Mtoto halali na hela
JF-Expert Member
- Aug 10, 2012
- 55,807
- 55,554
Kuna dada anawapenda, nadhani hata huku jf yupo.
Hahaha nani tena huyo
Mi napenda paka nilikuwa nae nyumbani...lakini kuna siku alinitisha...Unajua paka akiwa kwenye giza macho yake yanaonekana kama yanangaa....Sasa siku umeme ukakatika ghafla dah nilikuwa naona macho tu na nilikuwa mtoto around 9 dah nilidhani paka amekuwa vampire :lol:My Sistaz, Nyumba yenye paka siishi ndani humo!! toka utotoni mimi na paka ni East v/s West !! sijui nini kilinisibu? farkhina
Wewe hupendi nyau?
Mhhhh mmh mmh mmh....!!!
Niliwachukia walipoanza kutumika kwenye "ramli chonganishi" na akina dokta Manyaunyau....
Beautiful kittens n very very cute nilikuwa na mmoja chuoni tangu kakiwa kigoli, balehe uchumba, ndoa hadi watoto,
Wanyama ni kama binadamu kabla hajavunja ungo nilikuwa nalala naye, naenda naye darasani na pengine pote, alipokuja kupata mpenzi wa mtima wake safari nami zikapungua mno, nakumbuka jioni nikimwachia chakula kwenye sahani yake hali mpaka bebi wake aje
Siku anajifungua hakutaka niende popote nilikaa naye mpaka alipopata uchungu na hatimaye kujifungua vitoto vinne vicute hasa
Mshana hawa ni wanyama, hawajifungui ... wanazaa. Herehoa?
Halafu wana staha na aibu za kibinadamu kabisa, siku ya kwanza kumfuma na MKWE alikimbia na kujificha na alichelewa kurudi chumbani,alikuja mpaka dirishani akakaa hapo, yale madirisha ya wenzetu ni kimo cha kifua, nikambembeleza kama mzazi akaingia chumbani lakini alikuwa na haya na kujiona mkosaji kabisa
nilikua na paka wangu huyo simsahau alikua akinisaidia mambo mengi r.i.p my cat alikua akinifulia nguo na kunipigia pasi kitanda pia alikua akinitandikia na kunipikia kabisa na alikua msafi akiamka jambo la kwanza kupiga mswaki na kufagia uani i miss you my cat majonzi makubwa nayapata!!
Kuna dada anawapenda, nadhani hata huku jf yupo.
Mmmmh!
Hawa ukiwaweka nyumbani wataliwa na panya wote.
nifah unabisha