Wanawake wengi huomba kufanyiwa upasuaji badala ya kujifungua kawaida

Habari wakuu na wadogo wote.

Hii si habari njema hata kidogo. Kumekuwa na ongezeko la wanawake wanaojifungua kwa njia ya upasuaji kuliko njia ya kawaida. Na habari yakusikitisha ni kwamba, wanawake wengi huomba wenyewe kufanyiwa upasuaji.

Kwanza naomba nisiulizwe chanzo cha habari hii. Huu ni utafiti wangu binafsi, kutokana mizunguko ya kila siku na watu ninaokutana nao. Source kubwa ya habari hii ni mchumba wangu ambaye ni hufanya kazi kwenye idara ya afya sehemu fulani.

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa wanawake wengi kuomba wafanyiwe operation badala ya kusubiri kupush kama ambavyo imezoeleka. Kinachowapelekea wengi kupenda kufanyiwa upasuaji ni sababu za urembo tu na kupenda starehe. Hawana lingine. Yaani cosmetic and leisure reasons are behind the whole movement. Wapo wanaodai sehemu zao za siri zitatanuka na hivyo kupoteza mvuto baada ya kujifungua na wengine wakidai kujifungua kwa kupush ni maumivu sana hawawezi kuyavumilia. Wadada hawataki shida kabisa. Ikumbukwe hospitali binafsi ni biashara, na motive za kampuni (biashara) ni kumaximize profit. So ukija unataka kupasuliwa tutakupasua tu sisi tupige hela vizuri.

Kasumba hii inaendelea hata kwenye kunyonyesha watoto. Wanawake hawataki kunyonyesha watoto matiti yao kwa sababu wanadai yataharibika na kupoteza mvuto. Hali si shwari huko mahospitalini, hasa ya private ambako kuna uhuru wa huduma, specilists wengi wanafatwa na wadada wakidai wawapasue hawana mpango wa kupush. Uchunguzi umegundua wengi wa wanaopenda kupasuliwa ni wanawake wenye kipato cha kati ambao wanaweza kumuda gharama za upasuaji, either kwa bima au kwa kulipa cash. Ambao wengi ni wenye kiwango fulani cha elimu yaani tunaowaita wasomi huku katika jamii yetu.

Kule jijini Mwanza kuna afisa wa polisi mmoja mkewe alikua client wangu katika mambo fulani. Dada yule anayeitwa Eunice alikua na watoto 3 mwaka 2016. Watoto wake wote 3 aliwazaa kwa njia ya upasuaji ambapo kuna 2 au wote watatu (sikumbuki vizuri) wanafanana tarehe zao za kuzaliwa ikiwa ni juhudi zake mwenyewe kupitia kujifungua kwa njia ya upasuaji. Kimsingi yeye hataki kabisa masuala ya kuumia uchungu wakati wa kujifungua.

Hiyo ndio hali halisi
Madhara ya kuliwa 0713....
 
Asubiri kwanza akishakua mjamzito akafikisha wiki 41 apate uchungu siku 3 apelekwe leba njia ifunguke adi 8cm iishie hapo isiendelee kufunguka ndio atasema vizuri sitaki alama tumboni.
Hapo ndo ataelewa, unavumilia mtoto hatoki, njia imefunguka unafanyaje SASA mtoto aharibike au ufe kisa naogopa kovu
 
Back
Top Bottom