Ukipata audio yake tutafutie na hii:
Hii nyimbo inanikumbusha vile vijembe vya enzi hizo za wakongwe wa Taarab. Enzi ya Kina Siti Binti Saad.Hii jee X-paster unaijua ya Bi fatma Binti Issa
(inasemwa aliimba kwa kuwa watu walimsema ana 'uso wa basi' na anakunywa pombe)
Haya maumbile yangu
Chuki binafsi na choyo, nyoyoni za wasumbua
Kutwa kazi yenu hiyo, zimewajaa shakawa
Kwangu yepi muonayo, mageni msoyajua?
Kufanya niyapendayo, kwenu kosa limekuwa.
Hilo haliwezikani, na wala halitokuwa
Leo nakuelezeni, muache kunichungua
Msijitie shidani, haya nimejaaliwa
Kwani hasa jambo gani? Mie la kulaumiwa?
Nami ni mja mwenzenu, hata mkinichukia
Aibu yangu ndo yenu, kama mtafikiria
Kama baya kwenu nyie, kwangu nna ona sawa
Nawambia msikie, msio fahamikiwa
tena hadi msikie, kukaa kujizuzuwa
Lilobaki mniachie, sitaki kudhulumiwa
Wengi wamenihasimu, na thamani kunitoa
Mwapita kumwaga sumu, kila ovu kutupiwa
Bure mnanituhumu, ya fitina kuyagawa
Nami ni mwanadamu, si vyema kunibagua
Hata hiyo si mbaya, ivo nilikwambia hizi nyimbo zote ninazo?Mbona hiyo siijui...mie naijua "Bahati ikenda kombo" tu (@_@)
Bahati ikenda kombo, mwerevu huwa mjinga
huwa mjinga wa mambo, bahati ikikutenga
Jambo mzuri wa umbo, wabaya humsimanga
Paka Jimmy
Mwenzenu kanilemaza na kunivaa moyoni
Mengi yamenipendeza, msiulize kwa nini
Mengine ni miujiza, ameshushiwa mwandani
Ukweli haufichiki, kajaaliwa imani
Undani yeye hataki, penye kosa hubaini
Umbile hamithiliki, bashasha za kila fani
Mkweli kakamilia, anafahamu hisani
Mpole zake twabia, si mtu wa ushidani
Mzuri katimilia, hilo wazi muamini
Anajua nampenda, moyoni ameamini
Ameridhi kuniganda, katu hatubandikani
Popote nnapokwenda, yumo mwangu mawazoni
Mwenye roho ya imani, hakuna kuliko yeye
Ni kweli hatuachani, twapendana mimi naye
Du!
Mimi sina asili na aina hii ya mashairi, lakini ukiyasoma kwa utulivu yana mvuto wa pekee sana, na yanagusa hisia moja kwa moja!
Hakika watu wa pwani walikuwa na namna ya ajabu sana ya kuwasilisha ujumbe na kuwatunuku wawapendao!
X-Paster, FF, na Gaijin, endeleeni kutupa haya mahaba ya pwani!
Je siku hizi hakuna watunzi wa jinsi hii?
Gaijin,
Kwa aina hii ya sifa ilikuwa ngumu sana watu kuachana kirahisi!
Je fedha na kipato vikuwa na nafasi gani enzi hizo?...Mbona yaonyesha havikuwa na nafasi kabisa kwenye sifa za mwandani in controversy to today's situation?
Mkuu X-Paster,Ichukue hii siri, iwe kwako ni wasiya
Huwi katika wazuri, ila kwa njema tabiya
Uwe mwenye kusubiri, siivamie duniya
Tabia kitu azizi, kiumbe akiwa nayo
Si hoja sura nzuri, na watu kukusifiya
Au umbo la fakhari, mwenyewe kujivuniya
Huwi na nyingi jeuri, hayo yakasaidiya
Hata watu wa bara pia walikuwa na namna yao ya kufikishiana ujumbe, labda tu kwa udhaifu wa wataalam wetu wameshindwa kutuwekea kumbukumbu.
Hivi unamjuwa au kumkumbuka Marehemu Mzee Mwinamila, alikuwa ni kiongozi wa kikundi cha ngoma, kilichojulikana kwa jina la 'Hiari ya Moyo'? au Mzee mwingine ni Mzee Makongoro na nyimbo zake...
Nimekumbuka beti moja ya wimbo wa Mrehemu Mzee Mwinamila:
Upo hivi... "...Twaimba nyimbo…! Twaimba nyimbo mwisho wake tutakufwa lofwa...!
Sikumbuki tena muendelezo wake.
(hapa alikuwa na maana wanaimba nyimbo lakini matokeo yake mwisho watakufa masikini/lofa).
Na ni kweli, waimbaji wengi wa zamani na hata wa siku hizi mwisho wake wana sahaulika na wanakuja kuwa omba omba.
Kuna na huu mwingine nakumbuka beti zake chache... unaitwa "Madereva",
Unaanza hivi...
"Mtikisiko wa Wimbi, Maji Ya Kipwa Kimbia, Ukimsifu Mgema Tembo ulitia Maji... Madereva wenye fujo yafaa kuwakimbia.
Kibwagizo: Dereva kalewa pombe! haa! Sawa hiyo!?
Waitikiaji: Haataa, hiyo si sawa dereva wacha vituko!
Nyingine:
Kuleni kuku, mayai, mboga, samaki, maziwa, Na kujenga nyumba safi pa kulala pawe bora!
Mkuu, ahsante nami nafurahi kwa kufurahi kwako.Mkuu X-Paster,
Nimefurahia zaid hiyo sehemu ya kwanza ya ushairi!
Hakika huwezi kulinganisha na mambo ya "kuleni kuku mayai mboga samaki maziwa"...Utavipata wapi vitu hivyo maisha yenyewe haya?
Kwanza akina Makongoro na Mwinamila waliimba kwa miongozo ya siasa za wakati huo zaidi, na ni kama vile waliongozwa na wanasiasa!
Lakini kwa shairi kama za hapo juu ni tafsir ya hisia za mtu zimtokazo kunako moyo!
Aksante mkuu!
This propasal has made my day....lol... Dah!
umewaza nini MTM?? enways i have observed kasema NO!
Please do the needful na muoneshe kua you are man enough
hata kama ni mbibi... you will be the new Ashton Kutcher/Demi Mo'
Couple... so in love that age does not matter... I have special
interests ya kua brides maid....lol
Thats the spirit My dear, true love has no limits
Amenipiga kibuti but subra huvuta kheri na mie nipo tayari kusubiri, FF is the most resilient lady of JF, i like that strength and I am sure i will be a good man for her, and I am old too so together we can twist and turn the world, its gonna be a lethal combination, full of life and laughters
I am sure she will accept me as I am and you will be there as our chief of protocol
I am very optimistic and full of love
This is a very wonderful thread
Nothing gives me pride than seeing a man in lurve... for it is rare nowadays...
imagine my elation in knowing it is being directed at my twin FF... Dah!
En ways mtu akikupiga kibuti kwa mkwara wa 'am too old' me as a woman
takes it as she is trying to say "i love you too but don't you mind the age?"
With my help of coz we will eventually conquer her.... for love conquers all!!
And YES i do agree she is the mosr resilient lady of JF... For wengi wetu
upenda kufanya vile guys around us approve, instead of what we really believe in...