni muuzaji specific wa kuaminika na brands bora, nisije kuingia mikononi mwa matapeli nikauziwa vitu vya ajabu.
 
wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
21,407
2,000
Aina nzuri/brand? HP kuanzia 25 - 40.
Maksimamo ni 25 hadi 30 hyo 40 ni kubwa sana kwa matumizi ya kazi yako na nzuri iwe ya italy hata kampuni yoyoye ila iwe made in italy hataa ya germany zipo ila sio mpya ni used na kama ukipata ya hp 30 ina bei kuliko mpya ya italy.
Ila uwe makini hizo za germany ukikuta mpya nenda na fundi nyingi huwa za kusuka na nembo za kuchonga.
 
TensorFlow

JF-Expert Member
Feb 11, 2020
449
500
Maksimamo ni 25 hadi 30 hyo 40 ni kubwa sana kwa matumizi ya kazi yako na nzuri iwe ya italy hata kampuni yoyoye ila iwe made in italy hataa ya germany zipo ila sio mpya ni used na kama ukipata ya hp 30 ina bei kuliko mpya ya italy.
Ila uwe makini hizo za germany ukikuta mpya nenda na fundi nyingi huwa za kusuka na nembo za kuchonga.
Ahsante sana. Kuna mtu kipindi cha nyuma aliwahi kunitajia motor za UK, zipo hizo na zikoje au magumashi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom