Wanawake wenye akili/smart mnawapata wapi?

Wanawake wenye akili/smart mnawapata wapi?

Lavit

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Posts
16,489
Reaction score
38,389
Habari wakuu..

Uzi wangu hauna lengo la kubeza uwezo wa wengine wa kufikiri au kutaka kujikweza.

Siwezi sema niko smart sana ila angalau nina awareness ya mambo kadha kwa kadha, napenda kujifunza vitu vipya na maarifa ya ziada kila uchwao.

Shida yangu ni moja, sikumbuki kama nimewahi kuwa na mwanamke ambaye yupo vizuri/smart katika ufikiri na mambo yake kiujumla. Wanawake ninaowapata wanaishia kunidisappoint, unakuta mtu hata uelewa wa mambo yanavyoenda katika dunia ya leo hana kabisa.

Siwezi waita vilaza ila ni aina ya watu ambao hata ukiamua kumfundisha vitu basics kabisa inakuwa kama ni kutwanga maji kwenye kinu.

Zaidi ya umbea, kuingia insta na kupost status whatsapp unakuta hana cha ziada kingine.

Je, wanawake wote wako hivyo? Kama hawako hivyo je nyie wenzangu mnawapata wapi wanawake ambao wanaweza hata kukuletea zawadi ya kitabu ukisome?
 
Kuna maswali mengi inabidi uyajibu
1. Your neighborhood
2. Elimu yako
3. Kazi yako, Lawyer hawezi kuwa sawa na bodaboda ofcourse.
4.Kipato chako kitakuruhusu utembelee sehemu fulanifulani hivi wanapopatikana wa aina fulanifulani
5.Hobbies ulizonazo, mfano kutembelea Museums, Libraries, exhibitions fulani fulani, michezo ya aina fulani ni tofauti na mtu mwenye hobby ya kuangalia tu mpira nyumbani au movie au kupiga tu stories vijiweni.
6.Sehemu pia za Ibada, ( most of time si mara zote) utakutana na watu wanaojitambua.
Na kadhalika nyingine watusaidie wengine
 
Inawezekana shida ni wewe, wakati mwingine unaweza kuwa unaamini jambo ambalo halipo kiuhalisia inawezekana unaamini wewe ni ,,smart” lkn kumbe ni illusion, ni wewe jinsi unavyoona, kwani Wanawake ,,smart” wapo wengi tu, sasa kama unashindwa kuwatambua basi labda inawezekana tatizo halipo kwa Wanawake ,,smart”, ...
 
Mtoa mada umesema ukweli. Unakuta mdada mlisoma naye primary na secondary alikuwa smart sana. Sasa hivi ni majanga. Sijui ni nini kinatokea, wanakuwa wanajali zaidi mionekano yao na kuvutia wanaume kuliko intellectual development.
 
Mimi nafikiri kila mwanamke ni SMART na mwenye AKILI kulingana na mwanaume aliyenaye.

Chukua tu mfano wa kitu kilichooza na kunuka, wewe harufu itakukera na utaona ni uchafu lakini nzi huhisi harufu inayovutia na hufurahia chakula bora.

Wakati mwingine Mungu hutupa tunachostahili na sio tunachokitaka.
Huenda ukaona umepata mwanamke SMART kumbe mjuaji.

Hitimisho;- "Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali MKE MWENYE BUSARA, mtu hupewa na BWANA. Mithali 19 : 14. (Biblia).
 
Kuna maswali mengi inabidi uyajibu
1. Your neighborhood
2. Elimu yako
3. Kazi yako, Lawyer hawezi kuwa sawa na bodaboda ofcourse.
4.Kipato chako kitakuruhusu utembelee sehemu fulanifulani hivi wanapopatikana wa aina fulanifulani
5.Hobbies ulizonazo, mfano kutembelea Museums, Libraries, exhibitions fulani fulani, michezo ya aina fulani ni tofauti na mtu mwenye hobby ya kuangalia tu mpira nyumbani au movie au kupiga tu stories vijiweni.
6.Sehemu pia za Ibada, ( most of time si mara zote) utakutana na watu wanaojitambua.
Na kadhalika nyingine watusaidie wengine
Kuna wenye vyote hivyo lakini bado wanaambulia wanawake pasua kichwa.
 
Back
Top Bottom