Wapare, Wachaga: Matambiko yamepitwa na wakati

TAMBIKO ni nini?

Tambiko ni ibada kamili, na ili ufanye tambiko ni lazima iwepo madhabahu, awepo mkuu wa madhabahu (au kuhani wa madhabahu), iwepo sadaka au kafara ya madhabahu (ambayo ni damu ya kuku au mbuzi au ng'ombe au binadamu) na wawepo walinzi wa madhabahu.

Kafara ya madhabahu inapokuwa nyingi ndivyo mafanikio yanakuwa rahisi wakati wa kutambika hasa inapokuwa ni damu ya binadamu.

Zipo sababu mbalimbali zinazofanya watu watafute msaada kwa miungu mingine. Kwa ufupi ni kuomba ulinzi kwa watoto au ulinzi kwa wanaukoo, kuomba ulinzi wa biashara, masomo, kilimo nk. au kuomba mafanikio ya kifedha kwenye biashara, kilimo, ufugaji na uvuvi.

Taratibu za ibada za matambiko zinatofautiana kutoka eneo moja na eneo jingine, lakini jambo kubwa linalofanyika ni mkuu wa familia au mkuu wa ukoo ambaye ndiye kuhani wa madhabahu, kuwaalika ndugu wanaohusika na kufanya maandalizi ya tambiko, ubani huchomwa kwenye madhabahu kuwaita majini zipo dua za kuyaita husomwa na kuhani, chakula hupikwa na mnyama huchijwa, ni lazima achinjiwe kwenye madhabahu ya ukoo au familia.

Kabla ya vyakula kuanza kuliwa familia au ukoo ni lazima waapishwe, ni lazima uape. Kuna aina nyingi za viapo inategemea na aina ya shughuli. Mara nyingi damu huandaliwa kwenye kibuyu na huchanganywa na vitu vingine mbalimbali na kusomewa dua, kuhani hunyanyua kibuyu na kunywa damu, kisha inazungushwa kwa watu wote nao huinywa damu hiyo ya tambiko. Yapo maneno anayosema kuhani, kwamba yeyote atakayekwenda kinyume cha mambo hayo waliyokubalina basi balaa fulani na limpate.

Kisha damu hiyo hupewa majini yaliyohudhuria, nimesema damu inapokuwa nyingi, majini huifurahia sana, na huwapa nguvu ya ajabu wakisubiri maelekezo kutoka kwa kuhani.

Kuhitimisha kuhani huwaelekeza majini jambo wanalotakiwa kufanya, kama ni kupata mali au ulinzi, majini kabila ya kufanya lolote ni lazima yaende shimoni kwa mkuu kupeleka taarifa za kikao, kama waliomba ulinzi, kuzimu hurusha kamba isiyoonekana na kuwafunga wote walioshiriki kunywa damu kwenye kibuyu, binadamu na majini hufungwa pamoja.

Huko shimoni shetani anaitwa MKUU, siku ukibahatika kushuka usifanye kosa na kumwita shetani, utachapwa bakora zilizoenda shule. Mambo ya huko ni Mkuu nimekuja. Mkuu ninaondoka, Mkuu Mkuu Mkuu....

Nini hatima ya mambo haya.

Baada ya hiyo karamu ya kuzimu, wapo wanafamilia ambao hawataweza kufuata viapo walivyoapa na ikitokea hivyo, kumbuka kuzimu ilirusha kamba zikawafunga pamoja familia yote ambao ni mkataba kamili wa kisheria kati ya binadamu na kuzimu, na kwa kawaida mtu anayevunja mkataba kuna gharama zake na ni lazima ukoo au familia hiyo wazilipe, ni lazima.

Madhara ya adhabu hizi hudumu vizazi vitatu au vinne, pengine matatizo unayoyapata leo yalifanywa na mababu zako mwaka 1750.

Adhabu zenyewe zinafanana sana kwa wanaukoo wote walioshiriki na wanaozaliwa sasa na watakaondelea kuzaliwa, ndiyo maana utakuta watu wanasema ugonjwa huu ni ugonjwa wa ukoo wetu (Kamba hizo zilirushwa kutoka kuzimu) au kwenye ukoo wetu hakuna mtu anayeishi zaidi ya miaka 40, au kwenye ukoo wetu wasichana huzalia nyumbani na hawaolewi, au ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa wa ukoo wetu, au kwenye ukoo wetu hakuna mtu yeyote aliyesoma akamaliza elimu ya msingi, au kwenye ukoo wetu kila wakati tunapatwa na ajali za kila aina, ajali za magari, ajali za moto, ajali za kugogwa na nyoka, ajali ajali ajali...

Kama umeshaona picha za watumwa walivyokuwa wanafungwa kwa kamba na waarabu wakisafirishwa kutoka bara kuletwa pwani ndivyo hivyo hivyo hizo kamba zinavofunga familia.

Je suluhisho la mambo haya lipo?

Ndiyo lipo.....
 
Sioni tofaauti iliyopo kati ya torati na maisha ya wazee wa zamani kabla ya ukio wa dini! Ikumbukwe pia jamii ya kabla ya ukristo imebarikiwa kuliko sasa! Je sababu ni ipi?
 
walikuwa wanatoa kondoo/ng'ombe wanono kama kafara kwa Mungu.
 
neno la Mungu lilikuwa na mapungufu?!

Kutimilzwa ni kitendocha kutamatisha au kukamilisha jambo fulani hivyo mambo yaliyokamilishwa baada ya kuja kwa Yesu ni kutokulipa kisasi, kuto kutoa damu za wanyama kama maondoleo ya dhambi, kondoa ulaziama wa kwenda kuabudu Jerusalem, Kuja kwa Roho Mtakatifu, Kuondoa ulazima wa kuabudu huku umelielekea Hekalu la Mfalme Suleiman, Kutumia Damu ya Yesu kama itakasayo n.k

Agano la kale lina Torati na Manabii. Torati haina manabii.

Kuhusu manabii ndio agano la kale na jipya yote yanayo manabii na sanasana Kumbukumbu la Torati ndio Torati yenyewe ila kuna maagizo ya Mungu [Torati] ambayo yametolewa na Mungu kupitia manabii tofauti katika vitabu tofauti ndani ya Agano la kale ndio maana inaonekana kama Agano la Kale lote ni Torati.

Unaweza nipa maneno machache jinsi ya kuishika Torati kwa kipindi hiki cha Ukristo.

Shika NENO la Mungu ambaye ndiye YESU KRISTO.

[h=1]Luka 18 : 17-23[/h]18.17 Amin, nawaambia, Mtu ye yote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hauingii kamwe.
18.18 Tena, mtu mkubwa mmoja alimwuliza, akisema, Mwalimu mwema, nifanye nini ili nipate kuurithi uzima wa milele?
18.19 Yesu akamwambia, Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, naye ndiye Mungu.
18.20 Wazijua amri; Usizini, Usiue, Usiibe, Usishuhudie uongo, Waheshimu baba yako na mama yako.
18.21 Akasema, Hayo yote nimeyashika tangu utoto wangu.
18.22 Yesu aliposikia hayo alimwambia, Umepungukiwa na neno moja bado; viuze ulivyo navyo vyote, ukawagawanyie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha, njoo unifuate.
18.23 Lakini aliposikia hayo alihuzunika sana, maana alikuwa na mali nyingi.
 
TAMBIKO ni nini?

Tambiko ni ibada kamili, na ili ufanye tambiko ni lazima iwepo madhabahu, awepo mkuu wa madhabahu (au kuhani wa madhabahu), iwepo sadaka au kafara ya madhabahu (ambayo ni damu ya kuku au mbuzi au ng'ombe au binadamu) na wawepo walinzi wa madhabahu.

Kafara ya madhabahu inapokuwa nyingi ndivyo mafanikio yanakuwa rahisi wakati wa kutambika hasa inapokuwa ni damu ya binadamu.

Zipo sababu mbalimbali zinazofanya watu watafute msaada kwa miungu mingine. Kwa ufupi ni kuomba ulinzi kwa watoto au ulinzi kwa wanaukoo, kuomba ulinzi wa biashara, masomo, kilimo nk. au kuomba mafanikio ya kifedha kwenye biashara, kilimo, ufugaji na uvuvi.

Taratibu za ibada za matambiko zinatofautiana kutoka eneo moja na eneo jingine, lakini jambo kubwa linalofanyika ni mkuu wa familia au mkuu wa ukoo ambaye ndiye kuhani wa madhabahu, kuwaalika ndugu wanaohusika na kufanya maandalizi ya tambiko, ubani huchomwa kwenye madhabahu kuwaita majini zipo dua za kuyaita husomwa na kuhani, chakula hupikwa na mnyama huchijwa, ni lazima achinjiwe kwenye madhabahu ya ukoo au familia.

Kabla ya vyakula kuanza kuliwa familia au ukoo ni lazima waapishwe, ni lazima uape. Kuna aina nyingi za viapo inategemea na aina ya shughuli. Mara nyingi damu huandaliwa kwenye kibuyu na huchanganywa na vitu vingine mbalimbali na kusomewa dua, kuhani hunyanyua kibuyu na kunywa damu, kisha inazungushwa kwa watu wote nao huinywa damu hiyo ya tambiko. Yapo maneno anayosema kuhani, kwamba yeyote atakayekwenda kinyume cha mambo hayo waliyokubalina basi balaa fulani na limpate.

Kisha damu hiyo hupewa majini yaliyohudhuria, nimesema damu inapokuwa nyingi, majini huifurahia sana, na huwapa nguvu ya ajabu wakisubiri maelekezo kutoka kwa kuhani.

Kuhitimisha kuhani huwaelekeza majini jambo wanalotakiwa kufanya, kama ni kupata mali au ulinzi, majini kabila ya kufanya lolote ni lazima yaende shimoni kwa mkuu kupeleka taarifa za kikao, kama waliomba ulinzi, kuzimu hurusha kamba isiyoonekana na kuwafunga wote walioshiriki kunywa damu kwenye kibuyu, binadamu na majini hufungwa pamoja.

Huko shimoni shetani anaitwa MKUU, siku ukibahatika kushuka usifanye kosa na kumwita shetani, utachapwa bakora zilizoenda shule. Mambo ya huko ni Mkuu nimekuja. Mkuu ninaondoka, Mkuu Mkuu Mkuu....

Nini hatima ya mambo haya.

Baada ya hiyo karamu ya kuzimu, wapo wanafamilia ambao hawataweza kufuata viapo walivyoapa na ikitokea hivyo, kumbuka kuzimu ilirusha kamba zikawafunga pamoja familia yote ambao ni mkataba kamili wa kisheria kati ya binadamu na kuzimu, na kwa kawaida mtu anayevunja mkataba kuna gharama zake na ni lazima ukoo au familia hiyo wazilipe, ni lazima.

Madhara ya adhabu hizi hudumu vizazi vitatu au vinne, pengine matatizo unayoyapata leo yalifanywa na mababu zako mwaka 1750.

Adhabu zenyewe zinafanana sana kwa wanaukoo wote walioshiriki na wanaozaliwa sasa na watakaondelea kuzaliwa, ndiyo maana utakuta watu wanasema ugonjwa huu ni ugonjwa wa ukoo wetu (Kamba hizo zilirushwa kutoka kuzimu) au kwenye ukoo wetu hakuna mtu anayeishi zaidi ya miaka 40, au kwenye ukoo wetu wasichana huzalia nyumbani na hawaolewi, au ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa wa ukoo wetu, au kwenye ukoo wetu hakuna mtu yeyote aliyesoma akamaliza elimu ya msingi, au kwenye ukoo wetu kila wakati tunapatwa na ajali za kila aina, ajali za magari, ajali za moto, ajali za kugogwa na nyoka, ajali ajali ajali...

Kama umeshaona picha za watumwa walivyokuwa wanafungwa kwa kamba na waarabu wakisafirishwa kutoka bara kuletwa pwani ndivyo hivyo hivyo hizo kamba zinavofunga familia.

Je suluhisho la mambo haya lipo?

Ndiyo lipo.....
Nakukubali sana Majimoto kwa facts na details nakuomba uzidi kufunguka kama kule kwenye Biashara ya Uchawi.

Regards.
 
Last edited by a moderator:
[h=1]Luka 18 : 17-23[/h]18.17 Amin, nawaambia, Mtu ye yote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hauingii kamwe.
18.18 Tena, mtu mkubwa mmoja alimwuliza, akisema, Mwalimu mwema, nifanye nini ili nipate kuurithi uzima wa milele?
18.19 Yesu akamwambia, Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, naye ndiye Mungu.
18.20 Wazijua amri; Usizini, Usiue, Usiibe, Usishuhudie uongo, Waheshimu baba yako na mama yako.
18.21 Akasema, Hayo yote nimeyashika tangu utoto wangu.
18.22 Yesu aliposikia hayo alimwambia, Umepungukiwa na neno moja bado; viuze ulivyo navyo vyote, ukawagawanyie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha, njoo unifuate.
18.23 Lakini aliposikia hayo alihuzunika sana, maana alikuwa na mali nyingi.

mbona haya hayashikwi na kanisa la sasa, yalitimilizwa na kanisa la kwanza, iwaje unanipa peke yangu mzigo mzito, labda hata nawe haujashiriki kuufunga?
'umeuza mali zako zote na kuwapa mapato masikini'!

Hapa (20) hazikugusiwa amri kama nne za mwanzo zimepoteza umuhimu wake?
 
Wewe ni Mkristo?

Kama ndiyo nakushauri umuone Mchungaji wako kwa ufafanuzi zaidi.

Kama siyo nakushauri utafute kanisa linalohubiri wokovu lililo karibu nawe ili ukulie wokovu.
 
Kila kanisa linaubiri wokovu, sina uhakika kama kuna lisilo hubiri wokovu!

Kama kanisa lenu mnafuata maagizo yote ya Biblia nialike nijiunge.
Usisahau kanisa wanatakiwa kuishi pamoja mkishirikiana kwa kila jambo.
 
Nani kakuambia wachungaji hawafanyi matambiko! Kanisa la Roman Catholic hawazungumzii wala kukataza matambiko na wanafanya kwa siri!
 
Kila kanisa linaubiri wokovu, sina uhakika kama kuna lisilo hubiri wokovu!

Kama kanisa lenu mnafuata maagizo yote ya Biblia nialike nijiunge.
Usisahau kanisa wanatakiwa kuishi pamoja mkishirikiana kwa kila jambo.
Yah! Sure.
 
Aiyer, Ntuzu na Mkuu wa chuo kama mtaweza piteni hapa tupate elimu kidogo kutoka kwenu....michango yenu ndio shule yetu...Natanguliza shukrani kwenu.
 
Je suluhisho la mambo haya lipo?

Ndiyo lipo.....

(2 Samweli 22:6 Kamba za kuzimu zilinizunguka; Mitego ya mauti ikanikabili.)

Kumbuka kuwa mazindiko hayo hayakufanywa na wazazi wako, wala wewe hukuhusika kabisa, shughuli hii ilifanyika labda mwaka 1750. Umeishi maisha ya kumcha Mungu na hakuna wakati umenena makufuru kuhusu Mungu, lakini mkataba waliongia wakale zako ndio unasababisha matatizo makubwa maishani mwako, wamekufunga kiasi kwamba hufurukuti, kila mara ni mgonjwa, magonjwa yasiyosikia dawa chumbani kwako kumejaa dawa utafikiri ni phamacy, hadi mnayaita magonjwa ya ukoo. Pamoja na ulokole wako lakini maumivu unayoyapata hayana maelezo. Umewekewa mikono na Wachungaji wa kila aina tatizo linapungua, lakini baada ya muda linarudia palepale.

(Zaburi 116:3 Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni😉

Kushughulikia tatizo unatakiwa ujue chanzo cha tatizo lako, ukijua chanzo msiba wako utakuwa umekwisha.

Jambo la kufanya ni kuzikata hizi kamba za kuzimu, mtu mmoja kwenye ukoo anaweza kabisa kuwaokoa ndugu zake wote baada ya kamba kukatwa. Peke yako huwezi kuzikata kwani wewe ni mfungwa, lazima umpate mkataji na mpiganaji jasiri, kamba zinapokatika matatizo yote yanakoma. Kumbuka kuna jeshi kubwa la majini na mapepo yaliyokuwa yanawatumikisha, hawa huwa hawakubali muondoke kirahisi hivyo, vita mpya inaanza kuanzia wakati huo wakijitahidi kurusha kamba tena, unatakiwa usimame imara kwa maombi, kwani ahadi ya Mungu ni kweli na AMINA.

[Isaya 41:12 Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako.
13 Kwa maana mimi, Bwana, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia]

​
 
[h=1]Luka 18 : 17-23[/h]18.17 Amin, nawaambia, Mtu ye yote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hauingii kamwe.
18.18 Tena, mtu mkubwa mmoja alimwuliza, akisema, Mwalimu mwema, nifanye nini ili nipate kuurithi uzima wa milele?
18.19 Yesu akamwambia, Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, naye ndiye Mungu.
18.20 Wazijua amri; Usizini, Usiue, Usiibe, Usishuhudie uongo, Waheshimu baba yako na mama yako.
18.21 Akasema, Hayo yote nimeyashika tangu utoto wangu.
18.22 Yesu aliposikia hayo alimwambia, Umepungukiwa na neno moja bado; viuze ulivyo navyo vyote, ukawagawanyie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha, njoo unifuate.
18.23 Lakini aliposikia hayo alihuzunika sana, maana alikuwa na mali nyingi.

Kwenye Biblia ya Raman hakuna hayo makatazo!
 
hivi vitu vinaenda na imani,kuna familia zinaweza kuwa ni nzuri sana kwenye kutambika lakini ni malofa wa kutupa,what i know kwenye kila mafanikio lazima kuwe na nguvu ya ziada,whether ni ya shetani au ya Mungu,hivyo basi ukifanya yale yampendezayo Mungu lazima utafanikiwa tena ni zaidi hata ya hayo matambiko
 
Kutimilizwa ni kuondolewa kwa mapungufu yaliyomo kwenye Torati baada ya kuja kwa Yesu na kukamilisha kazi yake.

Kwenye torati kuna unabii wa nyakati za mwisho mf. kitabu cha Daniel so lazima nabii kama hizo zitimie.

KUTIMILIZWA HAKUNA MAANA KWAMBA KUONDOA MAPUNGUFU!

KUTIMILIZA kuna Maana ya KUJAZIA NA NDIO MAANA YESU ANASEMA ATA ILE YODI MOJA AU NUKTA HAITAONDOKA!

Sasa huko KUONDOA KWAKO MAPUNGUFU UNAKITOA WAPI? huoni Yesu alikua anataka Watu WAFANYE HAKI KUANZIA ROHONI NA SI KUCHUKULIA SHERIA KM MATENDO? nitakutolea mfano hapa kidogo ktk hili ili uone KULE KUJAZIA KWA SHERIA AU KUTIMILIZWA!

SHERIA ktk Kutoka 20 inasema USIZINI.

Kuzini ni tendo ambalo mtu akifanya anakua amevunja SHERIA Hiyo ya kwamba USIZINI KWA KUFANYA LILE TENDO LENYEWE LA KUJAMIANA!

Lkn Yesu anataka HAKI ianzie moyoni huku akiwa hapingi ile SHERIA kuu isameyo USIZINI BALI ANAONGEZA KWA KUSEMA KWAMBA "NA MTU YEYOTE AKIMUANGALIA MWANAMKE KWA MATAMANIO AMEKWISHA ZINI NAYE" huku NDIO KUJAZIWA KWA SHERIA AU KUTIMILIZWA NA SI KWAMBA ETI KULIKUA NA MAPUNGUFU NDIO YESU AKAONGEZEA!

Sijui mpk hapo iko sawa? Maana nimeona pleo anatembea Na wewe akiwa KM hajarizika Na hoja zako!

Thx!
 
Last edited by a moderator:
Aiyer, Ntuzu na Mkuu wa chuo kama mtaweza piteni hapa tupate elimu kidogo kutoka kwenu....michango yenu ndio shule yetu...Natanguliza shukrani kwenu.

Nimeshakuja Mkuu!

Lkn matambiko AU KAFARA asili Yake AU yalianzia Wapi Mkuu?

Labda mleta HOJA ANGEWEZA KUTUELEWESHA HILI KWANZA ILI TUPATE PA KUANZIA!
 
Back
Top Bottom