Guasa Ambonii
JF-Expert Member
- Aug 13, 2015
- 8,545
- 10,304
Nimesoma bandiko lako kisha nikamfikiria mtunzi namna alivyo kuwa katika mashimo ya Mfalme Suleiman namna watu weupe wale walivyotumia nguvu na akili zao ili haki ipatikane ili kuwaaminisha watu waweza kuwakubali waliwaambia mambo ya kupatwa kwa mwezi na kweli tukio likatokea na watu kuanza kuwakubali tizama namna walivyo mpigania faulata ambae angetolewa kafara usiku ule wa ngoma.Sina sababu ya kupingana na wewe katika hili, ila jambo moja ni dhahiri nalo ni kwamba vilifanya watu wasome sana na kufurahia hadithi hizo...mimi nakumbuka nikiwa darasa la tatu Mwalimu wa Kiswahili alikuwa anatusomea hadhithi kutoka kitabu kile cha Mashimo ya mfalme Suleiman mpaka unajona kuwa labda uko katika nchi ya wakukuana...Yaani kila wakati tulikuwa tunaomba Jumanne ifike haraka tupate kusikia tunavyosomewa hadithi ile, na mwalimu yule alikuwa anasoma kwa mbwembwe mpaka raha....
Kuna mabaya mengi ya wazungu lakini kuna mazuri mengi pia...Sasa whether mabaya yanazidi mazuri au mazuri yanazidi mabaya this is a subject for discussion....
Nami kuna upande nakubaliana nawe ila kiufasaha fasihi au kazi za sanaa kwa ujumla wake ni kuchukua yale mazuri na kuacha mabayanakubaliana upande mmoja na ndugu aliyeleta hoja kuwa vitabu kama vya "mashimo ya mfalme sulemani"hiki cha ''umsolopagaz"''jamaa hodari kisiwani''rabson crusoe na vingine vilikuwa na mrengo wa kutukuza uzungu na vilijengewa mawanda hayo huku vikimdogoesha na kuharibu utu wa mwafrika hasa unapokisoma ''between lines"lakini kwa ufundi wa lugha na unyumbuliko wa kimshono wa matukio ni moja ya vitabu vilivyoweza kufanikiwa sana.Pia matumizi ya lugha hasa ni yenye utajiri mwingi wa lugha za picha ambazo ni aghalabu sana kutoka akilini mwa msomaji.Aina hii ya uandishi ni nadra sana kuikuta leo .
It's OK. As long as inakupa "Authentic pleasure" mkuu. Mkate umepakwa siagi tamu unang'ara lakini kwa ndani "umepatwa" na sumu kali ya kumdogosha Mwafrika kuwa chombo cha mzungu kiuchumi na kitamaduni. Hali hii bado haijabadilika. Ajenda tu ndo zinabadilika.Waafrika tulikuwa hatutembei bila nguo? Waafrika tulikuwa hatuli matunda mwitu? Waafrika hatukuwa tunakula nyama mbichi? Waafrika hatuna African magic? Waafrika tulikuwa hatukeketi wadada? Waafrika hatukuwa tunarithi wajane? Waafrika mzazi akifariki, ndugu wa mume wanakwenda kunyanganya mali za watoto? Waafrika hatukuwa tunazuia mama waja wazito wasile samaki nyama mayai maziwa?
Sijui unaikataa vipi literature. Ragged trousered anthropist. It's fictitious novel. Inachora wahusika kulingana na mazingira ya wakati huo.
Wonderful asante sana kaka[emoji120] [emoji120] [emoji123] [emoji109] [emoji115]Bougwan salaam mkuu!
Je umechoka sana kuwinda jana?
Bougwan nitakupa hadithi nayo ni ya mwanamke nawe unisikize
Alikuwepo mtu na ndugu yule mtu alikuwa na mwanamke lakini yule mtu alikuwa na mkewe kipenzi akimpenda sana akawa anamfanyia istihizai. Lakini yule mwanamke alikuwa mwerevu na moyo wa kisasi akamwambia yule mtu fanya vita na ndugu yako nami nitakusaidia
yule mtu akajua yule mwanamke ni muongo lakini kwa kuwa alimpenda sana akakubali kufanya vita na ndugu yake.
Hata vita vile vikaua watu wengi mpaka yule ndugu akamtumia salaam yule mtu "ndugu yangu tulipokuwa wadogo tulicheza pamoja na tulipokuwa wakubwa tulienda kupigana vita pamoja tukagawana mateka mwanamke kwa mwanamke ng 'ombe kwa ng'ombe nimekukosea nini mbona wataka kuniua ndugu yangu kipenzi ?
Yale maneno yakamfanya yule mtu moyo wake ukawa mzito akakomesha vita na kuja kuishi na yule ndugu yake kwenye jumba lao. Siku zikapita akaja yule mwanamke na kusema tusahau yaliyopita nitakuwa mke wako mwema yule mtu akajua kabisa yule mwanamke ni muongo lakini kwa sababu alimpenda sana akakubali basi usiku ule ule walio oana yule mwanamke akanyata mpaka penye chumba cha yule ndugu akamuua kisha akarudi taratibu kama simba aliekwisha kula shibe yake na kumuwekea shoka lile lenye damu.
Asubuhi watu wakaenda kuwaamkia wafalme wakakuta yule ndugu kauwawa akaenda kumpa khabari ndugu yake wakamkuta ndio kwanza aamke na pembeni yake kuna shoka la damu wakavikumbuka vile vita! tizama kamuuwa ndugu yake wakataka kumkamata akakimbia na njiani akakutana na yule mwanamke akamuuwa !lakini mauti ya yule mwanamke hayakuweza kufuta dhambi aliyoifanya yule mwanamke kwani mzigo wa dhambi yake umetwikwa mabegani pa yule mwanaume peke yake basi yule alie kuwa mkuu zamani hutembea tembea mbali na kwao hana mke wala nyumba hivyo basi atakufa kama mnyama aliepigwa na jina lake ni twezo katikati ya watu wake kwani watu husema alimuua ndugu yake Lousta kwa hila nyakati za usiku.
Kisha yule mzee mzulu akakiinamisha kichwa chake nikaona jinsi hadithi yake inavyo muhuzunisha kisha akanyanyua kichwa na kusema
Mimi ndio mtu yule bougwan kama mimi nilivyo ndiyo utakavyo kuwa! chombo mchezo wa kuchezea ng 'ombe abebae mzigo wa dhambi wa mtu mwingine! Alipo kuchoma kisu na kupiga deraya yako nilikuwepo ulipomuacha atereze kama nyoka katika miamba nikajua amekuroga kwa uzuri wake na nikasema mtu aliependa njia iliyonyooka sasa kachagua njia iliyo potoka nisamehe baba yangu kama maneno yangu ni makali lakini yanatoka katika moyo uliojaa usionane nae tena nawe utashuka katika kaburi lako kwa heshima vinginevyo nawe utakuwa kama mimi pengine wa haki zaidi kuliko mimi kwa ajili ya uzuri wa mwanamke unao chakaa kama vazi likiisha valiwa.
Hadithi ilipoanza kufanana na bwana good (bougwan )alibadilika na uso wake kuwa mwekundu kisha kwa aibu akasema "siku tegemea kama katika maisha yangu kufundishwa ustaarabu na mzulu ni kweli nilitakiwa nimkamate sorais nina stahili adhabu yoyote toka kwenu.
Shukran swahiba tunadokoa dokoa tukikumbukaWonderful asante sana kaka[emoji120] [emoji120] [emoji123] [emoji109] [emoji115]
Hicho kitabu ni cha Sir Rider Haggard, 'King Solomon's Mines' Out of print.Kwa dar nina uhakika waweza kukibahatisha kwenye old bookstalls. Siijui vizuri dar, ningekuelekezaKitabu hicho kinapatikana wapi pls