Nyerere na fitna za Upemba na Uunguja

dullyhami

JF-Expert Member
Jun 4, 2012
563
195
Na Ahmed Rajab

ALIPOFARIKI dunia Mwalimu Julius Nyerere
Oktoba 14 mwaka 1999, gazeti la Guardian la
Uingereza liliniomba niandike makala maalumu ya
kuyatathmini maisha yake.
Nilipokuwa naanza kuiandika tathmini hiyo
iliyochapishwa siku ya pili yake, niliyakumbuka
aliyowahi kuyasema Mwenyekiti Mao wa China
kumhusu Josef Stalin, mtawala wa pili wa
Muungano wa Sovieti baada ya Vladimir Lenin.
Nami nikayatumia maneno hayohayo kuanzia
makala yangu kwa kuandika: Julius Nyerere was
"a great leader who made great mistakes," as one
ruler once famously said of another. (“Julius
Nyerere alikuwa “kiongozi mkubwa (adhimu)
aliyefanya makosa makubwa,” chambilecho
mtawala mmoja aliyewahi kumuelezea hivyo
mtawala mwenzake.)
Nyerere alifanya makosa ya kinadharia, ya kifikra
na ya kiutendaji katika utekelezaji wa sera zake.
Sikulidhukuru jina la Stalin kwa sababu sikutaka
wasomaji wangu wafanye kosa la kudhania
namfananisha Nyerere na Stalin. Siamini kama
Nyerere alikuwa na uovu wa Stalin. Na kama
ilivyokuwa kwa Stalin si yote ya Nyerere
yaliyokuwa maovu. Alitenda mema yanayostahiki
sifa.
Watu wa kale wasema: “Kheri ya mja ni ulimi
wake na shari ya mja ni huohuo.” Kwa ulimi
wake Nyerere aliwahi kutamka maneno ya maana
na mengine ya kibahaluli. Baadhi ya maneno yake
yalikuwa kama lulu na baadhi yalikuwa kama
utumbo kama pale, kwa mfano, aliposema kuwa
hakuna watu waitwao Waswahili. Nilimsikia
akiyasema hayo alipotoa hotuba katika ukumbi
wa London School of Economics alipokuwa
ziarani London kabla ya kuuacha urais.
Yote hayo yaonyesha kwamba Nyerere alikuwa
mja, mtu kama watu wengine. Hakuwa Mungu,
hakuwa malaika. Wala hakuwa mtume na hata
hakuwa mpigaji ramli. Na si kila alichokitamka
kilikuwa sahihi. Lakini binadamu yule alikuwa na
ulimi uliowalaza wengi na kuwafanya waache
kufikiri kwani alikuwa na kipaji cha kuwafanya
waamini kwamba kila alilolisema lilikuwa la kweli
kabisa na hivyo hapakuwa na haja ya kumfanya
mtu mwengine alifikirie. Ilikuwa nadra kumpata
mtu aliyethubutu kumpinga au kumkosoa, hasa
kadamnasi. Walikuwapo waliochelea kukiona cha
mtema kuni na wengine waliridhia kuwa
vibarakalla vya kuitika tu ‘hewala bwana.’
Moja ya makosa makubwa aliyoyafanya Nyerere
kwa kusudi au kwa sadfa, ni hilo la kuwafanya
wananchi wenzake waache kufikiri na wawe
wanayafuata tu aliyokuwa akiyasema bila ya
kuyazingatia au kuyapima.
Miongoni mwa aliyowahi kuyasema Nyerere ni
kuwa ati iwapo Zanzibar itaachana na
Tanganyika basi Tanganyika kutakuwa shuwari
lakini Wazanzibari wataanza kubaguana baina ya
Wapemba na Waunguja na halafu wataendelea
kutafutana asili zao.
Tangu wiki iliyopita waandishi kadhaa wa Bara
wamekuwa wakiyanukuu haya kana kwamba ni
maneno yenye ukweli usiopingika. Hii ni fitna tu;
na inatumiwa kuwatisha na kuwagawa
Wazanzibari.
Wakoloni walipowaona wanaowatawala
wanaungana kuwapinga, basi walitumia mbinu ya
kuwagawa wazidhoofishe nguvu zao ili waendelee
kuwatawala.
Mbinu kama hiyo inatumiwa siku hizi na baadhi
ya viongozi wa CCM wa Bara pamoja na baadhi
ya waandishi wa huko huko Bara ‘walioshtushwa’
na mwamko wa kisiasa uliowafanya Wazanzibari
wawe na ujasiri wa kuujadili kwa mapana na
marefu Muungano wa Tanzania.
Ujasiri huo umewafanya wengi wao waseme
kwamba ama wanaupinga muundo wa sasa wa
Muungano au hawautaki kabisa na wanataka
Zanzibar iwe dola huru yenye mamlaka yake
kamili.
Huo si mwamko wa leo au wa jana; tumekuwa
tukiugusia miaka nenda miaka rudi lakini
tukionekana kuwa ni wazushi na wazandiki. Sasa
mambo yanajidhihiri yenyewe. Matokeo yake ni
kwamba waliokuwa wakijidanganya sasa
wamegutuka na hawajui jinsi ya kulizuia hilo
wimbi la uzalendo Wakizanzibari minghairi ya
kutumia hoja finyu za kikabila na udini.
Mmoja amefika hadi ya kuandika kuhusu
‘Waarabu’ na ‘watu Weusi’ kana kwamba hao
wanaonasibishwa na uarabu ni wa rangi aina ya
pekee iliyo tofauti kabisa na ya Wazanzibari
wasio na asili ya Kiarabu. Mwandishi huyohuyo
alitishwa na sura rahimu ya Sheikh Farid Hadi
Ahmed, mmoja wa viongozi wakuu wa Uamsho.
Aliandika kwamba baada ya kuiona picha ya
Sheikh Farid yalimjia mawazo kwamba Uamsho si
jumuiya ya kidini na wala si ya Wazanzibari na
kwamba Sheikh Farid ametumwa (hakusema na
nani) kuwafitinisha Wazanzibari. Alichotaka
kusema mwandishi huyo ni kwamba kwa vile
Sheikh Farid ana asili ya Kiarabu basi Uamsho
inataka kuurejesha usultani.
Ni uchambuzi uchwara, tena wenye kutumia lugha
ya kibri. Unashtua kwa vile ni ‘uchambuzi’ wa
hatari unaofanana na simulizi za Wahutu wa
Rwanda kabla ya mauaji ya kimbari ya mwaka
1994 nchini humo.
Hizi fitna za ‘Upemba’ na ‘Uunguja’, za ‘ubwana’
na ‘utwana’ na za ‘ugaidi’ wa Uamsho ni fitna
zinazotiwa na watu walio maluuni. Lengo lao
kubwa ni kuwapotosha Wazanzibari wauzime
mjadala wa Muungano. Hawajali iwapo
watalitimiza lengo hilo kwa kuyakiuka maadili ya
uongozi au ya uandishi.
Hila wanazotumia ni kwanza, kuwafitinisha
Wazanzibari kwa kutia fitna za kikabila na za
kidini. Kwa mfano, wanawatisha wahafidhina wa
CCM/Zanzibar, wale wenye kusherehekea
kaulimbiu ya ‘Mapinduzi Daima’, kwa kuwaonya
ya kuwa Uamsho ina “msukumo wa kiarabu” na
kwamba kusudio lake ni hatimaye kuyapinga
Mapinduzi na kuirejesha Zanzibar katika
‘utumwa’. Maneno ya kijinga kabisa.
Hila yao ya pili ni kuwagonganisha vichwa
Waunguja na Wapemba kwa kutumia hoja zisizo
na mshiko wowote wa kimantiki. Wanasema
wamewapata Wapemba wengi wenye kutaka
Muungano uendelee kama ulivyo. Wamewahoji na
matamshi yao kusambazwa na magazeti fulani
nchini. Huu ni mfano mzuri wa propaganda ya
kitoto.
Hila yao ya tatu ni kutumia lugha kuparaganya
mambo. Ingawa Uamsho ni jumuiya kamili wao
badala yake wanasema kuwa hiki ni kikundi. Sio
kundi bali ‘kikundi.’ Na wanaishtumu jumuiya
hiyo kuwa ‘inawatumia’ baadhi ya vijana kufanya
vitendo vya kihuni vya kuchoma moto makanisa.
Hakuna ushahidi wa hili.
Nne, wanajaribu kuwatisha Watanzania na hasa
wakuu wa dunia hii kwa kuifananisha Jumuiya ya
Uamsho na mitandao ya kigaidi ya Al-Qa’eda,
Boko Haram na Al-Shabab. Bila ya shaka wenye
kueneza fitna hii hawajui walisemalo na
wanajikashifu si mbele ya Watanzania wenzao tu
bali hata machoni mwa balozi za nchi za
Magharibi.
Sijui kama wanaelewa ya kuwa maofisa wa
baadhi ya balozi za Magharibi wameshakutana
na viongozi wa Uamsho katika juhudi zao za
kuitathmini Jumuiya hiyo na wanayaelewa
makusudio halisi ya Uamsho.
Kwa hakika, kinyume na wanavyoandika baadhi
ya waandishi wa Bara, Jumuiya ya Uamsho
haikuzuka juzi. Imekuwako kwa muda wa
takriban miaka 10 sasa. Jumuiya hii ni kama
mwavuli ambao chini yake kuna jumuiya
mbalimbali za Kiislamu, pamoja na ile ya
maimamu.
Uamsho imekuwa ikiendesha harakati zake kwa
msaada wa taasisi za nchi za Magharibi. Ilikuwa
miongoni mwa waangalizi rasmi wa Uchaguzi
Mkuu uliopita na ripoti yake kuhusu uchaguzi huo
ni ya kupigiwa mfano kwa maelezo yake ya kina.
Kati ya wafadhili wa Jumuiya hiyo katika harakati
hizo za kuangalia uchaguzi lilikuwa shirika la
USAID la Marekani. Hata vizibao wanavovaa
baadhi ya viongozi wa Uamsho na vikuza sauti
vyao walipewa na Wamarekani wakati huo wa
uchaguzi uliopita.
Wenye kujuwa mambo watakwambia kwamba
kuna tofauti kubwa kama ya mbingu na ardhi kati
ya jumuiya ya Uamsho na mtandao wa Al-Qa’eda
au kundi la al-Shabab. Huwezi kabisa
kuzifananisha falsafa zao au makusidio yao. Hata
Boko Haram nayo licha ya mbinu inazozitumia
inatofautiana sana na al-Qa’eda.
Huko Zanzibar mafatani hawa wana washirika
wanaojulikana. Nao ni wale wanaochomwa na
kuwapo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).
Ndiyo maana wakaruka harakaharaka kuwatupia
lawama za machafuko ya hivi karibuni viongozi
wa CUF waliomo kwenye SUK na kutaka
watimuliwe kutoka serikalini. Na ni wao
waliohusika na vipeperushi vilivyotolewa wiki
iliyopita kuwafitinisha Wapemba na Waunguja.
Na ni haohao wenye kujaribu kuwachimba waasisi
wakuu wa Maridhiano yaani Rais mstaafu Amani
Abeid Karume na Maalim Seif Sharif Hamad.
Inasikitisha kuwaona baadhi ya Wabara wenye
kujigamba kuwa ni wasomi wakitaka mijadala ya
kisiasa ipigwe marufuku katika majukwaa ya
kidini. Hawaelewi kwamba ni dhima ya dini za
Ukristo na Uislamu kuzungumzia na kuyatafutia
ufumbuzi mambo yanayoyagusa maisha ya kila
siku ya waumini wa dini hizo. Na mambo hayo
yawe yepi kama si ya kisiasa?
La kutisha ni kuwa ‘wasomi’ hao wanamtaka
Rais Jakaya Kikwete awachukulie hatua za
kimabavu wakuu wenzake walio serikalini kwa
kisingizio kuwa ati wanaunga mkono harakati za
Uamsho.
Ulimwengu haukufunga macho wala haukuziba
masikio. Unawaona na kuwasikia. La ajabu ni
kwamba wanasiasa na waandishi wenye
kuchochea hisia kama hizo wamesahau ni nyakati
gani tulizo nazo na ni ulimwengu gani tulio nao.
Katika ulimwengu wao wa leo Wazanzibari
wanasema hawakubali tena kugawanywa kwa
propaganda za kikabila au za kidini.
Inatisha kwamba kuna wanasiasa na waandishi
waliosahau kwamba siku hizi kuna Mahakama ya
Jinai ya Kimataifa (ICC) na mahakama nyingine
mahsusi za kimataifa, mithili ya ile Mahakama
Maalumu ya Sierra Leone. Mahakama kama ile ya
Sierra Leone inaweza kuundwa mara moja na
Umoja wa Mataifa kuwatia adabu wenye kupalilia
fitna zinazoweza kuzusha mauaji ya kimbari.
Ni hiyo Mahakama Maalumu ya Sierra Leone
iliyomhukumu Charles Taylor, rais wa zamani wa
Liberia, kifungo cha miaka 80 baada ya
kupatikana na hatia ya kuishushia nakama Sierra
Leone.
Dhana waliyonayo baadhi ya wasomi na
waandishi wa Bara ni kwamba viongozi wa
Uamsho ni mijitu isiyosoma. Kuna mmoja
aliyepandwa na jeuri na kuandika kwamba mbali
na kujua kusoma Qur’an viongozi hao ni watu
wasiojuwa kuandika wala kusoma.
Ukweli ni kwamba viongozi wa Uamsho ni
wasomi waliohitimu masomo ya chuo kikuu na
wana shahada za juu za uzamili katika fani
mbalimbali kama vile za uhandisi, sayansi na
jiografia. Ni wasomi wa nyanja zote — za dini na
dunia.
Mfano mzuri ni Sheikh Msellem ambaye mbali na
kuwa gwiji wa tafsiri ya Qur’an pia alisomea
taaluma ya hali ya hewa.
Baadhi yao walisoma katika Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam ambako walivutiwa na hotuba za kidini
za Professor Malik, mtaalamu wa fani ya
hesabati, ambazo ziliwashajiisha na kuwafanya
wawe na mwamko wa Kiislamu. Wengine
walisoma kwenye vyuo vikuu vya nje vikiwemo
vile vya Sudan, Saudi Arabia na Qatar.
Ni wazi kutokana na ripoti na taarifa zao kwamba
baadhi ya wasomi na waandishi wetu wa Bara
wanawadharau Wazanzibari. Nadhani hizo dharau
zao ndizo zinazowafumba macho wasiweze kuona
nani hasa aliyechochea fukuto hili la upinzani
dhidi ya makandamizo ya walioshika hatamu za
utawala wa Muungano.
Maandishi yao yamebainisha wazi kwamba
hawaamini ya kuwa Unguja na Pemba si majimbo
wala koloni za Bara. Inakirihisha kuona namna
wengi wao wanavyozitapika hadharani chuki zao
(na udini uliowapamba) bila ya hata staha na
uvumilivu wa kimaadili.

Raia Mwema
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
13,281
2,000
Aisee hivi chuki ni kipaji?naona babu zenu waliotaka kuwekwa daraja special nchi hii wamewarithisha chuki kubwa sana.
 
Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
14,777
2,000
Jamaa mwongo sana kwanza Guardian wamwambie aandike yeye kuhusu Nyerere? Pimbi kabisa huyu.
 
dullyhami

JF-Expert Member
Jun 4, 2012
563
195
Hongera sana Sheikh Ahmed Jabir kwa umahiri na weledi wako juu ya makala hii ya kusisimua.... nadhani ndugu zetu wa upande wa pili wameelewa vizuri sana, ndio maana hawana la kusema ispokuwa ni kejeli na dharau kwa muandishi, hii inainyesha jinsi gani lecture ilivyowaingia... Heko mwandishi endelea kutupa soma kwa kutumia vyema kalamu yako...
 
kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,092
2,000
Na Ahmed Rajab

ALIPOFARIKI dunia Mwalimu Julius Nyerere
Oktoba 14 mwaka 1999, gazeti la Guardian la
Uingereza liliniomba niandike makala maalumu ya
kuyatathmini maisha yake.
Nilipokuwa naanza kuiandika tathmini hiyo
iliyochapishwa siku ya pili yake, niliyakumbuka
aliyowahi kuyasema Mwenyekiti Mao wa China
kumhusu Josef Stalin, mtawala wa pili wa
Muungano wa Sovieti baada ya Vladimir Lenin.
Nami nikayatumia maneno hayohayo kuanzia
makala yangu kwa kuandika: Julius Nyerere was
"a great leader who made great mistakes," as one
ruler once famously said of another. ("Julius
Nyerere alikuwa "kiongozi mkubwa (adhimu)
aliyefanya makosa makubwa," chambilecho
mtawala mmoja aliyewahi kumuelezea hivyo
mtawala mwenzake.)
Nyerere alifanya makosa ya kinadharia, ya kifikra
na ya kiutendaji katika utekelezaji wa sera zake.
Sikulidhukuru jina la Stalin kwa sababu sikutaka
wasomaji wangu wafanye kosa la kudhania
namfananisha Nyerere na Stalin. Siamini kama
Nyerere alikuwa na uovu wa Stalin. Na kama
ilivyokuwa kwa Stalin si yote ya Nyerere
yaliyokuwa maovu. Alitenda mema yanayostahiki
sifa.
Watu wa kale wasema: "Kheri ya mja ni ulimi
wake na shari ya mja ni huohuo." Kwa ulimi
wake Nyerere aliwahi kutamka maneno ya maana
na mengine ya kibahaluli. Baadhi ya maneno yake
yalikuwa kama lulu na baadhi yalikuwa kama
utumbo kama pale, kwa mfano, aliposema kuwa
hakuna watu waitwao Waswahili. Nilimsikia
akiyasema hayo alipotoa hotuba katika ukumbi
wa London School of Economics alipokuwa
ziarani London kabla ya kuuacha urais.
Yote hayo yaonyesha kwamba Nyerere alikuwa
mja, mtu kama watu wengine. Hakuwa Mungu,
hakuwa malaika. Wala hakuwa mtume na hata
hakuwa mpigaji ramli. Na si kila alichokitamka
kilikuwa sahihi. Lakini binadamu yule alikuwa na
ulimi uliowalaza wengi na kuwafanya waache
kufikiri kwani alikuwa na kipaji cha kuwafanya
waamini kwamba kila alilolisema lilikuwa la kweli
kabisa na hivyo hapakuwa na haja ya kumfanya
mtu mwengine alifikirie. Ilikuwa nadra kumpata
mtu aliyethubutu kumpinga au kumkosoa, hasa
kadamnasi. Walikuwapo waliochelea kukiona cha
mtema kuni na wengine waliridhia kuwa
vibarakalla vya kuitika tu ‘hewala bwana.'
Moja ya makosa makubwa aliyoyafanya Nyerere
kwa kusudi au kwa sadfa, ni hilo la kuwafanya
wananchi wenzake waache kufikiri na wawe
wanayafuata tu aliyokuwa akiyasema bila ya
kuyazingatia au kuyapima.
Miongoni mwa aliyowahi kuyasema Nyerere ni
kuwa ati iwapo Zanzibar itaachana na
Tanganyika basi Tanganyika kutakuwa shuwari
lakini Wazanzibari wataanza kubaguana baina ya
Wapemba na Waunguja na halafu wataendelea
kutafutana asili zao.
Tangu wiki iliyopita waandishi kadhaa wa Bara
wamekuwa wakiyanukuu haya kana kwamba ni
maneno yenye ukweli usiopingika. Hii ni fitna tu;
na inatumiwa kuwatisha na kuwagawa
Wazanzibari.
Wakoloni walipowaona wanaowatawala
wanaungana kuwapinga, basi walitumia mbinu ya
kuwagawa wazidhoofishe nguvu zao ili waendelee
kuwatawala.
Mbinu kama hiyo inatumiwa siku hizi na baadhi
ya viongozi wa CCM wa Bara pamoja na baadhi
ya waandishi wa huko huko Bara ‘walioshtushwa'
na mwamko wa kisiasa uliowafanya Wazanzibari
wawe na ujasiri wa kuujadili kwa mapana na
marefu Muungano wa Tanzania.
Ujasiri huo umewafanya wengi wao waseme
kwamba ama wanaupinga muundo wa sasa wa
Muungano au hawautaki kabisa na wanataka
Zanzibar iwe dola huru yenye mamlaka yake
kamili.
Huo si mwamko wa leo au wa jana; tumekuwa
tukiugusia miaka nenda miaka rudi lakini
tukionekana kuwa ni wazushi na wazandiki. Sasa
mambo yanajidhihiri yenyewe. Matokeo yake ni
kwamba waliokuwa wakijidanganya sasa
wamegutuka na hawajui jinsi ya kulizuia hilo
wimbi la uzalendo Wakizanzibari minghairi ya
kutumia hoja finyu za kikabila na udini.
Mmoja amefika hadi ya kuandika kuhusu
‘Waarabu' na ‘watu Weusi' kana kwamba hao
wanaonasibishwa na uarabu ni wa rangi aina ya
pekee iliyo tofauti kabisa na ya Wazanzibari
wasio na asili ya Kiarabu. Mwandishi huyohuyo
alitishwa na sura rahimu ya Sheikh Farid Hadi
Ahmed, mmoja wa viongozi wakuu wa Uamsho.
Aliandika kwamba baada ya kuiona picha ya
Sheikh Farid yalimjia mawazo kwamba Uamsho si
jumuiya ya kidini na wala si ya Wazanzibari na
kwamba Sheikh Farid ametumwa (hakusema na
nani) kuwafitinisha Wazanzibari. Alichotaka
kusema mwandishi huyo ni kwamba kwa vile
Sheikh Farid ana asili ya Kiarabu basi Uamsho
inataka kuurejesha usultani.
Ni uchambuzi uchwara, tena wenye kutumia lugha
ya kibri. Unashtua kwa vile ni ‘uchambuzi' wa
hatari unaofanana na simulizi za Wahutu wa
Rwanda kabla ya mauaji ya kimbari ya mwaka
1994 nchini humo.
Hizi fitna za ‘Upemba' na ‘Uunguja', za ‘ubwana'
na ‘utwana' na za ‘ugaidi' wa Uamsho ni fitna
zinazotiwa na watu walio maluuni. Lengo lao
kubwa ni kuwapotosha Wazanzibari wauzime
mjadala wa Muungano. Hawajali iwapo
watalitimiza lengo hilo kwa kuyakiuka maadili ya
uongozi au ya uandishi.
Hila wanazotumia ni kwanza, kuwafitinisha
Wazanzibari kwa kutia fitna za kikabila na za
kidini. Kwa mfano, wanawatisha wahafidhina wa
CCM/Zanzibar, wale wenye kusherehekea
kaulimbiu ya ‘Mapinduzi Daima', kwa kuwaonya
ya kuwa Uamsho ina "msukumo wa kiarabu" na
kwamba kusudio lake ni hatimaye kuyapinga
Mapinduzi na kuirejesha Zanzibar katika
‘utumwa'. Maneno ya kijinga kabisa.
Hila yao ya pili ni kuwagonganisha vichwa
Waunguja na Wapemba kwa kutumia hoja zisizo
na mshiko wowote wa kimantiki. Wanasema
wamewapata Wapemba wengi wenye kutaka
Muungano uendelee kama ulivyo. Wamewahoji na
matamshi yao kusambazwa na magazeti fulani
nchini. Huu ni mfano mzuri wa propaganda ya
kitoto.
Hila yao ya tatu ni kutumia lugha kuparaganya
mambo. Ingawa Uamsho ni jumuiya kamili wao
badala yake wanasema kuwa hiki ni kikundi. Sio
kundi bali ‘kikundi.' Na wanaishtumu jumuiya
hiyo kuwa ‘inawatumia' baadhi ya vijana kufanya
vitendo vya kihuni vya kuchoma moto makanisa.
Hakuna ushahidi wa hili.
Nne, wanajaribu kuwatisha Watanzania na hasa
wakuu wa dunia hii kwa kuifananisha Jumuiya ya
Uamsho na mitandao ya kigaidi ya Al-Qa'eda,
Boko Haram na Al-Shabab. Bila ya shaka wenye
kueneza fitna hii hawajui walisemalo na
wanajikashifu si mbele ya Watanzania wenzao tu
bali hata machoni mwa balozi za nchi za
Magharibi.
Sijui kama wanaelewa ya kuwa maofisa wa
baadhi ya balozi za Magharibi wameshakutana
na viongozi wa Uamsho katika juhudi zao za
kuitathmini Jumuiya hiyo na wanayaelewa
makusudio halisi ya Uamsho.
Kwa hakika, kinyume na wanavyoandika baadhi
ya waandishi wa Bara, Jumuiya ya Uamsho
haikuzuka juzi. Imekuwako kwa muda wa
takriban miaka 10 sasa. Jumuiya hii ni kama
mwavuli ambao chini yake kuna jumuiya
mbalimbali za Kiislamu, pamoja na ile ya
maimamu.
Uamsho imekuwa ikiendesha harakati zake kwa
msaada wa taasisi za nchi za Magharibi. Ilikuwa
miongoni mwa waangalizi rasmi wa Uchaguzi
Mkuu uliopita na ripoti yake kuhusu uchaguzi huo
ni ya kupigiwa mfano kwa maelezo yake ya kina.
Kati ya wafadhili wa Jumuiya hiyo katika harakati
hizo za kuangalia uchaguzi lilikuwa shirika la
USAID la Marekani. Hata vizibao wanavovaa
baadhi ya viongozi wa Uamsho na vikuza sauti
vyao walipewa na Wamarekani wakati huo wa
uchaguzi uliopita.
Wenye kujuwa mambo watakwambia kwamba
kuna tofauti kubwa kama ya mbingu na ardhi kati
ya jumuiya ya Uamsho na mtandao wa Al-Qa'eda
au kundi la al-Shabab. Huwezi kabisa
kuzifananisha falsafa zao au makusidio yao. Hata
Boko Haram nayo licha ya mbinu inazozitumia
inatofautiana sana na al-Qa'eda.
Huko Zanzibar mafatani hawa wana washirika
wanaojulikana. Nao ni wale wanaochomwa na
kuwapo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).
Ndiyo maana wakaruka harakaharaka kuwatupia
lawama za machafuko ya hivi karibuni viongozi
wa CUF waliomo kwenye SUK na kutaka
watimuliwe kutoka serikalini. Na ni wao
waliohusika na vipeperushi vilivyotolewa wiki
iliyopita kuwafitinisha Wapemba na Waunguja.
Na ni haohao wenye kujaribu kuwachimba waasisi
wakuu wa Maridhiano yaani Rais mstaafu Amani
Abeid Karume na Maalim Seif Sharif Hamad.
Inasikitisha kuwaona baadhi ya Wabara wenye
kujigamba kuwa ni wasomi wakitaka mijadala ya
kisiasa ipigwe marufuku katika majukwaa ya
kidini. Hawaelewi kwamba ni dhima ya dini za
Ukristo na Uislamu kuzungumzia na kuyatafutia
ufumbuzi mambo yanayoyagusa maisha ya kila
siku ya waumini wa dini hizo. Na mambo hayo
yawe yepi kama si ya kisiasa?
La kutisha ni kuwa ‘wasomi' hao wanamtaka
Rais Jakaya Kikwete awachukulie hatua za
kimabavu wakuu wenzake walio serikalini kwa
kisingizio kuwa ati wanaunga mkono harakati za
Uamsho.
Ulimwengu haukufunga macho wala haukuziba
masikio. Unawaona na kuwasikia. La ajabu ni
kwamba wanasiasa na waandishi wenye
kuchochea hisia kama hizo wamesahau ni nyakati
gani tulizo nazo na ni ulimwengu gani tulio nao.
Katika ulimwengu wao wa leo Wazanzibari
wanasema hawakubali tena kugawanywa kwa
propaganda za kikabila au za kidini.
Inatisha kwamba kuna wanasiasa na waandishi
waliosahau kwamba siku hizi kuna Mahakama ya
Jinai ya Kimataifa (ICC) na mahakama nyingine
mahsusi za kimataifa, mithili ya ile Mahakama
Maalumu ya Sierra Leone. Mahakama kama ile ya
Sierra Leone inaweza kuundwa mara moja na
Umoja wa Mataifa kuwatia adabu wenye kupalilia
fitna zinazoweza kuzusha mauaji ya kimbari.
Ni hiyo Mahakama Maalumu ya Sierra Leone
iliyomhukumu Charles Taylor, rais wa zamani wa
Liberia, kifungo cha miaka 80 baada ya
kupatikana na hatia ya kuishushia nakama Sierra
Leone.
Dhana waliyonayo baadhi ya wasomi na
waandishi wa Bara ni kwamba viongozi wa
Uamsho ni mijitu isiyosoma. Kuna mmoja
aliyepandwa na jeuri na kuandika kwamba mbali
na kujua kusoma Qur'an viongozi hao ni watu
wasiojuwa kuandika wala kusoma.
Ukweli ni kwamba viongozi wa Uamsho ni
wasomi waliohitimu masomo ya chuo kikuu na
wana shahada za juu za uzamili katika fani
mbalimbali kama vile za uhandisi, sayansi na
jiografia. Ni wasomi wa nyanja zote - za dini na
dunia.
Mfano mzuri ni Sheikh Msellem ambaye mbali na
kuwa gwiji wa tafsiri ya Qur'an pia alisomea
taaluma ya hali ya hewa.
Baadhi yao walisoma katika Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam ambako walivutiwa na hotuba za kidini
za Professor Malik, mtaalamu wa fani ya
hesabati, ambazo ziliwashajiisha na kuwafanya
wawe na mwamko wa Kiislamu. Wengine
walisoma kwenye vyuo vikuu vya nje vikiwemo
vile vya Sudan, Saudi Arabia na Qatar.
Ni wazi kutokana na ripoti na taarifa zao kwamba
baadhi ya wasomi na waandishi wetu wa Bara
wanawadharau Wazanzibari. Nadhani hizo dharau
zao ndizo zinazowafumba macho wasiweze kuona
nani hasa aliyechochea fukuto hili la upinzani
dhidi ya makandamizo ya walioshika hatamu za
utawala wa Muungano.
Maandishi yao yamebainisha wazi kwamba
hawaamini ya kuwa Unguja na Pemba si majimbo
wala koloni za Bara. Inakirihisha kuona namna
wengi wao wanavyozitapika hadharani chuki zao
(na udini uliowapamba) bila ya hata staha na
uvumilivu wa kimaadili.

Raia Mwema
Mbona kama propaganda ya ISIL. Kuzungusha zungusha maneno hata hueleweki nia yako nini.
 
aluba-k

Member
Nov 2, 2014
16
0
mmmh!huwa najiuliza sana mbna kila wakat huyo ahmed rajab anaandka abt nyerere? this is not the first time naona hili, nadhani ana taaluma kubwa sana but bado hajawa objective ktk uandshi wake ni subjective sana... ajarb kuwa objective mana habari gani isiyo na mizania?...
 
idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
23,881
2,000
Mkuu uliopita na ripoti yake kuhusu uchaguzi huo
ni ya kupigiwa mfano kwa maelezo yake ya kina.
Kati ya wafadhili wa Jumuiya hiyo katika harakati
hizo za kuangalia uchaguzi lilikuwa shirika la
USAID la Marekani. Hata vizibao wanavovaa
baadhi ya viongozi wa Uamsho na vikuza sauti
vyao walipewa na Wamarekani wakati huo wa
uchaguzi uliopita.
Nimeamini kila penye kundi la kigaidi USA yupo nyuma yao.!
 
yogan1

Member
Oct 18, 2014
21
0
Ukitafakari kwa kina utamuelewa anamaanisha nn uandishi mahiri huu.Wengi wa wanahabari hawajui kuwa siku moja wanaweza kuwajibika kwa habari zao!.Haya ahsante Ahmed Rajab
 
bantulile

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,573
1,250
Nimesoma hadithi hii sijamaliza, lakini sijui mantiki yake hasa ni kusema ubaya wa Nyerere au kutetea ubaguzi wa upemba na uunguja? Ubaguzi wa uunguja na ubpemba hakuanzisha Nyerere alifafanua historia. Ubaguzi huanza kidogokidogo na huendelea kukua. Anayepinga hili hamping mwalimu Nyerere anapinga historia. Hakuna mahali Nyerere amewahi kuwazuia watu kufikiri. Kufikiri ni kitendo ambacho hakizuiliki kwa sababu hufanyika ndani ya ubongo wa mtu na ubongo hauonekani. Kama kuna jambo ambalo binadamu ana uhuru binafsi basi ni kufikiri maana mtu anaweza kulala na mke wake kitandani huku akimfikiria hawala yake na mke wake asijue na wala asizuie. Kusema Nyerere aliwazuia watu kufikiri ni kumpa uwezo wa kimungu
Na Ahmed Rajab

ALIPOFARIKI dunia Mwalimu Julius Nyerere
Oktoba 14 mwaka 1999, gazeti la Guardian la
Uingereza liliniomba niandike makala maalumu ya
kuyatathmini maisha yake.
Nilipokuwa naanza kuiandika tathmini hiyo
iliyochapishwa siku ya pili yake, niliyakumbuka
aliyowahi kuyasema Mwenyekiti Mao wa China
kumhusu Josef Stalin, mtawala wa pili wa
Muungano wa Sovieti baada ya Vladimir Lenin.
Nami nikayatumia maneno hayohayo kuanzia
makala yangu kwa kuandika: Julius Nyerere was
"a great leader who made great mistakes," as one
ruler once famously said of another. ("Julius
Nyerere alikuwa "kiongozi mkubwa (adhimu)
aliyefanya makosa makubwa," chambilecho
mtawala mmoja aliyewahi kumuelezea hivyo
mtawala mwenzake.)
Nyerere alifanya makosa ya kinadharia, ya kifikra
na ya kiutendaji katika utekelezaji wa sera zake.
Sikulidhukuru jina la Stalin kwa sababu sikutaka
wasomaji wangu wafanye kosa la kudhania
namfananisha Nyerere na Stalin. Siamini kama
Nyerere alikuwa na uovu wa Stalin. Na kama
ilivyokuwa kwa Stalin si yote ya Nyerere
yaliyokuwa maovu. Alitenda mema yanayostahiki
sifa.
Watu wa kale wasema: "Kheri ya mja ni ulimi
wake na shari ya mja ni huohuo." Kwa ulimi
wake Nyerere aliwahi kutamka maneno ya maana
na mengine ya kibahaluli. Baadhi ya maneno yake
yalikuwa kama lulu na baadhi yalikuwa kama
utumbo kama pale, kwa mfano, aliposema kuwa
hakuna watu waitwao Waswahili. Nilimsikia
akiyasema hayo alipotoa hotuba katika ukumbi
wa London School of Economics alipokuwa
ziarani London kabla ya kuuacha urais.
Yote hayo yaonyesha kwamba Nyerere alikuwa
mja, mtu kama watu wengine. Hakuwa Mungu,
hakuwa malaika. Wala hakuwa mtume na hata
hakuwa mpigaji ramli. Na si kila alichokitamka
kilikuwa sahihi. Lakini binadamu yule alikuwa na
ulimi uliowalaza wengi na kuwafanya waache
kufikiri kwani alikuwa na kipaji cha kuwafanya
waamini kwamba kila alilolisema lilikuwa la kweli
kabisa na hivyo hapakuwa na haja ya kumfanya
mtu mwengine alifikirie. Ilikuwa nadra kumpata
mtu aliyethubutu kumpinga au kumkosoa, hasa
kadamnasi. Walikuwapo waliochelea kukiona cha
mtema kuni na wengine waliridhia kuwa
vibarakalla vya kuitika tu ‘hewala bwana.'
Moja ya makosa makubwa aliyoyafanya Nyerere
kwa kusudi au kwa sadfa, ni hilo la kuwafanya
wananchi wenzake waache kufikiri na wawe
wanayafuata tu aliyokuwa akiyasema bila ya
kuyazingatia au kuyapima.
Miongoni mwa aliyowahi kuyasema Nyerere ni
kuwa ati iwapo Zanzibar itaachana na
Tanganyika basi Tanganyika kutakuwa shuwari
lakini Wazanzibari wataanza kubaguana baina ya
Wapemba na Waunguja na halafu wataendelea
kutafutana asili zao.
Tangu wiki iliyopita waandishi kadhaa wa Bara
wamekuwa wakiyanukuu haya kana kwamba ni
maneno yenye ukweli usiopingika. Hii ni fitna tu;
na inatumiwa kuwatisha na kuwagawa
Wazanzibari.
Wakoloni walipowaona wanaowatawala
wanaungana kuwapinga, basi walitumia mbinu ya
kuwagawa wazidhoofishe nguvu zao ili waendelee
kuwatawala.
Mbinu kama hiyo inatumiwa siku hizi na baadhi
ya viongozi wa CCM wa Bara pamoja na baadhi
ya waandishi wa huko huko Bara ‘walioshtushwa'
na mwamko wa kisiasa uliowafanya Wazanzibari
wawe na ujasiri wa kuujadili kwa mapana na
marefu Muungano wa Tanzania.
Ujasiri huo umewafanya wengi wao waseme
kwamba ama wanaupinga muundo wa sasa wa
Muungano au hawautaki kabisa na wanataka
Zanzibar iwe dola huru yenye mamlaka yake
kamili.
Huo si mwamko wa leo au wa jana; tumekuwa
tukiugusia miaka nenda miaka rudi lakini
tukionekana kuwa ni wazushi na wazandiki. Sasa
mambo yanajidhihiri yenyewe. Matokeo yake ni
kwamba waliokuwa wakijidanganya sasa
wamegutuka na hawajui jinsi ya kulizuia hilo
wimbi la uzalendo Wakizanzibari minghairi ya
kutumia hoja finyu za kikabila na udini.
Mmoja amefika hadi ya kuandika kuhusu
‘Waarabu' na ‘watu Weusi' kana kwamba hao
wanaonasibishwa na uarabu ni wa rangi aina ya
pekee iliyo tofauti kabisa na ya Wazanzibari
wasio na asili ya Kiarabu. Mwandishi huyohuyo
alitishwa na sura rahimu ya Sheikh Farid Hadi
Ahmed, mmoja wa viongozi wakuu wa Uamsho.
Aliandika kwamba baada ya kuiona picha ya
Sheikh Farid yalimjia mawazo kwamba Uamsho si
jumuiya ya kidini na wala si ya Wazanzibari na
kwamba Sheikh Farid ametumwa (hakusema na
nani) kuwafitinisha Wazanzibari. Alichotaka
kusema mwandishi huyo ni kwamba kwa vile
Sheikh Farid ana asili ya Kiarabu basi Uamsho
inataka kuurejesha usultani.
Ni uchambuzi uchwara, tena wenye kutumia lugha
ya kibri. Unashtua kwa vile ni ‘uchambuzi' wa
hatari unaofanana na simulizi za Wahutu wa
Rwanda kabla ya mauaji ya kimbari ya mwaka
1994 nchini humo.
Hizi fitna za ‘Upemba' na ‘Uunguja', za ‘ubwana'
na ‘utwana' na za ‘ugaidi' wa Uamsho ni fitna
zinazotiwa na watu walio maluuni. Lengo lao
kubwa ni kuwapotosha Wazanzibari wauzime
mjadala wa Muungano. Hawajali iwapo
watalitimiza lengo hilo kwa kuyakiuka maadili ya
uongozi au ya uandishi.
Hila wanazotumia ni kwanza, kuwafitinisha
Wazanzibari kwa kutia fitna za kikabila na za
kidini. Kwa mfano, wanawatisha wahafidhina wa
CCM/Zanzibar, wale wenye kusherehekea
kaulimbiu ya ‘Mapinduzi Daima', kwa kuwaonya
ya kuwa Uamsho ina "msukumo wa kiarabu" na
kwamba kusudio lake ni hatimaye kuyapinga
Mapinduzi na kuirejesha Zanzibar katika
‘utumwa'. Maneno ya kijinga kabisa.
Hila yao ya pili ni kuwagonganisha vichwa
Waunguja na Wapemba kwa kutumia hoja zisizo
na mshiko wowote wa kimantiki. Wanasema
wamewapata Wapemba wengi wenye kutaka
Muungano uendelee kama ulivyo. Wamewahoji na
matamshi yao kusambazwa na magazeti fulani
nchini. Huu ni mfano mzuri wa propaganda ya
kitoto.
Hila yao ya tatu ni kutumia lugha kuparaganya
mambo. Ingawa Uamsho ni jumuiya kamili wao
badala yake wanasema kuwa hiki ni kikundi. Sio
kundi bali ‘kikundi.' Na wanaishtumu jumuiya
hiyo kuwa ‘inawatumia' baadhi ya vijana kufanya
vitendo vya kihuni vya kuchoma moto makanisa.
Hakuna ushahidi wa hili.
Nne, wanajaribu kuwatisha Watanzania na hasa
wakuu wa dunia hii kwa kuifananisha Jumuiya ya
Uamsho na mitandao ya kigaidi ya Al-Qa'eda,
Boko Haram na Al-Shabab. Bila ya shaka wenye
kueneza fitna hii hawajui walisemalo na
wanajikashifu si mbele ya Watanzania wenzao tu
bali hata machoni mwa balozi za nchi za
Magharibi.
Sijui kama wanaelewa ya kuwa maofisa wa
baadhi ya balozi za Magharibi wameshakutana
na viongozi wa Uamsho katika juhudi zao za
kuitathmini Jumuiya hiyo na wanayaelewa
makusudio halisi ya Uamsho.
Kwa hakika, kinyume na wanavyoandika baadhi
ya waandishi wa Bara, Jumuiya ya Uamsho
haikuzuka juzi. Imekuwako kwa muda wa
takriban miaka 10 sasa. Jumuiya hii ni kama
mwavuli ambao chini yake kuna jumuiya
mbalimbali za Kiislamu, pamoja na ile ya
maimamu.
Uamsho imekuwa ikiendesha harakati zake kwa
msaada wa taasisi za nchi za Magharibi. Ilikuwa
miongoni mwa waangalizi rasmi wa Uchaguzi
Mkuu uliopita na ripoti yake kuhusu uchaguzi huo
ni ya kupigiwa mfano kwa maelezo yake ya kina.
Kati ya wafadhili wa Jumuiya hiyo katika harakati
hizo za kuangalia uchaguzi lilikuwa shirika la
USAID la Marekani. Hata vizibao wanavovaa
baadhi ya viongozi wa Uamsho na vikuza sauti
vyao walipewa na Wamarekani wakati huo wa
uchaguzi uliopita.
Wenye kujuwa mambo watakwambia kwamba
kuna tofauti kubwa kama ya mbingu na ardhi kati
ya jumuiya ya Uamsho na mtandao wa Al-Qa'eda
au kundi la al-Shabab. Huwezi kabisa
kuzifananisha falsafa zao au makusidio yao. Hata
Boko Haram nayo licha ya mbinu inazozitumia
inatofautiana sana na al-Qa'eda.
Huko Zanzibar mafatani hawa wana washirika
wanaojulikana. Nao ni wale wanaochomwa na
kuwapo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).
Ndiyo maana wakaruka harakaharaka kuwatupia
lawama za machafuko ya hivi karibuni viongozi
wa CUF waliomo kwenye SUK na kutaka
watimuliwe kutoka serikalini. Na ni wao
waliohusika na vipeperushi vilivyotolewa wiki
iliyopita kuwafitinisha Wapemba na Waunguja.
Na ni haohao wenye kujaribu kuwachimba waasisi
wakuu wa Maridhiano yaani Rais mstaafu Amani
Abeid Karume na Maalim Seif Sharif Hamad.
Inasikitisha kuwaona baadhi ya Wabara wenye
kujigamba kuwa ni wasomi wakitaka mijadala ya
kisiasa ipigwe marufuku katika majukwaa ya
kidini. Hawaelewi kwamba ni dhima ya dini za
Ukristo na Uislamu kuzungumzia na kuyatafutia
ufumbuzi mambo yanayoyagusa maisha ya kila
siku ya waumini wa dini hizo. Na mambo hayo
yawe yepi kama si ya kisiasa?
La kutisha ni kuwa ‘wasomi' hao wanamtaka
Rais Jakaya Kikwete awachukulie hatua za
kimabavu wakuu wenzake walio serikalini kwa
kisingizio kuwa ati wanaunga mkono harakati za
Uamsho.
Ulimwengu haukufunga macho wala haukuziba
masikio. Unawaona na kuwasikia. La ajabu ni
kwamba wanasiasa na waandishi wenye
kuchochea hisia kama hizo wamesahau ni nyakati
gani tulizo nazo na ni ulimwengu gani tulio nao.
Katika ulimwengu wao wa leo Wazanzibari
wanasema hawakubali tena kugawanywa kwa
propaganda za kikabila au za kidini.
Inatisha kwamba kuna wanasiasa na waandishi
waliosahau kwamba siku hizi kuna Mahakama ya
Jinai ya Kimataifa (ICC) na mahakama nyingine
mahsusi za kimataifa, mithili ya ile Mahakama
Maalumu ya Sierra Leone. Mahakama kama ile ya
Sierra Leone inaweza kuundwa mara moja na
Umoja wa Mataifa kuwatia adabu wenye kupalilia
fitna zinazoweza kuzusha mauaji ya kimbari.
Ni hiyo Mahakama Maalumu ya Sierra Leone
iliyomhukumu Charles Taylor, rais wa zamani wa
Liberia, kifungo cha miaka 80 baada ya
kupatikana na hatia ya kuishushia nakama Sierra
Leone.
Dhana waliyonayo baadhi ya wasomi na
waandishi wa Bara ni kwamba viongozi wa
Uamsho ni mijitu isiyosoma. Kuna mmoja
aliyepandwa na jeuri na kuandika kwamba mbali
na kujua kusoma Qur'an viongozi hao ni watu
wasiojuwa kuandika wala kusoma.
Ukweli ni kwamba viongozi wa Uamsho ni
wasomi waliohitimu masomo ya chuo kikuu na
wana shahada za juu za uzamili katika fani
mbalimbali kama vile za uhandisi, sayansi na
jiografia. Ni wasomi wa nyanja zote - za dini na
dunia.
Mfano mzuri ni Sheikh Msellem ambaye mbali na
kuwa gwiji wa tafsiri ya Qur'an pia alisomea
taaluma ya hali ya hewa.
Baadhi yao walisoma katika Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam ambako walivutiwa na hotuba za kidini
za Professor Malik, mtaalamu wa fani ya
hesabati, ambazo ziliwashajiisha na kuwafanya
wawe na mwamko wa Kiislamu. Wengine
walisoma kwenye vyuo vikuu vya nje vikiwemo
vile vya Sudan, Saudi Arabia na Qatar.
Ni wazi kutokana na ripoti na taarifa zao kwamba
baadhi ya wasomi na waandishi wetu wa Bara
wanawadharau Wazanzibari. Nadhani hizo dharau
zao ndizo zinazowafumba macho wasiweze kuona
nani hasa aliyechochea fukuto hili la upinzani
dhidi ya makandamizo ya walioshika hatamu za
utawala wa Muungano.
Maandishi yao yamebainisha wazi kwamba
hawaamini ya kuwa Unguja na Pemba si majimbo
wala koloni za Bara. Inakirihisha kuona namna
wengi wao wanavyozitapika hadharani chuki zao
(na udini uliowapamba) bila ya hata staha na
uvumilivu wa kimaadili.

Raia Mwema
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom