Wanawake wenzangu mnazoeaje maumivu haya ya tumbo?

Status
Not open for further replies.

Leejay49

JF-Expert Member
Feb 10, 2023
12,835
39,694
Habari ya asubuhi,

Wenzangu huwa mnazoeaje haya maumivu jamani?😓😓

Yaani iko hivi, tumbo linauma kama mtu yupo tumboni anavutavuta utumbo, yaani kama yuko na kijiko anakwangua ukoko kwenye sufuria vile. Sasa ushuke chini kiuno jamani, ni kinakamaaa kama sijui nini, ukijinyoosha tu maumivu yake ni shida khaa!🤨🤨

Kuja sehemu nyingine huku chini ni kama sindano zinachomwa chomwa huko ndani, ni full shida yaani haaaa.😭😭😭 Hapo bado uje kwenye matiti ni yanauma jamani,😥😥 yamesimaa halafu ni mekundu, yaana moto kama sijui kitu gani yaani, bra yenyewe nimepata shida kuvaa maana nikivuta tu mkanda nasikia maumivu sio ya nchi hii.

Yaani nimekunywa dawa zote unazozijua za kutuliza maumivu lakini wapi.😓😓 Wakasema ninywe maji ya moto ila nakaribia kumaliza chupa hapa lakini sioni dalili ya maumivu kupungua, mkojo tu unabana nikienda chooni kuchuchumaa nako tabu haaaa!😖😖

Yaani hapa niko ofisini siwezi kukaa, natembea tembea tu muda wote, nasubiri kila mtu aingie ofisini kwake nibebe PC yangu nikajilaze kwenye kochi la wageni pale reception. Maana nina tabu jamani kusimama muda wote, nikisema nikae yaani kama nakalia sindano haaa!😭😭

Wenzangu mnawezaje kuzoea, maana mimi nashindwa jamani? Sijui Mungu aliwaza nini kuniumba wa kike, naumia mwenzenu, 😥😥😥nifanyeje eti?
 
Habari ya asubuhi
Wenzangu hua mnazoeaje haya maumivu jamani
Yani iko hivi, tumbo linauma kama mtu yupo tumboni anavutavuta utumbo, yani kama yuko na kijiko anakwangua ukoko kwenye sufuria vile., asa ushuke chini kiuno jamani ni kinakamaaa kama sijui nini, ukijinyoosha tu maumivu yake ni shida khaa., kuja sehemu nyingine huku chini ni kama sindano zinachomwa chomwa huko ndani ni full shida yani haaaa ...
Hapo bado uje kwenye maziwa ni yanauma jamani yamesimaa halafu ni mekundu yana motoo kama sijui kitu gani yani,, blaa yenyewe nimepata shida kuvaaa maana nikivuta tu mkanda nasikia maumivu sio ya nchi hii...yani nimekunywa dawa zote unazozijua za kutuliza maumivu lakini wapi,, wakasema ninywe maji ya moto ila nakaribia kumaliza chupa hapa lakini sioni dalili ya maumivu kupungua, mkojo tu unabana nikionda chooni kuchuchumaa nako tabu haaaa ..
Yani hapa niko ofisini siwezi kukaa yani natembea tembea tu mda wote, nasubiri kila mtu aingie ofisini kwake nibebe PC yangu nikajilaze kwenye kochi la wageni pale reception maana nina tabu jamani kusimama mda wote...nikisema nikae yani kama nakalia sindano haaa....
Wenzangu mnawezaje kuzoea maana mimi nashindwa jamani,, sijui Mungu aliwaza nini kuniumba wa kike naumia mwenzenu ...nifanyeje eti???
Pole sana Dear
Tafuta pain killer,kuna pain killers kadhaa

Na hakikisha siku chache nyuma unakuwa unakunywa maji ya uvuguvugu,yanasaidia.

Maziwa kuvimba na kuuma ni kawaida.

Kuwa mwanamke si kazi ndogo wallah..
Nakuelewa sana
 
Asante. , sio kazi ndogo kweli
Tumia pain killer

Yai linapoachia humo ndani kwenye ovary,lazima maumivu upate,maana huo ni mwili, siyo chuma.

Tumia Pain killer za kawaida tu.. utakuwa poa.
Kunywa na vitu vya uvuguvugu...iwe utaratibu wako kila siku.

Wanawake kupumzika ni juu Mbinguni kwa Baba.
Kupumzika Mp ni hadi ubebe mimba,,
Ni moto juu ya moto,mp unapumzika,ila inaibuka kidedea nyingine ya kulea mimba.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom