Mheshimiwa Zitto,
Heshima mbele ndugu yangu, maneno mazito ila kama unavyojua hapa kuna kiporo, ambacho wana-JF tumekuwa tukikusubiri kwa hamu, tumeshasema sana kuwa tunaheshimu sana your presence hapa, na hasa mawe yako na pia the most important your vision kama kiongozi, tumekufagilia sana hapa kuwa tuna imani na wewe kama kiongozi mwenye vision, mimi ninakuomba tu-switch the subject,
Tunajua kuwa kuna mchezo mchafu uliochezwa na DR. NCHIMBI, katika kumpiga vita Amina Chifupa, mbunge wa CCM, asiwe mwenyekiti wa CCM-Vijana, in the process ya hiyo operation, kwa mshituko mkubwa hapa forum tukasikia ukihusishwa na kashifa nzima ya kumuangamiza Mbunge, Mwanamama Amina Chifupa, kisiasa, na sisi hapa forum sio wajinga wa kutojua kuwa jina lako kisiasa, sasa limechafuliwa kwa kiasi fulani, lakini tuliwahi kukuombea na kutabiri kuwa iko siku uta-bounce back,
Sasa tusingependa unafiki au umbeya, kama sio udaku, mimi kama mtu niliyekuwa ninakufagilia sana, na bado ninaendelea kukufagilia as a matter of principle, ningekuomba uiweke hii ishu to the rest, by coming clean hapa forum nyumbani kwako, na sisi tuta-spread the good and the bad news,
Wana-Forum, tungependa kujua exactly, What happened? WHY? na WHERE? kama sio WHY YOU?
Na ninakuhakikishia what ever you say, we will take it na case close, please come clean mheshimiwa!
Ahsante kwa kunielewa, ingawa ni nje ya hii topic ila the best time and place, ni sasa na hapa forum!!