Wapare, Wachaga: Matambiko yamepitwa na wakati

Wiyelelee

JF-Expert Member
Nov 9, 2012
1,071
347
Kuoa au kuolewa na makabila haya lazima uwe mvumilivu sana. Pengine watu hujitumbukiza katika uhusiano bila kufanya utafiti wa kina. Nilimsindikiza rafiki yangu kutoa mahali kwa Wapare na niliona mambo ya ajabu sana! Tukaambiwa twende akatabulishwe kwa mizimu ya Kipareni.

Nilishangaa wakati nashuhudia wanavyotambika. Tuliingizwa kwenye kinyumba kibovu sana! Kimejaa tunguli tupu! Wazee wakaongea maneno yao kwa Kipare ya kuomba dua! Wakachukua pombe na kuweka kwenye Kibuyu kikubwa, eti ni ya mizimu! Walisema baada ya dakika mbili mizimu itakuwa imekunywa pombe hiyo ikiashiria kwamba dua lao limekubalika. Wakafanya hivyo hivyo na nyama ya mbuzi na matabiko haya yanafanyika katika eneo wanaloita milima ya Wapare! Huko ndiko Wapare wanaendeleza FGM. Baadhi ya wanawake wengi wa kipare wamekatwa nani zao eti wasitamani wanaume na kuzuia wasitoke nje ya ndoa zao. Aibu kubwa Wapare nyie msioelimika!

Kwangu, naona kama Ndugu yangu amepotea kidogo kuoa kutoka kabila hili maana usiku huo hakulala kabisa. Aliogopa sana na kusikitika kwamba angejua…... Eti kila Mwaka wanatambika na lazima ahudhurie. Nadhani akiwa kama mwanamme, hayo matambiko hayamhusu kwa vile anatoka ukoo tofauti na kabila sio la Wapare. Nimemshauri asishiriki matambiko ya aina yeyote!

Ni bora wachaga na wa Pare wawe wanaoana wenyewe kwa vile wao ndo wenye matambiko haswaa kwa karne hii ya 21! December imekaribia utaona wanavyohangaika kwenda kutambika!

Badilikeni nyie!
 
ndg kwan umelazimisha uoe mpare/mchaga? na kama mlichukia na huyu jamaa yko mngemsusa uyo dem mbona mmekubal chezea papuchi wee
 
ndg kwan umelazimisha uoe
mpare/mchaga? na kama mlichukia na huyu jamaa yko mngemsusa uyo dem
mbona mmekubal chezea papuchi wee

Matambiko yanafanywa na makabila mengi sana sio wapare na wachaga tu,kaka yangu alioa mhaya akisimulia ya huko utachoka!
Na hao wapare/chaga si wote wanatambika,mimi nimeolewa na wapare na sijawahi kutambika hata siku moja!
 
Kama ni wewe ama ndugu yako kaolewa/kaoa huko uchaggani au upareni na akakutana na madhila haya usijaribu kuuaminisha umma kwamba haya yanafanyika ndani ya kabila zima,.

Tatizo siku hizi watu wanakutana vichochoroni na kuvikana pete za ndoa kiholelaholela tu pasipokujua maadili na tamaduni za mwenzake badala yake mnakuja kulialia na kutupia lawama kabila zima,.

Kila kabila lina mila zake nzuri na mbaya na siyo kila mtu ndani ya kabila hilo anazifuata mila hizo, wengine wanazipuuzia tu na maisha yanasonga wamemshika MUNGU!!

Mimi ni mchagga na unayoyasema sijawahi kuyaona wala kuyashuhudia ndani ya ukoo wala familia yetu!!
 
nani kakuambia kabila nzima wanafanya hiyo kitu inqtegemeana na familia zao na imani zao kuna wachagga hawajui hata mitambiko nini?
 

ya ngoswe muachie ngoswe
ya wapare na wachaga tuachie wenyewe
hamjalazimishwa muoe ww na huyo jamaa ako
si mngeahirisha eeboooo!!msituharibie mudi ya
kwenda kutambika mwisho wa mwaka sie!!
cc Eli79 njoo mnasemwa huku shemeji zangu!!
 
Last edited by a moderator:

ya ngoswe muachie ngoswe
ya wapare na wachaga tuachie wenyewe
hamjalazimishwa muoe ww na huyo jamaa ako
si mngeahirisha eeboooo!!msituharibie mudi ya
kwenda kutambika mwisho wa mwaka sie!!
Cc eli79 njoo mnasemwa huku shemeji zangu!!

kwani makabila mengine hakuna si wakaoe huko jamani...........

Kila siku wachaga wachaga....arghh
 
Moshi ndio kwetu. Tunatambika...mbuzi na mbege kwa sana tu ndio maana wenzio tuna win life daily. Wenzio tunaotesha maghorofa mjini kila siku cz tunajua umuhimu wa matambiko.

Kwanza kwa taarifa yako matambiko hata kwenye bible yapo na mitume na manabii wengi walikua wakitambika. e.g moses, cain and abel, yakobo etc. Wote hao agano la kale walikua wanatoa sadaka za kuteketeza.
Rejea agano la kale. Ndio maana sisi wachaga kwa mwaka tunafanya atleast twice. Hivi vitu vipo, vina exist na vina effect zake, nime vi prove mara kibao. Mimi ni mkristo damu lakini issue za matambiko nazijua zilivyo na zina mchango gani kwenye familia na ukoo wetu.

Your ignorance is the cause of your failure. Mimi nilikua nafanya biashara miaka nenda rudi nikawa sioni faida zaidi ya hasara na mabalaa kila kukicha mpaka nlipoenda kwetu Moshi nikaongea na wazee wa ukoo na kuwaambia matatizo yangu wakanipa detail zote na vitu vya kufanya...since then kila kitu kina run smoothly.

Hizi issue sio uchawi ni traditional beliefs & rituals
ambazo zina govern maisha yetu ya kila siku sema wengi hawajui tu. Kwenye bible zimeelezwa pia. Tunachofanya ni kuomba na kutoa sadaka in a traditional way...mambo ya kukeketa watoto wa kike na makafara ya watu hatufanyi sisi cz huo ndio ushirikina wenyewe. Kanisani naenda kila jumapili ila mila zina nafasi yake pia. Sikushikii fimbo uamini, take it or leave it !!
 
Samahani Kaka mm mpare tena msuya kwa baba na mbwambo kwa mama nikoo tofauti kabila 1cjawahi kuona hzo mambo usituharbie kabila na huko kukatwa Ww ndo ngariba ulisibitisha hyo tafuta lkuongea ,kwnda kila mwsho wamwaka nyumbni lzma mwenda kwao si mtoro kma Ww huendi kwnu utajijua lbda hapakuvutii ,chezea kilimanjaro Ww kijani inatawala milima yakuvutia ,
 

ya ngoswe muachie ngoswe
ya wapare na wachaga tuachie wenyewe
hamjalazimishwa muoe ww na huyo jamaa ako
si mngeahirisha eeboooo!!msituharibie mudi ya
kwenda kutambika mwisho wa mwaka sie!!
cc Eli79 njoo mnasemwa huku shemeji zangu!!

Asante kuniita shem langu....
Kama hawezi aachane na sie ati....
Hatuwezi acha mila zetu, ukilipenda boga basi na ua lake ulipende....
 
kwani makabila mengine hakuna si wakaoe huko jamani...........

Kila siku wachaga wachaga....arghh

hawajapenda boga hawa watu
wangependa boga na ua lake wangelipenda
hata lingekua na rangi dume!!waoaji gani wanamnanga
bi harusi mtandaoni lolz!!
 
Wapare gani unaowaongelea?
Wasame, Wagweno, or wote?
...
Mbona wasame wameacha hayo matambiko! Ni wachache sana wanaendelea na huo upuuzi! Hata kukeketa hawakeketwi tena!
Watake radhi wenzio kusema hawapaswi kuolewa na makabila mengine! This is pure DISCRIMINATION!
...
Mi na kapare kangu bariiida! Hajakeketwa na hapendi kabisa hayo mambo ya matambiko!
Jaribu kuspecify maelezo yako!
 
Mcheku WitnessJulius njoo inbox.
Mimi ni mpare kwa Baba na Mama na nnatoka jimbo la Anne Kilango huko same mashariki, Sijawahi ona wala kusikia issue hizo

Alafu mbona hajasema ni Upareni wapi aisee?
 
Wapare gani unaowaongelea?
Wasame, Wagweno, or wote?
...
Mbona wasame wameacha hayo matambiko! Ni wachache sana wanaendelea na huo upuuzi! Hata kukeketa hawakeketwi tena!
Watake radhi wenzio kusema hawapaswi kuolewa na makabila mengine! This is pure DISCRIMINATION!
...
Mi na kapare kangu bariiida! Hajakeketwa na hapendi kabisa hayo mambo ya matambiko!
Jaribu kuspecify maelezo yako!

teh teh kwahyo unakubali kuwa sio kitu kizuri?
 
Back
Top Bottom