Nyakageni
JF-Expert Member
- Feb 1, 2011
- 15,045
- 5,092
ni vizuri kuichimba historia ya Zanzibar ma muungano kwa makini kwa sababu wadau ni wengi na taarifa lazima zitatofautiana.Nawaapia badu unaweza kupata PhD ukiamua kutafiti mambo ya Muungano.Kwa kuwa upo muungano kwa miaka 48 sasa nafikiri tunahitaji majibu ya kisomi na kisayansi ya mambo makubwa manne:
1.Je sababu za kuungana mwaka 1964 zina mashiko yoyote kwa pande zote leo mwaka 2012?
2. Je tunahitaji Muungano tena? baada ya kupata jibu la swali la kwanza
3. Kama tunauhitaji je ni wa serikali tatu,moja,ama mfumo wetu wa mikoa tuubadili uwe wa majimbo yenye mamlaka sheria na mipango maendeleo na yote yawe na serikali badala ya mikoa hii inayotuzingua na serikali ya shirikisho kama Marekani?
4.Kama kura ya maoni ikionesha Wazanzibari wengi say asilimia 90 hawautaki Muungano na wakati huo huo asilimia 90 ya watu wa iliyokuwa Tanganyika wakuonesha kuutaka tutafanya nini na hawa watu asilimia10 walioko Zanzibar kwa mfano?
Tuone basi tunalijadili dude gumu kuliko suala la ndiyo/siyo
mkuu ubongo unao. Kudos.