Wengi hawajui kuwa ulimwengu unaongozwa kwa kuzingatia katiba, sheria na kanuni za aliyeiumba Dunia na ulimwengu

GRAMAA

JF-Expert Member
Nov 1, 2014
1,155
3,399
Yaani cha ajabu mpaka leo kuna watu wengi hawajui kama dunia na ulimwengu kwa ujumla unaongozwa kwa kuzingatia katiba, sheria na kanuni za aliyeiumba dunia na ulimwengu.

Watu wengi sana wamejikuta wanakumbwa na majanga magonjwa, ziki, vifo, kilema, umasikini, nuksi, mafuriko, ukame n.k kwa sababu tu wameshindwa kutii na kufuata sheria na katiba ya ulimwengu na dunia.

Na kwa bahati mbaya sheria hizi zinamuadhibu mtu yoyote bila ya kujali anaamini katika Mungu, Ibilisi, Shetani, Alien, Anunnaki, Mizimu, nature au kitu chochote kile.

Mfano mdogo ni kwamba haijalishi unaamini miungu, Mungu, mizimu au Alien, ikitokea umekanyaga moto ni lazima uungue tu.

Na bahati mbaya zaidi ni kwamba kutokuzijua sheria hizi hakufanyi mtu asiadhibiwe. Yaani ni kwamba ukikanyaga moto bila ya kuuona haiwezi kuwa sababu usiungue kwa sababu tu eti hujauona. Au ikitokea umekula sumu bila ya kujua kuwa ni sumu haiwezi kuwa ni sababu ya hiyo sumu isikuue au kukuletea shida.

Na bahati nzuri pia sheria hizi zipo katika kila kitu ukifanyacho kilasiku ya maisha yako. Iwe kula kwako, kulala, kuoga, kulima, kutembea, kuendesha vyombo vya usafiri, biashara, kuongea, elimu, ndoa, mahusiano. Yaani kila kitu ufanyacho kila siku kipo ndani ya katiba na sheria za ulimwengu.

Mfano mwingine mdogo ni mwamba ukitokea umevunja sheria ya ulimwengu ya ule au unywe nini, saa ngapi na kiwango gani basi ni lazima upate magonjwa hata kama ulikuwa hujui kuwa kuna sheria ya ulimwengu inayokuongoza katika suala la kula na kunywa.

Haijalishi wewe ni padre, sheikh, mchungaji, mganga wa kienyeji, mpagani au askofu, ikitokea umevunja sheria ya ulimwengu ya kula na kunywa lazima upate adhabu yako ya kisukari, presha, kiharusi n.k.

Na bahati mbaya tena ni kwamba ukivunja sheria hizi adhabu yake haifutwi kwa maombi, dua, matambiko au sala. Yaani hakuna mchungaji yoyote au sheikh yoyote atakayezuia asipate adhabu au faini yako.

Upatapo janga lolote lile inapaswa kwanza ujiulize umevunja sheria ipi ya ulimwengu na sio kukimbilia maji ya Mwamposa kwani hayatakusaidia kitu chochote.

Sheria hizi zinamuadhibu yoyote aliyezivunja, awe mtoto, mkubwa, mlemavu, kikongwe au chizi.

Yaani ikatokea mtoto au mlemavu alisiyejua kuogerea akaingia kwenye maji lazima apate adhabu yake. Au ikitokea mtoto au mlemavu alikuwa anachezea moto ndani ukashika vitu lazima nyumba iungue. Hakuna excuse ya umri, hali au jinsia kwa mtu yoyote atayevunja sheria hizi.

Haijalishi upo kanisani, msikitini, kwenye matambiko, gesti au madhabahuni, ikitokea umevunja sheria hizi adhabu yake inakukuta hapo hapo ulipo.

Kitu pekee kitakachomuepusha binadamu na majanga ya ulimwengu ni kutii katiba na sheria za ulimwengu tu na sio dini yako, sheikh wako, mchungaji wako au mizimu yenu.

Chukua hiyo na uifanyie kazi itakusaidia sana.
 
Andiko swafiii kabisa

Watu wanaendesha vyombo vya moto hovyo hovyo tena wakiwa wamelewa wakipata ajali wanakimbilia kusema et makafara wakati wamevunja sheria makusudi
 
Ingekuwa dunia inaadhibu watu kwa kutofuata sheria basi wanadamu wote duniani wangekuwa wameshaisha kwa sababu hakuna mkamilifu yaani mtu anaye fuata sheria 100%.
Lakini jambo jema kwetu wakristo ni kwamba mwokozi wetu Yesu kristo kajitoa kafara yeye peke yake kwa kukubali kufa kifo cha fedheha msalabani ili sisi wanadamu tumuchao tusihukumiwe kwa minajili ya kanuni na sheria za ulimwengu bali tuokolewe kila tuingiapo majaribuni.
 
Back
Top Bottom